CUF wazidi kuiandama CHADEMA

Wala siwashangai hawa CUF, wao wanadhani kwa kuishambulia CHADEMA ndio watapata umaarufu kumbe ndio Watanzania wengi tunazidi kuwaona wasanii tu/Magamba B.
 
..hao wamegoma tu kumuelewa Tundu Lissu.

..Lissu anatetea jambo lilelile ambalo CUF wamekuwa wakipigia kelele miaka mingi, nalo ni kurudishwa kwa serikali ya Tanganyika.

..nafasi ya Tanganyika lazima itambuliwe kwanza kabla ya kuanza kuijadili ktk ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

..kwenye mjadala mzima wa katiba sera za CDM zinakaribiana sana na sera za CUF, sijui kwanini viongozi kama Duni na Hamad Rashid wanashindwa kuliona hilo.

Wanasumbuliwa na Umimi , we ae the best KAFU we were the first on the matter sasa wanashangaa they cannot go back maana ndoa inawabana .They are just Frustrated
 
CUF vs Chadema

Because chadema is equal to CCM their mission and vision is the same..

They chadema and ccm lao moja ..kwa sasa..
 
Hata kama hamtaki. Tanganyika ni tanganyika na lazima tusemee maslahi yetu. Ccm b wasitufunike midomo
 
Nyakati zao cuf walikuwa wakiupinga muungano huu sana.... leo wamepata wapi nguvu za kuukubali? nini kimebadilika??? yaani wao wanaolingana na mkoa mmoja wa kwetu Tanganyika tuwe sawa wawakilishi??
Nyerere alikosea kwa hili kama alivyokosea na mambo mengine na hatuwezi kukubali kuburuzwa na kupoteza taifa letu Tanganyika.
 
zanzibar ni nchi itakayo fuata misingi ya kiislam na Rais ni lazima awe muislam, mpo hapo makaf...ri.
 
kuna swala la uhalali wa chadema kwani kuna uwezekanoi mkubwa sana kuwa zanzibar hawana wanachama au kwa hili la tundu likawapelekea katika hao wanachama wasiozidi 20 na wao kukisusa chadema. Hapo sasa, sijui tendwa ataamuwa vipi?

cuf ni chama cha nnchi ya jiran..yaani majirani zetu nchi ya zanzibar
 
zanzibar ni nchi itakayo fuata misingi ya kiislam na rais ni lazima awe muislam, mpo hapo makaf...ri.

machuo,mahospital.miradi,masekondari..rasilimali watu,,....hawa jamaa ni hatari je wasingekwa makafir wangefanya makubwa
 
R I P CUF. Hilo ndiyo kosa la hawa nyumba ndogo ya magamba badala ya kujenga chama lao wao kutwa kucha kuisakama Chadema, bure kabisa.

Kwani swala la Katiba si suala linalowahusu wengine? Msiwe na akili ndogo kama Tundu Lisu.

Maamuzi yeyote au mapendekezo yatolewayo na mtu binafsi, taasisi au chama yanayokuathiri, unahaki ya kuingilia na kupaza sauti. Duni amezungumza kwa hayo ya CHADEMA yanamhusu hata yeye na wataqnzania wote.

Eti mnataka tukae kimya ili mje mtuharibie nchi, angalia hawa hata siwaelewi. Wamesoma lakini hawajaelimika.
 
Kuna swala la uhalali wa chadema kwani kuna uwezekanoi mkubwa sana kuwa Zanzibar hawana wanachama au kwa hili la Tundu likawapelekea katika hao wanachama wasiozidi 20 na wao kukisusa chadema. Hapo sasa, sijui Tendwa ataamuwa vipi?
ndipo zitakapoaanza mbio rasmi za kuirudisha tanganyika-haitawezekana chadema ife eti kwa kukusa wanachama zenji-never...tanganyika itarud hapo kwa spidi zote
 
HIVI Bwana Juma Duni Haji na wenzake WANADHANI TUMESAHAU UBAGUZI WALIOMFANYIA DR SALIM AHMED SALIM wakisema kama anakuwa rais basi wanavunja muungano. KAMA WANATAKA NUSU KWA NUSU SAWA LAKINI NA SISI HIYO NUSU YA TANGANYIKA IONEKANE. TUFANYE SERIKALI 3. MUELEWENI TUNDU LISSU HAJAPINGA MUUNGANO HATA KIDOGO LAKINI KWA MANTIKI HUWEZI KUTAKA UPEWE NUSU YAKO WAKATI HATA ILE UNAYODAI NUSU YA TANMGANYIKA BADO UNASHARE. HIYO NI DOUBLE REPRESENTATION. WANAOMCHUKIA LISSU NI WA SABABU AMETUFUMBUA MACHO! CCM MTAJI WAO NI UJINGA WA WATANZANIA BASI. TUKIACHA KUWA WAJINGA NA UTOKUWA WAOGA CCM KWISHA. NDIYO MAANA NAWAPONGEZA WANAHARAKATI KWA KUSEMA wakaelimishe. MAJINGA TANZANIA NI MENGI NA HAYATAKI KUJIFUNZA! CCM WATATUNYWA MPAKA DAMU NA HAKUNA DALILI ZA HURUMA!
 
Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF bwana Juma Duni Haji ametetea vikali mswada wa katiba mpya uliopitishwa na bunge na kusema hata mwalimu Nyerere wakati wa uandaaji katiba ya mwaka 1977 aliteua wajumbe nusu kwa nusu kati ya Tanganyika na Zanzibar.Waziri huyo ameilaani Chadema na kumfananisha Tundu Lissu na mtu asiye na akili. Bwana Juma Duni Haji ameyasema hayo katika kipindi maalum cha dakika 45 ambacho kimerekodiwa na kitarushwa siku ya Jumatatu.
Tatizo la huu muswada wa katiba ni kwamba viongozi wengi wa CUF na CCM hawajui kwa nini wananchi tunahitaji katiba mpya. Huyu Juma Haji Duni na viogozi wengi wa Zanzibar siku zote huzungumzia maswala ya uongozi, uuwiano ktk viti vya uongozi lakini wanasahau wananchi wao na nafasi zao ktk muungano..Na kutoweza kujua kwa nini tunahitaji katiba mpya ndio maana katoa majibu kama haya..


Mwaka 1977 Nyerere na wajumbe wote wa kuunda katiba mpya ya mwaka huo ilitokana na Udikteta wa chama CCM. Ni katiba ilokuja kuvunja vyama vingi, kuunda dira ya Ujamaa na Kujitegemea, kutaifishamali za watu, vijiji vya Ujamaa na mengine mengi ambayo wengi wenu leo mnayalaani. Ssasa alitegemea kweli wananchi wangehusishwa ktk katiba ambayo leo hii tunaipiga vita?..

Yeye anataka turudie makosa yale yale ya kuunda katiba kwa kuwatazama wajumbe wa katiba na maridhio ya Vyama vya CCM na ASP badala ya maswala ya kikatiba ambayo yamepelekea maisha ya wananchi tuitake katiba mpya. Kwa nini viongozi wa Zanzibar siku zote huzungumzia WATU?...Nyerere hivi Nyerere vile, wakristu hivi wakristu vile...yaani ni ugonvi wa kutafuta nafasi za kula tu..
Hivi ikiwa rais wa Zanzibar hakuhusishwa na hata idea ya kuhitaji katiba mpya wala kuandikwa kwa muswada huu wa muungano, humuoni kama kuna makosa toka mwanzo.

Mh. Juma Haji Duni, mkuu wangu - Great minds discuss ideas, average minds discuss events, small minds discuss People...

- Sasa ajiulize kasimama wapi!
 
Duni analinda mkate wake wa kila siku but nina tamani kuona kuna jimbo liko wazi Pemba au Unguja then uchaguzi uitishwe nisiki hoja zao au wataamua kupeana tu ? Hakika CUF imeisha na huku bara ndiyo wasahau kabisa kupata kura hata moja .

unatumia m.atako au kichwa we sio bure cuf wasipate kura hata moja inakuja kwani usiongelee ccm inaonekana cuf inakuumiza sana. Hao ndio walio sababisha slaa akaibuka na zitto kama utakumbuka slaa alipewa usemaji kambi ya upinzani 2005 bila cuf kumpa unafikiri angekuwa wapi na cdm yenu
 
Kuna swala la uhalali wa chadema kwani kuna uwezekanoi mkubwa sana kuwa Zanzibar hawana wanachama au kwa hili la Tundu likawapelekea katika hao wanachama wasiozidi 20 na wao kukisusa chadema. Hapo sasa, sijui Tendwa ataamuwa vipi?
Kumbe upo!!!! Nilifikiri paycheck zimekata baada baada ya EL kuibuka kidedea kule NEC. Ni nini mipango yenu mipya unahamia kambi ya EL au au bado unakula za Nepi?
 
"" Yeye mwenyewe Mwl alishasema enzi za uhai wake kuwa wakati wa utawala wake yapo mengi mazuri waliyofanya na vile vile yapo mengi ya kijinga waliyafanya kwa kuwa wao hawakuwa malaika. Kinachotakiwa ni kuachana na ya kijinga na kuendeleza yale mazuri.

Inawezekana Duni anataka tuendeleze yale ambayo mwl aliyaita ya kijinga. Hapo ndo utakapojua mwl aliposema Wa Tz watu wa ajabu kabisa.

Namalizia kwa kumuuliza Duni: Hivi wakati wanatunga katiba yao Zanzibar, kuna Mtanganyika aliulizwa kutoa maoni. Si walimalizana wao kwa wao na kujitangaza kuwa Zanzibar ni NCHI. Sasa ya kwetu anayatakia nini?? ""

[COLwazanzibari wanajua inataka kuandikwa katiba ya jamhuri ya muungano, nasiyo ya tanganyika (hakuna bunge la watanganyika bali la watanzania); ndio maana wamekua interested kuchangia nafikiri.
 
Nimemsikia Duni Haji kwenye highlights za hicho kipindi.
Swali moja kwa Duni: Kwanza sitaki kuamini kuwa Duni tunayemjua amekuwa mvivu wa kufikiri kiasi hiki.

Namalizia kwa kumuuliza Duni: Hivi wakati wanatunga katiba yao Zanzibar, kuna Mtanganyika aliulizwa kutoa maoni. Si walimalizana wao kwa wao na kujitangaza kuwa Zanzibar ni NCHI. Sasa ya kwetu anayatakia nini??

Mkuu SMZ

Na wewe usifanye kosa kama la Duni?

Mimi ninashangazwa kwa nini katiba ya Tanganyika imewekwa kapuni.
Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ilitokana na Katiba ya Tanganyika ambayo ilifanyiwa marekebisho ili iweze kukidhi haja ya muungano.

Hapa suala lililo gumu kuelezeka na kufahamika ni vipi katiba ya Tanganyika iliwekwa boharini/ ghalani hata kwa mambo ambayo hayakuwa ya muungano. Wakati kuna haja ya kuwa na katiba ya Tanganyika vile vile kusema wazanzibari wakae kimya katika kujadili katiba ya Jamhuri ya muungano na kutetea maslahi yao si sahihi.

Hili la Katiba ya Tanganyika ni karata nzuri kwa Chadema, inaonekana hawajalifikiria hili.
 
Ki uweli kabisa Watanganyika hatuitaki Tanganyika yetu maana tungekuwa tunaitaka kweli tusingewaachia wanasiasa peke yao ndio wadai kwa niaba yetu, na hawa wenzetu wanzibari wanaajua huo uzaifu tuliokuwa nao...Tutaendelea kulalamika tu...
 
Back
Top Bottom