tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,238
- 4,464
N.B: Nimeiweka hapa kwenye siasa, maana Tz kila kitu ni siasa tu!
Nimekuwa na rafiki zangu wazalendo kuliko mimi (kama watatu) ambao wamekutana na mama huyu pale Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Kama kawaida ya mama huyu wote walikuwa wakifika ofisini kwake wanaishia kuondoka wamekwazika, bila kujali malengo yao thabiti ya kuanzisha hospitali na vituo vidogo vya afya nchini Tanzania, kwa lengo la kuboresha maisha ya mtanzania. Hawa ni watanzania ambao wametumia mali zao ili kufungua vituo vya afya nchini, biashara ambayo kwa hakika si ya kuaminika kwa nchi yetu ya Tanzania lakini wakiwa wanaongozwa na dhamira njema ya kusaidia wenzetu nyumbani wamethubutu kujaribu (Mmoja Marekani, mwingine Afrika Kusini, na wa mwisho yupo nyumbani Tanzania). (Tunamshukuru Mungu ndugu zangu hawa wote wamepata usajili baada ya kusota kwa miezi kadhaa wakisubiri kupata usajili).
Naambiwa Dr. Pamella Sawa ni Msajili wa Vituo vya Afya Binafsi na Umma wizara ya Afya. Kitengo ambacho kwa hakika kimekuwa kinazidi kufungia vituo vya watu binafsi kwa maelekezo kwamba havijatimiza vigezo wakati huo huo wakiviacha vituo vya serikali visivyohitajika hata kuwapo kwa jinsi visivyokuwa na sifa za kutoa huduma kwa wananchi.
Kitengo hiki kimekuwa kikipokea rushwa nyingi wawapo kuchunguza utendaji kazi wa vituo vya afya Tanzania, na mara zote wamekuwa wanatengeneza mazingira ya rushwa hata kama huna kosa.
Mtanzania msomi, Dr Pamella anasifika sana kwa kuheshimu raia wa kigeni hususani wahindi wenye vituo vyao vya afya nchini kwetu, huku akiwadharau Watanzania vijana kwa wazee ambao wanajitolea kutoa huduma kama hiyo. Ni mara nyingi utaona mhindi anaruhusiwa kuingia ofisini kwake bila kusubiri foleni ya watanzania waliokaa nje ya ofisi yake.
Ukiingia ofisini kwa Dr. Sawa (Yameshawahi nikuta wakati namsindikiza jamaa yangu kufuatilia usajili wa hospitali yake) utapokelewa kwa moyo mkarimu na wasaidizi wake ambao pia hawaishi kunyanyaswa na dada huyu mrembo lakini ghafla ukashangaa anakutoa kwa ukali kwa kisingizio cha kwamba wana mkutano au subiri mtu mwingine atoke (japo kuna watu zaidi ya watatu wanaotoa huduma katika ofisi yake).
Dr. Sawa anasifika kwa maneno makali ambayo baadhi ya nyakati huleta aibu kwa watanzania wanaoingia ofisini kwake. Watumishi wengi wizara ya afya ambao wanahitaji huduma katika ofisi yake huenda kuongea naye kwa woga mkumbwa utadhani yeye ni Simba, ingawa ana umbile dogo na lenye mvuto.
Wengine wanadai kwamba ati Sawa hutumiwa na baadhi ya rafiki zake kutoruhusu kupitisha maombi ya watu wengine wanaonekana ni hatari kwa vituo vingine vya afya kuendelea kupata wateja (sina uhakika maana maombi hupitishwa na board, ingawa yeye huhusika na hatua zote za kupitia maombi na pia ana nguvu sana kikaoni).
Tunashukuru serikali kutoa fursa sawa kwa wote, maana hata mwanamke msomi kama huyu anaweza kupata nafasi nzuri wizara ya afya makao makuu bila shida yoyote, lakini mambo anayowafanyia watanzania wenye moyo safi wa kutaka kuisaidia jamii yetu yanamfanya aonekane asiyefaa na kwa kweli anatakiwa ajirekebishe haraka.
Kama ni tabia zake za asili basi ajitahidi kuziweka kando pindi awapo kazini.
Lakini Tutafika tu!!!