Dada zetu mwatukwaza!~

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Kipimo mwatupimia,
Mwajua twapungukia,
Lakini mwasubiria
Kuona tutapatia;

Sifa mnatutajia,
Za yule mwatamania,
Kila tukiangalia,
Vijana tumefulia,

Twabaki twatamania,
Kama sungura wa hadithia,
Ya ndizi alizochukia,
Kwa kukosa kufikia,

Nguo tunazovalia,
Kamwe hatujapatia,
Haraka mwatuambia,
Ni vipi tungevalia,

Nywele tulivyochania,
Manukato mwachukia,
Viatu mwaangalia,
Na tai mwaivutia,

Kama kisu mwakatia,
Mitima mwaivunjia,
Na hata mkipatia,
Hasira twajisikia,

Tunda twalitamania,
Na penzi twarajia,
Donge limetushikia,
Kisu twakiruhusia,

Wachache wanapatia,
Kwa upole watwambia,
Bila ya kukejelia,
Na dharau kumwagia

Ya'raabi katujalia,
Shukuru twashukuria,
Bila nyinyi twaumia,
Kizani twajikutia,

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
[/QOUTE] Twabaki twatamania,
Kama sungura wa hadithia,
Ya ndizi alizochukia,
Kwa kukosa kufikia
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia
Njaa aliposikia , Sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda, porini kutemblea
Akayaona matunda ,mtini yameenea
Sungura akayapenda, mtini akasogea
Mtini akasogea, sungura nakuambia
 
[

Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia
Njaa aliposikia , Sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda, porini kutemblea
Akayaona matunda ,mtini yameenea
Sungura akayapenda, mtini akasogea
Mtini akasogea, sungura nakuambia[/QUOTE]

Mkulu long time kitambo,dah!!!! nimekumbuka mbali sana,enzi za suruali ya mchelemchele
 
sizitaki mbichi hizi sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
matunda akalilia sungura nakumbia


Kumbe bado tunakumbuka hehehe
 
MMK we hujui tu,Dunia ya sasa ni kukwazana.Wakaka wanawakwaza akina dada na akina dada wanawakwaza akina kaka.
 
sizitaki mbichi hizi sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
matunda akalilia sungura nakumbia


Kumbe bado tunakumbuka hehehe

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Mwisho wake akachoka, porini akakimbia,
Porini akakimbia, Sungura nakuambia!
 
jamani mbona mnakwenda auti ofu perimeta?, mambo ya sungura mjanja tena!, Lol.
twambieni jamani ZD,FL1,BHT, na wengineo, KWANINI MWATUKWAZA??
 
Ya'raabi katujalia,
Shukuru twashukuria,
Bila nyinyi twaumia,
Kizani twajikutia,


Duh!.....lol


 
[/QOUTE] Twabaki twatamania,
Kama sungura wa hadithia,
Ya ndizi alizochukia,
Kwa kukosa kufikia
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia
Njaa aliposikia , Sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda, porini kutemblea
Akayaona matunda ,mtini yameenea
Sungura akayapenda, mtini akasogea
Mtini akasogea, sungura nakuambia

hahaaaa PakaJImmy bana
 
jamani mbona mnakwenda auti ofu perimeta?, mambo ya sungura mjanja tena!, Lol.
twambieni jamani ZD,FL1,BHT, na wengineo, KWANINI MWATUKWAZA??
Hahahaaa,shemeji bana,tumeumbwa kwa ajili hiyo ya kuwakwaza.Si unakumbuka eva alimkwaza Adamu akampa tunda.Yani mama etu katurithisha tabia mbaya.
 
huyu mheshimiwa akiingia kwenye majukwaa mengine zaidi ya la siasa huwa ana mashairi tu. tunaomba na mashairi kwenye siasa pia mkuu
 
Mh hili shairi la leo kabambe. wadada nyie acheni kuwakwaza wakaka, vaeni nguo za heshima siyo mibano.
 
Kazi kwelikweli,leo babu kaingia kwa wapwa.Hivi Mwanajamiione katokomea wapi,siku nyingi kidogo.Nafikiri angeokoa jahazi maana na yeye kwa free style hajambo.
 
sizitaki mbichi hizi sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
matunda akalilia sungura nakumbia


Kumbe bado tunakumbuka hehehe

tusikumbuke mchezo? tuliimba lile shairi kila siku kwa wiki nzima
 
Maji yalozidi kina
Mbona mwayapenda sana
Bure mnakondeana
Kwa kutafuta mapana

Wewe ni mwanakijiji
Vipi wataka ya mji
Achana na kina Mwaji
Watafutao ulaji

Chagua wa kijijini
Asiyejua vimini
Achana na wa mjini
Usije fia majini
 
jamani mzee mwanakijiji wenzako mashairi hatuyajui lakini inaonyesha kuwa unalalamika mpenzi wako akikuelekeza yale ambayo ye hataki kama manukato, mavazi yako kwahiyo mkuu jirekebishe hayo ndo mapenzi bwana
 
Kwanini ujiumize?
Na kilio ujilize,
Mbona sisi tuko bize,
Wao ndo wanotabika

Tatizo umemwonesha,
Kwamba yeye ametosha,
Asemalo hutabisha,
kaka umejitakia

Mavazi akupangia,
Shati la pundamilia,
Na tai kama mkia,
Nakusihi umwepuke

Ndugu wapigishwa kwata,
Tena wapelekwa puta,
Hadi sasa unajuta,
Penzi limekuchuchia

We ndio mtafutaji,
unayeleta ulaji,
Mambo ya kiushikaji,
Ndiyo yanayokwangusha

Wadada tunao wengi,
Tena humu kenye bendi,
Unavyolia sipendi,
Kwanini wajiumiza?

Tafuta anolandana,
Alokuwa muungwana,
Akupe bila hiyana,
Penzi mkalidumishe

Mapenzi matamu sana,
Vya sirini kupeana
Tena bila ya hiyana
Kwa mahaba yalonona.

Kaditamati wa tama,
Nimefika kwenye boma,
Mzigo nautuama,
Kwaheri yakuonana.






 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom