Dada wa Tundu Lissu kuchaguliwa viti maalum hii CHADEMA ni ya familia?

Status
Not open for further replies.
Jamani hao waliochaguliwa ni wapambanaji. Sio kwamba wameokotwa nyumbani, Sofia Kawawa alikuwa mpambanaji na mumewe na wote walikuwa kwenye uongozi. Sofia alikua Mwkt wa UWT wakati mumewe akiwa Wziri mkuu, Katibu mkuu, waziri na katika nyadhifa mbali mbali. Na watu walijua Sofia alikua anapata uongozi kutokana na kujitoa kwake na sio kwa sababu ya mumewe. Mbona hamuwasemi kina Mapachu?

Hawa wa Chadema in founders na wamejitolea kijasiri wakati wengi wakiogopa kuonekana wanaipinga CCM wao walijitoa mhanga kwa hiyo huwezi kuwanyima haki yao kwa kuogopa mtaonekana kuna ukabila. Kama unataka jiunge hamasisha watu wa eneo lako halafu uone kama kuna atakaekuchakachua.

Au unataka dada yako akapewe viti maalumu wakati hata kadi ya chama hana? Waulize CUF kama wana wabunge wangapi wa viti maalumu kutoka Tanzania bara ambako mgombea uraisi wao kapata kura laki sita plus ambazo niu nyingi kuliko wapiga kura wote wa Zanzibar.
 
The Dreamer
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-online.png

JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

BASIASI
user-online.png

Senior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Respect acha kuandika ushabiki usio na maana k??
 
kwako mchungaji masanilo;

je ungelipenda kutomchagua mtu eti kwa sababu ni ndugu wa fulani?? Uoni kama huo ni ubaguzi mwingine?? Cha msingi hapa kama walivyosema wengi uwezi kujua mchango wa wahusika ktk chama kwahiyo kabla ya kuanza kuwashambulia watu angalia record zao halafu ndio u make judgement.
 
Kuna siku nilisema na sitoacha kusema ipo siku wenye macho watatambua nini maana ya chadema ona hizi sample ndogo tu

PHILEMON NDESAMBURO-MBUNGE MWANAE LUCY UWENYA MBUNGE,KUNA MKWEWE MBUNGE

HAYA ALIEKOSA URAIS DK SILAA,....MKEWE ROSE KAMILI MBUNGE

TUNDU LISSU ....MBUNGE ,DADA YAKE NAE KACHAGULIWA KWENYE VIT MAALUM MBUNGE....

HAWA NI BAADHI TUNAOWAFAHAMU WALE WA FREEMAN MBOWE SIJUI VIPI

ANYWAY TUWE MACHO NA HIVI VYAMA JAMANI TUNAPENDA MABADILIKO LAKIANI ISITOKEE IKAWA CHAMA CHA FAMILIA NAHISI MAALIMU SEIF ANGEKUWA AMEJAZA NDUGU ZAKE WENGI SANA LEO HII CUF..MUNGU AMUWEZESHE BABA YULE KAVUMILIA MPAKA LAST ANAKULA BATA NA SECURITY KALI

CHADEMA TUBADILIKE

hawa jamaa wametumia rasilimali zako kukijenga chama, vigezo ni wale waliopambana kukisaidia chama mfanao chiku abwao pale Iringa, sioni tatizo kwa mr slaa kwania amepigania jibo kazurumiwa, dada yake tundu lisu kwa mara ya kwanza tumepata mbuge Singida huoni ni mafanikio ?
 
Mimi hata siwashangai chadema kwa namna yoyote ile, ukiangalia hao ndugu zao ndio walitoil kuwapa suport wakati wa shida, wao ndo waliokua wanatoa tafu kifikra na kiushauri pia, so wao ndo wakwanza.

ninachoshangaaa ni nyie wana JF kushindwa kuwashangaa ccm ambao badala ya kuwaweka watu wenye cv zao(ambao wapo) wanaenda kuwapa vimada wao, wapo wengi sana humo ndani...sasa kuna wanawake wangapi ambao wapo kwenye system(ccm) toka long time lakini hawajawekwa badala yake wamewekwa vimada??? chadema ndo kinakua, na ukiangalia pande zote zile hao waliochaguliwa ndio waliokua vinara wa sehemu ambazo chadema inashikilia.
 
kama watu wanaogopa kujiunga na chadema au kutoa michango yao, mbona sebodo ambae ni mhindi kaisaidia chadema mamilioni ya pesa na mbona ktk mikutano yake chadema ilikuwa inahudhuriwa na watu wengi? Yaani wakati wa uchaguzi chadema ni peoples power!! Lakini wakati wa kugawana madaraka mnadai watu hawaiungi mkono upinzani ila familia na ndugu za viongozi na hapo kuhalalisha mgawo wa madaraka hii vipi lakini!!!!!!

Usishabikie tuu kwamba Chadema wamependelea. Tuambie nani alikuwa na sifa ya kupewa hivyo viti maalumu na akanyimwa kikapewa mke wa Slaa au ndugu wa kiongozi. Mama salma tumemsikia juzi baada ya mumewe kuwa raisi, hakuwahi kuwa mwana siasa. Rizi wani kajipendekeza na hata kujionyesha ana wadhifa wa kutoa maamuzi kuliko wahusika walioko kwenye potfolio.

Tofauti ya Chadema na ccm ni kwamba viongozi wa chadema wenye undugu kila mmoja kapata uongozi kutokana na uwezo na mchango wake kwenye chama, na sio kwa sababu ni ndugu wa kiongo. CCM viongozi wanabeba ndugu zao na kulazimisha kuwaingiza kwenye system bila kujali mchango na uzoefu kwenye chama. Kwa hio msilinganishe bila kupambanua.
 
Tusi-entertain hizi hoja za kipuuzi. Uteuzi wa viti maalum unaangalia zaidi sifa ya mtu, bila kujali anatoka kwenye familia ipi. Ni tofauti na CCM ambako umejaa uswahiba kila mahali. Angalia wabunge wa viti maalum.; wengine ni mahawara wa wakubwa wa CCM. Hii ni aibu! Huyo Christina Lissu ni kipanga sana, kama alivyo kaka yake TUNDU LISSU. Anastahili kabisa kuwemo kwenye viti maalum Chadema> Huwezi kumlinganisha Christina Lissu na kilaza kama VICKY KAMATTA ambaye mpaka sasa najiuliza atazungumza nini Bungeni kwani kichwani hamna kitu kabisa. Namfahamu vizuri sana.
 
Msiwalaumu sana, kwanza watu wenyewe hawa ni wale wachangiaji wa kubip na kuanzisha tu-thread ambako hakina kichwa wala miguu, kama wanavyofanya hawa
 
Kuna siku nilisema na sitoacha kusema ipo siku wenye macho watatambua nini maana ya chadema ona hizi sample ndogo tu

PHILEMON NDESAMBURO-MBUNGE MWANAE LUCY UWENYA MBUNGE,KUNA MKWEWE MBUNGE

HAYA ALIEKOSA URAIS DK SILAA,....MKEWE ROSE KAMILI MBUNGE

TUNDU LISSU ....MBUNGE ,DADA YAKE NAE KACHAGULIWA KWENYE VIT MAALUM MBUNGE....

HAWA NI BAADHI TUNAOWAFAHAMU WALE WA FREEMAN MBOWE SIJUI VIPI

ANYWAY TUWE MACHO NA HIVI VYAMA JAMANI TUNAPENDA MABADILIKO LAKIANI ISITOKEE IKAWA CHAMA CHA FAMILIA NAHISI MAALIMU SEIF ANGEKUWA AMEJAZA NDUGU ZAKE WENGI SANA LEO HII CUF..MUNGU AMUWEZESHE BABA YULE KAVUMILIA MPAKA LAST ANAKULA BATA NA SECURITY KALI

CHADEMA TUBADILIKE

mkiwa mnaleta maada mue mnaleta maada za maana tujadili sasa mnaleta mada gani hizi.!!!??
 
siongei na wambeya m na wewe nani mbeya unajua maana ya mbeya muulize mzazi wako akujulishe
maanayake tatizo la chadema amtaki ukweli ujinga ndio unaomaliza baddhi ya watu ona mpuuzi kama huyu ananyuka kupiga kelele nenda kaangalie kwenye majina uje uone m nawewe nani mbeya wa kina

nimegundua huyu jamaa anatoka bukoba nahisi ni yule mbunge ambaye alipoteza kiti chake kwa kula za maoni jimbo la nkenge ni d kamara angalia hizo blue highlited words:bowl:
 
BASIASI,

unaongea nini bwana, ccm kila mbunge yuko na mkewe na sasa mpaka wototo zao wanawaweka kwemye siasa. sasa wewe unataka kutuambia nini???

ccm chama cha nani sasa
chengeeeee.... au msekwa???
 
Mimi hata siwashangai chadema kwa namna yoyote ile, ukiangalia hao ndugu zao ndio walitoil kuwapa suport wakati wa shida, wao ndo waliokua wanatoa tafu kifikra na kiushauri pia, so wao ndo wakwanza.

ninachoshangaaa ni nyie wana JF kushindwa kuwashangaa ccm ambao badala ya kuwaweka watu wenye cv zao(ambao wapo) wanaenda kuwapa vimada wao, wapo wengi sana humo ndani...sasa kuna wanawake wangapi ambao wapo kwenye system(ccm) toka long time lakini hawajawekwa badala yake wamewekwa vimada??? chadema ndo kinakua, na ukiangalia pande zote zile hao waliochaguliwa ndio waliokua vinara wa sehemu ambazo chadema inashikilia.

