Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
" mna upotoshaji kwenye makala yako .... tumesema na tutaendelea kusema, na hizo fitna mnazolishwa na kuziamini hata hazitaturudisha nyuma katika dai letu la msingi nalo ni "SOVEREIGN ZANZIBAR" twataka Zanzibar yetu yenye mamlaka kamili, hatuna haja ya maili 10 za Tanganyika wala nini, chukuweni hatuna haja nazo tena, japo zilikuwa ni milki yetu, yaonesha wengi wenu hata hiyo historia ya MRIMA (Tanganyika) hamuijui. Sisi huku mashaAllah wengi wetu tunaijua historia ya Dola ya Zanzibar, wapi ilipotoka, ilipo leo na inapoenda. Ya nini kuharibu bisu langu kwa nyama isiyoliwa!"
Nguruwe ni nguruwe tu, hata akiwekwa lip stick domo ake halibadiliki, na siku zote umaarufu wa jogoo ni kuchinjwa tu. Kisiwani kuna watu wenye akili na busara, tena hao ni wengi zaidi kuliko watu wenye uchu, baada ya mwafaka kuja sasa wanajaribu kutafuta adui mwingine, hata wakijitenga na bara wataanza kutafuta mwingine. Utumwa wa kimawazo na hasa umaskini wa akili, unajionesha sana siku hizi hapa JF. Inaonekana watu hawajui ni nini maana ya muungano, badala ya kutoa hoja zenye akili za kutaka uvunjwe na wanaleta mipasho kama watu wasioenda darasa hata la madrasa. Get a life!