CV ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhani

Ni Mwanajeshi, Mzanzibari, mkristo, mwanasheria, "ameshafanya kazi na tume za uchaguzi zote mbili", umri wake ni miaka 70. Huyu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar atausimamia kwa juhudi zote.
 
CV ya Judge Ramadhani Mwaka 2010

Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.-

Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.

Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.
Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.

Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.

Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.

Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.

Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.

Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.

Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.

Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.

Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool.”
 
  • Thanks
Reactions: Gor
Good inaeleweka ila sasa akipata Urais . . . . . .ataandaa sera ya kupeleka watoto nje kusoma au ataimarisha elimu ya ndani??!!!
 
Atleast yeye watoto wake wamekubali kuajiriwa wanaishi kwa mishahara...wangekuwa wafanyabiashara ingekuwa habari ingine.....ila nilisikia kuwa ni mchungaji...sasa itakuwaje kuhusu kondoo wa bwana?...au ameamua kuacha wale 99 na kuamua kumtafuta huyu mmoja (taifa la tanzania) aliyepotea?

Hongera mzee nakuheshimu ila ujuwe bitta ni bitta murrrah....huku umekuja utachafuka mpaka basi.
 
kwa kifupi Jaji Mkuu Mstaafu ana watoto wanne, Francis, Bridget, Marina na Mathew. na wote wamesoma Uk-Liverpool na wamemaliza ila Mathew bado anaishi huko huko Liverpool. kwa hiyo hana jukumu la kusomesha labda wajukuu lakini watotot alishamaliza zamani. na majina hayo nimekutajia kuanzia first to last born.
 
CV ya Judge Ramadhani Mwaka 2010

Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.-

Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.

Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.
Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.

Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.

Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.

Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.

Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.

Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.

Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.

Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.

Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool."
Mbona watoto wako wote hawadhamini nchi yao kiasi kwamba wako nje tu....na kwanini ukiwa jaji haukuhakikisha watoto wa jamii maskini nao wanapata elimu na kuwa kama watoto wako?jibu wewe fisadi.A.R
 
kwa kifupi Jaji Mkuu Mstaafu ana watoto wanne, Francis, Bridget, Marina na Mathew. na wote wamesoma Uk-Liverpool na wamemaliza ila Mathew bado anaishi huko huko Liverpool. kwa hiyo hana jukumu la kusomesha labda wajukuu lakini watotot alishamaliza zamani. na majina hayo nimekutajia kuanzia first to last born.

1. Swali la msingi ni sera ya elimu na yeye kusomesha watoto nje. . . . . .Upi msimamo wake??!?
2. Watoto ni wake kasomesha yeye nje ya nchi na inasemekana wanafanya kazi huko, sababu ya maslahi??!! Uraia??!! Wanachukia Tanzania au nini hayo utasema waulizwe watoto fine. . . . .yeye akiwa CJ chini yake watumishi wangapi walipata scholarship ili kuongeza elimu nje ya nchi?????
 
Atleast yeye watoto wake wamekubali kuajiriwa wanaishi kwa mishahara...wangekuwa wafanyabiashara ingekuwa habari ingine.....ila nilisikia kuwa ni mchungaji...sasa itakuwaje kuhusu kondoo wa bwana?...au ameamua kuacha wale 99 na kuamua kumtafuta huyu mmoja (taifa la tanzania) aliyepotea?

Hongera mzee nakuheshimu ila ujuwe bitta ni bitta murrrah....huku umekuja utachafuka mpaka basi.

1. Wanafanya kazi wapi na kodi yao inakatwa wapi??!!
2. Anaweza asichafuke ila yakaongelewa ambayo asingependa watu wayaguse
 
Wasifu wa Jaji Mkuu msitaafu Agustine Ramadhan unajionesha hata kwa kumuangalia machoni. Katika watu waadilifu ambao nchi hii inajivunia ni pamoja na Agustine Ramadhan. Kila lakheri Jaji Mkuu mstaafu.
 
Back
Top Bottom