CUF wamtaka Jintao Z'Bar

Mkuu Ngekewa nimejaribu kusoma hapo juu, nimeshindwa kuelewa. Nilidhani mada iliyopo hapa ni kwanini Hu Jintao hakwenda Zanzibar na Wazanzibar wanaona sio fair. Sasa hili la mafisadi linahusika vipi ndugu yangu?



Mkuu mwenzangu kama utafatilia quote utaona kuwa mtu amegeneralize kuwa Wazanzibari wanapenda kulialia akimaanisha kuwa wao wanalalamika. Sasa nikujuvye kuwa hao Wazenji wanalalamika kwasababu kuna mambo yanayowakera na kila yakirejewa basi hawatoacha kulalamika kama sisi huku Mrima tunavyokerwa na ufisadi na kila mara hatuachi kulalamika nao na ndio maana nikasema kudai haki mtu hachoki na kama huku Bara kunavyochukuliwa hatuwa zidi ya ufisadi kwa kilio chetu cha kila siku pengine huku kulialia kwao kutawafanya muwape haki zao. usipofahamu nipo.
 
Mwiba,

Kaazi kweli kweli!

Yaani posts zako hakuna Thanks hata moja!!! kwa nini?

Fanya reality check...kuna taabu mahali nadhani!

Maneno mengi!!! Substance kidogo!!!

Samahani ndugu na rafiki yangu!

Pengine kama jina lake anawachoma wengi kwani ukweli unauma.
 
Bwana wa Arusha wana yao na husikia wakilalamika katika bunge la Tanganyika. Hawa Wazanzibari hawawakilishwi mambo yao kwenye Bunge la Tanganyika.
Jee unaonaje Ziara zikawa zinafanyika Zanzibar tu nanyi mkawa mnawakilisha na MH. Mbowe?


really? hao wabunge kutoka zanzibar huwa wanawakilisha maslahi ya nani kwenye bunge la jamhuri ya Muungano? tanganyika hakuna bunge.
 
really? hao wabunge kutoka zanzibar huwa wanawakilisha maslahi ya nani kwenye bunge la jamhuri ya Muungano? tanganyika hakuna bunge.

Masilahi ya Tanganyika ili ionekane kuwa upo uwakilishi wa Zanzibar. Kwa hakika sijawahi kusikia mbunge wa Zanzibar akizungunza mambo ya Zanzibar kwani kwa utaratibu hayashughulikiwi na Bunge. Mambo wanayoshughulika nayo ni machache yaliyolazimishwa na Muungano lakini wanalipwa hata kukaa wakati kukizungumzwa mambo ya Mwanza au KIgoma. Hii ni moja ya geresha za Muungano usidfahamika.
 
Back
Top Bottom