CUF yatangaza kutoshiriki uchaguzi wa Arumeru Mashariki

CUF wanajua hata wakishiriki hawatashinda ubunge Arumeru mashariki... Kimsingi hiki chama kinaelekea kufa; hakikubaliki kwa wananchi..... wanachama wa CUF wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko nchini kwa kukiondosha madarakani chama cha magamba wajiondoe CUF haraka... Jiungeni na chama cha upinzani kinachokubalika zaidi kwa wananchi.

chama gani cha upinzani kinacho kubalika nchi nzima acha uzuzu. Bahati mbaya mnaongea pumba na kulopoka.sidhani hata kilwa chama hicho kipo hata msimu uliopita hakikusimamisha mgombea
 
CCM B imeona iachie CCM A kushiriki uchaguzi huo.....................hii ni aibu kwa chama kinachoanza kuchagua sehemu za kugombea je ni lini wataieneza CUF?

acha uzezeta na ubwege hata hao unaosema miaka yote huwa wana chagua mahala pa kugombea ni ccm pekee ndo haichagui. Hebu wa pelekeni cdm wakagombee huko kilwa msimu uliopita hawakusimamisha mgombea.
 
Igunga walishika nafasi ya pili mwaka 2010!Pia uzini walishika nafasi ya pili (Kumbuka kuwa nafasi ya uwakilishi CHADEMA haikushiriki mwaka 2010 ilishiriki ubunge wa JMT)!

cdm ilishiriki JMT ilishika nafasi ya ngapi? Nailipata kura ngapi? Huku cuf iliyoshika nafasi ya pili ilipata kura ngapi ktk nafasi ya uwakilishi?
 
umesoma ukaelewa? Mtatiro kasema wana utaratibu wa kutoshiriki uchaguzi mdogo ikiwa ktk general election walikuwa watatu! Uzini walikuwa wa ngapi?

uzini pia walikuwa wa3 na pia ni uchaguzi mdogo.labda hayo ni kwa bara tu...wajipange kutafuta mkiti na katibu wenye muelekeo wa siasa na si Hasa-Nilikuwa napita tu
 
Igunga walishika nafasi ya pili mwaka 2010!Pia uzini walishika nafasi ya pili (Kumbuka kuwa nafasi ya uwakilishi CHADEMA haikushiriki mwaka 2010 ilishiriki ubunge wa JMT)!

LKN kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2010 pia CUF walikuwa wa 3,kwa maneno ya Mtatiro ina maana CUF pia hawatashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutimiza maneno yao?
 
Swali langu kwa CUF ni kuwa wataacha kuiita CHADEMA chama cha kindugu cha Wachagga? sababu kilishiriki Uchaguzi wa UZINI na kupata kura 540 hao sio Ndugu Wachagga!!!

Sababu CUF kinapenda sana Masuala ya Chuki, kimejiondoa ARUMERU sababu ya matatizo yake ya MRENGO WA CHUKI hakuna sababu nyingine... huko ARUMERU hakuna watu watakao shabikia CHUKI...
 
Hizi chaguzi kila siku zinatugharimu Watz. mamilioni kama sio matrilioni ya shilingi. Ni bora jimbo libaki wazi mpaka uchaguzi mkuu na fedha hizo zitumike kwenye mambo mengine ya muhimu zaidi. Tunao zaidi ya wabunge 300 wakuhangaikia posho zao tu!
Ni serikali ipi mkuu, yenye uwezo wa kutumia fedha hizo kwenye mambo muhimu? ..Waache kulipana posho? ..Safari za nje je?

..Kununua kofia na tshirt za kijani je?
 
Kila mmoja na kiwanja chake CUF wameona Arumeru sio kiwanja chao ni vizuri kujitambua.

Tusubiri Dr Mrema na TLP nae sijui hatakuja na kauli gani, pamoja na NCCR Mageuzi.
 
Naibu katibu mkuu wa CUF Mtatiro ameongea na waandishi na kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa Arumeru mashari kwa sababu kwamba wanautaratibu wa kutoshiriki uchaguzi mdogo ambapo walikuwa namba tatu uchaguzi mkuu uliopita.Hata hivyo Mtatiro ametangaza kuwa CUF itaunga mkono chama cha chochote cha upinzani chenye nia ya dhati ya kumsadia mtanzania wa Arumeru.
hawana jipya, wakae nje wawe watazamaji 2
 
sasa kama ndio hivyo kumbe na hata 2015 hawatashiriki general election kwasababu walikuwa watatu!

Umeniwahi "Principal", hawa CUF lazima watekeleze maagizo yote, halali na haramu toka kwa Mume wake. Ikifika 2015 watakuja na visingizio vingine-lazima walambe matapishi yao!
 
LKN kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2010 pia CUF walikuwa wa 3,kwa maneno ya Mtatiro ina maana CUF pia hawatashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutimiza maneno yao?

Mkuu unajua maana ya uchaguzi mdogo na General election?Mtatiro amesema uchaguzi mdogo wakishika nafasi ya tatu hawagombei sasa hiyo 2015 tena General Election still unajifanya hujui?Uchaguzi mdogo ni ule unaojitokeza kipindi kisichokuwa rasmi cha uchaguzi labda kufuatia kufa kwa kiongozi husika au Kujiuzulu au kukosa sifa za kuongoza eneo husika kwa wakati huo!Kwa maana hiyo hiyo 2015 hata Arumeru CUF watasimamisha mgombea maana huo hautaitwa uchaguzi mdogo!!

NB!Mimi si shabiki wa siasa wa chama chochote na sijawahi na sijafikiria bado kupiga kura maana mpaka sasa naona siasa za bongo ni za kuganga njaa tu!Lakini najaribu kukuelewesha maana ya kauli ya Mtatiro!!
 
cdm ilishiriki JMT ilishika nafasi ya ngapi? Nailipata kura ngapi? Huku cuf iliyoshika nafasi ya pili ilipata kura ngapi ktk nafasi ya uwakilishi?


CDM ilishika nafasi ya pili UZINI kwenye nafasi ya mbunge JMT!!Mkuu kukalili idadi ya kura kwangu huwa ni ngumu sana mimi huwa naridhika kujua nafasi ya chama au mgombea husika sehemu fulani,Nina imani hata wewe nikikuuliza KIKWETE,SLAA & LIPUMBA walipata kura ngapi uchaguzi mkuu wa 2010 itakuwa vigumu kwako kutoa jibu la haraka!!Lakini unaweza tembelea tovuti ya tume ya uchaguzi kupata detailed information!!
 
Back
Top Bottom