Cuf yaomba kuwasilisha bajeti kivuli ya upinzani baada ya ile ya chadema kuitwa rubbish

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Kutokana na mjadala unaoendelea Bungeni juu ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2012-13, Wabunge wa chama cha wananchi CUF wamemuomba Spika akiruhusu chama hicho kuandaa bajeti kivuli ya upinzani, baada ya ile iliyoandaliwa na Chadema kufananishwa naa rubbish, garbage na takataka kwani imeandaliwa hovyo hovyo na hivyo kukosa hadhi ya kuwa bajeti kivuli. Wabunge hao wamesema Chama chao kinamtalaam namba moja wa uchumi barani Africa na Dunia Prof Lipumba ambaye anaweza kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wachumi na watalaam wengine wa fani mbalimbali.

Toa maoni yako juu ya ombi hilo la CUF la kuandaa bajeti kivuli baada ya makamanda uchwara kushindwa kufanya hivyo
 
Nlitegemea waisaidie serikari kuleta bajeti nzuri. Kwani cuf nao ni wapinzani? Si ni ccm B?
 
sasa wajameni kwel ccm watakubali kuwa bajeti ya chadema ni nzuri? Au cuf nao wana vijimambo vyao ? Bajeti ya chadema ni nzuri sana na ccm lazima wakubaliane na hilo
 
mi huwa watu wa cuf wananishangaza sana hv chama kina watu wawil tu lipumba na seif? kila kitu wanaona wao wazzur . kwny mchang wake sikuona chocht cha maana amechangia ameishia kwny sm kisa yeye anatumia milion . kwny bajet kunaanishwa vyanz vya mapato kwny mchango wake hakuanisha chcht mbadala na kopi ya hiyo bajet anayo. sidhan kama hata anaelewa au alidhan ni kusoma tu pale mbele
 
Kutokana na mjadala unaoendelea Bungeni juu ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2012-13, Wabunge wa chama cha wananchi CUF wamemuomba Spika akiruhusu chama hicho kuandaa bajeti kivuli ya upinzani, baada ya ile iliyoandaliwa na Chadema kufananishwa naa rubbish, garbage na takataka kwani imeandaliwa hovyo hovyo na hivyo kukosa hadhi ya kuwa bajeti kivuli. Wabunge hao wamesema Chama chao kinamtalaam namba moja wa uchumi barani Africa na Dunia Prof Lipumba ambaye anaweza kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wachumi na watalaam wengine wa fani mbalimbali.

Toa maoni yako juu ya ombi hilo la CUF la kuandaa bajeti kivuli baada ya makamanda uchwara kushindwa kufanya hivyo

Wakaiwasilishe Zanzibar kwenye baraza la wawakilishi la uamsho, huku bara siyo sehemu yake.
 
labda wabadilishe kanunui tena, halafu kwa nini wasiombe watoe ya ccm then waandike wao kwani hiyo ndo imejaa madudu matupu
 
Cuf inamtegemea mtu mmoja tu kwenye uchumi akifa kwisha habari Yao Pamoja na kuwepo kwake pia cuf na ccm na viongozi wao ni DHAIFU
 
Uchumi ni taaluma aliyonayo mtu kutokana na elimu aliyopata, na uongozi ni kipaji pamoja na kwamba ni lazima kinolewe kwa mafunzo na experiences mbalimbali. Hoja yangu hapa ni kwamba, Lipumba anaweza kuwa mchumi bora lakini akawa kiongozi mbovu. Uongozi anaouonyesha kwenye chama chake ni ishara tosha kwamba atakapoiongoza Tanzania je itafanikiwa au la. Halafu kama bajeti ya Chadema imeitwa "rubbish" wasidhani kama ya cuf itatukuzwa na CCM labda ifanane na ile ya CCM kwa 100%
 
Tunasubiri kwa hamu bajeti kivuli ya CUF.

Lipumba yuko Dodoma na alifanya kikao na wabunge wa CUF na kuwaelekeza kukataa bajeti ya serikali itapendeza wakaja na bajeti yao ili tuweze kupima ubora wake dhidi ya ile ya serikali..... mkono mtupu haulambwi.
 
Wakaiwasilishe Zanzibar kwenye baraza la wawakilishi, ili tuone kama kweli n wapinzani au CCM B:flame:

kuwa CCM - B hakuondoa dhana ya uwajibikaji kwa taifa..... ni vema tukawapa ruksa CUF kuleta bajeti yao yamkini wataonyesha kuwa wao sio CCM - B kwa kila jambo.
 
Ruksa, wakiwasilishe kwenye bunge la kisiwandui.

Kisiwandui waliwakilisha kuhusu maoni ya muungano, wanataka muungano upigiwe kura suala ambalo linaonyesha kuwa wao CUF sio CCM - B kwa mambo yote. Tuwape fursa wanaweza kuwa na bajeti mbadala inayoweza kujadiliwa hapa JF na kutufanya tukasonga mbele.
 
Ni kweli Bajeti ya upinzani ni dhaifu sana...bora CUF nao walete yao tuone.
 
Back
Top Bottom