Dada yangu anaumwa ugonjwa wa ajabu!

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Habari zenu wanaJF hasa upande huu wa JF Daktari?

Dada yangu mwenye umri wa miaka 36 anaumwa ugonjwa ambao unamdhoofisha kila kukicha na ugonjwa huo
una dalili kuu ya kutoa sauti kubwa inayojitokeza kama mtu aliyeshiba sana na hewa inatoka kooni ila kwa sauti kubwa
ambayo inamfanya ata watu wamkimbie.

Sauti hiyo inatoka mithili ya mtu aliyekunywa soda yenye gesi nyingi (burp kwa lugha ya kiingereza). Dada yangu anazidi kukonda na anapokuwa
na hasira au kuchoka hali ya kuburp huongezeka sana hadi watu wanamkimbia.

Naomba mnisaidie kwa mwenye uelewa wa ugonjwa huu tafadhari!
 
Kuna roho nyingine chafu ndani yake amini, mi nadhani ajitahidi kwenda kwenye maombi, haijalishi imani yake kwani siku zote KRISTO NDIYE MSHINDI.
 
ameshajaribu kwenda hospitali....?

Hajaenda. Nilipatabkujua hali hiyo jana nilipoongea nae kwenye simu na nimemshauri afanye hivyo mara moja. Anasema amekuwa akienda kwenye maombi na hapati nafuu!
 
Kuna roho nyingine chafu ndani yake amini, mi nadhani ajitahidi kwenda kwenye maombi, haijalishi imani yake kwani siku zote KRISTO NDIYE MSHINDI.[/QUOTE

Naye anaamini hivyo na amekuwa akienda Karismatic RC kufanyiwa maombi kwa kuwa yeye ni RC. Pia anasema ni mizimu ya ukoo imeahamia kwake.
 
ana muda gani toka tatizo lianze?? je mmeshaenda hospital na kuchukua vipimo mbali mbali??
 
Duh, ndio nauskikia leo Mpwa, pole sana sana, ngoja tusikie wengine watufundishe na sie pia
 
Hajaenda. Nilipatabkujua hali hiyo jana nilipoongea nae kwenye simu na nimemshauri afanye hivyo mara moja. Anasema amekuwa akienda kwenye maombi na hapati nafuu!
mwambie aende hospitalini ..asiende kwenye waganga (wachawi)
 
hapo ni maombi tu, cse kwa me upande wangu cjawahi kuona ugojwa ka huo,na kwa maelezo hayo c zan ka kuna haja ya hospital,akisha amin tu ka atapona anakua kamshinda shetan kwa 50%,so nothin' but players.
 
Kama vp mlete Arusha kwenye maombi hapo UKUMBI WA SAFINA RADIO ulioko mtaa wa Mbauda na bila shaka majibu utapata Kamanda wangu. Mpe pole nyingi toka kwa WanaJF!
 
wakati afuatilia hosp. atumie tiba hii hapa, kuna jirani yangu alikuwa na hali kama ya dada yako nilijaribu kumpa hii dawa sasa ni mzima na anafanya kazi zake. ila asiache kwenda hosp. pia.
Vidonda vya tumbo
Jitahidi kukimbia vyakula vyenye tindikali?? (Acid) kama Limau, ndimu, binzari, maharage, pombe kali au pombe kwa ujumla nk ...
1. Dawa ya vidonda vya tumbo tumia Dawa ya Hii ya Kienyeji - Ukiamka Asubuhi kabla ya kula kitu kojowa mkojo wako mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja uwe anakunywa mkojo wako kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha uende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie jaribu kutumia hiyo Dawa itakusaidia Sana.
 
Dah, mpe pole. Kweli ni ugonjwa wa ajabu nami ndo kwanza nausikia! Binadamu hujafa hujaumbika, hivyo ni vizuri kumuomba sana mwenyezi ili atunusuru na haya! Atapona kwa uwezo wa Mungu
 
Habari zenu wanaJF hasa upande huu wa JF Daktari?

Dada yangu mwenye umri wa miaka 36 anaumwa ugonjwa ambao unamdhoofisha kila kukicha na ugonjwa huo
una dalili kuu ya kutoa sauti kubwa inayojitokeza kama mtu aliyeshiba sana na hewa inatoka kooni ila kwa sauti kubwa
ambayo inamfanya ata watu wamkimbie.

Sauti hiyo inatoka mithili ya mtu aliyekunywa soda yenye gesi nyingi (burp kwa lugha ya kiingereza). Dada yangu anazidi kukonda na anapokuwa
na hasira au kuchoka hali ya kuburp huongezeka sana hadi watu wanamkimbia.

Naomba mnisaidie kwa mwenye uelewa wa ugonjwa huu tafadhari!
Aende Hospital kwa matibabu. Asisahau kupima damu kubwa, Kale kaugonjwa kana sura nyingi sana!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom