CUF wafuta maandamano yao

No way kwa hali ya ubungo na usalama wa wamarekani ilikuwa lazima wakubali CUF nawapongeza...sasa ameondoka waombe tena watapewa kibali ni haki yao kimsingi
 
Golden Chance gani wakati walikuwa hawana la kusema au kuwakilisha mbali na makelele and mbio za barabarani
 
CUF- Tumeheshimu maslahi ya taifa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th June 2011 @ 07:23 Imesomwa na watu: 36; Jumla ya maoni: 0

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa kililazimika kusitisha maandamano iliyopanga kufanya jana baada ya kuombwa kufanya hivyo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Ofisa Habari wa CUF, Abrahaman Lugone aliliambia gazeti jana kuwa Pinda alizungumza moja kwa moja na mwenyekiti wa chama hicho Ibrahim Lipumba akamwomba wasitishe maandamano hayo kutokana na ugeni wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton.

Lugone alisema baada ya Pinda kuzungumza na Profesa Lipumba kuhusu ugeni wa Zaziri huyo wa Marekani, chama hicho kilitafakari ombi hilo na wakakubaliana kusitishwa kwa maandamano hayo kwa maslahi ya taifa.

Alisema uamuzi huo ulikuja baada ya Profesa Lipumba kufanya kikao cha dharura na wabunge wa chama hicho ambao walikuwa wamewasili Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki maandamano hayo.

Kikao hicho pia kwa mujibu wa Lugone kilihudhuriwa na wajumbe wa baraza kuu waishio Dar es Salaam, wakurugenzi wa idara za chama hicho na maofisa wa chama walijadiliana kuhusiana na maombi hayo ya Serikali.

"Baada ya majadiliano yale ndipo ikakubalika kuwa tusitishe maandamano ya leo (jana)," alisema Lugone ambaye katika mazungumzo yake alikiri kuwa ushauri wa awali uliokuwa umetolewa na kamanda wa polisi wa kanda ya Dar es Salaam Suleiman Kova, Mkuu wa Polisi IGP Saidi Mwema na ule wa Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa ulishakataliwa na chama hicho.

Alipoulizwa kwa nini hawakutoa taarifa kwa vyombo vya habari, Lugone alisema baada ya kikao kile cha dharura kumalizika Profesa Lipumba alizungumza na baadhi ya vituo vya radio ili kuwataarifu wafuasi chama hicho juu kusitishwa kwa mazungumzo hayo. "Pia tulizungumza na shirika la utangazaji (TBC) kwa kuwa tuliona kuwa tusingewahi taarifa za magazeti," alisema ofisa habari huyo.

Katika TBC, Profesa Lipumba alisema kwamba anabeba dhamana ya kisiasa ya kusitisha maandamano hayo, ambayo hata hivyo alisema yataitishwa tena katika siku nyingine.

Ofisa habari huyo alisema kwa kuwa maandamano hayo yaliandaliwa na chama, ofisi za wilaya za chama hicho mkoani Dar es Salaam zilitumika kuyataarifu matawi juu ya kusitishwa kwa maandamano hayo.

CUF ilipanga kufanya maandamano jana kulaani matukio yaliyofanywa na polisi katika wilaya ya Tarime mkoani Mara na Tabora wilayani Urambo.

Katika maeneo hayo baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo maandamano hayo awali yalizuiwa na jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Kova alipiga marufuku maandamano hayo kwa madai kwamba kutakuwa na ugeni wa Clinton.

Katika sababu zake alizozitoa, Kova alisema kutokana na ugeni huo ambao pia utaitumia barabara ya Morogoro itakuwa ni vigumu kwa jeshi hilo kutoa ulinzi kwa maandamano na mikutano ya chama hicho.

Pamoja na amri hiyo ya Polisi, CUF kupitia kwa naibu katibu wake mkuu Julius Mtatiro waliahidi kuendelea na mipango yao ya kuandamana kwa madai kuwa sababu za polisi zilikuwa ni ghiliba ya kutaka kukidhoofisha chama hicho na hivyo wasingekuwa tayari kuahirisha maandamano na mikutano yao.
 
CUF kweli CCM B, yani ujio wa Clinton wasitisha maandamano,mbona nchi za wenzetu viongozi kama hawa wakitia timu maandamano kila kona.Nafikili wangetumia ujio wake kufikisha ujumbe.
Hii ya CUF imenikumbusha mbali sana, huku mikoani kukiwa na ugeni either raisi,waziri mkuu,makamu wa raisi, mawaziri etc yani barabara zote zitasafishwa,mji utawekwa safi,zile barabara korofi wataweka vifusi akiondoka tu tabu ile ile kama kawaida.
 
tunawapongeza cuf kwa kusitisha maandamano .heshma kama hii ndiyo inayotakiwa.subirini mama clinton akiondoka ndio mlianzishe au vipi?
 
Hongereni sana CUF, Hongera bwana mtatiro kwa kuonesha umekomaa kiuongozi na kisiasa.

Nadhani unaweza kumshauri lipumba na mkakuza chama chenu kuliko kukaa na kusikiliza CDM au CCM wanataka mfanye nini.

Mimi binafsi sikuona haja ya kuandamania ubungo wakati kuna kiongozi wa kitaifa wa taifa lingine yuko mahali hapo, ni bora mngebadili eneo mapema na kama polisi hawakuwajuza kuhusu hilary kutembelea mitambo ya dowans wanapaswa pia kupewa lawama.

Kazi ya kiongozi ni kuamua vizuri, hakukuwa na haja ya kuandamana ili kumuonesha CLINTON, yeye atarudi kwao na madai yetu hayapaswi kusikilizwa na mataifa ya kibeberu.
Jambo muhimu ni kutizama kama mnaweza kuandamana tena kama ulivyosema, kwa sababu ajenda mnayo mkononi na haija-expire hakuna ubaya iwapo mtaandamana hata next week.

Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha hampotezi matumaini ya wananchi ambayo umeanza kuyasimamia.
Nafahamu lipumba ni kiongozi mzuri na hakuwa na msaada kama unaompa, just hold on na mtafanya vizuri.

Wanaowaita CCM B wasikutishe kwani CUF haikuibembeleza CCM waunde serikali pamoja. Ni matakwa ya wazanzibar na ni matakwa ya kikatiba, kilichoiweka CUF serkalini zanzibar ni ushindi mlioupata na siyo huruma ya CCM.

Wanaowaponda hawana hoja zenye mshiko, kazi ya chama cha siasa ni kutafuta dola na kutoa uongozi thabiti, kila mnapopata fursa ya kuunda serikali kwa nguvu ya kura zenu fanyeni hivyo. Njooni hadi mwanza hapa, nyamagana, ilemela na ukerewe jamaa wameanza kuchemsha, njooni mjiimarishe kwani uongozi siyo maneno matupu ni vitendo.

Wanaounda vyama kupiga tarumbeta waacheni waendelee, mwongo huumbuka hapahapa.

Aluta kontinyua mtatiro, mpiganaji nambari 1 utakayekumbukwa na vizazi vyote UDSM.
 
CUF kweli ni urojo mtupu hahhaas lipumbaaaaaaaa yaani eti mnaahirisha sababu hiyoooo? halafu mkiitwa ccm b mnakasisirika. hayo maandamano hayana nguvu tenaa.
 
Waziri mkuu aliwaomba CUF wasiandamane wakakubali, kama Prof. alivyoomba Magdalena aachiwe baada ya kuwekwa sero muda wa kutosha naye akakubali. Kwa ushauri wangu haipo haja ya kuandamana tena, labda waandamane kupongeza hatua ya Wamarekani kuanza kutatua matatizo yetu tuliyoshindwa wenyewe., na kumpongeza Mkuu kwa jukaribisha wageni wanaotujali. :cool2:JINO KWA JINO hapana!
 
Binafsi nashangaa hawa jamaa maana polisi iliwanyima kibali lakini wao wakasema ni lazima wataandama! Nawashukuru viongozi wa CUF kwa kupokea na kuubali ushauri.
 
Back
Top Bottom