CV ya Freeman Mbowe hii hapa

Status
Not open for further replies.

Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
390
368
Member of Parliament CV
mbowe2.png


Chanzo: Parliament of Tanzania

Anaandika Magoiga SN kutoka Mwanza

Hata Kama Elimu Yake Haina Umuhimu Lakini Historia ya Elimu Yake ni Muhimu Kwa Vizazi Vijavyo
Magoiga SN-Mwanza

Kama kuna kitu ambacho hakuna mtanzania anayekifahamu bayana ni elimu ya Freeman. Hakuna mtu yeyote ajuaye Freeman alisoma wapi elimu ya msingi, elimu ya sekondari wala chuo. Hakuna mtu hata mmoja ndani ya chama chake anayeweza kusema bayana kuwa anaifahamu historia ya kielimu ya kiongozi wao.

Mwaka 2015 Mtatiro alijaribu sana kufuatilia elimu ya Freeman ili aweze kuandika makala yake iliyochapishwa ktk gazeti la Mwananchi bila mafanikio. Hakuna taasisi yeyote nchini inayoweza kudhibitisha kuwa Freeman aliwahi kusoma ktk shule yao.

Hii ni hoja ambayo hakuna anayeweza kuijibu wala kupinga kwa hoja, sana sana wakijaribu kuijibu wataanza matusi, na kusema kuwa elimu ya Freeman haina umuhimu wowote ule kuifahamu. Kwanini wanatumia nguvu kubwa ya kurasa 100 kusema na kuelezea jinai ambavyo elimu ya Freeman haina umuhimu huku wanaweza kutumia ukurasa mmoja tu KUIJIBU HIYO HOJA NA KUWAFUNGA MDOMO WANAOHOJI??

Hapo ndipo ujue kuna shida mahala.
Lakini wanasahau kwamba, hata historia ya marehemu huwa kuna kipengele kinachoelezea historia fupi ya safari ya kielimu ya marehemu hata kama aliishia darasa la nne.

Katika moja ya Makala nzito kuwahi kuandikwa na Mtatiro anasema "wasomaji wataniqia radhi maana taarifa za kielimu za mtu huyu haziko wazi, hata tovuti ya bunge haina taatufa zake. Nimejaribu kuwasiliana na ofisi yake na watu wake wa karibu ndani chama chake, ambao wengine ni marafiki zangu, waliniahidi kunisaidia kuupata wasifu huo wa kielimu lakoni baadae wakakataa kuwa hawawezi kuutoa.. ", mwisho wa kunukuu

Maelezo Zaidi BONYEZA Hapo Chini Kusoma Alivyoandika Mtatiro Kuhusu Historia ya Elimu ya Freeman http://www.mwananchi.co.tz/…/1625946-2738300-1dq…/index.html

JE KWANINI HISTORIA YA ELIMU YA FREEMAN NI SIRI??
Katika moja ya sababu zinazoweza kusababisha elimu ya mtu kuwa siri kubwa ni ENDAPO ELIMU HIYO ilikuwa na matatizo makubwa au mtu huyo hakuwahi kusoma kabisa.

Ukitaka kutafuta historia ya kielimu ya Freeman hutaweza kuipata, na hakuna anayejua lolote, ndiyo maana wengi wanajaribu kuhoji huenda Jina Freeman hakuwahi kulitumia katika masuala ya Elimu hata siku moja (Hayo ni baadhi ya majibu dhania unayoweza kuyawaza)

Au kama aliwahi kulitumia, kuna mahala atakuwa alibadili jina na kutumia jina la mtu mwingine nk??
Freeman alisoma wapi shule ya msingi?? Hilo linajibika
Je Freeman alisoma wapi elimu ya sekondari (o level)?? Na alikuwa akitumia jina gani sekondari??

Na ni kwanini hakuna mtu yeyote anayejitokeza kusema kuwa alisoma na Freeman ?? Utawasikia watu wakisema walisoma na Nyerere, Mwinyi nk lakini hakuna anayesema. Alisoma na Freeman. Why?? Kama wapo bado binafsi sijawaaikia huenda baada ya makala hii nitawasikia waliosoma na Freeman ili niwaulize maswali

Ndugu yangu mmoja amenitaarifu kuwa Freeman alisoma elimu ya kidato cha sita (Form Six) pale IHUNGO sekondari Bukoba, lakini INASEMEKANA HAKUWA AKITUMIA JINA LA Freeman. Why?? IKIWA ni kweli, Ilikuwa vipi aende kidato cha tano na sita kwa jina tofauti na jina analotumia sasa?? Je alibadili jina au ALIIBA JINA LA MWANAFUNZI ambaye alikosa uwezo wa kifedha wa kuendelea na masomo??

Kuna habari inayosema kuwa Freeman alipata Ziro 'Form Six' Pia kuna habari zinazosema kuwa Mwaka 2007/2008 Freeman alijiunga Chuo kimoja huko Uingereza ambapo alikuwa akisoma masomo ya ngazi ya Diploma, lakini Marehemu Wangwe alipoanza harakati za kutaka kugombea Uenyekiti wa Chama, Freeman alilazimika kukatisha masomo na kurejea nchini ili Kulinda Kiti chake kilichokuwa hatarini kunyakuliwa kidemokrasia. Hapo ndipo Wangwe alipovuliwa nafasi zake zote ndani ya chama na kuambiwa kuwa ni msaliti.

