CUF wataka serikali ya umoja wa kitaifa bara

CCM wamelikoroga wacha walinywe wenyewe. Dawa ni kuwaondoa madarakani tu. Na hao CUF wameshazoea vya kunyonga,hawana jipya zaidi ya kujikomba kwa buzi lao magamba. HAKUNA MWAFAKA NA MAFISADI.
 
Hizo ni fikra za tamaa, suk imekuwa mwiba kwa wazanzibari, na hali ya maisha kwa wazanzibari bado mbaya afadhali ya jana sasa ndugu machano asitake lililolikuta zanzibari litokee Muungano (Bara) hiyo serikali kaeni nayo nyinyi sisi hatutaki na kama mtalazimisha mtaijenga nyinyi na ccm. kwa sasa cuf hamsemi tena yaliyo matumaini kwa wa tanzania bali mnafikiria "umoja wa kitaifa" hizo ni fikra hafifu zisizokuwa na mashiko kwa watu wa makini, mmepoteza ladha,. masikini weee
 
Kweli CUF wanapenda vya mteremko. Wameshindwa kwenye uwanja wa mapambano wanalilia vya kugawana.
 
CUF wasilete nuski ya serikali ya umoja wa kitaifa huku Tanganyika. Zanzibar hakuna la maana sana limefanyika kwenye hii serikali ya umoja wa kitaifa sana sana anayefaidi ni Maalim Seif. Wananchi wamebaki kama yatima hakuna wa kuwatetea. Meli imezama hakuna aliyewajibika, michango inamiminika kwa mamilioni lakini haijulikani hiyo michango ni ya kumsaidia nani na ni lini watu watasaidiwa.

Kama siasa zimewashinda wakae pembeni lakini wasitafute vyeo kwa kuwatoa kafara wananchi.
 
ccm wamewatuma cuf wawasemee baada ya kusoma alama za nyakati kwamba 2015 wanatolewa madarakani, ukizingatia watang'ang'ania madarakani wanajiwekea mazingira ya serekali ya umoja wa kitaifa ili wasishtakiwe.
 
Hivi hamjui nape aliwatoa udende cuf-bara alipowaibia siri kuwa siku hizi seif-mandevu anagonga wine huko ikulu ya zenji?!
 
Siasa za Tanzania zinanipa shida sana kuzielewa. Hasa hasa siasa za Zanzibar. CCM na CUF Zanzibar wamefunika kombe mwanaharamu apite wasubiri 2015. Tusubiri kama CUF wataambulia hata hivyo viti walivyovipata mwaka jana waombe mungu. CUF mpaka sasa watakuwa wamepoteza wapigakura wengi sana kiasi wengi wanajiuliza hii SUK imewasaidia nini zaidi ya ngonjera kibao. Yetu macho tulianza kuziona ngongera zao kule Igunga.
 
Back
Top Bottom