Dada zetu Mna Mambo!

Dada zetu twawapenda, Bila ninyi tunakonda,
Kila siku zikienda, twajuta tunayotenda,
Msiache kutupenda, twapenda mnavyopenda,
Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Vidole vinaniuma, kalamu naiachia,
Nililotaka kusema, hilo nimewaambia,
Hivyo kutama natama, miye nawabarikia,
Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Most wafikiri vita vya chini chini vya akina dada/mama vimeanza karibuni
it has always been so... ila sasa wamejiachia.... For zamani ilikua kwenye magoti
ya mama, majikoni, Vyumbani, majukaani.... tofauti tu it is in the open now...
thou kidogo nimeelezea out to context....

Tunashukuru utambuzi wako wa uwepo wetu.... Beautifully written.
 
KAKA zetu Mna Mambo!

Msema kweli hakika, huyo mpenzi wa Mungu,
Kalamu nimeishika, nilisemalo ni langu
Beti ninaziandika, mzisome kakazangu,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.

kaka zetu mwatutega, twategwa tukategeka,
Mikogo mnayomwaga, twajikwaa twaanguka,
Na nyuma mkigeuka, toba! Tunanusurika,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.

mkifungua mapochi, wagumu wanayeyuka,
dada kila akiona pochi, kiwewe kinamshika,
tena mbele yake pochi, miguu yatetemeka,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.

Hasa mnaponong'ona, mwatupandisha presha,
Tunabakia kuguna, na milio ya kutisha,
Na tukiwa tumenuna, kwq pochi mwatuchekesha,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Nguo zinavyowapendeza, mwatusukuma dhambini,
na mjuavyo kuchombeza, mwatuingiza majaribuni,
kaka zetu mwatuweza, mwajua mwafanya nini,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Mara mnatukonyeza, mwapiga jicho kwa vile,
Twabaki twajiuliza, ana nini kaka yule,
Tukija twajibamiza, twalishwa chenga za Pele,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Mwajua kutuchombeza, kama samaki na chambo,
Magoma tukiyacheza, kama ndege na ulimbo,
Wenzenu mwatumaliza, mkisimamisha ‘mtambo',
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Mwajua kututuliza, mwauma na kupuliza,
Tena mnatuliwaza, twalala twapitiliza,
Kweli mnatushangaza, twabaki twajiuliza
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Mengi tunawakosea, majumbani twawakimbiza,
Maneno twawatolea, na mengine ya kubeza,
Mengi tunawatendea, twatenda bila kuwaza,
kaka zetu mna mambo mambo yenye vijimambo!!

Mwisho mnakimbilia, kwa mwingine kutulia,
Mapenzi kutafutia, mahawara mwajipatia,
Mioyo ikitulia, kimoja mnazamia,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Wengine mwavumilia, na miaka inapita,
Watoto kutukuzia, kumbe mioyo yajuta,
Na siku ikifikia, na ninyi mbele mwapeta,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

Ukweli nawaambia, bila nyinyi tumekwisha!
Tunakaa twajutia, na mawazo tunakesha,
kwa mawazo twaumia, machungu yanatuzonga,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

kaka zetu twawapenda, Bila ninyi tunakonda,
Kila siku zikienda, twajuta tunayotenda,
Msiache kutupenda, twapenda mnavyopenda,
kaka zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo
!
 
Mwanakijiji vijimambo vyako vinatisha! Aisee yale mashairi yetu ya enzi zile yaliyoibwa na kuchapishwa unayo? Nataka kurudi kilingeni.
 
Mwanakijiji vijimambo vyako vinatisha! Aisee yale mashairi yetu ya enzi zile yaliyoibwa na kuchapishwa unayo? Nataka kurudi kilingeni.

aisee unakumbushia lile la "heri yetu wapagani"? nadhani ninayo.. I still have almost the whole collection ya 2001-2006.
 
aisee unakumbushia lile la "heri yetu wapagani"? nadhani ninayo.. I still have almost the whole collection ya 2001-2006.

sasa wale wezi wa mashairi yetu waliishia wapi? kainzi kalifanikiwa kuwashughulikia? naomba unitumie huo mkusanyiko. zangu sina hata moja.
 
Dah...naimiss ile bulogu ya Mapambazuko. Kuna mashairi mengi sana mle ambayo mistari yake ilinisadia sana...teh teh teh

That was like in '04 or '05
 
Nimekubali hasa point ya wanaume wanaotoswa na wake zao uishia kuwa walevi; japo si wote ila most of you guys maisha yanakwenda ndivyo sivyo mamsap akisema it's over.
 
Hiyana naweka nyuma,kutoa yangu maoni
Mwanakijiji we noma,unakipaji jamani
Sijaona wa kupima,hata uko marekani
Akujalize mwenyezi,utunze na utunzike

Madada zetu wa leo,burudani kila kona
Uzuri wa macho yao,wavutia kuwaona
Mimi kijana wa leo
Nawapamba wasichana,
Hongereni dada zetu,mwatushika saawia

Nanena nina hisia,si lazima wa amerika
Bongo wameijalia,kila mahali hakika
Mwanakijiji kasemea,nami mkono namuweka
Hongereni dada zetu,mwatushika saawia

Nina mengi ya kusema,leo natilia nanga
Kafunguka amesema,mwanakijiji kajipanga
Hongera nami nampa,asiwepo wa kupinga
Akujalize mwenyezi, utunze na utunzike
 
Mwanakijiji umenikumbusha mbali sana,enzi za!!!
Karudi baba mmoja,toka safari ya mbali,kavimba yote mapaja,na kutetemeka mwili,watoto wake wakaja,ili kumtaka hali.... Upo juu kama CHADEMA.
 
Back
Top Bottom