CV ya Sheikh Gorogosi

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Wana Jf, Nilipokea kwa masikitiko makubwa habari ya kifo cha Sheikh Gorogosi. Ufahamu wangu unanishawishi niamini kuwa alikuwa mtu muhimu ktk BAKWATA ingawa sifahamu kiwango chake cha elimu. Natamani kufahamu CV ya huyu ndugu yetu. Mwenye info naomba aimwage hapa jamvini.
 
Jamani wadau...nasikia sheikh Gorogosi ana shule kali sana sana ya elimu ya dini.....
amesoma chuo kikuu misri kama miaka 7 na chuo kikuu cha makka miaka kama 7...pia amesoma sana sheria za dini.....hadi leo nafikiri hakuna anaemfikia kwa elimu ya dini hapa tanzania......yaani ilikuwa karibia apate PHD ya elimu ya dini....hata sheikh Husein analijua hili...nimeumwa sikio na mdau mmoja nae ni mwana ulamaa....
 
Japo CV yake sina ila kwa kadri nilivyowahi kuzungumza nae, anaonyesha ilmu duniya anayo na sifa yake ya ziada ni heshima kwa mamlaka husilka. Sheikh Mkuu alipoakiumwa, Ni Gorogosi ndiye aliyeendesha Bakwata, hata ili fukuza fukuza, Sheikh Mkuu aliibariki.
Miongoni mwa wenye ilmu kubwa ya dini, ukiondoa Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, na Sheikh Nurdin Hussein Bafadhili, waliobaki wote badobado, Sheikh Yahya Hussein pia yupo, tatizo ni longolongo za unajimu na mambo ya majini.
Mungu awaweke mahali pema peponi, Sheikh Nurdin Hussein, Hemed Bi Jumaa na Gorogosi.
 
Mi nafikiri mpendwa wetu huyo ameshatangulia mbele ya haki so, sioni sababu ya kujaribu kumchimba yaliyokuwa maisha yake binafsi. cha muhimu ni kwamba alikuwa mtu muadilifu hilo kila mmoja anajua, hakuwa muongo, fisadi, mshirikina au mzinzi so may you please leave our beloved sheikh alone????
 
Japo CV yake sina ila kwa kadri nilivyowahi kuzungumza nae, anaonyesha ilmu duniya anayo na sifa yake ya ziada ni heshima kwa mamlaka husilka. Sheikh Mkuu alipoakiumwa, Ni Gorogosi ndiye aliyeendesha Bakwata, hata ili fukuza fukuza, Sheikh Mkuu aliibariki.
Miongoni mwa wenye ilmu kubwa ya dini, ukiondoa Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, na Sheikh Nurdin Hussein Bafadhili, waliobaki wote badobado, Sheikh Yahya Hussein pia yupo, tatizo ni longolongo za unajimu na mambo ya majini.
Mungu awaweke mahali pema peponi, Sheikh Nurdin Hussein, Hemed Bi Jumaa na Gorogosi.
sijui kwanini huwa nakuona msanii msanii fulani hivi wale madingi ambao wanawapaga story watoto wao kuwa walikuwa wa kwanza from STD one mpaka chuo kikuu...anyway ni JF lakn
 
Yo Yo,
Ungelimjua huyo aliyekuwa nyuma ya PC kuandika hayo na shughuli yake. Usingehoji wala kumwona msanii. ... eni wei, JF sote tunatumia majina bandia na tunavaa tabia na uhusika bandia, japo baadhi tunajuana fika!
 
Last edited:
Japo CV yake sina ila kwa kadri nilivyowahi kuzungumza nae, anaonyesha ilmu duniya anayo na sifa yake ya ziada ni heshima kwa mamlaka husilka. Sheikh Mkuu alipoakiumwa, Ni Gorogosi ndiye aliyeendesha Bakwata, hata ili fukuza fukuza, Sheikh Mkuu aliibariki.
Miongoni mwa wenye ilmu kubwa ya dini, ukiondoa Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, na Sheikh Nurdin Hussein Bafadhili, waliobaki wote badobado, Sheikh Yahya Hussein pia yupo, tatizo ni longolongo za unajimu na mambo ya majini.
Mungu awaweke mahali pema peponi, Sheikh Nurdin Hussein, Hemed Bi Jumaa na Gorogosi.

Niliwahi kujuzwa kuwa Marehemu alikuwa msomi mzuri hata kwa upande wa Ilimu Dunia. Aliwahi kufanya kazi Mamlaka ya Elimu katika nafasi ya Uandamizi. Aliacha kwenda BAKWATA lakini naambia alirudi tena na amekufa akihesabika kama Mfanyakazi wa Mamlaka. Nilijaribu kuhoji aliwezaje kutumikia vyeo viwili na vyote vikiwa ni vikubwa, mpaka sasa sijaridhika na majibu. Ila nimepewa mfano hai kuonyesha kuwa hakuwa pekee wa namna hii maana hata Padre Prof. Mkude, mwalimu wa UDSM anamajukumu kama marehemu
 
Yo Yo,
Ungelimjua huyo aliyekuwa nyuma ya PC kuandika hayo na shughuli yake. Usingehoji wala kumwona msanii. ... eni wei, JF sote tunatumia majina bandia na tunavaa tabia na uhusika bandia, japo baadhi tunajuana fika!
Mie nataka nimjue Mwenyeji Mungu.......huyo mkewe na wanawe ndio wamjue.....
 
Jamani wadau...nasikia sheikh Gorogosi ana shule kali sana sana ya elimu ya dini.....
amesoma chuo kikuu misri kama miaka 7 na chuo kikuu cha makka miaka kama 7...pia amesoma sana sheria za dini.....hadi leo nafikiri hakuna anaemfikia kwa elimu ya dini hapa tanzania......yaani ilikuwa karibia apate PHD ya elimu ya dini....hata sheikh Husein analijua hili...nimeumwa sikio na mdau mmoja nae ni mwana ulamaa....

Mkuu story yako imejaa nasikia nyingi kwa hiyo ni ngumu kujua kama ni kweli au la. Na mtu umesema kasoma Misri miaka 7 halafu akasoma na Mecca miaka 7 ukijumlisha miaka yote hiyo inakuja miaka 14. Sasa inachukua miaka mingapi kupata PhD ya dini kama mtu aliyesoma chuo kikuu miaka 14 hajaipata?
Halafu baada ya nasikia zote unakuja kusema hata sheikh Husein anajua hilo. Sasa iweje statement ya kwanza hauna uhakika halafi statement ya pili una uhakika? Very contradicting.
 
Pamoja na elimu zote bado waislamu watanzania hawajanufaika na uongozi wa Bakwata kwa kiwango kinacho stahili, kama mchangiaji mmoja aliposema kwamba ni watu watatu tu wenye kiwango hiko cha elimu katika population ya zaidi ya watu millioni 20 katika kipindi zaidi ya miaka 40.

Ili kumuenzi marehemu ni kukubali kuboresha pale walipofika Bakwata na kukwama kwa muda mrefu pamoja na kuruhusu mawazo mengi, kuongeza uwazi na ushirikishi katika kuongoza dini na kutengeneza fursa nyingi zaidi na kwa watu wengi zaidi. Pamoja na kuweka mfumo wa kisasa zaidi katika uongozi utakaokabili changamoto zinazo ikabili jamii ya waislamu kwa sasa na baadae, binafsi na naona jamii ya kiislamu inaenda nyuma kila kukicha ukilinganisha na jamii za dini nyingine hata hizi zinazojitokeza sasa.
 
Mkuu story yako imejaa nasikia nyingi kwa hiyo ni ngumu kujua kama ni kweli au la. Na mtu umesema kasoma Misri miaka 7 halafu akasoma na Mecca miaka 7 ukijumlisha miaka yote hiyo inakuja miaka 14. Sasa inachukua miaka mingapi kupata PhD ya dini kama mtu aliyesoma chuo kikuu miaka 14 hajaipata?
Halafu baada ya nasikia zote unakuja kusema hata sheikh Husein anajua hilo. Sasa iweje statement ya kwanza hauna uhakika halafi statement ya pili una uhakika? Very contradicting.

Uko juu

teteeeehehe
 
Jamani wadau...nasikia sheikh Gorogosi ana shule kali sana sana ya elimu ya dini.....
amesoma chuo kikuu misri kama miaka 7 na chuo kikuu cha makka miaka kama 7...pia amesoma sana sheria za dini.....hadi leo nafikiri hakuna anaemfikia kwa elimu ya dini hapa tanzania......yaani ilikuwa karibia apate PHD ya elimu ya dini....hata sheikh Husein analijua hili...nimeumwa sikio na mdau mmoja nae ni mwana ulamaa....
__________________

Re: CV ya Sheik Gorogosi Japo CV yake sina ila kwa kadri nilivyowahi kuzungumza nae, anaonyesha ilmu duniya anayo na sifa yake ya ziada ni heshima kwa mamlaka husilka. Sheikh Mkuu alipoakiumwa, Ni Gorogosi ndiye aliyeendesha Bakwata, hata ili fukuza fukuza, Sheikh Mkuu aliibariki.
Miongoni mwa wenye ilmu kubwa ya dini, ukiondoa Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, na Sheikh Nurdin Hussein Bafadhili, waliobaki wote badobado, Sheikh Yahya Hussein pia yupo, tatizo ni longolongo za unajimu na mambo ya majini.
Mungu awaweke mahali pema peponi, Sheikh Nurdin Hussein, Hemed Bi Jumaa na Gorogosi.

Labda nishereheshe kidogo point mbili tatu za hapo juu. Almarhuum Gologosi hakumaliza degree kule misri alikatiza bila kupewa kwani degree a dini misri ni ya miaka 10. Yeye alimaliza Saudia katika fani ya Sheria specilized katika social islamic.

Mpka umauti wake alikwenda Hija mara 14.

Kuna engi sana wenye visomo va juu sana katika dini nao woooote wakiongozwa na
Prof Juma Mikidadi ( B islamic law madina, m social islam madina, PhD islamic social islamic sScotland. huyu ni mbunge wa jimbo la kibiti aliyestahafu.

Kuna Sheikh Mattaka( aliyefukuzwa bakwata ) ana masters alizosomea Misri na madina za islamic culture. na sasa anfana masters mbili kwa mpigo Open Univ dar ( MA na LL M.

Kuna akina Khalifa Khamis ( yeye ana b islamic law na B mass com. .
Kuna sheikh Chizenga ana masters
Kuna sheikh Kilemile ana Bachelor aliyosomea Misri miaka 10.
Kuna sheikh Muharami Doga. ( Huyu ndio mkali wa Nahau ( bachelor in islamic law na bachelor in arabic literature.

Mtoto wa sheikh mkuu hemed bin jumaa, yeye ana masterd aliyyochukulia Saudia.
Kuna wengi.

Al marhum Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed ( yeye hakuwa na degrii yoyote bali alisomea ndumi tanga, kisha lamu.

Al Marhum sheikh Noordin husein hakuwa na degrii oote ee alisomea kilwa, tanga na lamu.

Vile vile sheikh Yahya husein hana degrii

Nasriyah Saleh Al-Nahdi.
Mapumzikoni
Mwera , Znz
 
Yote Tisa,kumi Shehe Gorogothi alikuwa mcha Mungu na mtii tumwache apumzike kwa amani.
 
Mbona hamkuuliza haya wakati yu hai, say ukishajua unataka kutupeleka wapi? Mwacheni apumzike kwa amani.
 
Mhh kwa sasa sisemi maana nikisema ntaambiwa nikasilimu au sijui nitoe shahada as if nimemshirikisha Mungu

lakini in short hakuna atakaye kuletea jibu sahihi wala atakaye kuletea scholarly papers au vitabu alivyoviandika huyu bwana

sana sana utapewa majibu ya kuwehua wehua tuu kisha baadae utaulizwa wewe mbona unagangania kutaka kujua shule yake..then watatumia tactic ya kukupa CV za wasio husika kabisa na hii thread

lakini usiseme maana ukisema utaonekana unalako jambo
 
Japo CV yake sina ila kwa kadri nilivyowahi kuzungumza nae, anaonyesha ilmu duniya anayo na sifa yake ya ziada ni heshima kwa mamlaka husilka. Sheikh Mkuu alipoakiumwa, Ni Gorogosi ndiye aliyeendesha Bakwata, hata ili fukuza fukuza, Sheikh Mkuu aliibariki.
Miongoni mwa wenye ilmu kubwa ya dini, ukiondoa Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, na Sheikh Nurdin Hussein Bafadhili, waliobaki wote badobado, Sheikh Yahya Hussein pia yupo, tatizo ni longolongo za unajimu na mambo ya majini.
Mungu awaweke mahali pema peponi, Sheikh Nurdin Hussein, Hemed Bi Jumaa na Gorogosi.

Acha kutufanya wajinga sisi

Kwanza Hakuna sheikh Nurdin Hussein Bafadhili

pili unamaana gani kusema kuwa waliobaki wote bado bado maana hiyo ni gross generalisation na kwa mtu wa calibre yako ulitakiwa uwe more careful kabla ya kutoa sweeping statements kama hizi
 
Back
Top Bottom