Dah!!Huyu dingi dah!!!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Huyu bwana mdogo ananiheshimu sana kutokana na anavyonijua.Ana mpenzi tangu anasoma form five, walikua na malengo ya kufika mbali.Kijana alimpoteza mama yake(alifariki) wakati yuko form one,hivyo ameishi na baba yake muda wote huu.Kijana mwaka jana amemaliza chuo,na muda huu anafanya kazi Nbc bank,kazi hii ana mwezi tu tangu aipate.Muda wa mwaka mmoja uliopita amekua akinilalamikia mpenzi wake kubadilika vituko haviishi,nimekua nikimshauri kuwa mvumilivu lakini kilichotokea juzi sijui hata nisemeje.Mpenzi wa kijana ana miaka 25 na kijana ana miaka 27,siku ya tukio majira ya saa 2 usiku alipigiwa simu na baba yake kuwa baba yake ana sapraizi.Kijana akaenda,akamkuta mpenzi wake yuko na baba yake,wakati hajajua kinachoendelea baba akamwambia kijana akae,akafanya hivyo,ndipo baba akamwambia kijana "unajua tangu mama yako atutoke nimekua mpweke sana,sasa huyu natarajia muda mfupi ujao awe nasi pale nyumbani,unasemaje?" Kijana akawa kwenye mshangao,ndipo alipokurupuka kutoka kwenye mshangao na kukubaliana na baba yake.Baadae kijana alimpigia simu mpenzi wake kumuuliza kulikoni binti akamwambia "kwanza naomb iwe mwisho kunipigia simu na kuanzia leo uniheshimu kama mama yako,mambo tuliyofanya huko nyuma yafanye historia.Sasa kijana amechanganyikiwa na anauliza,atawezaje kuishi na mama yake mpya wakati alikua mpenzi wake?Kijana hajui afanye nini,unaweza kumshauri afanye nini?
 
...Mhhh! Kweli duniani kuna mambo...Mababa wengine hawastahili kupewa hadhi hiyo ya kuwa Baba.
 
hivi bongo movies hizi
unashindwaje kumuuliza baba yako 'umemtoa wapi huyu msichana'?
mimi namjua sana na nashangaa umemleta home

halafu una miaka 27 na una mchumba hata baba yako asimjue?

hii kama filam aisee

sisemi kumtambulisha girlfriend kwa baba,
ila kibongo bongo baba anakuwa anajua wasichana wa mwanae jpo kwa kuwaona tu wamekuja home
 
Dogo achukulie poa tu,ndio ukubwa huo na hayo ndio'' malimwengu''
 
...Mhhh! Kweli duniani kuna mambo...Mababa wengine hawastahili kupewa hadhi hiyo ya kuwa Baba.

mtoto wa kike naye hajatulia tu!!kwa nini asingekataa,yeye alijua kuwa ana mtu lakini baba hakujua kama binti ana mtu!!mwenye kosa binti!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
...Mhhh! Kweli duniani kuna mambo...Mababa wengine hawastahili kupewa hadhi hiyo ya kuwa Baba.
BAK hapa sijaona kosa la baba......manake labda hakuwahi kujua kuwa binti yuko na kijana wake..........huyo binti ndie ambae hajatulia manake alikuwa na kijana na bado akamkubali mbaba!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
The Boss,acha kufikiri kwa upofu.Unaweza kumuuliza baba yako huyu msichana umemtoa wapi?Hebu acha utani.Pia kipi unachoshangaa umri wa miaka 27 mchumba wako asijulikane home?Mh!!!!Unaweza ukawa unaishi New York City!
 
Last edited by a moderator:
@Sweetlady kama kweli baba hajui kama binti yule alikuwa anatoka na mwanae basi hana kosa...labda binti kaficha ni jinsi gani alipata nafasi ya kufahamiana na Baba wa kijana. Inawezekana mwenye kosa ni binti labda alijilengesha kwa Baba au kosa lake ni kumtosa kijana baada ya kumpata dingi....Je, Baba akijua kwamba mwanae alikuwa anajinvinjari na huyo binti bado ataendelea na mipango yake?

Hili nalo neno aiseeeeee!!
 
Last edited by a moderator:
Amweleze ukweli Baba yake, maana kama akificha badae itakuwa mbaya zaidi, hasa Baba atakapogundua jambo
 
...Mhhh! Kweli duniani kuna mambo...Mababa wengine hawastahili kupewa hadhi hiyo ya kuwa Baba.
BAK sikupi like na wewe sweetlady umetoa like ya nini? natamani kungekuwa na kitufe cha thumb down. hivi wadhani kwa kosa la huyu baba kuwa na mapenzi na gf wa mwanae kunabadili nafasi ya yeye kuwa baba? dunian hata mtu akosee kitu gani bado kosa alilotenda halimbadilish kuwa mtu wala haliamfany akakosa hakia na heshima yake kama binadamu.

binafsi sijapendezwa kabisa na huyu dada kuwa mwepesi sana kwa baba mkwe ila pia nimefurah sana kuona kwamba Mungu kamuepushia huyu kijana dhahama. ndio maisha yalivyo.
 
Last edited by a moderator:
The Boss,acha kufikiri kwa upofu.Unaweza kumuuliza baba yako huyu msichana umemtoa wapi?Hebu acha utani.Pia kipi unachoshangaa umri wa miaka 27 mchumba wako asijulikane home?Mh!!!!Unaweza ukawa unaishi New York City!

kama baba kamuuliza mwanae 'unasemaje'
baada ya kumtambulisha sion why mtoto ashindwe hata kumfuata baba yake later na kuongea
hata kama sio kumwaga ukweli
 
@Sweetlady kama kweli baba hajui kama binti yule alikuwa anatoka na mwanae basi hana kosa...labda binti kaficha ni jinsi gani alipata nafasi ya kufahamiana na Baba wa kijana. Inawezekana mwenye kosa ni binti labda alijilengesha kwa Baba au kosa lake ni kumtosa kijana baada ya kumpata dingi....Je, Baba akijua kwamba mwanae alikuwa anajinvinjari na huyo binti bado ataendelea na mipango yake?

Kijana hajamuambia baba mahusiano yake na nimemwambia atulie!
 
@Sweetlady kama kweli baba hajui kama binti yule alikuwa anatoka na mwanae basi hana kosa...labda binti kaficha ni jinsi gani alipata nafasi ya kufahamiana na Baba wa kijana. Inawezekana mwenye kosa ni binti labda alijilengesha kwa Baba au kosa lake ni kumtosa kijana baada ya kumpata dingi....Je, Baba akijua kwamba mwanae alikuwa anajinvinjari na huyo binti bado ataendelea na mipango yake?

Mleta mada hebu tusaidie hapo red.....mwambie kijana amwambie babake kuwa huyo binti alikuwa mchumba wake then urudi uje utuambie baba amelipokeaje.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom