CUF wapeleka barua Ikulu ya kuonana na Rais

Hawana lolote, gere tu inawasumbua, CUF ni kwishney, tuliwazika siku walipojiunga na magamba
 
CUF wameunga mkono muswada tena kwa kelele na sasa muswada umesainiwa na rais hivyo kuwa sheria. Sasa CUF wanaenda kuonana na rais kwa lipi? Walichokita kimefanyika wanataka nini tena? Na kama CHADEMA hawakuomba kuonana na rais CUF walikuwa na mpango gani? walipanga kuonana na rais? Kwa nini hiki chama (CUF) kimeamua kuwa dalali wa ugomvi?

kuunga mkono muswada bungeni hakuzuii CUF kwenda Ikulu kama ambavyo kutoka nje ya bunge wakati muswada ukiwakilishwa hakuzuii chadema kukataliwa kwenda Ikulu
 
hebu tuwe wakweli.kati ya cdm na cuf, nani anamwonea wivu mwenzake kama sio cdm.au kwa vile cdm ni nyumba ndogo.
 
chadema walitoa tamko kwamba hawataki kuongozana na vyama vingine kwenda Ikulu kwa sababu eti wao walituma barua lakini pia vyama vingine vilishiriki kupitisha muswada ikiwemo CUF sasa CUF wanakwenda kivyao tunasema wasienda huu ni unafiki. kama chadema wangekaribisha vyama vingine kwenda Ikulu tungesema CUF wanafiki. tuwaache waende kivyao vyao


Ni lini walipata wazo la kuonana na rais? Ni baada au kabla ya CHADEMA kutangaza nia yao ya kuonana na rais? Na kama CHADEMA hawakuomba kwenda kuonana na rais CUF wangeenda kuonana naye? CUF wanafuata nini Ikulu? Muswada ulikuwa mbaya?
 
nao CUF na CCM wamezidi kudesa kila kitu kutoka chadema, sijui hawana planners kwenye chama.

chadema nao wanadesa hujui kwamba waanzilishi wa maandamano makubwa walivyosababisha vifo vingi ni CUF, hujui kwamba baadhi ya mbinu za siasa za upinzani chadema wamedesa CUF kama ambavyo CUF walivyokuwa wanasusia vikao vya baraza la wawakilishi? hujui kwamba chama cha kwanza cha upinzani kukutana na Rais Karume Ikulu ni CUF...... huwezi kuendesha siasa bila kudesa
 
chadema walitaka kunyang'anya mume wa CUF pasipo kufuata utaratibu. Utaingiaje nyumbani wa CCM bila CUF kuwepo? uliwahi kuona wapi mnamtembelea mtu halafu unasema mke wako nisimkute nyumbani kwako. Hapa Jf wanachadema ndio wanasema kuna ndoa kati ya CCM na CUF. Nini cha ajabu kama CUF wameomba kukutana na Rais

wewe huwa unamwomba nani ruhusa ya kukutana na mmeo?
 
cuf mnatakiwa kuwa wapole ili ndoa yenu Idumu,nyie ndoa na iheshimiwe,wapembeni hatutaki kusikia chokochoko na huyo kidume chako,we ushaolewa so kuwa mpole.:A S 465:


unataka CUF wawe wapole wakati chadema ndio wenye makosa wametuma barua ya kulazimisha uchumba kwa mume wa ndoa wa CUF
 
Mambo mengine ya ajabu sana
Wao waliunga mkono hoja 100% na kuwafanya Chadema ni hoja ya kujadiliwa bungeni wakalipwa 200000/= kila mmoja
Wana hoja gani tena mpya ndani ya siku chache tu hizi baada ya kupitisha mshwada wenye mapungufu mengi na ambao walijifanya hawayaoni na kuyasikia

Ushauri tu Wawahi mapema zaidi Kabla Mh Hajaenda Burundi kama alivyo aga maana akirudi tu Sisi tutakuwa tumeanza kudadavua Kila heri CHAMA CHA WANANCHI
 
.......kupitia kipindi cha tanzania tunayoihitaji, kinachorushwa na star tv, Mnyaa alisema, na ndivyo ilivyo kwamba wao tayari walishawasilisha rasimu ya katika serikalini, sasa hapa walitakiwa wawe inquisitive na kuona watoke vp, waachane na staili za kuiga.
hatimaye wa bia wa ccm cuf nao wanataka kwenda ikulu nao
source tbc newz
 
kuunga mkono muswada bungeni hakuzuii CUF kwenda Ikulu kama ambavyo kutoka nje ya bunge wakati muswada ukiwakilishwa hakuzuii chadema kukataliwa kwenda Ikulu
Mkuu kwa hali ilivyo hata wapinzani wote wataka nje ya ukumbi wa bunge miswada itapitishwa tu CCM wapo wa kutosha kabisa
 
CDM walienda na Maprofessa wawili na majembe matano, tuone CUF wataenda na wangapi kuacha Prof Lipumba.
 
CUF wameunga mkono muswada tena kwa kelele na sasa muswada umesainiwa na rais hivyo kuwa sheria. Sasa CUF wanaenda kuonana na rais kwa lipi? Walichokita kimefanyika wanataka nini tena? Na kama CHADEMA hawakuomba kuonana na rais CUF walikuwa na mpango gani? walipanga kuonana na rais? Kwa nini hiki chama (CUF) kimeamua kuwa dalali wa ugomvi?

Wanakwenda kumwambia Rais akiteua wajumbe wa Tume wawe kutoka bara nusu na visiwani nusu.
 
Nnachoshangaa kwani prez kusaini amesaini katiba ama mswaada wa sheria?afu wananchi ndo baada ya kamati watatoa maoni kama nilivoelewa sa ndiposa najiuliza mbona kuna vihelehele vingi sana kana kwamba katiba ndo imesainiwa?
 
Chuki Unafiki Fujo (a.k.a CUF)ndio maisha.Ni kuwafitini CDM mwanzo mwisho maana wanawafungua macho WATANGANYIKA.Hii ni hatari sana kwa ka-Kisiwa ketu na adui yetu Mkuu tunakwenda mwambia Jakaya Kikwete ni Tundu Lissu na maoni yake yanayodai Tanganyika.Kama CDM ngangari basi Sisi ni Ngunguri,wamemwaga ugali zetu mboga.:director:
 
Back
Top Bottom