Cyril Chami: Historia yake na ubunge wa Moshi Vijijini

Yeah wengi tunajua hayo, but give credit where credit is due, kwa jimboni kwake anajitahidi, wizara yake ni mchapakazi, mwaminifu maybe atapata kujutia na kurudia ndoa yake, who knows.
To be exseminarian is not a precondition that you are going to be a saint throughout your life you have to work hard to make your marriage survive to which he may have not been aware, but still there is always tomorrow. Give him a chance please. And to be honest can you be sure the ones you want to be elected would have all the qualities you enlist here rolled into one character? I wonder!

Ok Mama Joe nimekupata!!! Ila kwa ufupi walipofikishana na mke wake si rahisi kwao (hasa Chami kwani mke bado anaipenda ndoa yake) kujenga ndoa ile tena, to him he does not thinking of tomorrow for the marital union he had. And since he is very rigid, ni ngumu zaidi. Yaani kwa kifupi ana mambo ya kikoloni na ya kizee na mila za wachagga wa Kibosho!!! Sisemi kama mila ni mbaya ila ni pale ambapo hata msomi anakubali kuwa mke hana sauti, unaweza kumbiringisha kama pipa!!!!

Ila nahofia inaweza pia kuwa ngumu kudumu kwa relation nyingine!!! Due to his natural facts!!!!!!
 
Watanzania ni wataalamu sana wa kuishi na kutumia vitu "used" kuanzia nguo, magari, mke/mme, vyeti vya shule,.... Mwenzetu Chami naye anaelekea hukohuko kwa akina JK/Salma, JSM/ Anne Kilango, Msekwa/ Anna Abdallah, Mohamed Khatib/ Aisha Kigoda, Rashid Kawawa/...., mwacheni naye atafute used mwenzake!!
 
Maane,

1. Mbona wanaume/wanawake wakware wako wengi tu ktk jamii yetu?? Ukware may be ni reflexion yetu sisi wenyewe haswa Waafrika..saa ingine hatutosheki na mmoja! Na ndo maana HIV new infectin ni kubwa zaidi kwa wale wenye ndoa!

2. Mbona Clintion naye alikuwa Mkware??

Sitetei haya mambo..ila may be tusimwomee Chami. Kila mtu ana maisha yake binafsi. Tukuanza kuchunguzana hapa hakuna kiongozi aliye mkamilifu ktk haya mambo hata achunguzwe na UWT.

Ni kweli Mzalendohalisi!!! Clinton alipogundulika kuwa na kimada uliona jinsi ambavyo alikalishwa kitimoto kwenye Jury!!!! Ilikuwa the World History!!! Ila kwa hapa Tz tukifanya hivyo ni sawa na kufunga ofisi kwani hakuna kiongozi ata survive!!! Pengine tungeweka kwanza SI units mpya za uongozi bora halafu ndipo tuanze kwa kasi kwani zilizopo naona zina kasoro ndiyo maana maadili kwa viongozi wengi yapo chini mna, yaani ni aibu!!! Na si kwa wale viongozi waandamizi walio ndani ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma bali hata ishuke kujumuisha na wakurugenzi/ wakurugenzi wasaidizi/Principles, etc wa public service!!!! At least tukianza kumkunja samaki akiwa mchanga na mbichi baadaye tutakuwa na viongozi wa kitaifa wenye maadili!!
 
Watanzania ni wataalamu sana wa kuishi na kutumia vitu "used" kuanzia nguo, magari, mke/mme, vyeti vya shule,.... Mwenzetu Chami naye anaelekea hukohuko kwa akina JK/Salma, JSM/ Anne Kilango, Msekwa/ Anna Abdallah, Mohamed Khatib/ Aisha Kigoda, Rashid Kawawa/...., mwacheni naye atafute used mwenzake!!

Yaani Wildcard, inasikitisha!!! Tena hao ni wale ambao umeweza kukumbuka!! the list is endless hasa kama utajumuisha na wale ambao wameshaitwa mbele ya haki!!! Mimi nalia na ile tume ya Maadili ya uongozi wa Utumishi wa Umma.
 
Halafu tunakaa tunajadili jinsi ya kuumaliza wizi, ubadhirifu, rushwa, ufisadi wa mali za UMMA! Haya mambo yatagharamiwa na nini?
 
Hapo kwenye italic na red bolded sitasema sana!!!! Mhhh patamu hapo!!!!! ila jibu safi ninalo!!!!

Ni kweli kuwa mambo ya familia ni magumu ila na sisi wengine tunachangia kuyafanya magumu zaidi badala ya kutafuta solution ya kuyafanya mepesi na rahisi!!! Asikudanganya mtu, hakuna ndoa ambayo ni smooth hasa kwa ile miaka mitano ya mwanzo!!! Nimeipitia ndoa na nimeaona na niko ndani ya ndoa for years now. Wakati mwingine ni vema kufumbia macho mambo mengine for the sake of your marriage. Hakuna kitu kibaya kusikia jamii ikikutaja eti mke wako wa awali, mara mtalaka mara nini haileti picha nzuri!!! Kabla pia ya kuachana fikiria zaidi watoto, inatesa!!! Nikiwaza watoto mke/mume hata afanya kosa gani namsamehe!!! Kama ni uzinzi kwa mwenzangu for the sake of the kids sitamwacha ila nitajitahidi tu kuishi separately but under the same roof!!! Na from the begining weka wazi kwa mwenzako makosa ambayo akiyafanya yataleta hatari na hasara kwa familia, langu kuu ni kuwa mzinzi nje ya ndoa!!!! Bisha lakini huyo ndiyo msimamo wangu!!

Nchi zilizoendelea ili kuwa kiongozi usalama wa taifa unatizama hadi stability ya familia yako!!! Tz sijui vigezo vyao ni vipi!!!! Tunatakiwa nasi tuwe na SI Units za kimataifa. Na ndiyo maana serikali na rasilimali zake zinaishia kutunza vimada vya viongozi wetu!!!!! Imagine wakati Dr. Chami anateliwa kufanya kazi Ikulu tayari alishakuwa na mgogoro na familia, alipokuwa anagombea ni worse, alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri was even worse katika familia yake maana alijiona amepata sana na kumringia yule dada mkibosho mwenzake!!! Kwa mantiki hiyo hakupaswa kuwa katika system ya uongozi maana alishashindwa kwa familia yake. Hapa pia nawazungumzia wale viongozi wengine ambao wameshindwa familia kama Dr. Chami!!!

Mkuu naomba ufafanuzi kidogo, iwapo mtu akitaka kuteuliwa kwenye nafasi ya uongozi na hajaoa/kuolewa ina maana akeshachunguzwa aachwe kwa sababu hana familia na itapelekea kuwa kiongozi mbaya?
Na unaposema SI units za kimataifa unamaanisha nini hasa? Ninawafahamu watu kama Condoleezza Rice hawakuwa na familia na waliweza kuyatekeleza madaraka yao vizuri tu.
 
Kekuye,
Bila shaka umemsikia pia yule Gavana wa Jimbo la Oregon(nadhani) aliyekwenda kumtembelea hawara kule Argentina. MAADILI yanaanzia ndani ya mtu mwenyewe, kisha familia yake na baadaye inakuwa rahisi sasa kuiendesha ofisi ya UMMA.
 
Ni kweli. Hasa kwa hawa wenzetu ambao nafasi ikipatikana kwa namna yoyote ile ni lazima itumike kikamilifu. Mama Anna ametuharibia Mkapa wetu hadi basi.

Kwa kiasi nataka kukubaliana na wewe kuwa Anna kamharibu Mkapa na mawazo ya kifisadi, lakini na yeye Mkapa mbona aliishi naye muda wote huo hakuna kilichotokea kikubwa ila baada tu ya kufariki Baba wa Taifa akaanza kuyakubali hayo mawazo??????
 
Ok Mama Joe nimekupata!!! Ila kwa ufupi walipofikishana na mke wake si rahisi kwao (hasa Chami kwani mke bado anaipenda ndoa yake) kujenga ndoa ile tena, to him he does not thinking of tomorrow for the marital union he had. And since he is very rigid, ni ngumu zaidi. Yaani kwa kifupi ana mambo ya kikoloni na ya kizee na mila za wachagga wa Kibosho!!! Sisemi kama mila ni mbaya ila ni pale ambapo hata msomi anakubali kuwa mke hana sauti, unaweza kumbiringisha kama pipa!!!!

Ila nahofia inaweza pia kuwa ngumu kudumu kwa relation nyingine!!! Due to his natural facts!!!!!!

Thanks for understanding sio wakibosho tu, almost all sometimes (sorry ni wakwe zangu, ngoja niishie hapa)
Try to raise this issue when he comes to beg for votes next year, will add his value to women voters if he changes! Remain blessed
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 21 (9 members and 12 guests) Irimu, Jane Siku, Maane, Mopao Josee, MpendaTz, Mzalendohalisi, Nyauba, Ochu, WildCard

Jamani mada hapa ni makala ya Raia Mwema, sasa naona kuna mada mpya hapa ya mambo ya ndoa na mila na tusipoangalia muda si mrefu tutaingia kwenye ze utamu. Ile makala ni ndefu na ina hoja nyingi za kitaifa za kujadili kama vile kazi za Ikulu na kadhalika, lakini watu wanaondoka na kuanza kujadili ndoa.
 
Mkuu naomba ufafanuzi kidogo, iwapo mtu akitaka kuteuliwa kwenye nafasi ya uongozi na hajaoa/kuolewa ina maana akeshachunguzwa aachwe kwa sababu hana familia na itapelekea kuwa kiongozi mbaya?
Na unaposema SI units za kimataifa unamaanisha nini hasa? Ninawafahamu watu kama Condoleezza Rice hawakuwa na familia na waliweza kuyatekeleza madaraka yao vizuri tu.

Mkuu Kekuye naona pengine hukuelewa post yangu. Hebu rudia tena kuisoma. Nilichomaanisha ni kuwa wakati Chami anateuliwa nafasi mbalimbali kuanzia Ikulu hadi hapo alipo tayari alikuwa ameshaoa na mushkeli wa ndoa ulianzia kule Canada wakati anafanya PhD yake. Na pia simaanishi kama huna familia basi huwezi kuwa kiongozi, la hasha, Wanachofanya huwa wnachunguza conduct ya wazazi wako and a bit of family history na kidogo they walk in hata kwa extended Family (Traditional Family) wana - tress the leadership and conduct at family level na kwa kuongoza wengine if at all katika familia yako kuna aliyewahi kuwa kiongozi mahali fulani. Kwa hiyo ndugu yangu tujitahidi tuwe wazazi na viongozi wa mfano mzuri wa kuigwa ili tuwaandalie watoto wet njia ya uongozi.
 
Mkuu Wilcard nimekuelewa, ila shida yangu ni kuwa kama mtu ni muadilifu tu na ana uwezo wa kuiendesha ofisi ya umma ila SI unit inakosekana-hana familia katika maana ya kuoa/kuolewa ina maana mtu huyo atakuwa hafai kwa sababu hana familia ya kudhihirisha kuwa anafaa? Kwa maneno mengine, kuwa na familia ndiyo kigezo cha kuonyesha uwezo wa mtu kutekeleza dhamana aliyopewa na umma?
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 21 (9 members and 12 guests) Irimu, Jane Siku, Maane, Mopao Josee, MpendaTz, Mzalendohalisi, Nyauba, Ochu, WildCard

Jamani mada hapa ni makala ya Raia Mwema, sasa naona kuna mada mpya hapa ya mambo ya ndoa na mila na tusipoangalia muda si mrefu tutaingia kwenye ze utamu. Ile makala ni ndefu na ina hoja nyingi za kitaifa za kujadili kama vile kazi za Ikulu na kadhalika, lakini watu wanaondoka na kuanza kujadili ndoa.

Halisi ndugu yangu si kuwa tumeacha kuchangia mambo ya Siasa tukajikita kwa ndoa, at least for this!!! Jua kuwa ndoa ni mwanzo wa kila kitu, formation of the nuclear family!!! (Assuming that kila ndoa itajaliwa watoto).Ikikosewa tu ujue umeharibu mambo mengi!!!! Kusambaratika kwa ndoa nyingi kumeshababisha instability nyingi!!! Watoto wa mitaani (part), kutokuwa na kizazi kilichosoma kwa uhakika(nani atasomesha mtoto wa mtaani??), kuwa na young parents, kukithiri kwa umaskini, kuongezeka kwa social unrest and so many more!!! Sipendi wazazi waachane, kuna madhara mengi sana, mimi niko kwa upande wa watoto zaidi. siombe yakupate au yapate watoto au ndugu zako!!

Wale ambao wameishi na mzazi mmoja na mara nyingi mama wakati baba anatanua mitaani watakubaliana na mimi machungu yake!! Inauma na inabidi tuhamasishe wazazi wajaribu kupata suluhu ya matatizo yao just for the sake of their beloved children!!! Mtoto anapokuwa mara weekeend hii yuko kwa baba, mara kwa mama, mara ili kondoa purukushani basi wanahamishiwa boarding!!! Tuishie hapa.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 21 (9 members and 12 guests) Irimu, Jane Siku, Maane, Mopao Josee, MpendaTz, Mzalendohalisi, Nyauba, Ochu, WildCard

Jamani mada hapa ni makala ya Raia Mwema, sasa naona kuna mada mpya hapa ya mambo ya ndoa na mila na tusipoangalia muda si mrefu tutaingia kwenye ze utamu. Ile makala ni ndefu na ina hoja nyingi za kitaifa za kujadili kama vile kazi za Ikulu na kadhalika, lakini watu wanaondoka na kuanza kujadili ndoa.
Halisi, hata mimi nimeuliza huko nyuma mada hasa ni ipi inayozungumzwa hapa. Katika hayo mahojiano yamezungumzwa mengi lakini baadhi ya watu wengine wanajaribu kupotosha na kuleta mambo yao kwa madhumuni wajuwao wao. Kama mtu anaishu ambayo angependa kushirikisha wengine, basi aanzishe mada tofauti. Kama kuna mtu anaona huruma sana kwa ndoa ya mtu mwingine kuvunjika basi achukue hao watoto wanaosemekana wanateseka akawalee. Mke aliyeachwa hatujamsikia analalamika, wengine inawahusu nini? Kuna vyama vingi tu vya kutetea haki za wanawake, kama huyo mwanamke anaona kaonewa, kwanini asiwatafute wamsaidie! Kumbuka huyu ni Mbunge na Naibu Waziri, kama kungekuwa na malalamiko kutoka kwa mke wake, si TAMWA, TAWLER, UWT, WAWATA...taja yote wangemfungia kidete mpaka kieleweke. Turudini kwenye mada!!!!!
 
Kwa mke mwenye busara na msomi kama yule mke wa Chami hawezi kupeleleka masuala yake ya private kwenye kadamnasi!!! Siyo malezi na busara hizo!!!! These are personal matters!! Hivi kila mzazi akienda kwenye gazeti au forums au blogs kuweka matatizo ya ndani ya nyumba yake tutafika wapi??? Nafikiri msonganamo utakuwa mkubwa sana kama bile ilivyokuwa foleni ya chakula cha njaa miaka ya 1974!!!

Haya turudi kwenye mada: Cyril Chami: Historia yake na ubunge wa Moshi Vijijini. Nimesahau kuwa kampeni za 2010 zimeshaanza. All the best.
 
sasa ameshaoa mwingine? au yuko na kimada?

nadhani kuwa na mke/mwezi anaeleweka ni vema ili pesa zetu za kodi kama alivyosema Maane zisitumike vibaya kulea vimada!

Pia hii ni agenda ya kisiasa kwa 2010 kuwa hadi sasa hana mke!

Sasa sii vuzuri Naibu Waziri na Mbunge kuanza tu kuparamia wake za watu au wanawake ovyo ovyo!
 
huyu naye atupuumzishe sie..wakati wenzie akina Ndesamburo wanatengeneza noti yeye alikuwa bize ana sign mikataba inayofanana na ya akina Karl Peters

Huyu alipata kazi ikulu kwa nguvu ya fisadi mwanamke aka MAMA ANNA MKAPA ambaye ana undugu naye

Cha ajabu katika hiyo interview hajaelezea kuwa alikuwa kiongozi wa DARUSO aliyeongoza migomo wakati wa mzee Mwinyi

nashangaa hilo anaficha

Chami bora angeangalia namna ya kuwapatia watu wa jimbo lake zile umeme wa wind turbines alizowaahidi..

Ile DARUSO ya enzi za Mzee Ruksa ilikuwa kanyabwoya tu! Watu walikuwa wanaongoza migomo kumbe 'bosheni', yaani 'changa la macho'. Lakini kuna wengine waliingia mkenge wakidhani kuwa hao pia wenzao, na matokeo yake tumeyaona 'wamefulia' hadi leo hii!

Huyu Cyril Chami alipokuwa rais wa DARUSO mlimani aliwapotosha wenzie kina Matiko (aliyekuwa overall DARUSO president) na Haroun Kimaro aliyekuwa rais wa DARUSO Muhimbili. Wote sasa hivi hawajulikani walipo, yaani walipotea katika mazingira ya kutatanisha.
 
haya kweli jambo kuzua jambo,tumjadili kiongozi yupi tena?naona chami mshamfumua vya kutosha, haya alieanza atoe mahojiano ya gazeti na another minister.
 
Ile DARUSO ya enzi za Mzee Ruksa ilikuwa kanyabwoya tu! Watu walikuwa wanaongoza migomo kumbe 'bosheni', yaani 'changa la macho'. Lakini kuna wengine waliingia mkenge wakidhani kuwa hao pia wenzao, na matokeo yake tumeyaona 'wamefulia' hadi leo hii!

Huyu Cyril Chami alipokuwa rais wa DARUSO mlimani aliwapotosha wenzie kina Matiko (aliyekuwa overall DARUSO president) na Haroun Kimaro aliyekuwa rais wa DARUSO Muhimbili. Wote sasa hivi hawajulikani walipo, yaani walipotea katika mazingira ya kutatanisha.[/QUOTE]

Well said Mtu B!!!!! Watu walikuwa kazini and the mission was accomplished!!!!
 
Ile DARUSO ya enzi za Mzee Ruksa ilikuwa kanyabwoya tu! Watu walikuwa wanaongoza migomo kumbe 'bosheni', yaani 'changa la macho'. Lakini kuna wengine waliingia mkenge wakidhani kuwa hao pia wenzao, na matokeo yake tumeyaona 'wamefulia' hadi leo hii!

Huyu Cyril Chami alipokuwa rais wa DARUSO mlimani aliwapotosha wenzie kina Matiko (aliyekuwa overall DARUSO president) na Haroun Kimaro aliyekuwa rais wa DARUSO Muhimbili. Wote sasa hivi hawajulikani walipo, yaani walipotea katika mazingira ya kutatanisha.

....chami ni mtoto mdogo sana kwa haroun kimaro..[hakusoma nao wakati mmoja]...,huyu matiko kafulia kwa sababu alikuwa NCCR .....Ya mashushu...mnakumbuka strategy ya enzi zile ya system ilikuwa NCCR chama cha wasomi[the strategy to tap minds of really oppositions people like matiko...]...sasa angalia wapo wapi kina Lamwai[mwanasheria wa ccm] na tenga ....wote wanakula shushuu ...bora wawakumbuke kina matiko waliowateka akili.....ndio maana mrema alipoenda NCCR mwalimu alimcheka sana...na hata mwanaye makongoro alipooenda kule alizidi kucheka..mwisho ndio akasema NCCR chama cha mbwa!!![alijuwa ana maana gani kusema mbwa - si mnajuwa mbwa ni askari mzuri tu]

GT kwa sasa dr haroun kimaro ni marehemu ...alifia zimbabwe!!!!

kusema ule mgomo wa enzi ya mwinyi ulikuwa mdogo si sawa...kumbukeni ule mgomo ndio ulibadili kabisa sera ya elimu ya juu[haukusaidia]...ulipelekea kuleta cost sharing....kabla ya ule mgomo ..chuo kikuu ilikuwa kusoma bure..,na kula bure na kichele kidogo...baada ya mgomo ...ilipitishwa posho nafikiri 1,500 kwa siku..na ilikuwa haitoshi kabisa...baadaye ndio wakasema kama haitoshi wazazi waongezee...na ndio chanzo cha cost sharing...ule mgomo ulitumika kutuadhibu sana...
 
Back
Top Bottom