Dah. . .wanawake wengine bana!!!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,770
59,114
Kwa wale ambao bado hawajaolewa hua hawaishi kuonyesha na kuelezea namna gani wanaume walivyo wabaya hata kufanya swala zima la kuingia ndoani kuwa gumu. Walioolewa hawaishi kulalama namna waume zao walivyo wabaya ndoani hata kuona ndoa zao hazina furaha. Ila wote wanasahau kwamba kwa kiasi kikubwa wengi hua wanachangia ubaya wauonao kwa wanaume kama ambavyo wanaume huchangia ubaya (sio wote) wauonao kwa wanawake.

Kuna dada kaolewa miaka minne(4) iliyopita, na harusi yake ndo harusi pekee ambayo mimi nimewahi kuhidhuria mpaka leo hii. . .

Sina shaka kwamba alikubali mwenyewe kuolewa na siku ile aliifurahia maana alionekana mwenye furaha muda wote. Miaka minne baadae wamejaaliwa mtoto wa kike na maisha yao ni ya kawaida. Sasa wiki iliyopita alimuomba mumewe pesa ya mkaa, mume akawa hana. Alichofanya ni kwamba amemnyima chakula (anachonunua huyo huyo mume) mpaka leo hii. Yani "kwa eaha na shida (siku hizi inabidi mchungaji akisema . . . . na shida waseme "INATEGEMEA NI ZIPI" badala ya "NDIO NAKUBALI" za kinafiki) aliyotamka imekosa matendo.

Sasa mwanamke kama huyu, mume akimbadilikia au akimmwaga atamlaumu nani?Nae ataweza kusimama mahali na kusema wanaume ni watu wabaya? Kwanini asifanye shughuli ndogo ndogo nae awe anasaidia akiona mume mambo hayajamuendea vizuri sana kwenye shughuli zake?

Ahhhhh wanaume wengine mna kazi kweli aisee. . .nawapa pole wote mnaokaribia kupewa vichaa na wake/wapenzi wenu.
 
Sitaki kuingia sana kwenye timbili la kunyimwa menu huyo bwana mkubwa,wha i wanna knw ni kwanini umehudhuria harusi hiyo moja tu?Hapo ndo pamenivutia kwa kweli!Naomba kujua hili kwanza!
 
Hahahaha. . .kwasababu sio mchangiaji!!!Lolz

mende hamna tatizo lolote.
 
Last edited by a moderator:
hahahaha lizzy ni kweli kabisa wanawake wengi tunachangia hayo mambo,hata kama hana kazi but alipaswa kuridhika na kile alichojitahidi mwenzie kukileta nyumbani,kwa mwanamke mwenye akili angepikia hata kuni ama kukopa mkaa kwa siri ili kum2nzia mumewe heshima sio kumnyima chakula alichokitolea jasho.ningekua namjua huyo baba ningemtafutia dogo dogo lol
 
Hahahaha. . .kwasababu sio mchangiaji!!!Lolz

mende hamna tatizo lolote.

kanga%2Bmoko.jpg

Ukipitia huku utaona ndoa ndoano.
 
Mh!Lizzy ujue ni kazi sana kuishi kwa style ya kutochangia kwenye jamii hii ya dotcomu,unaweza tengwa flan hivi.All an all namkubali sana mtu anaeishi kinyume na mazoea,big up kama ni kweli. . . .
 
hahahaha lizzy ni kweli kabisa wanawake wengi tunachangia hayo mambo,hata kama hana kazi but alipaswa kuridhika na kile alichojitahidi mwenzie kukileta nyumbani,kwa mwanamke mwenye akili angepikia hata kuni ama kukopa mkaa kwa siri ili kum2nzia mumewe heshima sio kumnyima chakula alichokitolea jasho.ningekua namjua huyo baba ningemtafutia dogo dogo lol
Hahahaha. . .Jojeeta kweli hao wakitafuta nyumba ndogo inakua ngumu hata kuwalaumu.
 
Mkwe mzima msalimie muhusika nimemiss yeye sana bana mlete kipande hii

huyo dada alipaswa kuangalia je mume kumwambia sina pesa ni kweli na yeye kumyima chakula ni sahihi
kuna vitu vingine katika ndoa havivumiliki hata kama uliapa katika shida na raha lakini kuna vingine kama hiki kilikuwa ni cha kuelewana kutoka na hali may be waliyonayo
 
Mh!Lizzy ujue ni kazi sana kuishi kwa style ya kutochangia kwenye jamii hii ya dotcomu,unaweza tengwa flan hivi.All an all namkubali sana mtu anaeishi kinyume na mazoea,big up kama ni kweli. . . .

Kwanini iwe kazi?
Kazi inakuwepo tu kama na wewe ni bingwa wa kupelekea wenzako kadi. Mimi kabla hawajafikiria kunitenga nilishajitenga. Mambo ya kupangiwa mpaka kiasi chakuchangia kama vile nanunua kitu sifagilii.
 
Mkwe mzima msalimie muhusika nimemiss yeye sana bana mlete kipande hii

huyo dada alipaswa kuangalia je mume kumwambia sina pesa ni kweli na yeye kumyima chakula ni sahihi
kuna vitu vingine katika ndoa havivumiliki hata kama uliapa katika shida na raha lakini kuna vingine kama hiki kilikuwa ni cha kuelewana kutoka na hali may be waliyonayo
Ntamsalimia mkwe. . .ngoja achafuke vumbi kwanza huku kijijini tuone kama bado utampenda akirudi. . .lolzz

Hhhmmm. . .mkwe we unaweza ukapika chakula alichonunua mwenzio, ukala kwa amani kabisa huku yeye ukimnyima kisa tu hakuweza kununua mafuta ya taa/mkaa au kuni? Na hicho chakula asingeleta je?
 
Kwanini iwe kazi?
Kazi inakuwepo tu kama na wewe ni bingwa wa kupelekea wenzako kadi. Mimi kabla hawajafikiria kunitenga nilishajitenga. Mambo ya kupangiwa mpaka kiasi chakuchangia kama vile nanunua kitu sifagilii.

I like your tone!. . . .
 
hii thread Lizzy kaifungua si bure..........haya endeleeni kuchangia,mi napiga chabo tu hapa.
 
Kwa wale ambao bado hawajaolewa hua hawaishi kuonyesha na kuelezea namna gani wanaume walivyo wabaya hata kufanya swala zima la kuingia ndoani kuwa gumu. Walioolewa hawaishi kulalama namna waume zao walivyo wabaya ndoani hata kuona ndoa zao hazina furaha. Ila wote wanasahau kwamba kwa kiasi kikubwa wengi hua wanachangia ubaya wauonao kwa wanaume kama ambavyo wanaume huchangia ubaya (sio wote) wauonao kwa wanawake.

Kuna dada kaolewa miaka minne(4) iliyopita, na harusi yake ndo harusi pekee ambayo mimi nimewahi kuhidhuria mpaka leo hii. . .

Sina shaka kwamba alikubali mwenyewe kuolewa na siku ile aliifurahia maana alionekana mwenye furaha muda wote. Miaka minne baadae wamejaaliwa mtoto wa kike na maisha yao ni ya kawaida. Sasa wiki iliyopita alimuomba mumewe pesa ya mkaa, mume akawa hana. Alichofanya ni kwamba amemnyima chakula (anachonunua huyo huyo mume) mpaka leo hii. Yani "kwa eaha na shida (siku hizi inabidi mchungaji akisema . . . . na shida waseme "INATEGEMEA NI ZIPI" badala ya "NDIO NAKUBALI" za kinafiki) aliyotamka imekosa matendo.

Sasa mwanamke kama huyu, mume akimbadilikia au akimmwaga atamlaumu nani?Nae ataweza kusimama mahali na kusema wanaume ni watu wabaya? Kwanini asifanye shughuli ndogo ndogo nae awe anasaidia akiona mume mambo hayajamuendea vizuri sana kwenye shughuli zake?

Ahhhhh wanaume wengine mna kazi kweli aisee. . .nawapa pole wote mnaokaribia kupewa vichaa na wake/wapenzi wenu.

kudos kwa huu uzi da liz yan umewagusa wale wanaozan ndoa ni fasheni
 
Ntamsalimia mkwe. . .ngoja achafuke vumbi kwanza huku kijijini tuone kama bado utampenda akirudi. . .lolzz

Hhhmmm. . .mkwe we unaweza ukapika chakula alichonunua mwenzio, ukala kwa amani kabisa huku yeye ukimnyima kisa tu hakuweza kununua mafuta ya taa/mkaa au kuni? Na hicho chakula asingeleta je?

kumnyima chakula hata kama angekuwa hajaleta sio vizuri mnyima labda chakula kingine ndio maana nikasema huyo dada ameanzisha ugomvi usiokuwa wa lazima
 
Back
Top Bottom