CUF yataka serikali tatu

DSC_0351.JPG

Na Oscar Samba, AJTC
WAKAAZI wa Muyuni wilaya ya Kusini Unguja wamesema kuwa ni vyema katiba mpya ya Tanzania ikaainisha uwepo wa serikali tatu ili kuondokana na kero za Muungano zilizopo hivi sasa.
Wananchi hao walieleza hao jana huko Muyuni, wakati kamati ndogo ya Tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya ilipofika kijijini hapo.
Walisema kuwa kumekuwepo na kero nyingi za Muungano ambazo zimekuwa kilalamikiwa na kila upande, hivyo uwepo wa serikali tatu itazifanya kero hizo ziwe historia kwani kila upande utashughulikia mambo yake na yale ya Muungano kushughulikiwa na serikali hiyo.
Kwa upande wake Pandu Issa Pandu alipendekeza uwepo wa serikali tatu ikiwemo kurudi kwa serikali ya Tanganyika, Zanzibar na serikali ya Muungano ambayo itakuwa ndio msimamizi mkubwa wa Serikali zote mbili.
''Ninapendekeza tuwe na serikali tatu yaani ya serikali ya Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa ndio msimamizi wa serikali zote mbili na hizo mbili ziwe huru na zijitegemee kwenye mambo yake ya ndani'', alisema Pandu Issa Pandu (43).
Kero za Muungano zimekuja na kuongezeka siku hadi siku kutokana na kutoweka kwa Serekali ya Tanganyika yenye kusimamia mambo yake yasio ya Muungano.
Aidha ambali ya kujitokeza maoni hayo pia wapo wananchi wa shehia hiyo waliopendekeza Rais wa Zanzibar awe na madaraka kamili kuliko ilivyo hivi sasa.
Walisema mfumo uliopo hivi sasa unafanya kuonekana Tanzania kuwe na rais mdogo na rais mkubwa, hivyo Rais wa Zanzibar apewe mamlaka kamili.
Wananchi hao pia walitaka mfumo wa mambo ya nje ubadilike utoe nafasi kwa Zanzibar nayo kutambulikana nje, hali inayoifanya kuweza kunufaika zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
Naye Mwalimu Shukuru Ramadhani (28), akitoa maoni yake alisema suala la elimu ya juu lifutwe kwenye mambo ya Muungano kwani Zanzibar hainufaiki nalo.
''Tunataka suali la elimu ya juu lisiwe la Muungano na wizara ya Elimu ya Zanzibar iwe na Baraza lake la Mitihani, kwani tunahisi hatutendewi haki na Baraza la Elimu juu liliopo hivi sasa la Muungano'', alisema Mwalimu Shukuru Ramadhan.
Suali la elimu ya juu pia lilichangiwa na wanafunzi wa skuli ya Muyuni ambapo walitaka suala la elimu lienguliwe kwenye mambo ya Muungano, huku wakieleza kuwa NECTA inawadhulimu.

Serikali moja tu ndio suluhu ya kweli. Ikiwa Tanganyika kama State itaiuzia State dada ya Zanzibar umeme kwa bei ya Export huoni Zanzibar umeme utapanda? Mikoa mingi sasa ya bara haina umeme lakini Zanzibar umeme Buheeri saa zote, unadhani State ya Tanganyika itakuja kubali tena?
 
Hatutaki muungano, hatamkingangania vipi, na propaganda zenu za kidanganyika hazina nafasi. Chukueni umeme wenu kama mna ubavu kwa sababu mnafikiri mnatupa bure" tunalipa" Kazi yenu kuuwa vikongwe na walemavu na ufisadi juu ndio maana hamna umeme maeneo mengi ya Danganyika.Jamuhuri ya watu wa Zanzibar kwanza.
 
Mbona hizi habari hatuzisikii kutoka upande wa tanganyika ,Za zanzibar zinatangazwa kama mpira ama kweli zumari ikipulizwa Zanzibar walio maziwa makuu huhemkwa !
 
Mi na support kuwepo na serikali ya tanganyika kwa sababu sehemu nyingi zetu zinazorota kwa sababu hii serikali ya muungano haifuatilii vizuri. Mfano tukiwa na waziri wa afya ambae ni mzanzibari mnafikiri atajali maslahi ya daktari wetu au wakigoma yeye atajali vipi wakati anajua ndugu zake wako zanzibar wanapata huduma ya afya kama kawaida. Kwanini wizara zetu zinazoshuhulikia mambo ya bara zinapewa mawaziri kutoka zanzibar. Ushasikia mbara anapewa uwaziri kwenye serikali ya mapinduzi? Tushachoka kuonewa sasa zanzibar ni nchi kabisa ina kila kitu cha kuwawezesha wao kua nchi.. Huu muungano uko on paper tu bt realistically theres no such thing as muungano. Nchi moja ina marais 2 makamu wa rais watatu baraza la mawaziri mawili ushawahi kusikia wapi kitu ka hicho.
 
..serikali 3 is not the answer.

..huyo aliyependekeza serikali 3 hajui implications za hicho anachopendekeza.

..kukiwa na serikali ya muungano itakayosimamia serikali za TGK na ZNZ kutapelekea raisi wa muungano kuwa na madaraka juu ya maraisi wa TGK na ZNZ.

..pia tukumbuke kwamba ZNZ tayari ina serikali, ni TGK ambayo haina serikali. katika mfumo wa serikali 3 kitakachoongezeka, au kubadilika, ni TGK kuwa na serikali yake yenye mamlaka na majukumu kama iliyonayo serikali ya ZNZ iliyoko sasa hivi. kwa upande wa serikali ya ZNZ sidhani kama kuna kitakachoongezeka.

..kwa mtizamo wangu, serikali 3 does not solve matatizo ya muungano wetu. zaidi haitakidhi matamanio waliyonayo wa-ZNZ ya kuwa na mamlaka kamili ya kisiasa,kiuchumi,kijamii, na kiutamaduni.

..hatutaki serikali 3, hatutaki mkataba, LET ZANZIBAR GO!!!

NB:

..kuhusu baraza la mitihani, ZNZ wawe makini.

..muelekeo uliopo sasa hivi ni kuwa na mfumo mmoja wa elimu kwa nchi za AFRIKA MASHARIKI.

..kwa msingi huo sylabus, pamoja na baraza la mitihani, vitakuwa chini ya EAC.
 
Joka kuu, yaani nacheka sana nikisoma habari za WZNZ
Wanataka serikali 3, halafu hawataki mambo ya nje yawe ya muungano
Wanataka NECTA yao hawajui hawana bajeti ya elimu ya juu

Wamefundishwa serikali 3, masikini wanaimba tu hawajui hizo 3 ziweje na kwanini.

Hakuna serikali 3
Hakuna Mkataba
Hakuna mahusiano ya EU
Hakuna muungano wa Swiss (Mwanasheria wa Visiwani) Kwi kwi! mbavu zangu

Sasa wanaogopa kusema vunja muungano! nafasi hiyooo, wanarudi nyuma

LET ZNZ GO!
 
Huku kuwa na mfumo wa mmoja kwa Nchi zinazoifanya EAST AFRICA ni kutaka kuibiaana na hivi hamjui kuwa hadi hii leo Tanzania haijatia saini mambo haya, Kama mnataka kutawaliwa na mafisadi haya endelezi ujuaji wenu wa kuikataa Tanganyika.

Hamkumbuki nin kilitokea na kuvunjika umoja wa East Afrika ,wengine hadi hi leo hawajalipwa ,wangapi walipoteza mali zao .
 
hapo mwiba nakuunga mkono tanganyika irudi!
 
Sasa wanaogopa kusema vunja muungano! nafasi hiyooo, wanarudi nyuma

LET ZNZ GO!

Aloo hakuna anaegopa kuvunja Muungano zaidi ya WaTanganyika (Viongozi) ,tena wala usitie shaka na kuwa na wasiwasi hebu leo hii fanyeni maandamano kuidai Tanganyika muone Zanzibar kutatokea nini ? Unafanya mchezo Zanzibar wana uzalendo na hawaoni aibu kutamka kuwa wanataka nchi yao wajiendeleze kivyao , hebu jaribuni kidogo tu kwa maandamano au kama alivyowamegea Mheshimiwa Tundu Lissu ,changamkieni tenda ya kuwepo Tanganyika sio mnababaika humu JF na kujidai ushujaa wa mshumaa , WaZanzibari wameshaanza kuicheza hii ngoma ya kuikataa Muungano mmebaki ninyi mnasuasua humu JF ,mboni hao viranja wenu hawathubutu kusema kama mnavyosema humu ! WaTajuta !
 
Huku kuwa na mfumo wa mmoja kwa Nchi zinazoifanya EAST AFRICA ni kutaka kuibiaana na hivi hamjui kuwa hadi hii leo Tanzania haijatia saini mambo haya, Kama mnataka kutawaliwa na mafisadi haya endelezi ujuaji wenu wa kuikataa Tanganyika.

Hamkumbuki nin kilitokea na kuvunjika umoja wa East Afrika ,wengine hadi hi leo hawajalipwa ,wangapi walipoteza mali zao .

Mwiba,

..EAC inaiga mambo ya European Union na wanapata msaada na ushauri toka huko.

..pia hujasikia wa-ZNZ wanapendekeza "muungano wa mkataba" ambao utafanana na EU??

..suala kubwa ambalo Tanzania haijakubaliana nalo ktk EAC ni ardhi, mengine tumekubali.

..pia wa-ZNZ waelewe kwamba "UHURU" wanaoutaka hautapatikana hata ktk "muungano wa mkataba" unaofanana na EU.

..hebu chukulia suala kama la SARAFU ambalo ni prominent ktk "muungano wa kimkataba" wa EU. Tanganyika inaweza kuamua ku-devalue sarafu halafu ZNZ mkaingia ktk mtikisiko mkubwa wa kibajeti na kiuchumi.
 
serikali tatu itazifanya kila upande utashughulikia mambo yakena yale ya Muungano kushughulikiwa na serikali hiyo.
Ukishasema kila upande uwe na serikali yake ili kila upande ushughulikie mambo yake, utasemaje tena uwe na serikali ya Muungano kushughulikia mambo ya Muungano? Mambo ya Muungano yepi tena???

Serikali tatu itaturudisha hapa hapa tulipo kwa sababu huko huko kwenye serikali ya Muungano tutaanza kugombania mipaka ya kipi ni chako kipi ni changu.

Tunataka kila upande uwe ni"dola huru yenye mamlaka yake kamili."
 
Kwakuwa sasa sote tunaangalia mbele kwenye oshirikisho la Africak mashariki, sioni kwanini haka kamuungano uchwara kasifie mbali, ili kila nchi iwe na nafasi ya kujipeleka yenyewe huko kwenye hilo jitu EAC. Kuendelea kujadili kero zetu ndani ya muungano na ndani ya EAC nadhani ni kama kujiambukiza kipindupindu vile! ZNZ ipewe nafasi yake iwe huru!
 
Mie wasi wasi wangu ni jinsi watakavyo tally maoni ya wananchi, manake hapo kwenye picha naona kila mtu ana plain writing pad yake, namna nzuri ya kukusanya maoni yanayotolewa kwa focus group method unakuwa na mambo muhimu na unatatick kila mtu anapojata na kuandika wazo jipya. Pili ni kuredoki na kuja kusikiliza baadaye. Njia zote mbili hutumika ili kupata kitu kinachoitwa "meaning of the speaker and meaning of the word"
 
Sisi tunataka Zanzibar huru yenye mamlaka kamili.Nyinyi mkibaki na hilo jina la Tanzania,au lile mnalolichukia Danganyika, we don't really care. Jamuhuri ya watu wa Zanzibar Kwanza shengesha baadae.
 
Zanzibar tunataka tupumue, tuwe kivyetu.....hatutaki muungano wala EAC.Kama ikibidi ujirani mwema wala sio lazima
 
Aloo hakuna anaegopa kuvunja Muungano zaidi ya WaTanganyika (Viongozi) ,tena wala usitie shaka na kuwa na wasiwasi hebu leo hii fanyeni maandamano kuidai Tanganyika muone Zanzibar kutatokea nini ? Unafanya mchezo Zanzibar wana uzalendo na hawaoni aibu kutamka kuwa wanataka nchi yao wajiendeleze kivyao , hebu jaribuni kidogo tu kwa maandamano au kama alivyowamegea Mheshimiwa Tundu Lissu ,changamkieni tenda ya kuwepo Tanganyika sio mnababaika humu JF na kujidai ushujaa wa mshumaa , WaZanzibari wameshaanza kuicheza hii ngoma ya kuikataa Muungano mmebaki ninyi mnasuasua humu JF ,mboni hao viranja wenu hawathubutu kusema kama mnavyosema humu ! WaTajuta !
Nadhani umeijibu hoja ya Wazanzibar wengi tu ya kwamba kama kweli Tanganyika inaitawala Zanzibar basi Maandamano ya Zanzibar yangekuwa kasheshe lakini siku zote mnaandamana vizuri tu. Na hata mkizuiwa mnazuiwa na serikali lya Mapinduzi..

Jambo lolote kubwa linalotokea Zanzibar linahusu uchaguzi wa Zanzibar kwa mfano Maalim Seif na Karume mwaka 2000 Na sio sababu ya Lipumba kugombea Urais wa Jamhuri. Baraza la Mapinduzi linaitaka serikali ya muungano kuingilia maswala ya Zanzibar hapo ndipo utaona machogo tunaingia Zanzibar na bia nyie wenyewe kuelewa mnawapa sababu baraza la Mapinduzi kuendelea kushika utawala japokuwa leo chaguzi zenu kuna vyama vingi.

Sisi huku bara wala haitukereki kuwepo na muungano au laa hatujali kabisa maana vita yetu sisi ni utawala wa CCM. Tunapambana na chama ktk mahitaji yetu muhimu zaidi kama Umeme, Maji, Umiliki wa ardhi, Elimu na Afya maana pasipo haya juhudi na nguvu zetu kujaza pakacha zinapotea buree. Kifupi Wazanzibar wooote hamieni bara mtapokelewa na kuishi bila kuguswa maana chetu chenu vile vile.

Serikali tatu ni muhimu zaidi ktk kushinikiwa kuvunjika kwa muungano hivyo nadhani bora tuanze na hilo nina hakika pande zote mbili zitakuwa na sababu nzuri zaidi ya kuuvunja muungano..
 
Aloo hakuna anaegopa kuvunja Muungano zaidi ya WaTanganyika (Viongozi) ,tena wala usitie shaka na kuwa na wasiwasi hebu leo hii fanyeni maandamano kuidai Tanganyika muone Zanzibar kutatokea nini ? Unafanya mchezo Zanzibar wana uzalendo na hawaoni aibu kutamka kuwa wanataka nchi yao wajiendeleze kivyao , hebu jaribuni kidogo tu kwa maandamano au kama alivyowamegea Mheshimiwa Tundu Lissu ,changamkieni tenda ya kuwepo Tanganyika sio mnababaika humu JF na kujidai ushujaa wa mshumaa , WaZanzibari wameshaanza kuicheza hii ngoma ya kuikataa Muungano mmebaki ninyi mnasuasua humu JF ,mboni hao viranja wenu hawathubutu kusema kama mnavyosema humu ! WaTajuta !
Kwani anayedai kuwa koloni ni mtanganyika au mzanzibar? Tunasema hivi kama mnahisi mumeonewa sana na hakika mnahisia hizo, tamkeni mbele ya tume kuwa hamtaki muungano.

Mnaposema tuwe na mkataba kama wa Swiss(mwasheria wa unguja) kwi kwi! semeni mambo gani mnataka yawe ya mkataba?

Huyo aliyesema iwepo Tanganyika, nashangaa maana Tanganyika ikirudi hapo mtapoteza hata kidogo mlicho nacho.
Mkisema mkataba wa EU tunauliza wa mambo gani?
Sasa hivi Zbar ikijiunga na EAC kama nchi pekee itapoteza mambo mengi sana! hakuna nchi itakayokubali ubaguzi mnaowafanyia Watanganyika.

Tunachotaka kusema hapa ni kuwa tume hiyoo! sasa wekeni madumu ya mafuta na petroli pembeni Ongeeni hoja! ZNZ haitaki muungano, huku kumung'unya maneno ya mkataba wa Uswiss(mwanasheria wa BLW) ni upuuzi!

Tanganyika ikirudi kama alivyosema Mkandara muungano umekufa na ZNZ haitapata makataba wa Uswiss, Uchina, EU n.k
Lakini pia wanaotakiwa kudai Tanganyika wapo kimya! ninyi koloni mnawataka wadai wakati wao wana koloni!

Kelele zote sasa kimyaa! ukweli unadhihiri

LET ZNZ GO!
 
..serikali 3 is not the answer.

..huyo aliyependekeza serikali 3 hajui implications za hicho anachopendekeza.

..kukiwa na serikali ya muungano itakayosimamia serikali za TGK na ZNZ kutapelekea raisi wa muungano kuwa na madaraka juu ya maraisi wa TGK na ZNZ.

..pia tukumbuke kwamba ZNZ tayari ina serikali, ni TGK ambayo haina serikali. katika mfumo wa serikali 3 kitakachoongezeka, au kubadilika, ni TGK kuwa na serikali yake yenye mamlaka na majukumu kama iliyonayo serikali ya ZNZ iliyoko sasa hivi. kwa upande wa serikali ya ZNZ sidhani kama kuna kitakachoongezeka.

..kwa mtizamo wangu, serikali 3 does not solve matatizo ya muungano wetu. zaidi haitakidhi matamanio waliyonayo wa-ZNZ ya kuwa na mamlaka kamili ya kisiasa,kiuchumi,kijamii, na kiutamaduni.

..hatutaki serikali 3, hatutaki mkataba, LET ZANZIBAR GO!!!

NB:

..kuhusu baraza la mitihani, ZNZ wawe makini.

..muelekeo uliopo sasa hivi ni kuwa na mfumo mmoja wa elimu kwa nchi za AFRIKA MASHARIKI.

..kwa msingi huo sylabus, pamoja na baraza la mitihani, vitakuwa chini ya EAC.

Hayo maoni kajipange usubiri hilo tume utawaelezea.
 
Back
Top Bottom