I thought you were negative on anything done by CHADEMA, numekupa Thanks
 
Kuna siku nilisema na sitoacha kusema ipo siku wenye macho watatambua nini maana ya chadema ona hizi sample ndogo tu

PHILEMON NDESAMBURO-MBUNGE MWANAE LUCY UWENYA MBUNGE,KUNA MKWEWE MBUNGE

HAYA ALIEKOSA URAIS DK SILAA,....MKEWE ROSE KAMILI MBUNGE

TUNDU LISSU ....MBUNGE ,DADA YAKE NAE KACHAGULIWA KWENYE VIT MAALUM MBUNGE....

HAWA NI BAADHI TUNAOWAFAHAMU WALE WA FREEMAN MBOWE SIJUI VIPI

ANYWAY TUWE MACHO NA HIVI VYAMA JAMANI TUNAPENDA MABADILIKO LAKIANI ISITOKEE IKAWA CHAMA CHA FAMILIA NAHISI MAALIMU SEIF ANGEKUWA AMEJAZA NDUGU ZAKE WENGI SANA LEO HII CUF..MUNGU AMUWEZESHE BABA YULE KAVUMILIA MPAKA LAST ANAKULA BATA NA SECURITY KALI

CHADEMA TUBADILIKE

Haya mbona yalikuwepo tangu enzi za Mwalimu? Joseph Kizurira Nyerere, alikuwa waziri katika serikali ya kakake. Joseph Butiku alikuwa msaidizi maalumu ofisini ikulu kwa mjombake Nyerere na amepanda vyeo vikubwa tu humo. Bhoke Munanka alikuwa balozi na waziri katika nyakati tofauti. Col Dr Lawrence Mutazama Gama alikuwa shemeji wa Nyerere, kazi alizopewa katika serikali na chama cha shemeji yake orodha ni ndefu sana kuanzia TISS, ukuu wa mkoa, ubunge, katibu mkuu wa CCM nk. Gen Davidi Musuguri aliyekuwa mkuu wa majeshi enzi za Mwalimu ana nafasi pia kwenye family tree ya Nyerere. Rashidi Kawawa na mkewe Sophia walikuwa madarakani muda mrefu katika nafasi za juu kwenye CCM. Mzee John Malecela na kaka yake balozi Job Lusinde wamekula nchi sana madarakani. Wapo wengine wengi tu wa enzi hizo za Mwalimu.

Sina ushahidi kama yote hayo yalifanyika kwa nepotism, lakini inafaa kutazama mazingira ya nyakati husika na hatua ambazo wahusika walipitia, tusizungumzie kitu kama vile ni cha ajabu sana kimeanza leo, kumbe historia ipo. Hebu tupitie chimbuko lake kihistoria tuone kama tutarudi na majibu yaleyale na shutuma zilezile?
 
Mkuu mwanafunzi hawezi kuhalalisha kufeli kwake kwa kusema kwamba lakini wengi darasani nao walifeli. Hauwezi kufanya vitu kwa kisingizio kwamba fulani nae anafanya hivyo hivyo. Kama Chadema ina taka kuji tofautisha na CCM haiwezi kutumia CCM kama standard barer. Chadema ime campaign na inaendelea kujinadi kama chama mbadala. Sasa na wao wakiingia kwenye dimbwi ya kufanya yale yale ya CCM mbadala ita toka wapi.

CCM kujazana ndugu hilo swala liko wazi kabisa kama ulivyo ainisha hapo juu na mifano ni mingi zaidi ya hapo. Ila moja ya vitu vilivyo fanya watu waanze kuichukia CCM ni kuona kwamba CCM ni chama chenye "wenyewe". Ndiyo maana tuka hoja nafasi ya Ridhiwani na pia tuka hoji January Makamba kuingia kwenye siasa. Sasa leo Chadema ifanye hayo hayo kwa kisingizio kuwa CCM nao wanafanya?
Uko sahihi mkuu!si sawa kwa Chadema Kuiga mabovu ya Ccm,ama chama kingine chochote.lakini tukumbmbuke kuwa bado mtandao wa Chadema ni mdogo si km Ccm.unakuta bado watu waliotoa mchango mkubwa kwa chama ni wa eneo fulani,au wa familia fulani.kwa hali hiyo kunatokea hali ya kupata nafasi hizi kutoka eneo fulani au familia fulani.Nakumumbuka niliona baadhi ya criteria zilizotumika kuwapa marks wagombea wa viti maalum chadema.ELIMU ILIKUWA NA NAFASI KUBWA,IKIFATIWA NA UZOEFU KTK UONGOZI NA MCHANGO ULIOTUKUKA KWA CHAMA.YOTE HAYA NI KWA WALIOGOMBEA,KM HUKUGOMBEA WALA USILALAMIKE KUTOFIKIRIWA.
 
