CV ya Mbunge wa Chadema Maswa Mashariki Hon, Sylvester Mhoja

Member of Parliament CV

GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1743.jpg
First Name: Sylvester
Middle Name:Mhoja
Last Name:Kasulumbayi
Member Type:Constituency Member
Constituent:Maswa Mashariki
Political Party:CHADEMA
Office Location:Box 170, Ipililo Maswa, Shinyanga
Office Phone: +255 787 458107/+255 716 343727/+255 667 343727
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: skasulumbayi@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 1 January 1950
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Bugisi Primary SchoolPrimary Education--PRIMARY
Monduli Teachers' Training CollegeTeaching College19721973CERTIFICATE
Murutunguru CollegeCourse19781979CERTIFICATE
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Maswa East Constituency20102015
Maswa District Executive Director OfficeTeacher19732000
POLITICAL EXPERIENCE

JF Daima
:clap2:

KAMPENTE,
Kama umemsikiliza huyu mzee akiwatetea wafugaji na wakulima, basi hakuna haja ya CV maana bungeni haina kazi yoyote. Wabunge wenye PhD zao wanashindwa kujibu hoja, msikilize Maghembe anaposema.
Kama wewe ni muumini au umewahi kusoma vitabu vya Mungu **** Mfalme Suleiman hakuwahi kwenda shule lakini HEKIMA yake ilimfanya kuwa mteule wa Mungu.
Nakuomba sana wasilikize Wachumi daraja la kwanza BOT, wanavyotukana wenzao warudi darasa la kwanza hiyo MA yake inasaidia lolote.
 
Nipige Nisipigeee?.........Pigaaaaaaa aaaaa
Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .......Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mahindi yanaota na rangi ganiiiiiiiiiiiii?............K ijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mpunga unaota na rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?............... ............Kijaniiiiiiiii.
Piga makofi na vigelegele kwa chama cha mapinduzi.
 
Ni kweli QMadela Wa- Madilu, kwa zamani serikali ilikuwa sikivu kidogo inathamini maoni ya wasomi hata mwanafunzi wa chuo kikuu pia alikuwa anachukuliwa kama mtu muhimu sana. Lakini siku hizi baada ya bunge kuonekana ni ajira nzuri wakishaingia wanajiwekea mikakati ya asitoke kabisa na ukijifanya na usomi wako kupiga kelele unaambiwa umetumwa.

Kiukweli bunge letu limepoteza mwelekeo kama uliangalia jana muda mwingi wanabishana kuhusu kanuni wakati ilitakiwa mwenyekiti kutumia tu busara wakati mwingine kama mtu katoa hoja ya msingi bahati ameshindwa quote kifungu cha kanuni arekibishwe kisha aendelee kuchangia.

Kitu nilichojifunza jana wabunge wanapitisha vitu vingi vingine hawavijui na hata hao mawaziri wanawasilisha vitu ambavyo hawavijui, mfano mbunge wa Mbozi alisimama na kusema "haya mambo tunayojadili yameandikwa kwa kiingereza sijui yataandikwa lini kwa kiswahili kwani binafsi kuna kipengele sijakielewa labda wabunge wenzangu wakielewa" alivyosimama waziri Kombani I think na yeye akashindwa kutete na akikakiri kipengele kile kimekosewa, katika situation kama hii kuna uwezekano wa vitu vingi kupitishwa.

MY TAKE: Kuna haja ya kuanza kufikiria kuangalia kigezo cha elimu siku za usoni kwani muda kwani kazi ya mbunge kwa muda unaokuja itakuwa ni kujadili budget, miongozo mbalimbali pamoja na sera vitu ambavyo vinahitaji upeo kiaina, hii kazi ya jimboni kwangu hakuna maji sijui nini waachiwe madiwani kupitia halmashauri za wilaya husika watakusanya na kumpa mbunge akazunguze kwa niaba tena dakika tano tofauti na sasa hivi mtu anatumia dakika 5 kushukuru na dakika 10 anaongea vitu ambavyo angeongea dakika 4
 
Mwalimu huyo... sasa wewe kinachokushangaza nini? au tukuwekee ile ya Prof maji marefu?
 
Pamoja na kwamba MaPhD ya CCM ni uozo mtupu lakini tuwe wakweli. Kuchagua CV kama hiyo yenye certificate ya ualimu wa UPE kuingia bungeni ni udhalilishaji wa Bunge. Huyo jamaa wa Maswa kweli anaweza kuto hoja yoyote ya maana? hata alivyo tu anasikitisha. Kweli ukimpa kabrasha la page 30 akasome atakuja na lolote asubuhi. Give me a break- huyo Mhoja hafai kukaa mjengoni na sitegemei achaguliwe tena
 
KAMPENTE,
Kama umemsikiliza huyu mzee akiwatetea wafugaji na wakulima, basi hakuna haja ya CV maana bungeni haina kazi yoyote. Wabunge wenye PhD zao wanashindwa kujibu hoja, msikilize Maghembe anaposema.
Kama wewe ni muumini au umewahi kusoma vitabu vya Mungu **** Mfalme Suleiman hakuwahi kwenda shule lakini HEKIMA yake ilimfanya kuwa mteule wa Mungu.
Nakuomba sana wasilikize Wachumi daraja la kwanza BOT, wanavyotukana wenzao warudi darasa la kwanza hiyo MA yake inasaidia lolote.




Kwa CV ya huyu bora tusiwe na Wabunge.
 
huko Kenya Jaji wa Mahakama Kuu amesema hivi:

By excluding everyone who does not have post-secondary education, I find that Section 22(2) of the Elections Act DISCRIMINATES on the basis of status and social origin.Corrupt and unethical practices have resulted into poor governance.A requirement for post-secondary education doesnot provide the remedy(Sunday Nation,July 1,2012 pg 13)
Sasa mimi naona CV huwa haifanyi kazi,wala Degree huwa hautunzi uadilifu.Aina ya Shahada walizokuwa nazo Mawaziri na Wabunge wetu zingegeuza nchi hii kufanana na Afrika Kusini kama zingekuwa na maana.Badala yake hata waliojisema ni Wachumi Daraja la Kwanza hoja zinakuwa muflisi!Kwani jamaa aliyemshinda Profesa Sarungi si kaishia Standard Seven?

Well said mkuu. Kwani ma PhD ya hawa CCM yametufikisha wapi? Tanzania ya kina Nyerere iliyokuwa na wasomi wachache kabisa wa ngazi hiyo ilikuwa bora mara elfu kumi kuliko hii ya "wasomi" wanaotumia kwato kufikiri. Isitoshe walioishia darasa la saba na form four wengi walinyimwa fursa hiyo na jamii na si sahihi kuwanyanyapaa. Mwisho nasema tukiendekeza dhana ya aliyesoma zaidi apate nafasi kubwa zaidi ya uongozi tutaishia kuongozwa na genge hilihili lililoifisadi na kufilisi nchi maana wmeuhujumu mfumo wa elimu na kuhakikisha wakwao wanpata elimu bora, isiyo ya kutiliwa shaka ili washinde ushindani wowote kielimu na waendelee kutawala milele kupitia chama lao la kishetani CCM.
 
Ritz,
Mbunge mkuu wangu hata akiwa hakumaliza darasa la nne maadam anaweza kuzungumza na kutetea maslahi ya wananchi sidhani kama tunahitaji ubishi maana umeona mwenyewe kina Stella.. Ila sikumbuki kama Murutunguru kilikuwa Chuo tayari mwaka 1978 sina hakika japokuwa nilishaondoka Kibara..
Mkandara, |Murutunguru kilikuwa chuo cha uongozi cha CCM, ni matawi ya iliyokuwa Kivukoni.
 
Last edited by a moderator:
Ina tofauti na wale Ma PHd wa CCM, kwani huyu uwezo wake mkubwa sana, CV yake nzuri sana haina tatizo kwani anawakilisha wananchi kama Job description ya ubunge inavyotakikana. Na wale wenu wa PHd, ni pure head demolition, hawana kitu huko kichwani wamebaki kusema ndiyo na hapana na kuwasahau wananchi wao.
 
Mbona hiyo CV haina tatizo? Huyo Mh. amefundisha vijana wengi tu na sasa ni madaktari, wanasheria n.k. Tena ni bora yeye amesema ukweli kuliko magamba ambao kila mtu anajiita Dr. kwa Phd za online tena za kununua! Wote hao hawatusaidii kitu zaidi ya kufisadi nchi kila kukicha.
 
So what ? find something more sensible of national interest bring here ........so long as he can deliver.
 
Imetulia hiyo. Tunaomba CV ya Livingstone Lusinde
Member of Parliament CV

GENERAL
Salutation
Honourable
Member picture
1743.jpg

First Name:
Sylvester
Middle Name:
Mhoja
Last Name:
Kasulumbayi
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Maswa Mashariki
Political Party:
CHADEMA
Office Location:
Box 170, Ipililo Maswa, Shinyanga
Office Phone:
+255 787 458107/+255 716 343727/+255 667 343727
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
skasulumbayi@parliament.go.tz
Member Status:
Current Member
Date of Birth
1 January 1950
EDUCATION
School Name/Location
Course/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
Bugisi Primary School
Primary Education
-
-
PRIMARY
Monduli Teachers' Training College
Teaching College
1972
1973
CERTIFICATE
Murutunguru College
Course
1978
1979
CERTIFICATE
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name
Position
From Date
To Date
The Parliament of Tanzania
Member - Maswa East Constituency
2010
2015
Maswa District Executive Director Office
Teacher
1973
2000
POLITICAL EXPERIENCE

JF Daima
:clap2:
 
Mnako elekea mnataka wasio jua kusoma na kuandika wakose wawakilishi wao.
 
Sifa ya kuwa Mbunge ni elimu ipi kwani? Hii aliyonayo huyu haitoshi kwa mujibu wako mleta hoja? Anyway kwakuwa unahitaji kuwajua na wengine visomo vyao tuwekee na cv za hawa wafuatao:
1) Mh. Lusinde a.k.a. Kibajaji
2) Mh. William Lukuvi
3) Mh. Ngonyani a.k.a. Maji marefu
4) Mh. Komba
5)
endelezeni wadau.
 
Huyu mbunge mwenye hii CV pamoja na Prof Maji Marefu na Lusinde, wakati wa kuchambua bajeti ukiwaangalia jinsi walivyokuwa wakiwa kama wamemwagiwa maji akuna hata mmoja mwenye kuthubutu kuchangia bajeti wala kuomba muongozo kwa spika...chezea shule.
 
Back
Top Bottom