CV ya Dr Slaa From Certificate to PhD

Status
Not open for further replies.
Nyie wasomi wa wapi? Kama mtu ka skip ni kichwaaa! Mark mwandosya from bsc eng mpaka phd! Mnadiscuss vise versa!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hii topic tulijadili sana hapa mwaka jana Ritz, na nilidhani umeelewa. Na jitahada zilitumika sana kueleza elimu ya kanisa katoloki na utoaji wa vyeti wakati wa utawala wa Nyerere. Kama kuna mtu anaweza kuirejesha thread ya zamani naomba afanye hivyo.

NB: Hii topic umerudisha ghafla baada ya kuibuka uzi unaojadili CV/elimu ya Vicky Kamata. Sijui kwa nini unaona Dr Slaa wanatakiwa kujadiliwa katika level moja?

Haya maneno ni yako CV ya Slaa sio ya kwanza mie kuileta acha watu wajadili kuna members wapya wanaitaji kujua sio wote wana miaka mingi humu JF.
 
Nyie wasomi wa wapi? Kama mtu ka skip ni kichwaaa! Mark mwandosya from bsc eng mpaka phd! Mnadiscuss vise versa!
 
Huelewi kimya! Mtu akiwa na akili zisizo za kawaida anaskip! Ukifanya thesis unaweza kuruka! Kama aliruka ni extraordin
 
Haya nime-copy toka kwenye mjadala wa zamani. Huu mjadala ulinzia mwanabidii ukarukia JF. Nanukuu majibu ya mdau,


"Tukianza na Kipalapala, hapa mwanafunzi anasoma form 5 & 6 pamoja na masomo ya Theology na baada ya hapo huunganisha na degrii ya theology.

Kipalapla kama ilivyo Institutions zote za Kanisa Katoliki (kwa level ya Philosophy na Theology) iiko affiliated na vyuo vikuu mbalimbali duniani kutoka nchi moja hadi nyingine.

Mfano, wanaosoma Zomba Theological College Malawi (Theology) na Kachebere Philosophical College (Philosophy) mpakani mwa Malawi na Zambia wanafuata marking scheme ya Chancellor College - University of Malawi. Kuna chuo kingine kiko Balaka Consorsium Philosophical College nadhani kiko affiliated na St Urban University, Rome.

Missionary Institute London (MIL) iko affiliated kwa Middlesex University (chuo cha serikali cha Uingereza) na Luvein University (Belgium). Wanaofuata mfumo wa Middlesex University kupata BA wanasoma miaka 3 na passmark yao ni 40%. Wanaofuata mfumo wa Luvein University kupata BA wanasoma miaka 4 na passmark yao ni 60%. Muhula unaanza Oktoba na kwisha Juni (miezi 8).

Mfumo wa kutoa final mark ni 1) class presentation na participation 2) essay writing 3) oral examination 4) defence of dissertation mbele ya internal & external examiners. Pia mtu anayepata first class, papers zake lazima ziwe marked na internal na external examiners na ajadiliwe kama anastahili first class degree na siyo tu kupata kwenye karatasi. Pia anayeshindwa, paper zake zinasahishiswa na examiners tofauti ili kuonesha kashindwa kweli au kama amepunjwa marks.

Kwa Tanzania, kwa sasa vyuo vyote kwa level ya Philosophy na Theology viko affiliated na St Urban University, Rome. Zamani, falsafa ilikuwa miaka 2 (sasa ni 3) na teolojia ilikuwa miaka 3 (sasa 4).
Mtu akimaliza (Tanzania) alikuwa anapata certificate siyo kwa sababu masomo yalikuwa level ya chini ila kwa sababu maaskofu walikuwa hawajaridhia wahitimu wao kupata digrii licha ya kuwa walikuwa wanaombwa wanafunzi wapewe magamba kama ilivyokuwa kwenye vyuo vingine. Ilichukua muda kidogo.

Lakini kama mtu aliendelea na masomo ya juu walithamanisha masomo yale kwa chuo ambacho mtu anaenda kusoma maana content ya syllabus ya masomo ya falsafa na teolojia ni (universal) kwa vyuo vyote vya Kanisa Katoliki duniani tofauti ni kwa kila nchi wanaongeza mambo yanayohusu cultural understanding ya nchi husika including its legal system.

Uganda mtu akimaliza Jinja Philosophical College (Philosophy) anapata BA katika Philosophy. Akiendelea na Theology chuo kingine, anapata BA katika Theology na kuna vyuo vingine akimaliza Theology anapata MA. Inategemea chuo kina mfumo gani na kinafundisha nini - maana kuna baadhi ya masomo kama mtu hakuyafanya wakati wa philosophy atayafanya wakati wa theology.

Kwa baadhi ya vyuo, mtu mwenye BA ya Philosphy na BA ya Theology, akiendea na masomo ya juu 'specialisation', anaenda moja kwa moja kusoma PhD kulingana na vigezo walivyoweka (mfano, vyuo ambavyo vinafundisha Philosophy na Theology kwa pamoja).
Kwa baadhi ya vyuo masomo haya yanatenganishwa - yaani, mwanafunzi anaamua ku'specialise' kwenye pure philosophy au pure theology. Na katika masomo yote mwanafunzi anafundishwa the secular view na religious view.

Maana ni hasa kumwezesha mwanafunzi kupata "solid and consistent knowledge of man, the world and God... The students should rely on that philosophical patrimony which is forever valid, but should also take account of modern philosophical studies, especially those which have greater influence in their own country, as well as recent progress in the sciences. Thus, by correctly understanding the modern mind, students will be prepared to enter into dialogue with their contemporaries." ( Vatican II, Training of Priests, Paragrapah No 15).

Kuna vyuo kama alikosoma Dr Slaa lecturers wote ni wa level ya profesa na kwenda kusoma huko mpaka uwe 'exceptional student' nadhani kama sikosei wanachukua wale tu wenye 'first class'.

Kitu kingine ninachoona kinampa wasiwasi (jina limehifadhiwa) ni pale anaposoma "Canon Law" au "Catholic Education" kwa kudhani padre anasoma tu biblia au mafundisho ya Kanisa. Mfano, Dr Slaa amespecialise katika Canon Law ambayo ndiyo mother of secular law na kusoma Canon Law ni lazima kuanza na how law developed na mpaka kuja kugawanyika into secular na religious laws.

Advantage ya Dr Slaa si tu kwamba ana'knoweldge' ya Canon Law lakini pia nini kinaitwa secular law na kwa nini - tofauti na similarities. Mfano, definitions of what is an irregurality, malice aforethought, the difference between legality and validity of an act, what is a valid marriage and a legal marriage, etc.

All Catholic Universities undertake secular studies mfano ni Catholic University of East Africa (CUEA), Kenya, ambako hata Waislamu wanasoma huko, St Augustine, Mwanza, Luvein University etc. kwa hiyo mtu akihitimu kwenye vyuo hivyo, huwa haangaliwi kuwa amesoma elimu ya dini bali kwamba ni mtaalamu katika taaluma fulani aliyoisomea.

Tofauti kwa mapadre ni kwamba mfumo wao wa mafunzo unachukua muda mrefu na wanajifunza mambo mengi - maana hadi kufikia upadre ni mpaka uwe walau umesoma miaka 10 baada ya Form VI". (mwisho wa kunukuu)


Ukitaka mjadala mzima. https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/168414-kuhusu-cv-na-phd-ya-dr-slaa.html

Na wewe ni padre?
 
Huelewi kimya! Mtu akiwa na akili zisizo za kawaida anaskip! Ukifanya thesis unaweza kuruka! Kama aliruka ni extraordin
 
Unless kama kichwa kimejaa matapishi, lakini thread unayoleta hapa ipo majukwaani kwa miaka sasa. Shughulisha ubongo wako, sio kumtumikia mume bila kufanya hata vetting ya analokutuma.

Huyu jamaa ni mpuuzi sana anashindwa mdiscus fake Dr....analeta upuuzi wa kutumiwa na napi.....na waweza kuta ni mbumbumbu sana kajichokea mithri ya mgonjwa wa kwashiokohor......uwakala mwingine ni hatari sana....
 
Halafu kuna wazembe humu wanamwita Dr wakweli, sasa hiyo phd ameipataje wakati hata degree hana? Halafu mbona povu linawatoka kuhusu hii topic? CV za watu kibao zimemwagwa humu JF na mkazipoindea.
 
Halafu kuna wazembe humu wanamwita Dr wakweli, sasa hiyo phd ameipataje wakati hata degree hana? Halafu mbona povu linawatoka kuhusu hii topic? CV za watu kibao zimemwagwa humu JF na mkazipoindea.

Soma post No 9. halafu unganisha na link iliyopo.
 
Huyu jamaa ni mpuuzi sana anashindwa mdiscus fake Dr....analeta upuuzi wa kutumiwa na napi.....na waweza kuta ni mbumbumbu sana kajichokea mithri ya mgonjwa wa kwashiokohor......uwakala mwingine ni hatari sana....

Maneno mengi yanakutoka bure mie sina kitu ni masikini wakutupwa mnywa kahawa tu.
 
Hapa Dr Slaa alivyokuwa mbunge hana BA wala MA lakini ana PhD

Member of Parliament CV

GENERAL
Salutation
Honourable
Member picture
1253.jpg

First Name:
Dr. Wilbrod
Middle Name:
Peter
Last Name:
Slaa
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Karatu
Political Party:
CHADEMA
Office Location:
P.O. Box 119, Karatu - Arusha
Office Phone:
+255 784 666995
Ext.:
Office Fax:
+255 22 2668866
Office E-mail:
wslaa@parliament.go.tz
Member Status:
Current Member
Date of Birth
29 October 1948
EDUCATION
School Name/Location
Course/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
St. Thomas Aquinas University
Advanced Diploma in Rural Development
1980
1981
ADV DIPLOMA
TransWorld Tutorial College, London
Certificate in Management
1985
1985
CERTIFICATE
Kwermusl Primary School(Mbulu)
Primary Education
1958
1960
PRIMARY
Daudi Primary School
Primary Education
1961
1961
PRIMARY
Karatu Primary School
Primary Education
1962
1965
PRIMARY
Dung'unyi Seminary School
O-Level Education
1966
1969
SECONDARY
Itaga Seminary School
A-Level Education
1970
1971
HIGH SCHOOL
Kibosho Seminary School
Certificate in Philosophy
1972
1973
CERTIFICATE
St. Urban University, Rome
PhD (JCD) Law
1977
1981
PHD
Kipalapala Seminary
Certificate in Theology
1974
1977
CERTIFICATE
International Eye H. Centre
Certificate in Eye Health
1993
1993
CERTIFICATE
EMPLOYMENT HISTORY

JF Daima...:peace:


Kafungue kesi mahakamani wewe ni CCM utasikilizwa kwa kuwa ni Watanzania wengine wana jiuliza juu ya PhD za Nchimbi, Matayo , na mawiri kibao lakini serikali kimyaaaa
 
Huyo ndio rais wangu.. Makame na Kiravu walituwekea mtu dhaifu!

By the way... unatujazia server huu uzi upo mara nyingi sana humu
 
Hii topic tulijadili sana hapa mwaka jana Ritz, na nilidhani umeelewa. Na jitahada zilitumika sana kueleza elimu ya kanisa katoloki na utoaji wa vyeti wakati wa utawala wa Nyerere. Kama kuna mtu anaweza kuirejesha thread ya zamani naomba afanye hivyo.

NB: Hii topic umerudisha ghafla baada ya kuibuka uzi unaojadili CV/elimu ya Vicky Kamata. Sijui kwa nini unaona Dr Slaa wanatakiwa kujadiliwa katika level moja?
CV ya vick kamata? naona sasa mmeamua kuingia hadi jikoni . Laizma watoto wa baba wawe wakali
 
CV ya vick kamata? naona sasa mmeamua kuingia hadi jikoni . Laizma watoto wa baba wawe wakali

Siasa ngumu ndugu yangu na gharama za 'ueshimiwa' ni kubwa. kadhia tupu. Sasa tumeshambiwa hata mwaka wa kuzaliwa ni wrong.

NB: Umejaribu kutafuta hizo publications zake? Ningetaka sana kusoma hiyo ya microfinance kwa wanawake lakini nimefanya search sioni chochote!!!.
 
Ritz,

Kwa muda mwingi nimekuwa nikipuuzia post zako kwa sababu wewe mwenyewe umefanya iwe hivyo.

Hata hii nilitaka kupuuzia lakini nimeona nikushauri njia ambayo niliwahi kuitumia. Njia yenyewe ni hii.

Mimi ni mkatoliki. Ninapenda sana kujua mambo ya kanisa langu. Lakini kwa sababu sijawahi kupita Seminary nikadhani kufahamu mambo ya Kanisa langu ingekuwa rahisi kwa sababu mimi ni msomi na ninaelewa mengi.

Nilikwama. Kanisa Katoliki ukiliparamia ovyoovyo unaweza kuishia kuaibika kama inavyokutokea sasa. Labda uniulize ni kwa nini hapa duniani taasisi nyingi zikiwemo nchi kubwa zinaumbuka zinapolivamia Kanisa Katoliki kutaka kushindana nalo kwa hoja yoyote?

Jibu ni kwamba Kanisa katoliki ni taasisi pekee hapa duniani yenye umri mrefu kuliko taasisi yoyote. Hadi sasa ina umri wa miaka 2012.

Hivyo, usidhani kuna swali utalileta halafu Kanisa Katoliki likose majibu. Unaweza kukutana na mkatoliki ukakosa majibu lakini tatizo likawa ni huyo mkatoliki na si lenyewe kama Kanisa.

Ni kweli unaweza kuleta jambo humu JF na ukakuta wote wameshindwa kukujibu na wengine wakaishia kukutukana au kukukejeli. Mimi hao pia nawaonea huruma kwani ukweli ni kwamba majibu yako utashangaa kuona kwamba yalishatolewa miaka 500 iliyopita na wewe unarudia swali leo!

Mimi nilivyoona hivyo, nilicukua kama miaka mitatu najisomea tu mambo ya Kanisa langu. Ritz, nakujibu kiurafiki, kulielewa Kanisa Katoliki unahitajia uvumilivu wa hali ya juu kama umedhamiria kusoma mambo yake.

Mfano wa aibu mnazopata ni mwaka 2009 ambapo Waraka wa Kanisa ulitoka. Watanzania mlishangaa kana kwamba ni mara ya kwanza wakati waraka wa kwanza duniani ulitoka mwaka 1891 ukiitwa Rerum Novarum uliotolewa na Pope Leo XIII. Watanzania mkaaibika duniani kote kwamba ni washamba hawajui nyaraka za Kanisa Katoliki. Tena wakaaibika watu mashuhuri kama Kingunge!



Ona sasa topic unayoileta ya kuuliza Phd ya Dr. Wilbord Slaa. Ni wazi kwamba huelewei kwamba Kanisa Katoliki ndilo mama wa Sheria hapa duniani lakini kubwa zaidi Kanisa Katoliki ndilo mama wa mifumo ya elimu hapa duniani.

Ujerumani iliacha mwaka 1886 kukaguliwa sylabus na majesuit ambao ni mapadri wa Kanisa Katoliki ambao hapa nchini wanaendesha shule maarufu yaani Nyakahoja ya Mwanza na Loyola ya D'Salaam, St. Ignatius ya Dodoma na wamefungua Sekondari hapohapo Dodoma.

Uingereza nayo ilianza shule zake mapema kabla ya Ujerumani na ikafuata mfumo wake.

Lakini kote huko Kanisa likaendelea na mfumo wake mmja uitwao Licentiate au Licenciatura. Nenda kwenye website yoyote halafu soma kwa makini neno Licentiate ndipo utakuta mfumo waliosoma Dr. Slaa na wenzake wengi umejikita humo.

Hebu soma mfumo wa elimu wa nchi zifuatazo yaani Germany, Argentina, France, Australia, Canada, Belgium, Brazil, Bolivia, Costa Rica. Huko kuna vyuo wanafuata mfumo huu wa Licentiate. Huko kukuta mtu kamaliza Diploma halafu anapata Phd ndiyo maisha ya huko.

Sisi hapa Tanzania tuliamua kufuata mtindo wa Uingereza na hasa Oxford. Uingereza waliamua kubuni upya kabisa mfumo wa elimu.

Hivyo, Ritz na wenzako, unpouliza swali kama hili ni wazi kuwa inabidi ujikite maeneo ambayo ni wazi na wao upeo wao ni mdogo. Ungekuwa thread yako umeiandika kwa kiingereza na tukakutana kwenye anga za international threads na tunajadili mataifa mbalimbali ungeumbuka umbuko ambalo hutalisahau, kwani ni wazi wapo ambao wangeuliza umetoka nchi gani huelewi system hiyo ya Eductaion.

Mimi hata leo nikilichukia Kanisa Katoliki na nikaingia katika timu ya watu wanaolichambua kwa kuumbua mambo yake, basi ningekutana na nyinyi kisha nikawapa semina kwamba tubadili mbinu maana hizo mbinu zenu mtaishia kuumbuka tu.

Kawaulize waarabu ambao waliwahi kupiga kelele kuhusu Vatican kupewa ubalozi kwenye nchi kadhaa lakini jinsi wlivyozidisha kelele na wakikaa meza moja na Vatican wanajikuta na wao wanaishi kushawishika kufungua balozi nyingi kama Iran na kwingineko.

Waulize Russia ambako walikejeli sana Ubalozi huo na mwisho nao wakajikuta wanaufungua kwao. Wamarekani tangu mwaka 1871 walikataa ubalozi huo, wakajikuta mwaka 1994 wanaufunguwa kule Washington.

Leo wewe umeuliza swali kuhusu Phd. ya Dr. Slaa. Si mara ya kwanza unauliza hivi. NImesema ukisoma kuhusu Licentiate education system utajikuta umefunguka usichikijua na utashukuru Mungu kwamba unatumia ID ya jina la Ritz na hivyo aibu ya ushamba hutaipata maana hatukujui.

Soma tu utaelewa, document zipo tele. Ni kichwa chako tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom