Elections 2010 Daily News: Slaa will not be the fifth president of Tanzania!

Kajibuni kwenye Tanzaniadaima kila mtu na uwanja wake wa kujidai ati!

ha ha ha ... leo hadi masatu katokea?
Lakini Dailynews ni gazeti la serikali na sio la chama.
Ingekuwa Rai, mtanzania na tabloids zingine wameandika haya, nani angejali?
 
It is not fare to take bits and pieces of an article na kufikia conclusion. Uli takiwa kutoa the whole article wasomaji waone ni kwa nini conclusion hiyo ilifikiwa na hilo gazeti. Anyway down here I'll quote an article from the editor of Daily News. Somemi kitu kizima ndiyo mtoe hukumu.

kaka umetusaidia...hawa Jamaa zetu kwa kupindisha ndio zao...na ndio hukaa kujisiifisia eti Great Thinker...!!!
 
if DR SIRAHA will not be the next president and they believe on that..then they have to put back ''vote online" again and we will see who is gonna be the next president os TZ. My friends 100% these polls they real reflect the result of 31 october.mvua ya mawe inakuja . Lazima tuvapige kipunde du!!

DailyNews1.png
 
TENDWA atakuja kwenye madhabahu na kusema: " TULIKUBALIANA na vyama vyote kuwa MAGAZETI na TAHARIRI ziandikwe kwa utashi wa mmiliki au mkuu wa chombo kile"

Jamani hatuwezi kuandaa vipeperushi na kuvigawa kwa watu waelewe between the lines ya walichoandika?

Nahisi hiyo tahariri kama hajaandika MUHINGO akawatumia nao wakafanya MUTATIS MUTANDIS bila kuchuja neno.....
 
Acting Managing Editor/Editor;

Mkumbwa Ali, huyu aliwahi kufanya kazi pale Habari Corp, ile ya kina Salva, akitokea huko huko Daily News, kisha akarudi tena! Ni wazi anawaza ki mwaka 47 47 hivi, bado anaamini wao ndio cream ya waandishi wa habari hapa nchini, shame on him. Huyu ni majitaka mwingine, anazidi kummsiliba JK na tope.

Anataka kujilinganisha na majabali yale ya Raia Mwema, hapana hawafikii, huwezi kuli rank Daily News na Raia Mwema, daily news ni kipeperushi cha CCM na JK wao. Ametia aibu.
 
Do you guys really take seriously on Daily news, watu ambao waliripoti habari hii hapa chini makusudi kabisa kuupotosha umma. By the way sisi sasa ndiyo tunalipa umaarufu gazeti la daily news!


SHAME ON YOU DAILY NEWS!!!!!!!!!!!!!

Source: Bofya Hapa



Tanzania wins education MDG award

TANZANIA has won the United Nations award for its impressive progress towards attaining universal primary education, some five years ahead of the 2015 deadline set under the Millennium Development Goals (MDGs).

The Prime Minister, Mr Mizengo Pinda, received the award at a ceremony held at the Waldorf Astoria Hotel in New York on Sunday, describing it as a catalyst for the country to achieve all other MDGs ahead of the 2015 target.

The MDGs, endorsed by the world leaders in September 2000, set out eight targets which range from eliminating hunger, halving extreme poverty, halting the spread of HIV/AIDS and providing universal primary education - all by the 2015 target date.

"This award is like putting fuel of an engine'', said the premier amid applause from the hundreds who attended the function. Tanzania has succeeded by more than 95 per cent in attaining education goal through the universal primary school enrolment.

The UN also awarded Malawi for its success in eliminating hunger by enhancing food security. The award was presented to President Bingu wa Mutharika at the same occasion.

Mr Pinda, who is in New York representing President Jakaya Kikwete, at the 65th United Nations General Assembly (UNGA) and the three-day high level meeting to accelerate the implementation of the UN anti-poverty goals or MDGs, earlier met the UN Deputy Secretary-General, Dr Asha-Rose Migiro and the African Union representative to the UN, Ambassador Amina Salum Ali.

Meanwhile, about 140 world leaders yesterday attended the opening of the MDGs summit, where they are expected to measure progress towards achievement of the targets and review difficulties encountered in the process.

With just five years to go before the deadline for achieving the MDGs, the leaders will discuss how and where they can do more in the remaining period to defeat poverty, reduce hunger, stop environmental degradation, improve education, boost maternal and child health and reach the other remaining targets.

In another development, despite notable achievements in education, there are many challenges being faced in Zanzibar including overcrowded classrooms and inadequate facilities.

"We have recorded a lot of achievements in the past decade in education, including narrowing gender disparity in schools, but there is still much to be done," said Mr Mwalimu Abdallah Mzee, Deputy Principal Secretary in the Zanzibar Ministry of Education and Vocational Training at an evaluation seminar.

Mr Mzee said Zanzibar has reformed its education system, making compulsory education from nursery to form IV, instead of form three.
 
Slaa atibuliwa nyongo

• Wawataka wananchi Same kutomchagua Mathayo

na Janet Josiah

HATUA ya Mhariri wa gazeti la kila siku la serikali linalochapishwa kwa lugha ya Kingereza la Daily News kuandika tahariri inayoonekana kuingilia uhuru wa kupiga kura kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya wakati wake, kimewashtua mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mhariri huyo katika tahariri yake iliyochapishwa katika toleo la jana la gazeti hilo aliandika, Dk. Slaa hawezi kuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania na kwamba alikuwa akitarajiwa kuambulia kura chache kama zile alizopata aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi mwaka 1995, Augustine Mrema.

Tahariri hiyo ilikuwa na maudhui yanayoonyesha jinsi mhariri huyo wa serikali, alivyokerwa na habari ya gazeti moja la kila wiki, iliyotoa matokeo ya kura ya maoni kutoka kwenye mitandao ya kompyuta, yaliyokuwa yakionyesha kuwa Dk. Slaa alikuwa akiongozwa kwa kuungwa mkono na asilimia 76 ya Watanzania waliopiga kura kupitia mtandao huo.

Mbali ya hilo, mhariri huyo wa Daily News alionyesha kukerwa pia na hatua ya gazeti hilo kunukuu matokeo mengine ya kura za maoni kupitia mtandaoni yaliyofanywa kupitia tovuti inayomilikiwa na gazeti hilo hilo la serikali ambazo pia zilionyesha kuwa Dk. Slaa alikuwa akiongoza kwa kuungwa mkono. Hata hivyo gazeti hilo lilishayaondoa mtandaoni matokeo hayo.

Akizungumzia tahariri hiyo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Hedaru wilayani Same jana, Dk. Slaa alieleza kusikitishwa na hatua ya mhariri huyo ambaye kwa sasa anakaimu wadhifa wa Kaimu Mhariri Mtendaji, Mkumbwa Ali, kuandika tahariri potofu katika gazeti la serikali ambayo ina mwelekeo wa wazi wa kukipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete.

Dk. Slaa alisema hatua hiyo ya Mkumbwa anayelipwa mshahara wake kwa kutumia kodi za wananchi wote alikuwa ameyatumia vibaya madaraka yake ya uhariri na akaitaka serikali kumwajibisha mara moja kwa kosa hilo.

"Mhariri huyo hakupaswa kuandika kile alichokiandika huku akijua kuwa analipwa mshahara kwa fedha za kodi za Watanzania wote. Naitaka serikali imwajibishe mara moja na kama haitamwajibisha basi ajue siku zake zinahesabika kama zinavyohesabika siku za rais wake, Jakaya Kikwete…kwa sababu nguvu ya dola haitaweza kuishinda nguvu ya umma wa Watanzania walioamua kunichagua Oktoba 31 mwaka huu," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakimsikiliza.

Akifafanua, Dk Slaa alisema kilichoandikwa katika gazeti hilo la serikali ambalo kiitifaki mhariri mtendaji wake mkuu (Editor in Chief) ni Rais kinaonyesha kwamba iwapo yeye (Dk. Slaa) atashinda katika kinyang'anyiro hicho cha urais, basi hatapewa fursa ya kuongoza wananchi watakaomchagua.

Awali, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akizungumzia suala hilo, alimtaka mhariri huyo kujiuzulu wadhifa wake mara moja kwa kosa la kutumia madaraka yake vibaya na kulitumia gazeti hilo la serikali kwa maslahi ya CCM.

"Daily News isitumike kuwagombanisha Watanzania katika itikadi za vyama, Watanzania ni wamoja. Nataka ajiuzulu na serikali imuwajibishe mhariri huyu haraka kwa kuondolewa katika nafasi hiyo kwani amewadhalilisha sana Watanzania," alisema Mbowe.

Katika hatua nyingine, akihutubia mkutano huo huo, Dk. Slaa alieleza kusikitishwa na hatua ya Mkuu wa wilaya ya Same, Ibrahim Marwa kufika katika eneo hilo na kukaa eneo la wasikilizaji wa kawaida badala ya kupanda jukwaani walikokuwa viongozi wa juu wa CHADEMA kwa walivyopata kufanya viongozi wenzake wa kiserikali katika maeneo mengine.

Akizungumzia kitendo hicho, Dk.Slaa alisema amesikitishwa sana na hatua hiyo ya Marwa ambaye alimtaja kuwa ni rafiki yake cha kuonyesha ubaguzi kwa chama hicho kwani katika hali ya kawaida asingeacha kukaa jukwaani iwapo mkutano huo ungekuwa ni wa mgombea urais wa CCM.

"DC Marwa umekaa chini sisi tumekaa juu…nimesikitishwa sana na kitendo ulichokifanya. Sasa nategemea na rais wako atakapofika ukae chini kama ulivyofanya leo na usipofanya hivyo, nitakufa na wewe. Sikudhani kama ungefanya hivyo maana wewe ni rafiki yangu lakini umenisikitisha sana."

Akiwa katika jimbo la Same Magharibi, Dk. Slaa aliwataka wakazi wa jimbo hilo kutomchagua tena mbunge anayemaliza muda wake, Mathayo David, kwani ameshindwa kutekeleza ahadi zake mbalimbali ikiwemo huduma ya maji kwa wakazi wa jimbo hilo.

"Nimeambiwa Mathayo David anapita na kuwagawia rushwa ya mabati na sh elfu hamsini hamsini. Huko si kuwasaidia ….hajawafanyia chochote cha maana watu wa Hedaru. Hata huduma ya maji ameshindwa. Rushwa ya mabati na pesa sio suluhisho la matatizo ya watu wa Same waliopigika. Tutafanya mabadiliko katika jimbo hili, nipeni mbunge nifanye naye kazi, tubadilishe maisha ya watu wa Same," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa. Akiwa katika wilaya za Mwanga na Same jana, Dk. Slaa alifanya mikutano 10 ya akitumia helikopta.
 
Katika mabadiliko yoyote ya msingi lazima kunakuweko na vibaraka. Mabadiliko ya msingi ya kwanza ya Tanzania yalikuwa yale ya 1961, tulipopata UHURU. Haya yanayokuja sasa ni ya pili. Ni ya kubadilisha chama tawala kwa mara ya kwanza.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inabidika kusema itafanyaje kuhusu hili. Maana hili ni kama chombo cha serikali kutangaza matokeo kabla

Baraza la Habari nalo lazima litoe tamko. Ni njia za kuepusha machafuko.
 
Mhariri anaitwa MKUMBWA ALLY. Huyu anafahamika sana kwa kula RUSHWA, na ni kati ya wahariri waliopo kwenye payroll za mafisadi. Haishangazi kuona mafisadi hao hao wakimtumia kuua taaluma yake kwa kuandika ujinga kama huu. Kwa maoni yangu, huyu ana kesi ya kujibu. Nitashangaa sana iwapo hakutakuwa na hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake. Daily News, Habari Leo na Mtanzania/Rai wasi-underrate intelligence ya Watanzania.

...Mkumbwa Ally. Huyu jamaa si kuna wakati alikuwa na kesi ya rushwa hapo hapo Daily News ambayo ikaishia ishia tu hivi hivi??

 
Hivi ndivyo Mwananchi inavyosema juu ya upupu wa Mkumbwa wa gazeti la Ujinga wa KilaSiku (Daily News)

Gazeti la serikali lazua jambo

Thursday, 23 September 2010
Exuper Kachenje na Salim Said


MAONI ya mhariri yaliyotolewa kwenye gazeti la jana la serikali dhidi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, yameibua hisia kali baada ya makamu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kueleza kuwa yanauma, huku wanaharakati wakieleza kuwa ni ya hatari kwa demokrasia na ya uchochezi.

Katika majumuisho ya tahariri hiyo, gazeti hilo, The Daily News lilisema: "Na ukweli ni kwamba Dk Willibrod Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania."


Kauli hiyo ya gazeti hilo ambalo ni mdomo wa serikali limeibua hisia tofauti kutoka kwa wanasiasa, wasomi, wanaharakati ambao wamelaani na kutaka sheria ichukue mkondo wake.


Dk Slaa, ambaye anaonekana kuzoa mashabiki kadri siku zinavyokwenda, alisema: "Hii inaonyesha kuwa serikali ina mpango mchafu ndio maana wametumia gazeti la serikali.


"Lakini nguvu ya Dk Slaa itathibitishwa kwa kushinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Na kwa maana hiyo siku za mhariri zinahesabika."

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambaye alisema: "Tunataka uchaguzi huru na wa haki. Vyombo vya umma vinatakiwa kutumika kwa ajili ya umma na si CCM. Tuumesikitishwa na tahariri hiyo.

"Tunachotaka ni mhariri achukuliwe hatua haraka kwa sababu hiyo inaonyesha mkakati wa serikali si mzuri kwa wapinzani."


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana watu mbalimbali walioongea na Mwananchi walisema kitendo hicho cha gazeti la serikali ni cha kujaribu kuliingiza taifa kwenye machafuko.


Makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu alisema kauli kwamba Dk Slaa hataingia Ikulu, inaumiza lakini ni juu ya Chadema na Dk Slaa kuamua kulalamika kama wataona imemwathiri.


Jaji Makungu alisema Nec imesikia kauli hiyo lakini haiwezi kuifanyia kazi mpaka kuwe na mlalamikaji.


"Sijalisoma hilo gazeti hilo lakini kauli hiyo inauma... inatakiwa walioumizwa walalamike. Wakikaa kimya, sisi hatuwezi kuchukua hatua. Kamati ya maadili ipo; Chadema au Dk Slaa akilalamika, tutawaita wanaolalamikiwa," alisema Jaji Makungu.


"Tupo tayari kupokea malalamiko. Tuna kamati ya maadili, wakicomplain (wakilalamika), tutajadili na kutolea uamuzi."

Meneja wa kampeni wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amelitaka gazeti la Daily News kuutangazia umma wa Watanzania kuwa linamilikiwa na CCM badala ya serikali.

"Ni vyema Daily News ikawatangazia Watanzania kwamba wao ni gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sio la umma," alisema Profesa Baregu.


Alisema kwa muda mrefu gazeti hilo limekuwa likijionyesha dhahiri kufanya kazi za CCM badala ya kuutumikia umma.


Hata hivyo Profesa Baregu alisema gazeti hilo halina uwezo wa kuwashawishi Watanzania kwa sababu mzunguko wake ni mdogo sana na umeegemea zaidi kwenye wizara na taasisi za serikali.


Alifafanua kuwa CCM na vyombo vyake vya habari wamekuwa na jazba baada ya kuona mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amegeuka kuwa mtaji mkubwa wa Watanzania.


"Rais wa serikali ya awamu ya tano ataamuliwa na Watanzania kupitia kura zao na hakuna mtu yeyote wa kuchezea kura hizo," alisema Profesa Baregu.


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya alisema aliungana na Baregu kusema kuwa uamuzi wa kuchagua rais, wabunge na madiwani ni wa wananchi na unafanywa kwa njia ya kura zao na si chombo cha habari au waandishi.


"Katika kampeni kila mmoja anatoa ya kwake, lakini uamuzi ni wa wananchi. Si waandishi wanaoamua, gazeti au chombo chochote cha habari," alisema.


"Ni kura za wananchi. Ninavyojua mimi vyombo vya habari vinatakiwa kufuata maadili, viepuke vitu vinavyoweza kuleta mgogoro. Hatupaswi kuchochea migogoro. Tuwe makini."


