CUF wanaruka na kukanyagana

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Tofauti kubwa imeendelea kudhihirika kati ya CUF Zanzibar na CUF Tanzania, baada ya maoni ya Hamad Rashid juu ya muswada wa katiba kupingwa hadharani na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Julius Mtatiro leo.
Akihojiwa kwanza kwa njia ya simu, Hamad alisema kuwa muswada hauna tatizo, na wabunge watafanya kaz yao vyema kuhakikisha kuwa Watanzania watapewa kitu wanachokitarajia. Muda mfupi baadae alihojiwa Mtatiro ambaye alisema muswada ni mbovu na msimamo wa CUF ni kuwa haufai. Alipoulizwa kuhusu maoni yaliyotolewa na Hamad kuwa hauna tatizo, Mtatiro alisema hayo yalikuwa maoni ya Hamad binafsi, na sio ya chama.

Nikabaki najiuliza; CUF wana jukwaa gani refu la kuongelea zaidi ya bungeni?
Kama jukwaa refu ni bungeni, CUF bungeni wanawakilishwa na Wazanzibar (ukiacha mh wa Lindi), na maoni ya Hamad, bila shaka ndiyo maoni ya CUF Zanzibar.
Alafu nikajiuliza maoni ya Naibu katibu mkuu ndiyo maoni ya Katibu mkuu mwenyewe?!!!
 
Hapo ndiyo wana CUF wa huku bara waelewe kuwa wao ni maboya tu wenye chama wako huko visiwani,ieleweke wazi kuwa wazanzibari linapokuja jambo la kuhusu Zanzibar wao wanakuwa kitu kimoja bila kujali CUF au CCM, na kwa vile kule Zanzibar CUF na CCM wameunda serikali ya pamoja usitegemee kuwa Mzanzibari yoyoye hata akiwa CUF anaweza kuipinga CCM.Nyie wakina Mtatiro tieni akili, wenzenu wanawafanya nyie mavuvuzela tu.
 
Ni vizuri MTATIRO yeye aweke maslahi mbele ya CUF bara chama kiliasisiwa na Mapalala akaporwa na Kamahuru ya Pemba mwache asimamie wapenzi wa CUF Tanganyika bwana
 
Hii kali,bara wanapinga visiwani wanakubali!! mwisho kabisa seif anapigiwa saluti Prf.anaangukiwa na saluti
 
Tunakaribia kupata jibu ya swali lillilokuwa linatusumbua kwa muda sasa kuwa kuna CUF mbili na CCM mbili yaani ya bara na visiwani? Kwani hii ndiyo pekee ingewezesha CUF kuwa mbia wa CCM na mpinzani kwa wakati mmoja

Go - CUF Go!
 
Kumbe ndiyo maana wamechagua Dodoma na Dar pekee kwa sababu visiwani hawaoni tatizo na tukumbuke bara tuna more stake in the katiba after all visiwani tayari wana katiba yao na serikali yao.
 
CUF inakufa, na hii inatokana na dhambi ya usaliti. Wamepata kuunda serikali Zanzibar, sasa hivi CUF Zanzibar ipo upande wa CCM na kutokana na Chama hicho kuwa na nguvu huko, basi wanawaburuza CUF-Bara wawe kitu kimoja na CCM. Lakini ukweli ni kuwa CUF bara wanaanza kuchoka, Chama kitapasuka.
 
I call upon Mtatiro, to review his future political plan...
 
Back
Top Bottom