CV ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhani

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Wakuu nilikuwa naomba kama kuna mtu mwenye CV ya huyu bwana amwage hapa. Education and work experience ndo vya maana zaidi. Mambo mengine ni ya ziada! Natanguliza shukrani.

CV ya Judge Ramadhani Mwaka 2010

Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.-

Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.

Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.
Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.

Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.

Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.

Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.

Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.

Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.

Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.

Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.

Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool."
 
Justice Ramadhani is a Justice of Appeal of the Court of Appeal of Tanzania, Judge of the East African Court of Justice and Vice-Chairman of the National Electoral Commission of Tanzania.

He is also Registrar of the Anglican Church of Tanzania.
 
Jaji mkuu pia ni mwanajeshi mwenye cheo cha brigadia general
 
uliza wanasheria watakuambia what it takes to be a justice of appeal na jdg wa mahakama kuu. hiyo itakuwa education. work experience ni kwamba sasa yeye ni judge mkuu.
 
Code:
[FONT=courier new][COLOR=#000080]
   [SIZE=3][IMG]http://www.bongo5.com/images/stories/jaji_ramadhani.jpg[/IMG]

 [/SIZE][/COLOR][/FONT][SIZE=4][FONT=courier new]RAIS  Jakaya Kikwete amemteua Jaji Augustino Ramadhan kuwa Jaji Mkuu  wa nne  wa Tanzania, baada ya Jaji Mkuu Barnabas Samatta kustaafu rasmi. 

 Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi,   Phillemon Luhanjo jana, uteuzi wa Jaji Ramadhan ambaye ni Jaji wa   Mahakama ya Rufani kwa muda mrefu sasa, unaanza mara moja. 

 Taarifa hiyo ilielezea kuwa Jaji Ramadhani ataapishwa kesho jioni  Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Jaji Ramadhani ambaye ni mwenye vipaji vingi, kabla ya kuingia katika   shughuli za mahakama, alikuwa katika jeshi la Wananchi wa Tanzania   (JWTZ) akifanya kazi huko katika Idara ya Sheria na alitoka jeshini   akiwa na cheo cha Brigedia Jenerali. 

 Pia amewahi kuwa Jaji katika Mahakama ya Afrika Mashariki ambako   alikuwa yeye pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Jaji Joseph   Warioba, walikuwa wakiiwakilisha Tanzania. 

 Kwa upande wake, Kenya ilikuwa ikiwakilishwa na Jaji Moijo ole Keiwu   na Jaji Kassanga Mulwa walioteuliwa na Rais wa zamani wa Kenya, Daniel   arap Moi. 

 Kwa Uganda walikuwepo majaji Joseph Mulenga na Jaji Solony Bosse,   aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki. 

 Sambamba na hilo, Jaji Ramadhan pia ni mpiga kinanda maarufu katika  kwaya ya wa Kanisa la Anglikana jijini Dar es Salaam. 
 Taarifa iliyotolewa juzi kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari   (Maelezo), ilisema kuwa Mahakama ya Tanzania itafanya kikao maalum cha   kumuaga kitaaluma Jaji Msataafu Samatta, ambacho kitafanyika Julai 19,   mwaka huu kwenye jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo Kivukoni Front. 

 Taarifa hiyo ilieleza kuwa Jaji Samatta atastaafu ifikapo Julai 20,  mwaka huu. 

 Katika shughuli za kumwaga, atakagua gwaride la heshima mbele ya  jengo hilo. 

 Miongoni mwa watu watakaohudhuria siku hiyo ni Waziri Mkuu, Edward   Lowassa, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mary Nagu akiwemo Naibu wake,   Mathias Chikawe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika   ambaye atatoa hotuba. 

 Mbali na Jaji Samatta, Watanzania wengine wazalendo waliowahi   kushikilia nafasi ya Jaji Mkuu ni Augustino Saidi na Francis Nyalali. 

 Hii ina maana kwamba Jaji Ramadhan anakuwa pia Mzanzibari wa kwanza   kushika wadhifa wa juu katika duru za mahakama nchini Tanzania. 

 Source: Mwananchi[/FONT][/SIZE]
 
Kweli wanasheria hamjui education ya CJ wenu? Nikisema ana vyeti feki kuna mtu ana evidence ya kupinga?
 
luteniusu;luteni;kapteni;meja;lutenikanali;kanali;brigadiajenerali;mejajenerali; jenerali;lutenijenerali;field mashooo

Umekosea kidogo: kati ya Major General na genera kune Lieutenant General; wewe umemeka Lt. Gen. kuwa mbele ye Gen.

OK tumeambiwa kazi alizowahi kufanya; je jaji mkuu alipatia wapi elimu yake ya sheria? Jibu lake ni hili:

Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.

Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.

Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.
Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.

Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.

Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.

Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.

Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.

Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.

Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.

Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.

Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool.”
Naona kuwa huyu jaji, pamoja na kuwa ni mzanzibari, ni mtu ambaye sehemu kubwa sana ya maisha yake ameitumia akiwa Tanganyika. Sijui akiambiwa aamue kesi ya katiba kuhusu Muungano wa Tangayika na Zanzibar ataichukuliaje.
 
Kumbe amefanya sana kazi kwenye hizi tume za uchaguzi ZEC na NEC siyo?
Kumbe anajua vizuri udanganyifu wa mambo yao katika chaguzi zetu. Na hata katika kesi hii alikuwa na background ya mambo haya ya hivi vitume kichwani. Alichofanya ni kuwashawishi tu wenzie wakubaliane naye.
 
mtu anaweza kuwa hajasoma kivileee,ila akili na experiance yake maishani ndivo vvya msingi
madegree nini bwana?ni kuklemu tu sometimes (sio wakati wote)
nimeipenda CV yake
 
mtu anaweza kuwa hajasoma kivileee,ila akili na experiance yake maishani ndivo vvya msingi
madegree nini bwana?ni kuklemu tu sometimes (sio wakati wote)
nimeipenda CV yake

Totally agree...i wld prefer someone with extensive experience over an academic anytime!I've spent time with too many academics!In the end...they dont make a difference!
 
Back
Top Bottom