Alisema kitendo kilichofanywa na gazeti hilo ni cha hatari kwa sababu kinakandamiza demokrasia na kujenga hisia kuwa huenda kitendo kilichofanywa na gazeti kinashabikiwa serikali hivyo kuweza kuchochea vurugu ndani ya nchi.


"Kitendo kilichofanywa na gazeti hilo ni cha hatari kwani kinaweza kuchonganisha serikali na watu wake na wakaweza kufanya vurugu kwa kile wanachoweza kukiona hawatendewi haki," alisema.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Fordia, Bubelwa Kaiza alisema Daily News ni gazeti la serikali kwa maana hiyo, mhariri na wenzake hawawezi kujituma bali wametumwa na chama au serikali iliyo madarakani.


"Kwa maana hiyo si tu kwamba amekiuka maadili ya taaluma ya habari, lakini, yeye na wenzake wote hawafai kuwapo hapo na kwa kashfa hii, wanapaswa kujiuzulu mara moja kwa kusimamia uovu," alisema Bubelwa.


"Kama amekubali (mhariri) kutumika vibaya na maadili ya taaluma yake, ni kwamba amehongwa fedha au ameahidiwa cheo na kwa hiyo ni rushwa na ufisadi mkubwa wa matumizi mabaya rasilimali za umma."


Kaiza aliongeza kusema: "Kwa vyovyote huyo anayesemwa (Dk Slaa) ni bora zaidi kuliko hao wasiosemwa, awe ni rais na waziri mkuu waliopo madarakani au aliyejiuzulu. Hatupendi kuzungumzia masuala ya ndani ya watu, lakini wote tunawajua ‘A' to ‘Z' (mwanzo hadi mwisho)."


Hata hivyo, Kaiza alibainisha kuwa habari hiyo haiwezi kuathiri chochote katika uchaguzi mkuu ujao kwa sababu Daily News ni gazeti la Kiingereza na halina wasomaji wengi ambao ni wapigakura, lakini pia mzunguko wake ni mdogo sana.


"Linasomwa sana na watu wanaotafuta matangazo ya kazi, wageni, wizarani na watanzania wachache wanaopenda kutangaza kupitia gazeti hilo," alisema Kaiza.


"Ni vyema chama na mgombea aliyetajwa kwa kutumia sheria na vyombo vilivyopo akatetea haki yake kwa sababu ni jambo kubwa na la kustua hakutendewa haki."


Meneja kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana jana alikataa kuzungumnzia tuhuma zilizoelekezwa kwa chama hicho akieleza kuwa gazeti hili, halitendi haki kwa CCM.


"Lakini ninyi (Mwananchi) you never have good news for CCM (hamna habari njema kwa CCM) kila siku mkipiga simu ni habari mbaya, mnaandika habari mbaya tu za CCM, nzuri hamzioni," alihoji.


"Mara Mama Salma kafanya hivi, mara Ridhwani kafanya vile, why can't you be carrier of good news? Always you carry bad news? (wakati wote ni mabaya tu, hamwezi kuandika mema ya CCM?

"Tafadhali waulizeni Daily News suala hilo."
 
Mihariri mingine bwana yeye hajui kumkandia mgombea kwenye chombo cha serikari ni hatari, kama huyu mhariri ana akili iliyokomaa na hana utoto na alienda shule akaelewa vizuri taaluma yake ajifunze kilichotokea RWANDA!

Waharifu wengine walioshitakiwa mahakama ya mauaji ya kimbali ARUSHA, wengine walitumia vyombo vya habari vya serikali, hivyo hata yeye aelewe kuwa DAILYNEWS si gazeti la CHAMA, ni gazeti la SERIKALI na KODI ZA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI ndizo zinazoliendesha, hivyo anapaswa ajihudhuru katika wazifa, maana mpaka sasa sitalisoma tena hilo gazeti lenye mhariri asiyefahamu maana ya taaluma yake.

Hatari nyingine iliyopo mbele ni kutokea kwa ghasia, mfano ikitokea CHADEMA, wameshindwa wanaweza fanya kumbukumbu kuwa serikali (Kupitia dailynews) ilisema watashindwa hivyo tufanye fujo kupindua serikali maana haitaki mabadiliko, hivyo inaweza kuhatarisha AMANI tuliyo nayo!
 
Back
Top Bottom