CWT yasisitiza mgomo upo palepale Jumatatu tar 30/07/2012

Mbona maelezo yako yanaji contradict yenyewe?..
Umesema pesa zimetumwa kila mikoa na kila wilaya.. Iweje tena useme "Pesa zote zinaingia kwenye matumbo ya akina Mukoba"???...

Unaonekana unatumiwa na kina naniliu!
Wasalaam.

Ninachotaka kukufahamisha ni kuwa ukiwa kiongozi lazima very strategic.....CWT hawawezi kuitisha mgomo uanze baada ya kutoa notice serikalini ya saa 48, tena unatoa notice ijumaa saa 7 si upumbavu huo? ina maana serikali inafanya kazi kufungua ofisi jumamosi na jumapili au?

Ninanachokisema hapa ni kuwa viongozi wa CWT hawana dhamira ya dhati kuwakomboa walimu...wanaitisha migomo ya kishamba kama hii ili serikali ikizuia waseme eti tunaonewa...huo ni ujinga uliopitiliza.

kama kweli wapo stable kwanini wasingeitisha mgomo katikati ya mihula na wanasubiri shule zifunge ndio wajidai kuhamasisha migomo...huo ni udhaifu wa mukoba/CWT...! wanatumia pesa nyingi kwa kazi isiyo na tija? huo ni ujinga.

Ndio maana nasema wajinga ndio waliowao....walimu waaachane na usaanii huu wa Mukoba/CWT.
 
Toka hapa nyoka wa jangwani mbegu ya dhalimu! Mungu akuangalie kwd macho yote!

Nadhani wewe ni mmoja wa watu mnaofanya kazi huko CWT....hamuwezi kutmia zaidi ya milioni 200 kuhamasisha mgomo wa walimu hali mkijua wiki ijayo shule zinafungwa na mwalimu atatakuwa nyumbani, sasa huo mgomo utakuwa effect gani kwa serikali au wewe ni kilaza hujui hata kufikiria na kuona faida na hasara kwa pande hizi zote mbili...sio unaropoka tu ndugu!
 
Mbona madai yenu nifedha na kuboreshewa maisha tu, hivi mazingira ya kazi zenu ni conducive kweli? madawati, vyumba vya madarasa, upungufu wa vitabu na vitendea kazi, nyumba za walim ukosefu wa maabara nk si issue kwenu ila mishahara na malimbikizo ya malipo tu? hapo ndipo madaktari walipo wazidi!
MADAI ya Walimu yako 11 yakiwemo ya uboreshwaji wa mazingira ya kazi eg uwepo wa madarasa, vitabu, maabara na kupunguza IDADI ya wanafunzi ktk madarasa, uwepo wa walimu etc. chunguza kwanza Kabla ya kupost issue usiwe mbayuwayu na haya MADAI ni similar na Yale ya 2007 hakijabadilika kitu
 
Kwa ma
ra ya kwanza nataka kuona msimamo wa Mkoba mana yasije rudia yale ya Diamond Jubilee kawapa hope watu halafu siku ya mwisho kawatema! Naamini kwa sasa inabidi nasi Waalimu tuwe na umoja usio teteleka ktk kudai haki zetu za Msingi! naungana na wenzangu nipo tayari kwa mgomo
 
2ache siasa' walimu wana dai haki yao ya msing!..serekali imewazungusha toka ktambo sana..bila mikwara sekal itajsahau
 
CWT wana jengo kubwa na zuri sana pale Ilala. Nilimuuliza mwalimu mmoja, lile jengo linawasaidia vipi nyinyi kama mwanachama? Kwa kweli hakuweza kunipa jibu. Akaongezea kuniambia kuwa waalimu wote wanakatwa pesa kwa lazima kila mwezi kuchangia chama chao!
Hivi vyama wakati mwingine ni kwanyonya zaidi wafanyakazi kuliko kuwasaidia. Just imagine mamilioni yanatumwa kuhamasisha mgomo wa nini? Kama mmeamua kugoma ni swala la kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na kila mwalimu atasikia. Hapo hayahitajiki mamilioni kila mkoa na wilaya kama mnaendesha kampeni za uchaguzi.
Hayo mamilioni CWT ingeweza kununua property nzuri tu to add to its assets!
 
Katika madai yote ya walimu linalotia uchungu zaidi ni malipo ya malimbikizo yao ya mishahara, pesa za kupandishwa daraja na pesa za uhamisho. Hizi ni pesa ambazo walimu wamezifanyia kazi na haipaswi wasote kuzipata.
Mama Salma Kikwete ni mwalimu, hivi ameshindwa kabisa kumkumbusha "mzee" matatizo haya ambayo yeye anayajua vizuri haswa!
 
Rais CWT ahofia ya Ulimboka
• Awataka walimu waanze mgomo kesho

na Waandishi wetu
Tanzania Daima



amka2.gif
HOFU ya kutekwa, kuteswa na kupelekwa katika msitu wa Mabwepande kama ilivyokuwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, imeanza kumtesa Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mukoba alisema amekuwa akipata vitisho vya kumzuia kushiriki kwenye mgomo walioupanga kuuanza kesho, lakini amedai vitisho hivyo havimzuii kuendelea na mkakati wa kutafuta haki za walimu.

Mukoba alisema hata kama atapelekwa katika msitu huo uliojipatia umaarufu mkubwa kwa kutumiwa kuendesha vitendo vya utesaji na uuaji, bado ukweli utabaki palepale kuwa walimu wana madai ya msingi ambayo yamekuwa yakipigwa danadana na serikali.

Alibainisha kuwa watu wanaofikiri kuwa paka anaweza kugeuka simba wanajidanganya kwa sababu haki ya mtu haiwezi kuminywa na mtu yeyote hata kama ana madaraka makubwa.

"Unapomuona paka nyumbani kwako huwezi kumwita simba …eeh hata kama napata vitisho havitanifanya kuacha kutimiza majukumu yangu, hata kama mimi nitapata matatizo wapo watakaoendelea na kupigania haki za walimu, kwakuwa huwezi kuzuia na kumnyamazisha kila mtu, hasa katika masilahi ya taifa," alisema.

Alisema anaamini kuwa kile kilichomtokea Dk. Ulimboka hakitaweza kumtokea yeye kwa sababu watetezi mbalimbali na mikataba mingi ya kimataifa ipo na inasimamiwa kikamilifu na watu wasiopenda haki za watu zipotee.

Mukoba alisema serikali haina haja ya kutoa vitisho kwa walimu kuwa mgomo wao ni batili bali iueleze umma ni kesi gani na namba ngapi iliyopo mahakamani inayozuia mgomo huo.

"Serikali imezoea kupiga porojo za kisiasa, porojo zao hazituzuii wala kutunyamazisha kuendelea na msimamo wetu wa kuanza mgomo kesho," alisema.

Fomu za serikali
Serikali imesambaza fomu kwa maofisa elimu wa wilaya ikiwataka wazigawe kwa walimu na wajaze haraka ili wabaini wanaounga au kupinga mgomo huo.

Fomu zimeandikwa maneno ya ‘Haraka Sana', zina sehemu mbalimbali ambazo zinamtaka mwalimu kuandika namba yake ya hundi, kuunga mkono mgomo au kutounga mkono.

Kwa mujibu wa Mukoba, sehemu ya namba ya hundi imewekwa mahususi kuwakata mishahara walimu watakaoshiriki kwenye mgomo huo.

"Nawaomba walimu waendelee na msimamo wao, maana wasiposimama imara kutetea haki zao hakuna atakayewasaidia, mgomo huo hautaathiri utumishi wao, kwa kuwa umezingatia sheria," alisema na kukiri kuwa kutakuwa na vitisho na propaganda nyingi kutoka kwa waajiri.

Kuhusu suala la serikali lililopo mahakamani, Mukoba alisema hatua hiyo haiondoi taratibu za mgomo na kuongeza kwamba serikali isitake kutumia kivuli cha mahakama kukandamiza haki za walimu ambao wamezingatia taratibu na sheria zote za nchi katika mgomo huo.

Juzi CWT kilitangaza mgomo rasmi huku kikikamilisha taratibu za mgomo kwa kupiga kura kuunga au kukataa mgomo huo, ambapo kati ya walimu 183,000 walimu 153,848 sawa na asilimia 95 ya walimu waliunga mkono kufanyika kwa mgomo.

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali na CWT kushindwa kufikia makubaliano katika siku 30 walizoipa kuanzia Juni 25 mwaka huu.

Madai makubwa ya walimu katika mgomo huo, mbali na malimbikizo ya madeni yao ya huko nyuma, pia wanataka ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho za kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55 na walimu wa masomo ya sanaa asilimia 50 na posho za mazingira magumu asilimia 30.

Mara baada ya tishio hilo la CWT, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi ya Rais (Ikulu), kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo, juzi ilitoa taarifa kupinga mgomo huo kwa madai kuwa ni batili, kwa sababu kuna kesi mahakamani inayozihusu pande hizo mbili.

"Kwa sasa shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa Julai 27, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika mahakamani na mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne Julai 31, 2012 saa sita mchana ili kuiwezesha mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi. Kwa hiyo mgomo huo si halali kwa vile shauri hilo bado liko mahakamani," ilisema.

Maandalizi mikoani
Mkoani Mbeya, Kaimu Katibu wa CWT Mkoa wa Mbeya, Felix Mnyanyi, alisema mazungumzo kati ya walimu na serikali yameshindikana baada ya kuthibitishwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na kesho walimu watagoma.

Mkoani Mara, Mwenyekiti wa CWT wilayani Bunda, Francis Ruhumbika, amewataka walimu wote kushiriki kwenye mgomo huo kwa kutokwenda kwenye vituo vyao vya kazi.

 
Acha kutumika wewe,kama wametumia hyo 240 kwa wilaya zote tanzania still bado naona ni ndogo sana,mgomo upo palepale walimu msimsikilize huyu mtoa pumba hapa anatumika na TISS kuwaaribia moods!!!
 
mgomo upo pale pale na nchi haitatawalika....ndo manake mpaka 2015 yaani lazima watu wawe wametepeta vibaya sana ...walidhni kuwa raisi ni kupigiwa ving'ora eeeh
 
Nipo sehemu moja kijijini huku maeneo ya Serengeti nimekaa na walimu s/m wanasema mgomo uko palepale. Ni mara yangu ya kwanza kuona kuna muamko mkubwa wa walimu sasahivi.

mimi bado ni Thomaso hadi nione!!
 
jamani hivi kunawatu wanaumwa ugonjwa wa akili humu jf na nahc mto mada ndo mwenyekiti wao?

Hivi usemapo waalim wote wanakwenda kuhesabu sensa unahakika? shule nifundishayo mimi tupo waalim dip, degree na wa degree za uza ambao kwa ujumla wetu tupo 69 lakin hakuna hata mmoja anayekwenda kwenye sensa sasa wewe unasemaje waali wote??acha uongo kabisa na unafiki natumesha kugundua wewe upo ili kuwatete waliokutuma. sisi hatutetereki na si wajua form six wapo wenye mitihani ya mock??? sasa kesho ni mgomo wala halina ujanja ila kwa kuwaonena huruma wanafunzi hawa tutawasimamia mitihani yao ya Mock n awakimaliza tunaungana na wengine kwenye mgomo nia hapa hatutak hawa form six kuwalostisha lkn pia uwezo huo tunao ishu ni kwamba itakuwa dhambi sana kuwadisturb ktk ya mithani.
 
Ni walimu gani hao wanaolipwa sh.700,000?.Ninatambua walimu wako wa ngazi mbali mbali.Ngazi za chini kama wa shule za msingi wanalipwa around 200,000 na hao 700,000 ni graduates na Masters level.Lakini kwenye soko la ajira hiyo siyo mishahara hata kidogo.Kwahiyo TISS msitupotoshe wananchi na kutufanya wote ni wapumbavu.Mnatumia akili ndogo kuongoza akili kubwa za walimu.
 
walimu kazeni kamba hii hela wala si kitu kikubwa haki yenu tukopamoja mmenyanyasika kwa muda mrefu sana
 
jamani hivi kunawatu wanaumwa ugonjwa wa akili humu jf na nahc mto mada ndo mwenyekiti wao?

Hivi usemapo waalim wote wanakwenda kuhesabu sensa unahakika? shule nifundishayo mimi tupo waalim dip, degree na wa degree za uza ambao kwa ujumla wetu tupo 69 lakin hakuna hata mmoja anayekwenda kwenye sensa sasa wewe unasemaje waali wote??acha uongo kabisa na unafiki natumesha kugundua wewe upo ili kuwatete waliokutuma. sisi hatutetereki na si wajua form six wapo wenye mitihani ya mock??? sasa kesho ni mgomo wala halina ujanja ila kwa kuwaonena huruma wanafunzi hawa tutawasimamia mitihani yao ya Mock n awakimaliza tunaungana na wengine kwenye mgomo nia hapa hatutak hawa form six kuwalostisha lkn pia uwezo huo tunao ishu ni kwamba itakuwa dhambi sana kuwadisturb ktk ya mithani.

sasa wewe mwalimu,mmeambiwa wote kesho msiende kufanya kazi wewe unaenda kusimamia mitihani ya mock...kweli Mkoba ana kaazi.
 
sasa wewe mwalimu,mmeambiwa wote kesho msiende kufanya kazi wewe unaenda kusimamia mitihani ya mock...kweli Mkoba ana kaazi.

ni kweli kabisa kwamba tulinatakiwa tusiende but on other hand tumewafikiria wanafunzi wa kidato cha sita ambao kimsingi kabisa tukwalostisha hapa watarudi kuumia vyeti vya form 4.

ingawa tuko kwenye mgomo basi tuasimamia mtihan tu na hapa tumejaribu kuanalia psycholojia ya watahiniwa kama wakiajaumauishwa uwezekano wao wa kufanya vby ni mkubwa sana so to be fair tuanwakonsida na si kwa shule zote ni za high school tu ambazo ziko TAHOSSA kanda ya mashariki, form fives na wengine hawafundishwi wala hawatamuona awe wa zam ama wa daras ama wa somo na zikipita siku mbili hakieleweki basi waungane na sisi waanze maandaman kila shule kwenda halmasjhauri kudai waalim hawapo mashuleni. na ndo utakapo patikana hapo.

kwanza impact ya huu mgomo hatutaki iende kwa hawa form six just kwasababu hatutaki kuwakwamisha ila mbona mtakiona wanafunzi watakapo tujoin? ndipo nchi itakapo shindikana kutawalika na this time mgomo huu wanafunzi wetu wapo nyuma yetu.
 
Back
Top Bottom