Kuna siku nilisema na sitoacha kusema ipo siku wenye macho watatambua nini maana ya chadema ona hizi sample ndogo tu

PHILEMON NDESAMBURO-MBUNGE MWANAE LUCY UWENYA MBUNGE,KUNA MKWEWE MBUNGE

HAYA ALIEKOSA URAIS DK SILAA,....MKEWE ROSE KAMILI MBUNGE

CCM
1.YUSUF MAKAMBA + JANUALY MAKAMBA = UFISADI
2.JK+ SALMA +RIZ1 + MIRAJI + MWENYEKITI WA CHIPUKIZI WA CCM TAIFA, NI MTOTO MDOGO WA KIKWETE.
3.KIGHOMA MALIMA = ADAM MALIMA
4. RASHIDI KAWAWA = VITA KAWAWA + ZAINABU KAWAWA.
5.AMOSI MAKALLA = MTOTO WAKE CHIPUKIZI TAIFA NA MTOTOWA JK.
6.KARUME SR = KARUME JR
7.MWINYI SR = MWINYI JR
8.MSEKWA= ANNA ABDALA
9.MALECELA = ANNE KILANGO:rip:
 
mimi binafsi naukubali sana uteuzi wa mwaka huu, sioni kama kunaupendeleo wa aina yeyote ile, huu upendele watu wanaousema unaletwa na waandushi wa habari uchwara, ambao wapo kwaajili ya kuidhoofisha chadema.
Kama inakumbukwa vizuri baada ya mchakato kuahirishwa na dr Kitilia Mkumbo chadema walitangaza hadarani tu atakayepata viti maalumu ni yule atakaye isaidia Chadema katika majimbo.
Kama tunavyojua kinadada zetu wengi ni waoga wa kingia kwenye siasa, embu niambieni ni mwanamke yupi aliyegombea kwa tiketi ya chadema aliposhindwa hakupita kwenye huu uteuzi wa vti maalumu?
kuanzia Anna KUMU......kIGAMBONI
Regina Mtema....kilombero
Rose kamili.....Hanang
na kunammoja aligombea zenj.......
 
Tatizo ni wasomi wakina dada wangapi ni wanachama wa chadema ambao hawakupata ubunge wa viti maalum na waka lalama? Tatizo watu ni waoga kujitoa wakidhani kukumbatia ccm ndo bora zaidi. Wapiganaji wote waliojito muhanga wamekumbukwa. Sifa za kuchaguliwa zilielezwa na Dr Mkumbo........nadhani sasa watanzania wataiunga mkuno chadema ili wapate uviti maalum
 
Mkuu mwanafunzi hawezi kuhalalisha kufeli kwake kwa kusema kwamba lakini wengi darasani nao walifeli. Hauwezi kufanya vitu kwa kisingizio kwamba fulani nae anafanya hivyo hivyo. Kama Chadema ina taka kuji tofautisha na CCM haiwezi kutumia CCM kama standard barer. Chadema ime campaign na inaendelea kujinadi kama chama mbadala. Sasa na wao wakiingia kwenye dimbwi ya kufanya yale yale ya CCM mbadala ita toka wapi.

CCM kujazana ndugu hilo swala liko wazi kabisa kama ulivyo ainisha hapo juu na mifano ni mingi zaidi ya hapo. Ila moja ya vitu vilivyo fanya watu waanze kuichukia CCM ni kuona kwamba CCM ni chama chenye "wenyewe". Ndiyo maana tuka hoja nafasi ya Ridhiwani na pia tuka hoji January Makamba kuingia kwenye siasa. Sasa leo Chadema ifanye hayo hayo kwa kisingizio kuwa CCM nao wanafanya?

MKUU, argument yako katika huu mjadala imekaa vizuri. Haiwezekani kuhalalisha kosa walilofanya CHADEMA katika uteuzi wa viti maalum kwa sababu CCM wamezidi. Nilitarajia CHADEMA wana set standards baada ya CCM kushindwa kwa sababu ndio chama kinachochukuliwa hivi sasa kama mbadala wa CCM.

Kama ni vigezo, yupo mgombea ambaye ni Afisa Utumishi jiji la Mbeya, ni mhitimi wa Chuo Kikuu, amehatarisha hadi ajira yake, wakati wasomi wengi ni waoga kujibainisha na vyama vya upinzani yeye alithubutu, wapo wengine waliosaidia sana ushindi wa Mr II pale Mbeya ni wasomi wazuri tu, bado Mbeya haina mwakilishi katika hivyo viti 23.

Tukitaka mabadiliko ya kweli tuache hizi double standards kwa hawa wanasiasa ama sivyo hakutakuwa na mabadiliko
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom