CUF yapeleka wafuasi Arusha na mabasi kutoka Dar

wakodi hata behewa 20 za train kwenda Arusha! wataisoma namba ya M4C! MKE KAPEWA MAJUKUMU NA NI LAZIMA ATII LA SIVYO ATATALAKIWA, wanajua kuna vimwana vingine vinanyemela kuolewa na nyinyiem, kwa hiyo inabidi wajitume vilivyo. Mme kaacha hela ya manunuzi, mke anapaswa kwenda kufanya manunuzi
 
Kuna uwezekano wanakwenda kufanya fujo. Si tumeambiwa kuna mkakati wa kutumia CUF kuleta fujo kwenye mikutano ya Makamanda ili kupata sababu ya kusitisha M4C?

Mkutano wa Lissu unaweza kuwa lengo la kuingia gharama kubwa kupeleka wapiganaji wa CUF Arusha. Tuwe macho.
 
Inawezekana malori yatabeba watu kutoka Tanga.
 
Kuna uwezekano wanakwenda kufanya fujo. Si tumeambiwa kuna mkakati wa kutumia CUF kuleta fujo kwenye mikutano ya Makamanda ili kupata sababu ya kusitisha M4C?

Mkutano wa Lissu unaweza kuwa lengo la kuingia gharama kubwa kupeleka wapiganaji wa CUF Arusha. Tuwe macho.

Nadhani viongozi wa Arusha mnaona huu ushauri.Fanyieni kazi.
 
''Tunakwenda kumpokea Profesa wa Ukweli!!

Atatua kesho KIA akitokea ulaya alikokwenda kutatua mdodoro wa sarafu ya Ulaya.

Somo la Igunga hatukuelewa vizuri ngoja tujaribu Arusha mjini huenda tukabahatika''
 
Hapa Mlandizi nimeshuhudia wakipakia vijana kuelekea Arusha ndani coaster yenye bendera za cUF
 
Katika kuficha aibu kesho na kuiongopea dunia kwamba kinaungwa mkono Arusha,chama cha wananchi-CUF kimepeleka maelfu ya wafuasi wake kutokea Dar kwenda Arusha.Kwa mujibu wa shuhuda wetu amekutana na msururu wa mabasi yapatayo saba-7 yakiondoka Ubungo huku yakipambwa bendera za CUF na nyimbo za hamasa za wafuasi hao.
Wachunguzi wa siasa wanasema ni aibu kubwa kwa chama kusafirisha wafuasi umbali wa mwendo wa saa 10 kisa kujaza uwanja na kuhalalisha hila chafu dhidi ya vyama vingine.

Source:Facebook Wall Page-Mwasiwelwa Perfect.

Tatizo la CDM ni kile waswahili wanachosema 'Kijiba cha roho' kwani wanapoona wenzao wamefanikia basi wao huwauma sana, huu ni ushadadiaji sana wa siasa bila kujua maana yake ni nini. CDM kila sehemu wanataka wao waonekana ni vinara , hata pale pasipo stahiki mfano misibani na makanisani. Km na cuf na wao wamekubalika arusha shida iko wapi? hii thread imekaa kimajungu, fitna, jazba na kimagumashi zaidi. Nenda kajipange upya , jana mmefanywa vibaya mza leo mmeanza mengine tena

Waje na watu wakufanya fujo, wawape bendera na gwanda za cdm ili kesho magazeti yauze na Tendwa aongee!
 
''Tunakwenda kumpokea Profesa wa Ukweli!!

Atatua kesho KIA akitokea ulaya alikokwenda kutatua mdodoro wa sarafu ya Ulaya.

Somo la Igunga hatukuelewa vizuri ngoja tujaribu Arusha mjini huenda tukabahatika''

Hongereni sana.
 
Ni maajabu lakini ni kweli, mabasi zaidi ya 10 aina ya coaster, yakiwa yamepambwa kwa bendera za CUF, nayakiwa yamejazwa kwa level seat wanachama wa CUF, yameondoka Dar kuelekea Arusha hivi leo.

My take: siasa za komedi zimeanza. Kama mapokezi makubwa ya Lipumba arusha yanahitaji wanachama kutoka Darkwenda Arusha kwa mamia, hapo ujue kuna mushkeli.

Source: mimi mwenyewe nipo njiani natoka Tanga kwenda Dar,nimekutana nayo, nimeyahesabu hadi nimeshindwa. Nimewauliza baadhi ya wanachama hao katika gari moja lililokuwa limesimama iliabiria wachimbe dawa. Wamenijibu kwamba wanakwenda kuwaonyesha watu wa Arusha maana halisi ya 'Ngunguri'... Hata hivyo baada ya kuona scaff ya CHADEMA kwenye gari yangu, walianza kunirushia matusi ya nguoni.a
 
Back
Top Bottom