CUF wanatumiaje ruzuku yao bara?

Mkuu Ngekewa nilikuwa nazungumzia wakati kabla ya Uhuru, hivi vyama vilipata fedha toka kwa wanachama wao. Ndio nikaandika sioni sababu sasa hivi vyama vya siasa kupewa fedha yote hiyo ya walipa kodi.

Sasa wasipopewa fedha hizo hizo EPA si zitakuwa maradufu?
 
Kwa kiasi ambacho CUF wanapokea inakuwaje hawana mbunge Tanzania bara? au kushindwa vibaya kama kule Mbeya au Tarime? Kwanini hata maeneo ya pwani ambapo naweza kusema ni ngome yao (Tanga, Dar, Pwani) hawana mbunge hata mmoja!

Hivyo unaamini kuwa Fedha ndio kila kitu? Basi CCM isingeshindwa kupata viti kule Pemba na CUF wangeanza kupata viti vingi kule Umguja.
Hata hivyo CCM walistahili kushinda nchi nzima kwa vile walikuwa na ruzuku mara kumi zaidi ya CUF na mabilioni ya wananchi kwa kupitia EPA. Nafikiri pesa si suluhisho bali ni kukubalika na wananchi. Tatizo la CUF kutopata nguvu BARA ni kasumba yetu:
-CUF chama cha kidini
= CUF ni chama cha Waarabu
= CUF kinataka kuleta usultani
-CUF viongozi wake wabaguzi
Mpaka hapo wananchi wa Bara watakapoondokana na dhana hiyo iliyojengwa makusudi na CCM hata wapate pesa za EPA CUF wataendelea kusuasua tu Bara.
 
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza juu ya swali hili bila mafanikio kwani kila unapotaka kuuliza anayeweza kuwa na majibu sahihi anakuwa mkali kweli kweli hii ni kwa sababu ukweli ni kwamba pesa yote inayopatikama inakwenda Pemba na kidogo Unguja na huku Bara hakuna kitu, mfano mikoa ya magharibi mwa Tanzania ofisi za CUF zinakatisha tamaa ya maisha kabisa na kibaya zaidi Mkiti wa Taifa hana Say yoyote katika chama hasa juu ya matumizi ya Ruzuku! huo ndio ukweli anayebisha aje hapa tupeane data
 
Kwa maana nyingine mnataka kusema kuna ufisadi ndani ya CUF ,hapo mtakuwa sio mmepotea dira tu ,bali hata mnakokwenda hamkujui ,maana ukipoteza dira unaweza kubahatisha na kusema labda ni huku au kule.Nyinyi hampo mawazo yenu yamefilisika na kuona kuna ufisadi tu ,sasa kuna ufisadi ,haya nini faida mmepata hadi hii leo toka muoneshe na kugawa data za mafisadi naona mnapiga makelele mengi sana kiasi ya nchi kutikisika na wengine kuporomoka lakini data zinaonyesha walioporomoka wamepata pa kukamata na wanapanda juu.Au uongo ?

Fedha ipo na inatunzwa kushinda serikali inavyotunza fedha yake na haitumiki kwenye kampeni kama wengine mlivyopendekeza ,CUF haitatumia fedha kumlaghai mwananchi na kumdanganya au kununua uhuru alionao wa kuchagua kumnunulia kanga au kumuwekea pipa la mvinyo,Wanachama ndio watachangia kampeni za Chama Chao pale sehemu husika na Chama kitatoa sehemu ndogo tu ya kusaidia kama kuna kukodiwa jenerataz na vifaa vyengine muhimu na sio kuandaa masufuria ya pilau ,hilo halipo.
Halafu mnashindwa kuelewa kuwa CUF ni Chama Cha Wananchi tofauti na vyama vingine ambavyo huwa ni vya kundi fulani tu au genge la watu ,kuna vyama kibao havina hata ofisi katika upande wa pili wa Muungano nikikusudia kule Zanzibar.

Ilivykuwa hiki ni Chama Cha Wananchi kama kinavyojulikana kwa lugha yetu ya kiswahili ,wananchi wenyewe ndio wakukiendeleza na si kutegemea feza ya ruzuku na kwa msisitizo huo ndio ukaona Chama kimeenea sehemu kubwa hapa Tanzania ,kwani wananchi wamekipokea kama Chama chao wanachotarajia siku yeyote ile watakiwezesha kukipa dhamana ya kuwaongoza na kuwakata vichwa hadharani mafisadi wote pindipo watakuwa na hatia ya kuhujumu core ya uchumi wa Tanzania ,hivyo wataishia jela milele ikiwa watashindwa kurudisha senti tano ya mwisho wa fedha waliyokwiba au kuhujumu na kama haitoshi mali yao yote sio itasimamishwa bali itafilisiwa.

Kuna mtu amesikika akisema kuwa CUF haina mbunge hata mmoja T/Bara ni kweli inawezekana hivyo kwani ndivyo ilivyopangwa na Sultani CCM maana Sultani CCM ndio mwenye kushika vyombo vyote vya nchi hii ,anaamua na kupanga atakavyo hakuna wa kumzuia ,polisi wanafuata amri yake,majeshi wanafuata amri zake mahakama wanafuata amri zake ,sasa unategemea nini kama hao wengine sio walishinda ,bali waligaiwa hizo nafasi za ubunge ,huo ndio ukweli ,nafasi hizo wanazoringia ni za kugaiwa kutokana na mipango ya Sultani CCM ili atumie nafasi hizo kujificha ,kuna wangapi waligombania nafasi na hata kura yao haikuonekana kwa maana walipata sifuri ,inamaana hata yeye mwenyewe hakujipigia kura ,hapana hiyo ni mipango ya Sultani CCM kudhoofisha upinzani na kuudhalilisha ,wapi tunaelekea ni katika kuidai katiba mpya ya Nchi hii ,hili si lakulichezea au kulifanyia mchezo ni jambo la kufa na kupona ikiwa tunataka haki itendeke ni lazima Katiba ibadilishwe ,mahakama ziwe huru na hizi tume za kila siku ziwe huru ,zaidi ya hapo Sultani CCM kwa kutumia mawakala wake aliowapenyeza kila sehemu ndio watakuwa wakitupangia matokea na wakijaza kasumba waTz kuwa bila ya wao nchi haitakalika ,siku moja hii ruzuku itakuja kugomewa kwani inaonekana ni rushwa wanayopewa vyama vya upinzani ili kutishiwa kukoseshwa ruzuku ikiwa watasimama kidete ,ni wakati tu ndio tunaokwenda nao.

Naona Pro Safari ameaanza ,sijui ndio haya aliosema atayaandika hadharani ,aloo ataandika mengi sana na kutoa nyaraka nyingi sana ila ndio hivyo ameshapigwa na chini,sasa ndio anakata roho ,na inaonyesha alikuwa na agenda ya kuzivalia njuga hizi fedha ,ni hatari sana ,amemulikwa na kukurupushwa.
 
Ubishi hausaidii lolote! ukweli ni kwamba fedha ya CUF inatumiwa na maalimu seif alone ndio maana mikoa mingi ya bara haina hata ofisi za mikoa au wilaya kama watakavyoiita na wengine wamefukuzwa kwenye ofisi zao kwa kushindwa kulipa pango la ofisi la mwezi la Tshs 20,000/= tu nikutajie mkoa gani?
 
Hebu taja tuone ? Sasa utajenga kanisa au msikiti wakati hakuna waumini :D
 
vyovyote itakavyokuwa CUF imewekwa mkoni na maalim Seif, na ule msemo wa mzigo mzito mpe mnyamwezi ndio unapodhihirika hapo kwa Lipumba kuubeba mzigo huo
 
Last edited:
Kwa kiasi ambacho CUF wanapokea inakuwaje hawana mbunge Tanzania bara? au kushindwa vibaya kama kule Mbeya au Tarime? Kwanini hata maeneo ya pwani ambapo naweza kusema ni ngome yao (Tanga, Dar, Pwani) hawana mbunge hata mmoja!

Nafikiri unahitaji kwenda ndani zaidi katika uchambuzi wako. Ni busara ukajiuliza suala la nyongeza . Ni kwa nini hiyo CUF ikawa na uwezo wa kushinda kule Chanja-Mjawiri na Chokocho tu? na siyo popotepale pengine katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Alioleta hii ronyo anaweza kuweka na barua ya mwanzo ilikuwa na madai gani mbona naona kuna usanii ndani yake, inaonyesha kuna barua iliyoandikwa tarehe 17/02/2009 na hii iliyojibiwa tarehe 19/2l2009.

Inatoka kwa nani inakwenda kwa nani kukosekana kwa hayo itabidi upeleke hii mada kwenye udaku.
 
Tabora mjini ambapo CUF wanapaita Pemba B, wamefukuzwa kwa kushindwa kulipa pango na kwa sasa ofisi ina mama lishe na pembeni mwenye jengo kaweka Pool table, na viongozi wa CUF kwa wanakutana pembezoni mwa gest moja iliyopo jirani na ilipokuwa ofisi hiyo
 
Kama ni hio hakuna tatizo ,jamaa walikula fedha walizopelekewa,sasa huwezi kulaumu kuwa hawapelekewi ruzuku,pesa imepelekwa na wao wameitafuna tofauti na Pemba ambako wananchi wanataka mageuzi ya kweli hivyo wanakuwa waaminifu na hawababaiki kama wa huko ambao wakipewa bakuli la pombe anaachia kila kitu.
 
...tofauti na Pemba ambako wananchi wanataka mageuzi ya kweli hivyo wanakuwa waaminifu na hawababaiki kama wa huko ambao wakipewa bakuli la pombe anaachia kila kitu.
Pemba wakipewa nibu ya tende inakuaje? tena ile ya mtaimbo wa kwanza!
 
Hapo inabidi polisi azungume nao akiwa kama mita kumi si mchezo wanajua polisi anaeingia kwenye angazao hukumu yake ni kifo kwa kukatwa kichwa na sio kukatwa kuchinjwa.
 
Kwa kiasi ambacho CUF wanapokea inakuwaje hawana mbunge Tanzania bara? au kushindwa vibaya kama kule Mbeya au Tarime? Kwanini hata maeneo ya pwani ambapo naweza kusema ni ngome yao (Tanga, Dar, Pwani) hawana mbunge hata mmoja!

Hili swali linashangaza sana, ina maana ushindi hupatikana ukiwa na fedha. Kama ni hivyo CCM yenye ruzuku kubwa mno na pia rasilimali kibao ambazo walijilimbikizia toka mfumo wa chama kimoja ingechukua majimbo yote. Na ukumbuke CCM wanatumia hata rasilmali za Serikali. Kwa nini kwa mafedha yote hayo CCM wasishinde Pemba nako?.

Uchaguzi wa 1995 ambao ulikuwa wa kwanza wa vyama vingi, CUF iliweza kupata viti Unguja na Pemba, na wakati huo walikuwa hawana ruzuku. Sasa hii iliwezekanaje. Sasa fedha sio sababu ya kushinda, lakini inarahisisha kufanya zile shughuli za chama zinazoweza kusaidia ushindi. Hata CHADEMA ni ya tatu kwa kuwa na ruzuku, nayo haina Mbunge hata mmoja Visiwani (Unguja na Pemba).

Hivyo, kama CCM ikiweka tume huru, na mazingira ya uchaguzi yakawa huru, wapinzani nina uhakika wataongezeka kwa idadi kwenye nafasi ya Udiwani na Ubunge. Lakini kwa mazingira ya hii tume ya uchaguzi tuliyokuwa nayo, na TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa madiwani, hapa tunajidandanya kuweza kupata kile wananchi tunachotaka.
 
Pemba wakipewa nibu ya tende inakuaje? tena ile ya mtaimbo wa kwanza!

Wewe Kibunango, wakati mwingine acha utani wakati watu wanapojadili mustakabali wa Taifa. Kila siku wanywa tende, huna msamiati mwingine. Kuwa CCM sio sababu ya kila kitu cha mpinzani ukione ni upuuzi, wote tuko TZ tunapata matatizo sawa, labda useme mwenzetu na ndugu zako wote mko matawi ya juu.
 
Hili swali linashangaza sana, ina maana ushindi hupatikana ukiwa na fedha. Kama ni hivyo CCM yenye ruzuku kubwa mno na pia rasilimali kibao ambazo walijilimbikizia toka mfumo wa chama kimoja ingechukua majimbo yote. Na ukumbuke CCM wanatumia hata rasilmali za Serikali. Kwa nini kwa mafedha yote hayo CCM wasishinde Pemba nako?.

Uchaguzi wa 1995 ambao ulikuwa wa kwanza wa vyama vingi, CUF iliweza kupata viti Unguja na Pemba, na wakati huo walikuwa hawana ruzuku. Sasa hii iliwezekanaje. Sasa fedha sio sababu ya kushinda, lakini inarahisisha kufanya zile shughuli za chama zinazoweza kusaidia ushindi. Hata CHADEMA ni ya tatu kwa kuwa na ruzuku, nayo haina Mbunge hata mmoja Visiwani (Unguja na Pemba).

Hivyo, kama CCM ikiweka tume huru, na mazingira ya uchaguzi yakawa huru, wapinzani nina uhakika wataongezeka kwa idadi kwenye nafasi ya Udiwani na Ubunge. Lakini kwa mazingira ya hii tume ya uchaguzi tuliyokuwa nayo, na TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa madiwani, hapa tunajidandanya kuweza kupata kile wananchi tunachotaka.

Ndio maana yake lakini inaonekana wana agenda ya siri ,si tunafahamu vyombo vya habari vinavyotika kupotosha ukweli ,sasa hata Mwanakijiji nae anatumika ndio maana yake.
 
Mkuu Ngekewa nilikuwa nazungumzia wakati kabla ya Uhuru, hivi vyama vilipata fedha toka kwa wanachama wao. Ndio nikaandika sioni sababu sasa hivi vyama vya siasa kupewa fedha yote hiyo ya walipa kodi.

Labda wakati ule wananchi wenyewe walikuwa pamoja katika harakati za Mapambano na hivyo walikuwa tayari kujitolea kwa ajili ya vyama vyao. Hivi sasa huyo mwanachama anataka alipwe POSHO la kuhudhuria mkutano wa chama unafikiri watachanga kwa ajili ya kuwapa viongozi watanuwe matumbo yao. Itakapofikia kutokuwepo kwa ruzuku ni CCM pekee wataendesha shughuli kwani wao wanayo serikali na viongozi wao ni wakuu wa serikali hivyo hutumia fedha na nyenzo za serikali kuendesha shughuli za Chama.
 
Kwa maana nyingine mnataka kusema kuna ufisadi ndani ya CUF ,hapo mtakuwa sio mmepotea dira tu ,bali hata mnakokwenda hamkujui ,maana ukipoteza dira unaweza kubahatisha na kusema labda ni huku au kule.Nyinyi hampo mawazo yenu yamefilisika na kuona kuna ufisadi tu ,sasa kuna ufisadi ,haya nini faida mmepata hadi hii leo toka muoneshe na kugawa data za mafisadi naona mnapiga makelele mengi sana kiasi ya nchi kutikisika na wengine kuporomoka lakini data zinaonyesha walioporomoka wamepata pa kukamata na wanapanda juu.Au uongo ?

Fedha ipo na inatunzwa kushinda serikali inavyotunza fedha yake na haitumiki kwenye kampeni kama wengine mlivyopendekeza ,CUF haitatumia fedha kumlaghai mwananchi na kumdanganya au kununua uhuru alionao wa kuchagua kumnunulia kanga au kumuwekea pipa la mvinyo,Wanachama ndio watachangia kampeni za Chama Chao pale sehemu husika na Chama kitatoa sehemu ndogo tu ya kusaidia kama kuna kukodiwa jenerataz na vifaa vyengine muhimu na sio kuandaa masufuria ya pilau ,hilo halipo.
Halafu mnashindwa kuelewa kuwa CUF ni Chama Cha Wananchi tofauti na vyama vingine ambavyo huwa ni vya kundi fulani tu au genge la watu ,kuna vyama kibao havina hata ofisi katika upande wa pili wa Muungano nikikusudia kule Zanzibar.

Ilivykuwa hiki ni Chama Cha Wananchi kama kinavyojulikana kwa lugha yetu ya kiswahili ,wananchi wenyewe ndio wakukiendeleza na si kutegemea feza ya ruzuku na kwa msisitizo huo ndio ukaona Chama kimeenea sehemu kubwa hapa Tanzania ,kwani wananchi wamekipokea kama Chama chao wanachotarajia siku yeyote ile watakiwezesha kukipa dhamana ya kuwaongoza na kuwakata vichwa hadharani mafisadi wote pindipo watakuwa na hatia ya kuhujumu core ya uchumi wa Tanzania ,hivyo wataishia jela milele ikiwa watashindwa kurudisha senti tano ya mwisho wa fedha waliyokwiba au kuhujumu na kama haitoshi mali yao yote sio itasimamishwa bali itafilisiwa.

Kuna mtu amesikika akisema kuwa CUF haina mbunge hata mmoja T/Bara ni kweli inawezekana hivyo kwani ndivyo ilivyopangwa na Sultani CCM maana Sultani CCM ndio mwenye kushika vyombo vyote vya nchi hii ,anaamua na kupanga atakavyo hakuna wa kumzuia ,polisi wanafuata amri yake,majeshi wanafuata amri zake mahakama wanafuata amri zake ,sasa unategemea nini kama hao wengine sio walishinda ,bali waligaiwa hizo nafasi za ubunge ,huo ndio ukweli ,nafasi hizo wanazoringia ni za kugaiwa kutokana na mipango ya Sultani CCM ili atumie nafasi hizo kujificha ,kuna wangapi waligombania nafasi na hata kura yao haikuonekana kwa maana walipata sifuri ,inamaana hata yeye mwenyewe hakujipigia kura ,hapana hiyo ni mipango ya Sultani CCM kudhoofisha upinzani na kuudhalilisha ,wapi tunaelekea ni katika kuidai katiba mpya ya Nchi hii ,hili si lakulichezea au kulifanyia mchezo ni jambo la kufa na kupona ikiwa tunataka haki itendeke ni lazima Katiba ibadilishwe ,mahakama ziwe huru na hizi tume za kila siku ziwe huru ,zaidi ya hapo Sultani CCM kwa kutumia mawakala wake aliowapenyeza kila sehemu ndio watakuwa wakitupangia matokea na wakijaza kasumba waTz kuwa bila ya wao nchi haitakalika ,siku moja hii ruzuku itakuja kugomewa kwani inaonekana ni rushwa wanayopewa vyama vya upinzani ili kutishiwa kukoseshwa ruzuku ikiwa watasimama kidete ,ni wakati tu ndio tunaokwenda nao.

Naona Pro Safari ameaanza ,sijui ndio haya aliosema atayaandika hadharani ,aloo ataandika mengi sana na kutoa nyaraka nyingi sana ila ndio hivyo ameshapigwa na chini,sasa ndio anakata roho ,na inaonyesha alikuwa na agenda ya kuzivalia njuga hizi fedha ,ni hatari sana ,amemulikwa na kukurupushwa.

DU PUNDE TU NILIMSOMA AKISEMA KUWA APAKAZIWA UCAFU? Hii ndio raha ya uhuru!
 
Jamani 2.6 billions sii pesa nyingi hivyo! Ni 100 m kwa mwezi! sasa niambie Jamhuri ilivyo kubwa uanzie Matawini, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa kwa mikoa 26..tangu kule Muleba, hadi Mbinga mpaka Macho Manne- Pemba. Bado hujalipia magari, kampeni mbali mmbali, vikao mabli mbali na posho za waheshimiwa kama Seif na Lipumba! Chaguzi ndogo n.k

Hizi dola kama milioni 2 kwa mwaka sii pesa nyingi! Ni lazima tu CUF wawe na vyanzo vingine vya mapato!
 
Back
Top Bottom