CUF wazidi kuiandama CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF bwana Juma Duni Haji ametetea vikali mswada wa katiba mpya uliopitishwa na bunge na kusema hata mwalimu Nyerere wakati wa uandaaji katiba ya mwaka 1977 aliteua wajumbe nusu kwa nusu kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Waziri huyo ameilaani Chadema na kumfananisha Tundu Lissu na mtu asiye na akili. Bwana Juma Duni Haji ameyasema hayo katika kipindi maalum cha dakika 45 ambacho kimerekodiwa na kitarushwa siku ya Jumatatu.
 
R I P CUF. Hilo ndiyo kosa la hawa nyumba ndogo ya magamba badala ya kujenga chama lao wao kutwa kucha kuisakama Chadema, bure kabisa.
 
Kwali nyani haoni.....la mwenzake, hivi wewe huona wanachokifanya viongozi wa Chadema, kina Tundu Lissu, Dk Slaa, wanavyoisakama hiyo Cuf? Ndio siasa zetu za Tanzania mwenzeko hakimwaga mboga wewe unamwaga ugali!
 
hivi Zanzibar wana masilahi gani? Mbona hivyo. Sasa naichukia rasmi ZENJI. Mnatuamria maisha yetu! Wake up watanganyika, tuidai nchi yetu
 
Duni anatetea serikali ya umoja wa kitaifa iliyotokana na uhuni wa chama cha mapinduzi.
 
Nataman Tendwa angekuwa na akili akiona hiki chama! Utadhani ni chama cha wananchi wa Z'bar! Yaani likizungumzwa swala la z'bar wao ndio wanakuwa wasemaji! Hawa walioko bara nani anawasemea? Na kama ni chama cha waz'bar peke yao, kwanini Tendwa anakiacha kwenye orodha ya vyama?
 
Chatema wamekwisha...wamezikurupukia thiatha dha tanzania thatha zinawatokea puani...tena wanaenda ikulu kujimalidha dhaidi, waulidheni nccr ilikuwa na vichwa zaidi hivi vya chadema wa leo, miaka ya 90 leo wako wapi, walikuw wakiongozwa na kilaza mrema kama kilaza mbowe, poleni vijana wenzangu mlioko chadema...njooni chama dume ingawa kuna changamoto za hapa na pale.....
 
Kuna swala la uhalali wa chadema kwani kuna uwezekanoi mkubwa sana kuwa Zanzibar hawana wanachama au kwa hili la Tundu likawapelekea katika hao wanachama wasiozidi 20 na wao kukisusa chadema. Hapo sasa, sijui Tendwa ataamuwa vipi?
 
hivi Zanzibar wana masilahi gani? Mbona hivyo. Sasa naichukia rasmi ZENJI. Mnatuamria maisha yetu! Wake up watanganyika, tuidai nchi yetu

Kwa jinsi tunakoelekea, zenj ikubali kuwa mkoa, ima muungano ufe!
 
Duni anatetea serikali ya umoja wa kitaifa iliyotokana na uhuni wa chama cha mapinduzi.

Ataijua CCM kwamba siyo rafiki 2015! Nawasikitikia sana akina Mtatiro kwasababu sijui kama watapata hata mbunge mmoja wa kuchaguliwa toka ktk jimbo huku Tanganyika ktk uchaguzi ujao.
 
Chatema wamekwisha...wamezikurupukia thiatha dha tanzania thatha zinawatokea puani...tena wanaenda ikulu kujimalidha dhaidi, waulidheni nccr ilikuwa na vichwa zaidi hivi vya chadema wa leo, miaka ya 90 leo wako wapi, walikuw wakiongozwa na kilaza mrema kama kilaza mbowe, poleni vijana

wenzangu mlioko chadema...njooni chama dume ingawa kuna changamoto za hapa na pale.....

Nina wasiwasi kama wewe ni mtanzania kweli.
 
Hapa hoja ya Tundu Lissu ina mantiki au haina. Mtu anapojaribu kuwaandamana CDM lazima ajibu hoja zilizotolewa na siyo kuanza kubwabwaja bila kutoa jawabu la hoja. Mambo ya 1977 hayawezi kuendelea kuenziwa kila kukicha wakati hayatusaidii leo 2011. Nani leo 2011 utamdanganya duniani hapa kuwa mwaka 1977 watanzania walikuwa wachache wenye kupinga mambo ndani ya chama kimoja, leo 2011 watu hatuna chama, watu wengi wana vyama vyao na wanaweza kuona nchi zingine mambo yanavyoenda. Hatuwezi kuendelea kurudia rudia mambo yasiyotupa ufanisi badala yake tunaendelea kukumbatia wezi kila kona ya nchi.CUF waendelee kukaa na CCM meza moja kwani ni wamoja. kwanza sidhani kama hayo maneno kasema Duni, huyu bwana namheshimu kwa kujenga hoja, kama kasema hayo basi Zanzibar wanayoshughuli.
 
Chatema wamekwisha...wamezikurupukia thiatha dha tanzania thatha zinawatokea puani...tena wanaenda ikulu kujimalidha dhaidi, waulidheni nccr ilikuwa na vichwa zaidi hivi vya chadema wa leo, miaka ya 90 leo wako wapi, walikuw wakiongozwa na kilaza mrema kama kilaza mbowe, poleni vijana wenzangu mlioko chadema...njooni chama dume ingawa kuna changamoto za hapa na pale.....
Wewe endelea kuamini hivyo, sina chama lakini kwa pumba hizi unaonyesha bado unatumia Diapa.
 
Kuna swala la uhalali wa chadema kwani kuna uwezekanoi mkubwa sana kuwa Zanzibar hawana wanachama au kwa hili la Tundu likawapelekea katika hao wanachama wasiozidi 20 na wao kukisusa chadema. Hapo sasa, sijui Tendwa ataamuwa vipi?

Magamba yamegoma kuvulika bosi wako nape kasusa sasa sidhani kama atakuwa bado na uwezo wa kukulipa wewe,rejao,mwita25
,ritz na wenzenu wengine,anzeni kufanya mazoezi ya kujitegemea,uharo jf payroll won't exist any more,nape kwisha habari yake
 
Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF bwana Juma Duni Haji ametetea vikali mswada wa katiba mpya uliopitishwa na bunge na kusema hata mwalimu Nyerere wakati wa uandaaji katiba ya mwaka 1977 aliteua wajumbe nusu kwa nusu kati ya Tanganyika na Zanzibar.Waziri huyo ameilaani Chadema na kumfananisha Tundu Lissu na mtu asiye na akili. Bwana Juma Duni Haji ameyasema hayo katika kipindi maalum cha dakika 45 ambacho kimerekodiwa na kitarushwa siku ya Jumatatu.

Tuwaelewe je wa zanzibar mara oho hatutaki muungano oho nusu tz na musu zenji tuwaelewe je?
 
Kwali nyani haoni.....la mwenzake, hivi wewe huona wanachokifanya viongozi wa Chadema, kina Tundu Lissu, Dk Slaa, wanavyoisakama hiyo Cuf? Ndio siasa zetu za Tanzania mwenzeko hakimwaga mboga wewe unamwaga ugali!

Lakini ukweli utakuwa palepale gata kama ukimwaga vyote
 
Magamba yamegoma kuvulika bosi wako nape kasusa sasa sidhani kama atakuwa bado na uwezo wa kukulipa wewe,rejao,mwita25
,ritz na wenzenu wengine,anzeni kufanya mazoezi ya kujitegemea,uharo jf payroll won't exist any more,nape kwisha habari yake

umenena mkuu yaani hawakuonekana kabisa kuchangia zile threads za lowassa kabisa sijui walipatwa na "stroke"
 
Nimemsikia Duni Haji kwenye highlights za hicho kipindi. Anasema eti Mwl aliunda tume ya watu 20 toka bara na 20 toka visiwani wakati wanarekebisha hii katiba mwaka 1977, Anashangaa Lissu haelewi kitu gani na anaenda mbali hadi kumtukana.

Swali moja kwa Duni: Kwanza sitaki kuamini kuwa Duni tunayemjua amekuwa mvivu wa kufikiri kiasi hiki.

Hebu yeyote mwenye akili timamu atueleze ni wapi pali[poandikwa kwamba Yote yaliyosemwa na kufanywa na Mwl Nyerere ni MSAHAFU au BIBLIA kwamba hayawezi kubadilishwa??Achilia mbali heshima aliyoiacha.

Yeye mwenyewe Mwl alishasema enzi za uhai wake kuwa wakati wa utawala wake yapo mengi mazuri waliyofanya na vile vile yapo mengi ya kijinga waliyafanya kwa kuwa wao hawakuwa malaika. Kinachotakiwa ni kuachana na ya kijinga na kuendeleza yale mazuri.

Inawezekana Duni anataka tuendeleze yale ambayo mwl aliyaita ya kijinga. Hapo ndo utakapojua mwl aliposema Wa Tz watu wa ajabu kabisa.

Namalizia kwa kumuuliza Duni: Hivi wakati wanatunga katiba yao Zanzibar, kuna Mtanganyika aliulizwa kutoa maoni. Si walimalizana wao kwa wao na kujitangaza kuwa Zanzibar ni NCHI. Sasa ya kwetu anayatakia nini??
 
Back
Top Bottom