CUF wanatumiaje ruzuku yao bara?

La!! Hapana, kauli zangu zinakanyagana na zako. Kauli zangu ziko wazi kuwa CCM wamepandikiza mbegu ovu juu ya CUF (nataja CCM kwa kuwa haina mtetezi hapa jukwaani na naogopa kuanzisha kukanyagana kwengine nikiwataja wahusika wengine. wa kusambaza mbegu hizi).Mpaka hapo tutakapotoka kwenye kasumba hizo CUF hata ipate fedha kiasi gani haitaweza kuwa na nguvu Bara.

Ngekewa hapo umeniacha kapa mkuu,nimesoma posting hii zaidi ya mara tatu lakini sijaambulia kitu hapo,hata hivyo nadhani Ndege ya Uchumi alikuwa akimjibu Gozigumu.
 
la!! Hapana, kauli zangu zinakanyagana na zako. Kauli zangu ziko wazi kuwa ccm wamepandikiza mbegu ovu juu ya cuf (nataja ccm kwa kuwa haina mtetezi hapa jukwaani na naogopa kuanzisha kukanyagana kwengine nikiwataja wahusika wengine. Wa kusambaza mbegu hizi).mpaka hapo tutakapotoka kwenye kasumba hizo cuf hata ipate fedha kiasi gani haitaweza kuwa na nguvu bara.



mbona hiyo kazi ilikuwa yangu na wala sitaki msaada.
 
Ngekewa hapo umeniacha kapa mkuu,nimesoma posting hii zaidi ya mara tatu lakini sijaambulia kitu hapo,hata hivyo nadhani Ndege ya Uchumi alikuwa akimjibu Gozigumu.

Ndio kanyaga yenyewe hiyo na kwa taarifa yako mimi ni supporter wa Gozi. Pengine nilishituka kutoka usingizini.
 
Mwiba there sometime lazima tukubali kuwa hata vyama vyetu vina mapungufu... Kutokiri hili maana yake the same na wanaCCM ambao hawaamini au hawataki kuamini Chama chao kina mapungufu mengi tu....

Kuna Nukta moja ambae aliigusa Nungunungu huko nyuma alisema tatizo la CUF ni UBAKHILI...believe me or not serious political party lazima kiwe na mtandao wa kuhahikisha yale wanayoyafanya yanakuwa public ili ku-gain wanachama.

Labda nikuulize kwanini hadi sasa CUF hawana Gazeti...?kumekuwa na mission ambayo either imepangwa au au watu kuichukia CUF kutoandikwa vyema kwa magazeti au vyombo vya Habari like redio...hata wakati wa Uchaguzi...The same CUF wangeweza kuwa media zao wenyewe tu...assume pesa za propagation hamnazo, pesa mnazo pata mnawekeza alau kuwa na Redio na gazeti na website ambayo ipo update...(sio blog)..ilifika kipindi website ya CUF kujaa porns....kwakuwa kulikuwa hakuna updates or whatever....?ikawekwa thread hapa...i think walirekebisha..tuseme hata kumlipa web admin tu awe anapost news za CUF mnashindwa? Mnategemea Huruma ya Vyombo vya Habari ambavyo tunadai hapa jamvini Vimenunuliwa...?

Pia sense ya kuwaona wabara hawaaminiki au watu wa kununuliwa si sense njema, wakati tunapotafuta kuwawin wananchi maneno ya Kejeli au kebehi si mahala pake...Lazima tujue Historia ya kila sehemu ambayo jamii yetu imetoka...ukiiingalia uwelewa wa siasa znz na bara tofauti kidogo na hasa kutokana na mambo ya kihistoria...Ukiangalia ukubwa wa ZNZ na bara tofauti..within 2 weeks unaweza maliza Unguja na Pemba yote kutembelea na kufanya ushawishi...Bara ni tofauti...DSM pekee yake shughuli ipo kubwa..so

Matumizi ya pesa mnayopata kama mnataka kuwin na sio kuwacheza shere wananchi...lazima muweke strategies za namna ya kuwafikia wananchi

Rais wa Senegal ilimchukua miaka takriban 25 au more tangu akiwa mpinzani hadi kuwa rais...Kimsingi yapo ya Kujifunza kutoka kwake.(sina Hakika kama wapinzani kwa umoja wao au kwa ubinafsi wao au kwa level ya Mgombea kama wamefanya hata visiting tu...).namna gani aliweza kuwa-win wananchi...ni Hesabu tu ambazo vyama vyetu vinaweza kufanya. Bahati mbaya hatupigi Hesabu...Tunachofanya ni kusubiri uchaguzi na yaliyojiri baada ya uchaguzi kutushughulisha hadi uchaguzi mwingine.....Matokeo yake the only options itakayokuja ktk vichwa vyetu ni mapinduzi...!!!

Let us assume...Mnachokipata ni Kidogo sana...lkn kwa udogo wake fanyeni kitu wananchi wakione...let us say Mkajenga shule alau moja na Zahanati moja..kwa mwaka..!!!Hili hamshindwi ila Hamjaamua(Tusisubiri kupata Governmet ndo tufanye..let us wananchi watuhukumu)...amini hata wananchi wengine watakuja kuwaunga Mkono...na Hili si tu kwa CUF hata na vyama vingine...Kama hatuna Culture ya kutoa Vidogo tuvipatavyo, Je tukipata vingi tutatoa?...we need to build that culture!!!

Believe me kitakachomrudisha Muungwana madarakani ni hizi shule za kata, na plan za zahanati...pamoja na mapungufu yaliyopo...wale wananchi wanafeel kuwa atleast mwanae amepata njia ya kuelekea Juu...

Please let us take these as challenges on the way to 2010 election...na sio usaliti kama wengine wanavyotaka tuamini...!!!
 
Kwa kiasi ambacho CUF wanapokea inakuwaje hawana mbunge Tanzania bara? au kushindwa vibaya kama kule Mbeya au Tarime? Kwanini hata maeneo ya pwani ambapo naweza kusema ni ngome yao (Tanga, Dar, Pwani) hawana mbunge hata mmoja!

Hawa wanapata kiasi hicho cha ruzuku kutokana na idadi ya wabunge wao kutoka Pemba. Hata wakikosa mbunge hata mmoja kutoka bara wataendelea kupeta kutokana na ngome yao ya huko pemba. Kwa nini basi wasijijenge kuliko walikokuwa na uhakika badala ya kujiingiza kwenye masuala ambayo hawana hata interest nayo? CUF hawafichi kuwa priority yao ni Pemba na wanajiona kama chama cha wazanzibari. Kwa msingi huo basi wanachofanya kina mantik maana siku Muungano utakapotoswa nao watabaki kwenye himaya yao.

Dawa ya upuuzi huu ni kuangalia upya mgao wa constituencies. Au vyama vingine vya upinzani kuwa serious huko bara ambako nao wamejikita.

Amandla.........
 
Back
Top Bottom