Elections 2010 CUF sasa yairarua CHADEMA Igunga; Hamad Rashid Mohamed asema CHADEMA sio chama cha kitaifa

WANASIASA WA TANZANIA BWANA! UCHORO SANA.

SASA KAMA CHADEMA SIO CHAMA CHA KITAIFA, Mhe HAMAD RASHID SI AENDE KWA MSAJILI WA VYAMA ILI CHADEMA KIFUTWE KWA KUKEUKA SHERIA ZA USAJILI WA VYAMA?
 
Huyo hamadi bila kuitaja chadema hawezi kujenga hoja kwani anajua kwa kuitaja chadema ndio anapata attention.
Naona marupurupu ya kiongozi wa upinzani bado yanamtoa roho.
Mwenziye Mbowe hana shida na hayo marupurupu ndio maana hata shangingi alilirudisha.
Poor hamadi, anazidi kwisha.

Nani alikuambia Mbowe alirudisha shangingi lake ? mpaka sasa analitumia ! uliza watendaji wa bunge watakuambia
 
Majira News



Mbunge wa Lindi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Salum Baruani akihutubia wananchi wa Kijiji cha Ngwamashimba wilayani Igunga wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona jana.

*Yadai haijakomaa kisiasa, si cha kitaifa

Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewataka wananchi wa Igunga kutokipigia kura Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa si chama cha kitaifa na hakijakomaa kisiasa.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohamed, wakati akimnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Bw. Leopold Mahona katika viwanja vya Barafu mjini hapa.

Mbunge aliwahi kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni kabla ya Bw. Freeman Mbowe wa CHADEMA kuchukua nafasi hiyo, alidai kuwa chama hicho hakijakomaa kisiasa ndiyo maana kinajihusisha na vitendo vya vurugu ikiwemo kumwaga tindikali, kupiga risasi na mengine na kwamba hiyo inaonesha hakiwezi kuleta maendeleo ya wananchi.

Alisema chama hicho kina ubinafsi, ndiyo maana kilijitenga bungeni na kuunda umoja wa wabunge wa CHADEMA peke yao tofauti na wakati alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo alishirikisha wabunge wa vyama vyote vya upinzani wakiwemo wa chama hicho bila ubaguzi.

Alidai sera za CHADEMA hazina tofauti za CCM ambao wanagawa madaraka kwa watoto wao, ndugu na jamaa badala ya kufuata utaratibu wa uongozi katika jamii.

Bw. Rashid aliyewasili mjini hapa juzi na helkopta ya CUF kujumuika na wabunge wengine wa chama hicho hivyo kufanya idaid yao kufikia 20, alisema chama chake ni cha kitaifa ambacho kina viongozi pande zote za muungano.

“Makamu wa Rais Zanzibar ni Katibu Mkuu wa CUF, sisi wabunge wa Zanzibar tumekuja kwa gharama zetu kumsaidia mwenzetu aingie bungeni kuwakomboa watu wa Igunga, niambieni CHADEMA kuna kiongoi gani Zanzibar,” alihoji Bw. Rashid.

Alisema wananchi wa Igunga wakitaka maendeleo ya kweli wamchague, Bw. Mahona kuwa mbunge kwa kuwa wana kila sababu ya kufanya hivyo ili kubadilisha maisha yao.

Naye Meneja Kampeni wa mgombea wa CUF, Bw. Antony Kayange, alisema wapiga kura wasipoteze muda kukipigia kura CCM kuwa wanakumbuka kumleta Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli kuwaongopea.

Alisema anawadaganya kujenga daraja la mto Mbutu ambalo limeahidiwa kujengwa miaka mingi iliyopita bila ahadi hiyo kutimizwa.

“Huyu Magufuli amekuwa madarakani kwa miaka 11 mbona hata siku moja hakufikiria kuja Igunga angalau kuona kero za wananchi, leo anakuja kudanganya kujenga daraja la Mbutu huo ni uongo, msikubali kurubuniwa kupigia kura CCM,” alisema Bw. Kayange.

Naye Naibu Katibu wa CUF Tanzania Visiwani, Bw. Ismail Jussa, alisema wananchi wa Igunga wasikubali kudanganywa na vyama vingine kwa kuwa wataendelea kukabiliana na matatizo waliyonayo bila kupata ufumbuzi.

Alisema katika majimbo ambayo CUF inaongoza yana maendeleo makubwa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kujenga hoja za wananchi na kuziwasilisha serikalini kufanyiwa kazi.

Mgombea ubunge Bw. Mahona akiomba kura kwa wananchi alisema kamwe hatakimbia jimbo lake kama wanavyofanya wabunge wengine bali atatumia muda wake mwingi kuwatumikia wananchi wa Igunga.

Siku zote nasema CHADEMA sio chama cha siasa, na ni kosa kubwa kukisajili kwa msajili wa vyama vya siasa. Wao ni WANAHARAKATI ambao wanatakiwa waajili NGO chini ya wizara ya mambo ya ndani
 
Natamani mlioko humu siku moja mpande kwenye haya majukwaa ya kisiasa nione na kusikia mtasema nini.
 
CUF ni chama cha kidini,ukimuondoa mtatiro ambaye naye naona siku hizi ana SIJIDA,kuna kiongozi gani mwingine ambaye sio muislamu,CUF hawana hata mbunge mmoja wa dini ya kikristu,ni chama cha waarabu.

Mkuu Omega,
Naomba unisaidie na hapa hichi ni chama cha dini gani?

Mbunge wa Iringa Mjini Mchungani Peter Msingwa.
mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse.
Mgombea urais Padre Slaa.
Mbunge wa Arusha Mjini Goodbless Lema, huu mwaka 1999 wakati anakaa Mwanza alikuwa na Kanisa lake maeneo ya Pasiansi.
Kaka unaishi kwenye nyumba ya vioo halafu unaanza vita vya mawe? Hawa ni CDM
 
Hii nguvu wanayotumia kukashfiana baina ya vyama laiti kama wangewekeza hivyo hivyo kuelezea uzuri wa sera zao labda ccm wangeshaondolewa siku nyingi.

Unatueleza kuwa wale wabaya, sawa tumekusikia; lakini hiyo haikufanyi wewe uwe chaguo mbadala na iwapo hamkujipambanua vizuri, watu wa vijijini siku zote wanaona bora 'zimwi likujualo'
 
Huyu Mzee kweli anazeeka vibaya anatakiwa apumzike asije akafia jukwaani iv swala lakwamba wanatumia gharama zao ni swala lakuwaambia Wanaigunga kwanza linawahususu nini!!ni nani amewaita kama sio kujipendekeza na viherehere vyao huyu Jamaa huwa ye anawaza ni vipi atapiga ela ndomana Kihoro cha ule uongozi wa kambi ya upinzani bado una muuma sana.
 
Kwa hiyo Hamad Rashid (CUF) wameshahakikisha kuwa CDM ndiyo waliomwagia mtu tindikali, na kupiga risasi? mbona hajamalizia na kuchoma banda la kuku? Wakati waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani anasema jeshi la polisi litatumia kila aina ya nyenzo zake kuwapata waliohusika na kumwagia mtu tindikali, yeye Hamad anajua kuwa ni CDM, yaani ni mjuaji kuliko Polisi.Yaani anathibitisha kuwa wapo pamoja na propaganda za ccm katika kuwahadaa wananchi.

Katika watu ambao wanatuhakikishia kuwa CUF ni mke wa CCM ni huyu bwana. Anazidi kuwaharibia CUF, ndiyo maana hata wakamtimua kwenye kuongoza kambi yao ya wabunge.
 
Waangalie tu hizi kampeni zao za Ubaguzi zinaweza kuwafanya hata wasifikishe kura 5,000 huko Igunga! Sembuse zile 11,000 wanazojitambia nazo...
 
Muulizeni Huyo Hamadi Rashid Mahamuma kuwa hiyo Helkopter wamelipiwa na nani? maana kunatetesi kwamba CCM ndiyo imegharimikia kupatikana kwa hiyo Chopa anayojidai nayo. Yaani leo Hamad kupanda hiyo Chopa tayari CCM wamekuwa Malaika kwake. Siasa uchwara. Damn.
 
Hamad..anatabia za Kishoga sana...na hilo ndo litamponza KATIKA SIASA ZA MBELENI...AU anataka kuolewa mke wa 2? maana CDM wakichukua madaraka, CCM ni mke mkubwa, basi CUF atakuwa nyumba ndogo, labda ndo analoogopa na kuanza kuropoka. Shame up on Sherrif Hamd
 
Nilisema hapa jf kuwa yule kiongozi wao cuf aliyepigwa na green gurd yaacheni kwani hayo ni mambo ya ndani ya mke na mume wataelewana hao, watu wakapuuza wakaendelea kuilaani ccm, kiko wapi sasa! mnaumbuka, mssipende kuingilia mambo ya ndani ya mume na mke
 
Back
Top Bottom