CUF yamjia juu Edward Lowassa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

Na Grace Ndossa

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema hakuna sababu ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, kukaripia vyombo vya
habari na madai ya kuwaonea huruma Watanzania na kuwalaumu wenzake wakati na yeye ni sehemu ya matatizo yao.

Pia CUF imesema Bw. Lowassa hana sababu ya kulaumu umaskini wa Watanzania bali ashauriane na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wenzake namna gani waache maslahi binafsi na kutetea Mtanzania mnyonge anayeteseka kwa matendo yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge wa CUF, Bw. Shaweji Mketo, ilieleza kuwa chama hicho kinamtaka Bw. Lowassa kutafakari utendaji wake kabla ya kujiuzulu uwaziri Mkuu.

Taarifa hiyo ya CUF iliseleza kuwa, Bw. Lowassa anajifanya kuwa na uchungu na matatizo yanayowakabili Watanzania wakati yanasababishwa na chama chake naye ni mhusika, hivyo dawa ni kukaa pamoja kuangalia jinsi ya kuyatatua.

Ilieleza kuwa Bw.Lowasa alikuwa kwenye serikali ya sasa kabla ya kujiuzulu na kwamba hadi sasa ni kiongozi muhimu ndani ya CCM kama mjumbe wa vikao vya juu vya chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Monduli hivyo matatizo ya Watanzania wanayowapata hivi sasa na yeye ni mmoja wapo kati ya watu waliochangia.

Chama hicho pia kilihoji sababu ya viongozi wa CCM ambao hawapo madarakani kwa sasa kujitokeza kukosoa mambo mbalimbali na kutoa mfano wa siku ya maadhimisho ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

"Mfano amesikika mkongwe wa CCM, Bw. Kingunge Ngombale-Mwiru alipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mwalimu Nyerere akiikaripia CCM akiitaka ifuate misingi ya azimio la Arusha na mfumo wa CCM aliyoiacha mwalimu Nyerere," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya CUF.

Taarifa hiyo ilisema CCM inajitahidi kuitumia Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kama njia ya kuonesha kwamba wanavijana makini kama vile Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Bw.Ole Millya, aliyewarubuni Watanzania kuhusu uhalisia wa chama hicho.

Ilieleza kuwa tatizo la CCM ni mfumo wa chama hicho unaotengeneza viongozi wanaopatikana kwa fedha na kwa kuzingatia maslahi ya mtu na mtu ama mtandao kwa mtandao na kwamba haiwezi kujirekebisha na kuwa chama cha kuwasaidia Watanzania kuvuka kutoka kwenye umasikini.

"CCM ilizaliwa, ikakua, imezeeka na sasa inaelekea kufa, kwa hiyo CUF inawataadharisha Watanzania kwamba wasije wakadanganyika na vituko vya kauli zinazotolewa na baadhi ya wana CCM kwa lengo la kuhakikisha inabaki madarakani,"ilieleza taarifa hiyo.
 
cuf hawa nao wamepoteza mwelekeo kabisa! inshu ya meli ilikuwa nzito ndo wangetolea kauli sio hili la Lowassa kuitisha press kisha kuishia kupiga porojo tu na vitisho
 
Wapemba wamekufa zaidi kwenye ile meli .KAFU mko serikalini na mna waziri anaye husika moja kwa moja .Mwenye meli ni Kada wa CCM , je taarifa yenu kwa vyombo vya habari kuhusu lile iko wapi ? Mmefikia wapi na issue ile ?

Ishawahi kusikia mke anamshtaki mume wake na kumfungulia kesi? Labda awe hayupo tayari kuendelea na hiyo ndoa.....
 
Lakini nyie si mke na Mume! Kwanini ushauri kama huu msipeane chumbani? Sie hatuna haja ya kuusikia ushauri mnaopeana wa kijinga humu jamvini.
 
KAFU wanatuzuka ndiyo namna yao hawa.Kwani Igunga mlionaje ? Hakuna kitu hawa .Wakatoe matamko kule Zenji kwanza juu ya Meli ndiyowaje kwa Lowasa wao si Chama tawala ?Au ni threat sasa huyo lowasa kwa mlo wenu ?
 
Wapemba wamekufa zaidi kwenye ile meli .KAFU mko serikalini na mna waziri anaye husika moja kwa moja .Mwenye meli ni Kada wa CCM , je taarifa yenu kwa vyombo vya habari kuhusu lile iko wapi ? Mmefikia wapi na issue ile ?

Na wengi wa waliokufa ni wapiga kura wapemba wa CUF, kwa hiyo itakapofika 2015 CUF kura zenu hazitatosha na ndiyo itakuwa mwisho wa muafaka ndoa itavunjika, kazi mnayo
 
Mambo ya ndoa magumu.Nasikia wameandikiwa na Nepi hilo tamko wakasaini tu.Vita ya makundi magamba.
 
Muafaka umevunjika? waache usanii hawa CUF chama ambacho ni kitengo cha magamba.
 
Ndoa bado changa,hawajajuana tabia vizuri,wataelewana tu,tucje tukaharibu bure ndoa yao!
 
Seif Sharif Hamad keshaolewa uko ZNZ, hamuoni siku hizi yupo very smart jamani? Ananyoa ndevu, ananyoa nywele, anapika, anaosha vyombe, anafua nguo.
 
Back
Top Bottom