Dada zangu naomba kukuulizeni!

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Hivyo kati ya mapenzi mliyopewa na wazee na mapenzi ya uwili (ndowa au urafiki wa kimwili) ni penzi lipi unalithamini kuliko jengine. takuwa vizuri mkitaja na sababu.
 
Au unamaanisha hapo una mzazi na pale mume afu wote wanahitaji msaada wako ktk muda mmoja kwa hiyo mie nianze na yupi kumsaidia?
 
Mapenzi hayo yako tofauti kabisa na hayaingiliani. Penzi la wazazi ni la pekee na la mwenza kadhalika. Ukitaka kuyashindanisha unajitafutia matatizo. Moyo wako ni mkubwa mno, hawa wote wanaenea humo ikiwa ni pamoja na watoto mtakaojaaliwa, na itabaki na nafasi ya marafiki pia.
Mwenza haji kum-replace mzazi. Ana nafasi yake pekee.
 
penzi la mzazi lina nafasi yake na kamwe hawa ndio watu pekee ambao hawawez kukubadlisha ama kukukana wewe ama kuachana na wewe. ndio watu ambao nafasi yao haina masimulizi wala vizio vya kupimia na haifanani na ya mwenza hata siku moja.

mwenza huyu ni yule ambaye umemchagua wewe ama tuseme ni created love yako, hii na yenyewe inapitia mlango tofauti ambao wazazi hawapitai and Mungu ni wa ajabu huwez ama hawawez kupiitia mlango mmoja na wote hubaki moyoni na nafasi ikawa wazi kwa mapenzi mengine kama ya watoto na marafiki.

kumbuka upenzi wako kwa wazazi ulikuwa ni genuine love ambayo lazima wangekupa na wewe uwape na haisukumwi na hisia za kingono but intimate love huwa ni kwa mwenza na husukumwa kingono. these two are incomparable.
 
Mbona hujauliza wakaka/wanaumeeee...............!!
Au wenyewe hawajali mapenzi ya wazazi.......?:A S embarassed:
 
Mbona hujauliza wakaka/wanaumeeee...............!!
Au wenyewe hawajali mapenzi ya wazazi.......?:A S embarassed:

Wanaume na mama zetu upendo wetu ni wa asili haitakiwi hata kuulizwa.. Ni ngumu sana mwanaume kumpenda mwanamke kuliko mama yake..
 
cjamwelewa mleta uzi
Binaadamu huwa na vitu alivyovithamini na huenda vitu hivyo vikawa kwenye kundi moja, lakini lazima kutakuwa nadaraja kati ya vitu hivyo.
Naam, kupendwa ni kuzuri lakini mapenzi yepi unayaweka katika daraja la juu na yepi yanafuata? 1. Mapenzi ya wazee wako kwako na 2. mapenzi ya mwenza wako yaani mume au boyfriend?
 
Hili swali kama hujalimalizia vile
Nahisiniko wazi! Mapenzi uliyopewa na wazazi na uliyyopewa na unaeshirikiana nae kimwili, yepi unayaona yana maana zaidi kwako? Kumbuka kuwa nakubali kuwa yote yana thamani kwako lakini kama kuyapata ni moja tu utachagua mapenzi ya wazazi au mapenzi ya mshiriki wako?
 
uliza vizuri basi uumebania maneno au?

Sijabania kitu hapo! Ulipendwa na wazazi wako tangu tumboni hadi sasa na ukateuwa mwenzako wa kukupa raha za matamanio yako. Ukitafakari yepi unaona yana tija zaidi kwako kuliko yale mengine?
 
Au unamaanisha hapo una mzazi na pale mume afu wote wanahitaji msaada wako ktk muda mmoja kwa hiyo mie nianze na yupi kumsaidia?
La si hivyo!Tuchukulie hivi;Unathamini jitihada za mtu juu yako na mapenzi ni zawadi kwako. Sasa kati ya mume na wazazi wako wepi unahisi wana mchango mkubwa wa kukupenda kati ya wazee na mumeo?
 
Mapenzi hayo yako tofauti kabisa na hayaingiliani. Penzi la wazazi ni la pekee na la mwenza kadhalika. Ukitaka kuyashindanisha unajitafutia matatizo. Moyo wako ni mkubwa mno, hawa wote wanaenea humo ikiwa ni pamoja na watoto mtakaojaaliwa, na itabaki na nafasi ya marafiki pia.
Mwenza haji kum-replace mzazi. Ana nafasi yake pekee.

Ninachojaribu kujuwa ni kuwa lipi unalithamini zaidi? Maana ya zaidi ni kuwa hicho kitu kipo mbele ya mwenziwe. Sijui lakini nahisi kuwa lile la wazee lina thamani ya pekee.
 
penzi la mzazi lina nafasi yake na kamwe hawa ndio watu pekee ambao hawawez kukubadlisha ama kukukana wewe ama kuachana na wewe. ndio watu ambao nafasi yao haina masimulizi wala vizio vya kupimia na haifanani na ya mwenza hata siku moja.

mwenza huyu ni yule ambaye umemchagua wewe ama tuseme ni created love yako, hii na yenyewe inapitia mlango tofauti ambao wazazi hawapitai and Mungu ni wa ajabu huwez ama hawawez kupiitia mlango mmoja na wote hubaki moyoni na nafasi ikawa wazi kwa mapenzi mengine kama ya watoto na marafiki.

kumbuka upenzi wako kwa wazazi ulikuwa ni genuine love ambayo lazima wangekupa na wewe uwape na haisukumwi na hisia za kingono but intimate love huwa ni kwa mwenza na husukumwa kingono. these two are incomparable.

Naaam! Namkumbuka Babu yangu aliyeniambia mke kaja ngomani, ikivunjika.............
 
Rudia swali tafadhali

Unataka kutowa zawadi kwa mtu aliyekupa mapenzi na zawadi hiyo ni moja tu.
1.Kuna wazee waliokupenda na kukuengaenga na kukufanya hivyo ulivyp sasa.
2.Kuna guy lenye kukupatpat na kukupa vineno vizuri, kucheza na wewe kwenye sita kwa sita na kushirikiana nawe kutengeneza kiumbe ambacho utakipenda kuliko kitu chengine duniani(mtoto).
Sasa zawadi yako utampa nani na kwanini?
 
Back
Top Bottom