CUF wameshtukia nini kidongo chekundu kwa ghafla namna hii??

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
Katoliki wasogeza mkutano wa CUF


na Asha Bani

amka2.gif

MKUTANO mkubwa wa hadhara uliokuwa ufanywe na Chama cha Wananchi (CUF) katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam kesho, umeahirishwa kutokana mkutano wa kimataifa wa uponyaji unaoendeshwa na Kanisa Katoliki, jimbo la Da es Salaam.
Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho jana, ilisema kuwa mkutano huo umeahirishwa baada ya majadiliano ya muda mrefu kati yao, Kanisa Katoliki na mamlaka za wilaya ya Ilala.
“Tumekubaliana kuwa Wakatoliki waendelee na mkutano wao wa kimataifa wa uponyaji ambao utachukua takriban mwezi mzima.
Maombi yetu na yao yalifika pamoja sasa kilichofuata ni kukubaliana na kwa sababu chama chetu hakina makuu tumekubali kuwapisha wenzetu kwa sababu itakuwa vigumu wao kukatisha mkutano wao halafu waendelee tena,” alisema Mtatiro.
Alisema kuwa walitizamia kupata kiwanja kingine lakini utafiti umeonesha uwanja huo wa Jangwani ndiyo pekee unaoweza kuhimili shughuli za chama chao kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa hiyo wanasubiri Wakatoliki wamalize kisha watafanya mkutano wao.

Mtatiro aliongeza kuwa kwa sasa wanaendelea na operesheni mbalimbali na wiki ijayo watakuwa mkoa wa Morogoro kwenye baadhi ya wilaya.
Hivi karibuni vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA vimefanya mikutano ya kuhamasisha uhai wake jijini Dar es Salaam iliyofanyika kwenye viwanja hivyo vya Jangwani na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi.

 
ni kweli chama cha watu makini ila siasa itabaki kuwa mchezo mchafu......
 
Kama CCM walikwishafanya mkutano inatosha sasa CUF wanataka kurudia yaleyale au ni kukazia?
 
wameogopa kuwa na mskitiki wao maarufu wa Mtoro sasa wanataka kuonyesha kwamba si Uislam ni Chama kwa kwenda Jangwani
 
ndo nn sasa yaani udini umekujaa moyoni sasa ushaanza kutokea machoni,huoni chochote zaidi ya udini habith la amar ww
wameogopa kuwa na mskitiki wao maarufu wa Mtoro sasa wanataka kuonyesha kwamba si Uislam ni Chama kwa kwenda Jangwani
 
wapendwa njiwa, Lunyungu, mtznunda Dabudee Chatumkali, na wengine,

hebu angalieni statement hii:

Alisema kuwa walitizamia kupata kiwanja kingine lakini utafiti umeonesha uwanja huo wa Jangwani ndiyo pekee unaoweza kuhimili shughuli za chama chao kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa hiyo wanasubiri Wakatoliki wamalize kisha watafanya mkutano wao.

concern yangu ni kuwa, iweje siku zote CUF wamekuwa wakifanya mikutano yao kidongo chekundu ila sasa mtatiro anasema ni jangwani pekee ndo panaweza kukusanya wanacuf wa dar. wale waliokuwa wakikusanyika huko nyuma ni wanacuf wa wapi? au ndo mtindo wa kuiga mikumbo ya ccm na cdm waliowatangulia? ina maana ubunifu siku hizi umeisha kabisa hadi kila kitu watu wanaigana? hata viwanja vya mikutano imekuwa kuigana?

hahahaaaa

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom