Dada zanguni jamani!nipeni ukweli!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Nitabaka gani linaongoza kwakuvunja ndoa?Maana naona mtu kaolewa mwezi kaachika je msababishaji ni nani??Mume mke??
Au siku hizi ni fashion kuingiza na kutoa??
 
KakaKiza uchokozi huooooooooooo! Ingawa mie sio mwanamke najitosa mzimamzima na kimbelembele juu kujibu. Kwa haka kamfume dume unategemea jibu gani toka kwa jamii. Eti huwa tunasema wanawake wngi huwa wanaficha 'their true colour not until they get married', teteteeeeeeeeee, wanaume wengi huwa tunapenda wadada wabadilike to our advantage not otherwise. Ni mtazamo tu jamani msijenge chuki, mweeeeeeee!
 
Nitabaka gani linaongoza kwakuvunja ndoa?Maana naona mtu kaolewa mwezi kaachika je msababishaji ni nani??Mume mke??
Au siku hizi ni fashion kuingiza na kutoa??

Kumbe wameulizwa akinadada .....dah! ngoja nijisepeshe.
 
Nitabaka gani linaongoza kwakuvunja ndoa?Maana naona mtu kaolewa mwezi kaaa je msababishaji ni nani??Mume mke??
Au siku hizi ni fashion kuingiza na kutoa??

Mi kwa upande wangu niseme, men wanaongoza for 80 percent, women wanafuatia kwa just 20 percent, wanaume wengi ndio wanaoharibu familia, wana kero za kipumbavu na maudhi kedekede but mi naamini silaha moja kubwa kwa mwanamke kuishi vizuri kwenye uhusiano ni kujitahidi kujiongezea kipato cha kutosha, kuwa na kipato kizuri na pia kumheshimu Mume wako, because wanaume wengi wanapenda kuwanyanyasa wanawake kwa pesa zao, ukiwa mfano na nyumba yako au nyumba zako mwanaume anayetaka kukunyanyasa sababu ya mali anakuogopa, wanaume wanapenda anapokuacha uteseke but akijua utaendelea kupendeza kwa sana, atasita kufanya hivyo na kwa upande mwingine pia wanawake tupendane kama wanaume, sio kukaa kufurahia na kuchekelea matatizo ya mwanamke mwenzio, tunawaumiza wenzetu, watoto wao na kuharibu familia zao kwa ujumla, it's not good waheshimiwa.
 
Nitabaka gani linaongoza kwakuvunja ndoa?Maana naona mtu kaolewa mwezi kaachika je msababishaji ni nani??Mume mke??
Au siku hizi ni fashion kuingiza na kutoa??

Hii ya kuoa na kuachika ingelikuwa halali kwa Mungu mi ningeoa wanawake elfu kidogo
 
hivi neno tabaka na neno jinsia yana maana moja??????????

tabaka mimi naelewa ni mfano 1.rich class 2.middle class
3.low class
 
hivi neno tabaka na neno jinsia yana maana moja??????????

tabaka mimi naelewa ni mfano 1.rich class 2.middle class
3.low class

hata kwenye mapenzi? Maana kuna stori za wake za matajiri kubanjuka na wachunga ng'ombe. Fafanua mkuu
 
asilimia kubwa n wanaume japokuwa ndoa ikivunjika mwanaoke ndo ananyooshewa kdole!
 
wanaume ndo visababishi hasa wakishapata vijisent kidogo tu hupumbazwa na ya ulimwengu na kujiona yeye kidume,kuendeleza mfumo dume na kusahau kuishi kwa akili,upendo na hekima na wake zao.pia wanaume weng wakioa wanasahau majukumu yao kama mume.
 
Nitabaka gani linaongoza kwakuvunja ndoa?
Hapa sijakuelewa unaposema tabaka unamaanisha nini.Nieleweshe!

Maana naona mtu kaolewa mwezi kaachika je msababishaji ni nani??Mume mke??
Mume na Mke hawa wote ni wasababishaji wa kuvunjika kwa ndoa yao, kwa kushindwa kuitambua misingi imara ya ndoa, kuikubali na kuamua kwa umoja wao kuiishi kwa lengo la kuijenga ili hatimaye iweze kusimamisha jengo imara ambalo litageuka kuwa nyumba(familia) yenye furaha na amani siku zote za maisha yao hadi kifo kitakapowatenganisha hao wanandoa husika.

Kumbuka ndoa si lelemama, kamwe usiingie ktk ndoa kwa majaribio eti kwasababu; umri unaruhusu au pesa zinaruhusu au rafikiyangu kaolewa/ kaoa au tamaa zinginezo za mwili. Ukifanya hivi hakika nakwambia tegemea matokeo kama haya ya kuvunjika baada ya mda mfupi pia inaweza kukufanyia ki2 kibaya ambacho kitakupelekea majuto ya milele na kutafuta pa kukimbilia pasipokimbilika.

Au siku hizi ni fashion kuingiza na kutoa?
Fafanua hapa pia unaposema kuingiza na kutoa una maana ipi?
 
Ni tabaka gani unazunzumzia mkuu, manake neno tabaka ni pana mno katika mapenzi, kwani kuna umri,kiuchumi,kielimu,kidini n.k, hivyo be specific hapo kaka, manake hadi kufikia hatua ya kuvunjika kuna mabo mengi yakichangiwa na sababu mbalimbali.
 
Nitabaka gani linaongoza kwakuvunja ndoa?Maana naona mtu kaolewa mwezi kaachika je msababishaji ni nani??Mume mke??
Au siku hizi ni fashion kuingiza na kutoa??


Haya mambo hayana formula bwana inaweza mwanaume akawa kisababishi au mwanamke. lakini kikubwa cku hizi watu wanaoana kama fasheni hakuna kujuana kwa undani misingi ya kupata mchumba imekuwa mibovu watu wanazingatia sura na umbo na upande mwingine waangalia chapaa.
 
Back
Top Bottom