Dada yangu anatishia kujiua, nishaurini tafadhari

Kuna roho mbaya inamtafuta, roho ya mauti. Sasa, dawa ni maombi tu. Hakuna namna. Alipoona fedha yake kaimaliza bila hata chochote alichoifanyia ndio mwanzo wa kujikataa. Anadhani kumuua mwanaye ndio njia pekee ya kumuepusha na dhiki mwanaye. Hayo ni mawazo mabaya ya kishetwani.
Ukijidanganya na kumleta akae kwako ndio kumharibu kabisa. Mpeleke kwanza kwa maombi akiisha tulia kidogo ndo umlete akae kwako huku ukihakikisha maombi hakosi. Akiisha funguka, mfundishe namna ya kujiendeleza. Umesema anavyo viwanja 2 uza kimoja ujaribu kujenga nyumba ndogo tu ya 2 rooms. Ahamie ajisikie kuwa ana kwake. Pole ploe ataanza kujiona wa maana. Hivi sasa amejidharau
 
Wew uko wap?? Upo mbali nae?? Kama ndivo Fanya hima uende mahala alipo kwa usalama wa mtoto,,afu yy angalia jins ya kurud nae mahali unapoish kwa usalama wake!! Ningejua alipo ningekutunzia mtoto kwan yy ana kosa had ahukumiwe kifo??? Fanya hima dada uhai hauuzwi Dukan,,,wambie hao majiran ikiwezekana wariport police
 
Asante kwa ushauri ndugu, wazo lako ni jema sana
 
Wew uko wap?? Upo mbali nae?? Kama ndivo Fanya hima uende mahala alipo kwa usalama wa mtoto,,afu yy angalia jins ya kurud nae mahali unapoish kwa usalama wake!! Ningejua alipo ningekutunzia mtoto kwan yy ana kosa had ahukumiwe kifo??? Fanya hima dada uhai hauuzwi Dukan,,,wambie hao majiran ikiwezekana wariport police
Asante sana mie nipo chalinze vijijin na yeye yupo dar es salaam. J3 nitaenda huko
 
Wewe Fanya hivi kamnunilie hiyo sumu kisha mpe mwambie tutakuja kufuata maiti kuzika ataacha vituko vyake huyo anafanya hivo anajua kuna mtu anaemjali
Akinywa kweli? Uso wangu nitauweka wapi? Mtoto wa watu ndo nitaitwa majina yote mabaya hapa duniani
 
Ana umri gan?
Ameolewa?
Anaishi na Nan zaid ya mtoto?
Anafanya kaz gan serikalini?
Zaidi ya mkopo unahisi ana tatzo gan jingine?
La mwisho msaidie kumpa hope ila kujiua hawez.... Mm ni mnyalukolo nina experience.
Ana miaka 40, hajaolewa. Anaishi yy na mwanae. Ni mwalimu katika shule fulani hapo dar es salaam. Ni kweli nahisi ana tatizo zaidi ya haya yanayomsumbua japo siamini kiviileee. Ndikusa tulongane kuinbox.
 
Wazazi wako wako wapi? hii ni issue ya mama zaidi ya wote . ..huyo mtoto baba yake yuko wapi? Hilo ni janga la family . ..wewe ni kijana shupavu sana na unaupendo mkubwa lakini sidhani kama utamuweza wewe mwenyewe maana huyo dada amechanganyikiwa . ..jaribu kupata professional help au makanisani . ..pole sana
 
Ndugu usiombe yaani hapa najiona nazeeka kwa mawazo
Pole sana, uzeni hivyo viwanja (japo kwa awamu hii lazima muuze kwa bei ya hasara) pia jaribu kuwashirikisha ndugu zako na baba wa huyo mtoto muone ni jinsi gani mnaweza kulimaliza hilo deni
 
Si anakatwa huo mkopo through salary? Sasa unahaha nini mtu kakopa kaenda kuhonga? Mkopo 7m/= plus ribs 3m/= plus za mtaani.
 
Kinywa kinaumba. Ukweli atajiua na mtoto. Kwanza kamchukueni mtoto haraka sana. Pili mpelekeni kwenye Maombi. Tatu mpelekeni katika vyombo vya sheria kwa kuwa anatishia uhai wake binafsi na mtoto
 
Sioni kwann awe na stress kwasababu zifuatazo

1.kama amekopa kwenye mabenk kwa dhamana ya kazi yake serikalini asiwe na hofu maana mabenk hayamharasi MTU wanakata chao juu kwa juu ila ingekuwa MTU binafsi angemsumbua sana.

2.Waite ndugu muone jinsi ya kumsaidia ndugu yenu hususan kumlipia hayo madeni ya riba.

3.mtafutieni nyumba mumlipie kodi walau ya miezi sita na iwe ni mbali na huo mtaa anaokaa sasa aliozinguliwa na mwenye nyumba.

4.asithubutu kuacha kazi na kwa mwenendo huo wa kulewa chakari anaweza kupoteza kazi angalieni hilo lisitokee maana stress zitazidi Mara alfu moja na hatimaye ni kifo au ugonjwa wa akili.

4.msaidieni aweze kubajeti hela kidogo anayoipata baada ya deductions za mikopo

5. Mtembeleeni kwa kumpa faraja onyesheni mnamjali

6.mpendeni mtoto wake sana hii itamfariji na kumuongezea matumaini

Juu ya yote ni ibada kanisani au msikitini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom