CUF watishia kujilipua

Nikisemaga kuwa wapinzani hawana sera mnaona natetea CCM.

CCM kweli inaelekea nayo kufilisika ila wapinzani ndio walishafilika na kujichokea kabisa.

Alitakiwa Maalim au profesa asimame na kuwaomba wasifanye hayo, badala yake wamekaa kimya!
 
Swala hili ni very sensitive. I don't support hawa jamaa kujilipua kwani hawezi solve tatizo. Bali nashangaa kwa nini JK anaweza kuwa kinyonga na kugeuka maamuzi ya Mkamba na Seif?

Nimepata siki more than 95% ya wabunge wa pemba ni CUF, sasa najiuliza jee ni haki kwa chama chenye wabunge zaidi 95% ndani ya pemba kutokuwa na wawakilishi ndani ya serikali? Wakati JK and CCM plays politic Wapemba wanashindwa kupata matibabu, wanashindwa kupeleka watoto wao kwenye shule bura sababu tuu walichagua CUF kwenye general election.

Pemba hata Umeme ni tabu, mafuta ni tabu, na pemba ndio wakulima wakuu wa visiwani kule.

I support swala zima la kutokutuma chakula unguja, however i condem swala la kujilipua mabomu.

Wewe Mheshimiwa Bwana, Sasa una condemn nini si supoort tu na hilo la kujiripua. Unguja haitegemei chakula au matunda au mazao kutoka Pemba. Hivyo wakipeleka- wasipeleke siyo tatizo. Kuna Bunge na kuna Baraza la Wawakilishi. Hivi kweli unajua umuhimu wa vyombo hivyo kwa mujibu wa mfumo wetu wa Utawala. Na jee hao wenye wabunge 95% Pemba wamezuiwa kuvitumia vyombo hivyo. Jee wanaifanya kazi yao (efficiently) kupitia vyombo hivyo?Hayo ndio ya kujiuliza. Na jee hilo wanaolotaka kupendekeza lifanyike hivi sasa si wameruhusiwa wakae kwenye meza ya mazungumzo na kulijadili na wenzao. Wewe unataka wakubaliwe tu kila wakitakacho. Upo wapi uadilifu hapo?
 
kwanza hakuna pahala ambapo cuf kimetoa tamko la kujitoa muhanga.
pili, cuf kwa nguvu zake imeshindwa kuleta muafaka zanzibar, au niseme imechaguliwa kuongoza nchi na walio wengi lakini imeshindwa kutawala, na hawana cha kufanya zaidi ya kusema fanyeni wenyewe mfanyalo.
tatu, pemba kusema inataka serikali yake ni just means ya kumshinikiza kikwete ashughulikie suala la muafaka, hakuna mtu atakayefanya hivyo.
nne, cuf inaweza kuwa haina sera wala maana, lakini kwa wakazi wa zanzibar WAO wameona kuwa cuf ni better kuliko ccm.
 
Mie naunga mkono kwa wapemba kujitenga, kama hali ya huko ni mbaya namna hiyo. yaani kama hakuna basic needs na wanakataliwa na wenzao wa Pemba na kuona kama ni wakuja, basi wajitenge. Kuna maana gani, yaani inakuwa kama wa Pemba ni kama vibarua tu na wakulima. Waachieni basi hata karafuu yao wauze wenyewe. Wamechoka ndio maana wakaamini kuwa CUF kama chama kinaweza kuwaletea uhuru wa kiuchumi na unafuu vilevile. Kwani kama CCM wangepeleka basic needs unafikiri hawajamaa wangetamka kujitenga? Mbona wakazi wa Dar hawajatamka kujitenga, ni wakazi wa Kigoma,Mtwara na huenda hata Songea na Rukwa watakuja tamka hayo maneno. Wapeni haki halafu mtaona kama watatamka hayo maneno ya ``mabaya``
 
Mimi Napenda Tuwaulize Makamba , Kikwete , Karume Na Kingunge Tuchukulie Cuf Wamekubali Hio Kura Ya Maoni Kuhusu Mustakbali Au Aina Ya Serikali Wanayotaka Watu Wa Zanzibar . Sasa Tuseme Swali La Kura Ya Maoni Litakuw " Jee Unakubali Kuundwa Serikali Shirikishi Itayopatikana Baada Ya Uchaguzi Wa Zanzibar Ili Kuweka Uwiano Wa Kiutawala"
Jee Serikali Ya Ccm , Makamba .kingunge Karume Watakua Upande Gani Wa Kura Ya Maoni ??????? Watawambia Wana Ccm Zanzibar Wakubali Serikali Shirikishi Au Watawambia Wakatae?????????? Naomba Maoni Yao . Naomba Kikwete , Makamba Na Kingunge Atujibu. Maaana Ipo Wazi Cuf Wao Watasema Tunakubali Jee Ccm Upi Utakuwa Msimamo Wao Kwenye Kura Ya Maono ?????////
 
Jarida hili linapotosha.

1. Wapi hapo inaonyesha 'wafuasi' wamesema hivyo zaidi ya mfuasi mmoja, muimba tenzi?

2. Huyo mwimbaji ana nguvu ya kutoa tamko la CUF au kutumbuiza?

3. Waandishi waliwauliza wasemaji wa CUF kuhusu hilo, au wameliachia achia jambo linaning'inia hewani ili waje kutudanganya 'CUF wametoa tamko?'

4. Pia, nipe nukuu ya hata sentensi moja ya maneno yake mwenyewe. Usinitafsirie peke yake. Tafadhali ndugu muhariri.

Jamani hawa waandishi ni waongo, wachovu. Hawana hiyo taaluma hata kama wameenda shule za uandishi. Mimi sio CUF lakini nataka ukweli kwanza, kabla sijajadili lolote. Bongo hakuna Media!

Hii habari ina nia ya kuuza gazti tu kwani alotoa rai ni tu mmoja na imeshakuwa CUF na kuonyehsa kuwa ni uchochezi walitumia jina la pili la huyo msoma utenzi ambaye jina lake ni Hamad ili kupotosha, mwandishi makini anayetaka ujumbe uwafikie wasomaji wake angetumia jina lake la kwanza ili kutafautisha baina ya Seif na huyo jamaa.

Ama katika hoja ya kutokupeleka mazao Unguja ni moja ya mikakati ya kudai haki na kama hoja ni kuathirika kwa wananchi wa kawaida ni sawa kwani ni wao wanaoshabikia kutokupatikana kwa Muafaka , ni wao na si viongozi waliokuwa wakipita katika magari na kukejeli wenzao. Kwa hivo wacha wasome kwa vitendo kuwa likiingia janga na wao wataathirika na kuhusu CUF walioko Unguja watavumilia au watazifata hizo bidhaa huko Pemba.

Lazima hatua zichukuliwe bila hivyo CCM watakuwa kila siku wanafanya watakalo wakijua kuwa kuna mazumbukuku wachache wanawashabikia.
 
Hii habari ina nia ya kuuza gazti tu kwani alotoa rai ni tu mmoja na imeshakuwa CUF na kuonyehsa kuwa ni uchochezi walitumia jina la pili la huyo msoma utenzi ambaye jina lake ni Hamad ili kupotosha, mwandishi makini anayetaka ujumbe uwafikie wasomaji wake angetumia jina lake la kwanza ili kutafautisha baina ya Seif na huyo jamaa.

Ama katika hoja ya kutokupeleka mazao Unguja ni moja ya mikakati ya kudai haki na kama hoja ni kuathirika kwa wananchi wa kawaida ni sawa kwani ni wao wanaoshabikia kutokupatikana kwa Muafaka , ni wao na si viongozi waliokuwa wakipita katika magari na kukejeli wenzao. Kwa hivo wacha wasome kwa vitendo kuwa likiingia janga na wao wataathirika na kuhusu CUF walioko Unguja watavumilia au watazifata hizo bidhaa huko Pemba.

Lazima hatua zichukuliwe bila hivyo CCM watakuwa kila siku wanafanya watakalo wakijua kuwa kuna mazumbukuku wachache wanawashabikia.

Mimi naungana na waliopendekeza kuwa heading ya hii thread ibadilishwe!
 
CCM wamezoea kuharibu Zanzibar na kuwasukumizia lawama watu wengine. Safari hii tusiwape nafasi ya kukwepa lawama. Tusisahau chochote kitakachotokea Zanzibar, chanzo chake ni maamuzi ya ovyo ya mkutano wa halmashauri kuu ya CCM huko Butiama.
 
Umaskini uliokithiri wa ndugu zetu wa Pemba utakwamisha utekelezaji wa maamuzi haya ya kisiasa. Soko kuu la mazao yao ni Unguja na yeyote anayewakataza wasipeleke mazao yao huko hawatakii mema, anataka kuwaona wakifa njaa. Wenzetu waarabu wanajilipua lakini familia zao zinabaki kwenye mazingira mazuri, I dont think this will be the case kwa hawa ndugu zetu, viongozi waache kuwajaza wananchi ujinga wa kisiasa, there must be lots of other more meaningful and realistic options. Labda tunaweza kuwasaidia viongozi wa CUF kufikiri ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa hapa kabla mambo hayajawa mabaya kwa ndugu zetu.
 
Hivi kweli haya maneno wamesema CUF kweli?

Hayo ndio maswali yatakayo okoa nchi kutoka kwenye janga la kutokuwa na Media.

Mwandishi mwongo. Ni mtu mmoja tu kaimba kwenye tenzi, halafu gazeti likasema 'wafuasi' wa CUF wamesema. Big, big difference. Ni uongo kwa sababu anataka kuonyesha picha isiyo kuwa ya kweli kwamba ni wengi ndani ya CUF wanafikiri hivyo. Mwandishi wa kweli angeenda uliza wasemaji, viongozi wa CUF, kama wako nyuma ya hayo mawazo ya mfuasi mmoja. Mwandishi hakuuliza makusudi kwa sababu alitaka alete kichwa cha habari kinacho ning'inia hewani cha uwongo.

Na ndo maana hakuna hata nukuu ya sentensi hata moja ya maneno ya huyo mtu mwenyewe. Na hatujui context. Kwa sababu ni mtumbuizaji, inawezekana alitoa kichekesho kibaya. Hatujui lolote. Mwandishi kaacha issue ining'inie hewani makusudi.
 
Kuhani mkuu,
Mtanisamahe wakubwa lakini mimi nimewahi kumsikia Seif kwa mdomo wake akiwashauri vijana kuchukua hatua hizo ati yeye kisha ifanya kazi yake.... Nilishtuka sana kusikia hivyo, hii ilikuwa ktk mkutano alofanya na vijana wa ZNZ - Canada.
Swali aloulizwa na kijana mmoja lilikuwa hivi:- Unaturuhusu vijana kuchukua silaha na kuanziisha mapambano dhidi ya serikali dhalimu ya CCM..
Yeye alijibu kwamba fanyeni mtakachoweza... Yeye kazi yake kisha imaliza akiwa na maana aligombea Urais na akashindwa kwa njama za serikali hiyo hiyo..
I was there! from that day simpendi huyu jamaa hata kwa kulumangia!
 
hayo ndio mambo ya akili kweli? hawa ndio tuwaachie nchi watawale?

sasa jee watawaambia pia wahame unguja warudi pemba?

maana wanachekesha sana hawa watu na wavae mabomu na vifaru

warudi kwenye mazungumzo wazungumze sio vitisho na upuuzi

Hayo ya kujilipua..kwa kweli nisingependa yatokee..ila hili suala la watu wa pemba kurudi kwao pia nachukulia kama suala la localization of the development efforts in a collactive manner..kutokana na ukweli kwamba wapemba wengi wamekuwa wakisifika sana kwa kuendesha biashara mbali mbali haswa zile za maduka, basi ni vyema wakatumia busara kuhamishia nguvu zao nyumbani..pemba ili kuweza kujenga mtaji wa eneo husika ambalo kwa kusema ukweli limetengwa sana kimaendeleo,ambayo utengwaji huo umekaa kisiasa zaidi..KURA..Kuwadanganya watu wazima kila siku kwamba kutakuwa na serikali ya mseto..huku wakipigwa danadana na miaka ikizidi kuenda kunadhirisha wazi kwamba suala la muafaka linafisadiwa na either halipo ama linahitaji muujiza..Hivyo ni vyema wakatumia fursa waliyo nao kujiendeleza kwao ikiwa ni pamoja na kuinua huduma za jamii ambazo zimedorora mno hapo pemba..Maoni yangu tu..
 
MKANDARA

naomba kukuliza

How good is your knowledge of ZANZIBAR POLITICS?



Tafadhali naomba utujulishe hilo
 
Umaskini uliokithiri wa ndugu zetu wa Pemba utakwamisha utekelezaji wa maamuzi haya ya kisiasa. Soko kuu la mazao yao ni Unguja na yeyote anayewakataza wasipeleke mazao yao huko hawatakii mema, anataka kuwaona wakifa njaa. Wenzetu waarabu wanajilipua lakini familia zao zinabaki kwenye mazingira mazuri, I dont think this will be the case kwa hawa ndugu zetu, viongozi waache kuwajaza wananchi ujinga wa kisiasa, there must be lots of other more meaningful and realistic options. Labda tunaweza kuwasaidia viongozi wa CUF kufikiri ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa hapa kabla mambo hayajawa mabaya kwa ndugu zetu.

unaposema kuna other meaningful options, bora ungezitoa kuliko kusema hii njia siyo sahihi lakini njia sahihi huitaji.
 
Ndugu zangu wanaforum mimi napenda kwanza kuunga mkono hoja za wapemba za kutaka kujitenga . kwa nini naunga mkono?
Kwanza serikali ya Mapinduzi haiwatambui Rasma kama ni raia sawa wa Zanzibar wenye haki sawa kama wenzao wa Unguja
Pili serikali ya Zanzibar yenyewe mara zote imesema na hakuna amekanusha ya kwamba haiwezekani kwa MPEMBA kuongoza serikali ya Zanzibar
Haya yamekua yakitamkwa ndani ya Baraza la wakilishi , mikutano ya hadhara na hakuna asojua mpaka juzi ndani ya mkutano wao wa Butiama wamesema wazi
Nafasi zote za serikali ya Zanzibar zimeshikiliwa na watu wa unguja japo wapemba wapo wengi wenye uwezo
Hakuna Mpemba katika baraza la mapinduzi
Nafasi zote za masomo ya juu zinakwenda kwa watu wa Unguja na CCM
Kuna hujuma za makusudi zimefanywa dhidi ya wapemba kuwadhuru kama kisa cha kutiliwa sumu kule pemba
Ingawa serikali ya Muungano huwa inawavumilia Wapemba kwa kuwapa nafasi muhimu kama DR. Shein na Salim Ahmed na Dr, Omar wote walikua ni wakuonyeshWa mfano katika uongozi wa nchii hii hawa HAWANA hata chembe ya UFISADI lakini subutu huyu Shein aseme tu nataka mimi kugombea Urais wa ZANZIBAR HATA FORM HATOPEWA NA CCM UNGUJA
Haya ya ubaguzi na ufashisti maaana huuu ni ufashisti kubagua raia wako kuwa ni watu wa daraja la pili
Haya yakifanyika Huko za Zanzibar Dhambi kubwa ni kwa Serikali ya Muungano kutojali na kuvumilia hali hii ya CCM wenzao Unguja la ajabu wao Bara hawana Tabu na WAPEMBA
KUNA SABABU NYINGI ZA JAMAA ZETU KUJITENGA
UNAPOMWAMBIA MTU NDANI YA NCHI YAKE KWAMBA WEWE MPEMBA HUWEZI KUTAWALA NCHII HII BASI MAANA YAKE HUWATAKI BORA WAWE MBALI NA WEWE YAANI TAYARI UMEWAPA RUHSA KAMA WANATAKA KUJITENGA BASI RUHSA
WATU WANASEMA KWA NINI WAPEMBA HAWAJENGI KWAO WAKATI WANAUWEZO? LAKINI JAMANI NI SERIKALI NDIO INTAKIWA IPELEKE MAJI . UMEME BARABARA , BANDARI , AIRPORTS NA MASHULE KAMA WAFANYAVO UNGUJA
KUNA VISA VINGI VYA KIBAGUZI KUNA JAMAA ALITAKA KUFUNGUA HOSPITAL KUBWA PALE WETE MSAADA WA KUTOKA NJE AKANYIMWA KIBALI ATI ASAIDIE ZILIZOPO
KUNA WATU WALITAKA KUJENGA BARABRA YA GANDO KWENDA WETE SERIKALI IKAKATAA MPAKA LEO GARI HAZIPITI WATU WATEMBEA KWA MIGUU
HATA USAFIRI WA BAHARINI UNAPIGWA VITA KWENDA KATI YA PEMBA , MOMBASA NA TANGA ILI WAPEMBA WASIFAIDI KUJIENDELEZA
KUNA WAKATI BEI YA PETROL PEMBA ILIKUA CHINI KULIKO UNGUJA , HII NI KUTOKANA NA SOKO HURIA BAI IKAAMULIWA IPANDISHWE IWE SAWA NA UNGUJA HUU NI UBAGUZI WA HALI YA JUU
PEMBA MARA NYINGI KUNA TOKEA UKAME NA HALI YA NJAA IKITOKEA HAKUNA WA KUWASAIDIA SERIKALI YA UNGUJA HAIJALI BALI HUTOA KEJELI HATA SERIKALI YA MUUNGANO NAYO HUKAA KIMYA IKITOKEA NJAAA SEHEMU NYENGINE BASI HARAKA MISAADA INA PELEKWA
MIAKA YA NYUMA WAPEMBA WALIKUA WANASAFIRI KUTOKA TANGA KWENADA PEMBA HALI YA HEWA ILICHAFUKA BASI WAKAPIGA SOS YA KUOMBA MSAADA NA WALIPIGA RADIO CALL IKAPOKELEWA LAKINI HAWAKU PATA MSAADA NA ROHO ZAO 25 ZIKAPOTEA KISA ATI BOTI ZA KMKM HAZIKUA NA MAFUTA
WAKATI PEMBA KUKIWA NA NEEMA YA CHAKULA WATU WA PEMBA HUUZA KWA WINGI CHAKULA CHAO KWA NGUGU ZAO WA UNGUJA LAKINI PEMBA KUKIWA NA NJAA BASI WAPEMBA HAWARUHUSIWI KUPELEKA CHAKULA KUTOKA UNGUJA HII NII AIBU
HIVYO WANAZO SABABU NA NIA YA KUJITENGA WAO NI BINAADAMU NA WAMESOMA VYA KUTOSHA KUENDESHA NCHI YAO KAMA WAPEMBA .CCM TAYARI IMESHAWAFUKUZA KWA HIYO WAO WANATAMKA TU KWAMBA JAMANI WENZETU TAYARI WAMETUTOA KATIKA SERIKALI HIVYO TUNAKAA KWETU NA SERIKALI YETU MAANA KATIKA HIO HATUNA NAFASI SASA HUUUU SII UHAINI
 
siasa za vitisho hazijatatua matatizo; leo hii israel na palestina licha kulipuana na kuuana wamefikia karibu kwenye suluhisho la mgogoro wao kwa kiasi gani?

Kuna mambo mengine ni mazuri kutia hamasa lakini haya manufaa yoyote yale.

Ndugu yangu wee!!! Kweli wewe ni Mtanzania halisi tena original..... Fundi wa maneno meeeeeeeengi... bila matendo!!! Wakenya wangekuwa na roho kama yako leo kusingekuwa na Grand Coalition Government.... Waafrika kusini wangekuwa na mawazo kama yako leo hii Kaburu bado angekua kwenye usukani.... Viongozi wengi wa Kiafrika ni kama Punda... hawaendi bila kiboko... na hilo ndio tatizo hasa tulilonalo Watanzania... na CCM wanababaisha kwa sababu wanajua sisi ni watu wa maneno meeengi... bila matendo.... TAFAKARI
 
Sasa mnapiga makele wakati Wapemba wametishia tu ,ila kama wakifanya kweli itakuwaje ,tato mnachanganya hisia na ujumbe wanaowakilisha WaPemba,ionekane tu kuwa wanachokitetea Wapemba kinagusa Taifa zima,shida na taabu wanazozipata wao zimejaa na kuenea Tanzania nzima ,kunatokea malalamiko kuwa mahospitali hakuna dawa,mashuleni hakuna walimu wenye kiwango ,na huduma nyengine mbovu kila kona ya Tanzania ,na yote haya yanatokana na utawala mbovu wa CCM ,mtu anaweza kusema ndani ya CCM si wote wabovu nakubaliana nae,ila ndani ya Serikali na vigogo wa Chama kumekuwa na rushwa ya kitaifa na kimataifa ,hivyo hata awemo ndani ya CCM kiongozi mzuri mbio zake zitakwama au juhudi zake zitakwamishwa.
Pemba ni kisiwa kidogo sana hivyo shida na madhila yanapotokea huwakumba watu wote tena kwa wakati mmoja ,maana ikizima genereta moja basi ndio Pemba nzima hakuna umeme usitegemee kama mtaa wa pili au mkoa mwengine kuna umeme ni pemba nzima halikadhalika na maji nayo ndio hivyo hivyo ,yaani mtoto alimuuliza baba yake ..eti baba CUF imeshinda ,,,baba akauliza kwa nini mwanangu...mtoto akamjibu baba yake kuwa nimeona maji yanatoka kwenye bomba !!!
Unajua kama watu wa pemba hivi sasa wamekaa kama mabundi mchana hawaoni vizuri lakini usiku utawashangaa wanavyoona na kukatiza njia za vichochoroni ,yaani mtu anaendesha baiskeli kwenye kiza totoro na anakwenda spidi.Dhiki za maisha zimewafanya wabadilike na hali ya mazingira.
 
Back
Top Bottom