Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,416
- 2,264
Mkuu, hapo kwenye rangi isomeke Kibunango...Kibunago twashukuru sana kwa habari. Nina swali hile safari rally ilifia wapi na bongo rally gani ni maharufu au inajulikana kimataifa
Safari rally bado ipo ila sasa ipo chini ya jina la Kenya Commercial Bank, na ni baada ya kuondolewa katika Mashindano ya Mbio za Magari Duniani (WRC) mwaka 2003, kwa sababu tele zikiwemo za kushindwa kwa maandalizi na usalama. Zaidi KCB Safari Rally bado inatambuliwa na FIA na ipo kwenye kalenda ya mashindano ya magari ya Afrika(African Rally Championship) yanayotambuliwa na FIA.
Kwa Tanzania mashindano ya magari yanayotambuliwa na FIA ni yale ambayo yamekuwa yakidhaminiwa na Kobil na yanajulikana kama Kobil Tanzania Rally na mwaka jana yalifanyika katika jiji la Dar es Salaam. Aidha kuna mashindano madogo ya magari katika ngazi ya kitaifa na kimataifa katika mikoa ya Arusha na Morogoro. Aidha Zanzibar kipitia Tigo wamewahi kuandaa mashindano ya magari katika ngazi ya kitaifa.
Kwa habari zaidi unaweza kutembelea site ya African Rally, WRC na FIA