Freeman aliwahi kufanya kazi Benki Kuu katika kitengo muhimu kwa muda mrefu. Bado haijulikani aliweza vipi kupata kazi benki kuu ilihali kidato cha nne hakuwa amefaulu, na kidato cha sita inadaiwa kuwa alipata Ziro?? Lakini baadaye jibu likapatokana kuwa Aliyekuwa Gavana wa Benki kuu wakati huo alikuwa Baba Mkwe Wake Mzee Mtei, Mwasisi wa CDM ambaye baadae Kibwetere alimuoa binti yake, na Freeman akapewa uenyekiti wa chama.

Kitu pekee ambacho kinajulikana kuhusu elimu ya Mbowe ni kuwa ANAWEZA KUSOMA NA KUONGEA KIINGEREZA KWA WASTANI. Ingekuwa kiingereza ndiyo kipimo cha usomu Freeman angekuwa amefaulu vyema
Je umeelewa nini mpaka sasa kwa ufupi??
Je Freeman alifeli 'form four'?

Je ni kweli kuwa alijiunga' Form Six' kwa kutumia jina la mwanafunzi mwingine aliyefaulu ila hakuwa na fedha. Zamani ulikuwa ukinunua jina la mwenye akili asiye na pesa
Je ni kweli kuwa 'Form Six' alipata Ziro, ila huwezi kupata jina la Freeman maana hakuwa anatumia jina lake wakati huo. Kumbuka alikuwa anatumia jina la mwanafunzi mwingine.

Alifanya Kazi benki kuu kwa kupewa na Baba Mkwe wake wa Sasa, hakuwa na vigezo vya kitaaluma kufanya kazi aliyokuwa akiifanya Benki Kuu. Maana baba mkwe wa sasa ndiye aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu. Huyo huyo ndiye akiyemkabidhi chama baada ya kumuoa binti yake.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]: Baada ya andiko hili, watu watajitokeza ili kuelezea jinsi wanavyoifahamu historia ya kielimu ya Freeman, tutaweza kulinganisha habari zao na hizi zilizoandikwa hapa mpaka tutakapoupata ukweli. Historia ni muhimu sana, vizazi vijavyo vitashindwa kuandika vitabu kuelezea Shujaa wao Freeman kwa kukosa taarifa muhimu sana kumhusu

[HASHTAG]#FreemanAmesomaWapiFormFour[/HASHTAG]??
[HASHTAG]#FreemanAmesomaWapiFormSix[/HASHTAG]??
[HASHTAG]#FreemanAmesomaWapiFormChuo[/HASHTAG]??
[HASHTAG]#NaniAliwahiKusomaNaFreeman[/HASHTAG]??
[HASHTAG]#FreemanAlifauluVipi[/HASHTAG]??

Tutakuwa tukipokea majibu na kulinganisha na uhalisia, mpaka pale hoja nzima itakapopata majibu. Usishangae kuona wafuasi wengi wakijaribu kukwepa hoja kwa kuleta matusi, mzaha na dhihaka. Wengine watasema weka wewe CV yako kwanza nk wavumilie maana huo ndiyo uwezo wao

INAENDELEA.....................
Magoiga SN-Mwanza
Mwenyekiti wa Muda-CCM Tawi la Mitandaoni
 
gamba wewe... tuwekee ya chenge, mwigulu,mkapa,ballali,karamagi,maige,mataka,kafumu,ndulu,werema,jaji wa kesi - lema na mpendazoe,pinda,nape...kisha tuambie cv zao zimeisaidia vipi nchi hii ....then peruuz na kudadis cv za lula da silva, abeid amani karume relate na michango yao kwa watu wao....
 
Hizi sredi za CV za wabunge mbalimbali siku hizi zimekuwa zikichipua kama uyoga vile hapa jamvini.
 
Mwigulu anasema Uslama wa Taifa ni chombo kitakatifu kisihojiwe kitu chochote, je hawapati fedha kuwokana na kodi ya Watanzania?
 
Fasheni hii. Unacopy cv ya mtu na kudelete contents na kupaste JF.
Unaonekana un a thread nyingi! kweeeeeeek!
 
Akitaka kufanya vizuri kwenye siasa akasome umri unamruhusu, asikubali kushindwa na akina lyatonga, Hatutaki visingizio elimu hio ni ndogo kwa sasa

hiyo cv sio sawa, coz Mh. Mbowe baada ya kuukosa Urais mwaka 2005, alikwenda Oxford kama sio Havard, aliposomea degree ya Utawala! ukiwauliza wanaokumbuka, watakukumbusha ni chuo gani hasa
 
Mtoa thread hajui maana ya CV - msamehe bure. Ila nasikitika nimepoteza muda wangu kuchungulia madudu haya!
 
gamba wewe... tuwekee ya chenge, mwigulu,mkapa,ballali,karamagi,maige,mataka,kafumu,ndulu,werema,jaji wa kesi - lema na mpendazoe,pinda,nape...kisha tuambie cv zao zimeisaidia vipi nchi hii ....then peruuz na kudadis cv za lula da silva, abeid amani karume relate na michango yao kwa watu wao....
Mi sio gamba. lakini ingia hapa uone CV zao. lakini usikate tamaa ya kuongozwa nao.
Parliament of Tanzania
 
gamba wewe... tuwekee ya chenge, mwigulu,mkapa,ballali,karamagi,maige,mataka,kafumu,ndulu,werema,jaji wa kesi - lema na mpendazoe,pinda,nape...kisha tuambie cv zao zimeisaidia vipi nchi hii ....then peruuz na kudadis cv za lula da silva, abeid amani karume relate na michango yao kwa watu wao....

Vipi unataka kuwaajiri?
 
watu wakiambiwa ukweli wanakuja juu..! yeye mwenyewe hajakanusha wala kuomba marekebisho kwenye tovuti ya bunge.Makuwadi kama kawaida ni kutoa mitusi kwa mleta uzi..!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom