CUF wafuata mkia wa CHADEMA kuwaunga mkono maandamano nchi nzima

Apr 9, 2011
38
3
Chama cha wananchi CUF kimeamua kuandaa maandamano ya nchi nzima ya kupinga mauaji na unyanyasaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi hapa nchini, hayo lalielezwa na naibu katibu mkuu wa CUF Julius Mtatilo wakati alipokuwa akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari.

CUF ilidhihilisha kuwa kumbe CHADEMA wako sahihi kabisa jinsi wanavyofanya maandamano yao japo vyama vingine vya siasa vinawapinga,

Haya maandamano ya CUF wameamua kuyaandaa baada ya mtu mmoja kupigwa risasi na polisi na kufa hapohapo huko Tabora na mbunge wa viti maalumu kukamatwa na polisi kwa kusema kuwa anafanya mikmutano bila kibali..
Hayo ndiyo yaliyojili ndugu zangu
Chanzo cha habari ni CLOUDS TV.
 
Maandamano yafanywe na wengine akifanya CDM ni jambo baya! Mwisho wa siku wote watarudi kudai haki zao zinazo potezwa kwa maandamano ama kama yale ya Afrika Kaskazini au kama ya CDM. Peoplezzzzzzzzzzzzzzzz Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer
 
Nilifikiria CUF wame forego their civil liberty kutokana na ushirikiano wao na ccm, kwa maana wamepiga kelele sana kuwapinga chadema wanapopigania CIVIL LIBERTY za watanzania kwa kutumia nguvu ya umma.

Ukistaajabu ya musa, utaona ya filauni!
 
CUF kuna mke mdogo na mkubwa, mke mdogo ndio hawara ya CCM na mke mkubwa hayuko tayari kuchezewa na mwanaume mwingine, hapo ndo patashika ya nguo kuchanika mwaka huu.
 
Ndoa yao imekuwa marriage of betrayal and convenience!

CUF ina mke mkubwa na mdogo, mke mdogo katekwa na dume lenye uchu wa vimwana, mke kubwa kakataa kwani nuksi kwake kuchanganya damu. Mwaka huu ni pata shika ya nguo kuchanika, piga huku piga kule, kila wanapojaribu kugeukia kupata nafuu ni makonde tu, kweli inakolea.
 
huu nao ni ujinga wa kisiasa kama sio upumbavu. hata wakiuawa wayu wangap kwa kuwa tu inaaminika ni wafuasiw a chadema basi cuf hawaandamani kupinga wala hawawaungi mkono chadema katika kupinga, akiuawa mmoja tu anayesadikiwa kuwa mwanachama wa cuf utasikia,,, aaa kumbe chadema wao sahihi!!... mazezeta haya!! ndo yanaamka sasa na kubaini uvunjwaji wa haki za binadamu baada ya mtu wao kuuawa. kumbe hata mtu wa ccm akiuawa na ccm wataamka!

siasa gani hizi hadi watu mtu wako auawe ndo ujue thamani ya binadamu na ukatili wa polisi? ina maana tanzania ya leo chama kinapanua domo lake pale tu mwanachama wao anapouawa?

nashauri chadema wajitokeze katika maandamano yatakayoitishwa na cuf kulaani mauaji haya ili kuonyesha kuwa chadema wanalaani mauaji ya raia yanayofanywa na polisi bila kujali itikadi za kisisa na hapo watadhihirisha ukomavu wao na kupata crediti zaidi katika harakati zao za kutetea haki za binadamu
 
Naomba maandamano ya CUF yaongozwe na viongozi wakuu wa CUF akiwemo Maalim Seif. Bila Maalim Seif hayo maandamano hayatakuwa na maana kwani chama bila viongozi wakuu ni unafiki na uzandiki.
 
Chadema ni kama katapila linachonga barabara na wengine wanafuatia,tulivyoanza Chadema kufanya maandamano Cuf walitutupia vijembe sn Leo wanakula kile kile walichokitapika.Chadema go go go peoplesssssssss powerrrrrrrrrrrrrrr .
 
Back
Top Bottom