CUF sasa wawapigia magoti CHADEMA

Ritz, busara kidogo inaweza kuhamisha mlima. Kusoma UDSM sio tija, nimesoma hapo, JK amesoma hapo so what? Viongozi wengi walioko madarakani wamesoma hapo lakini tupo hapa tulipo!!

Usomi sio kigezo pekee cha uongozi bora.

Really only those days not this world! ukipenda usikose busara na hekima
 
Hoja ya msingi ni 'umuhimu wa vyama vilivyo nje ya serikali ya Muungano kushirikiana'. CDM watafanya uamuzi baada ya kuangalia faida na hasara za ushirikiano huo.
 
Kwa habari ya CDM kufadhiliwa na kada wa CCM, Sabodo, sioni tatizo. Tatizo ni USAFI wa ufadhili wenyewe. Mzee Sabodo usafi wa biashara zake hautiliwi shaka, ni miongoni mwa matajiri wachache wa nchi hii ambao ni wafuasi safi wa falsafa za Mwalimu na mchambuzi aliyebobea wa masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii - laiti kama ungekuwa umewahi kusoma angalau makala zake ungefahamu kitu fulani kumhusu. Huwezi hata kwa nukta wala yodi moja kumlinganisha Mzee Sabodo na sijui na mijizi gani ile.

Kuhusu CUF kuipa kwanza talaka CCM ili kunda kambi ya upinzani Bungeni mimi nadhani ni kinyume chake; CUF waombe kwanza talaka (na sio kutoa) - na bahati mbaya mwenye mke anaweza kuamua kutoitoa hiyo talaka - kazi ipo.
 
Cdm wana option 2. Wawakubali then wakiboronga wawatimue, au wawakatae then wakiwahitaji wacwapate tena. Binafsi naona wawakubali, wakiboronga wawatimue. bado ni mapema kucontain matatizo yao na kuyarekebisha.
 
hahahaha!!!

kwani ukihitimu madrasa al sul unakuwa msomi?

kama ni hivo mimi nitaslimu kwa kuwa nina ham kweli ya kuitwa msomi.

1.Ibrahim lipumba UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
2.Juma Duni UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
3.Ismail Jussa UNIVERSITY OF HULL CITY. UK
4.Hamad Rashid UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
5.Julius Mtatiro UNIVERSITY OF DAR ES SALAA
6.Maalim seif UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
hiyo ndio safu ya viongozi wa CUF sasa sijui utasilimu dini kama ulivyosema..basi kama uwezi kusilimu nipe tig...unadhani watu wote wajinga kama wewe kwanza na wasiwasi na Elimu yako kama umesoma chuo basi chuo cha kata kama viongozi wako kina mbowe na wenzake..Viongozi wasomi Chadema ni wawili tu ZITTO na LISU..UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.
 
Kwa habari ya CDM kufadhiliwa na kada wa CCM, Sabodo, sioni tatizo. Tatizo ni USAFI wa ufadhili wenyewe. Mzee Sabodo usafi wa biashara zake hautiliwi shaka, ni miongoni mwa matajiri wachache wa nchi hii ambao ni wafuasi safi wa falsafa za Mwalimu na mchambuzi aliyebobea wa masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii - laiti kama ungekuwa umewahi kusoma angalau makala zake ungefahamu kitu fulani kumhusu. Huwezi hata kwa nukta wala yodi moja kumlinganisha Mzee Sabodo na sijui na mijizi gani ile.

Kuhusu CUF kuipa kwanza talaka CCM ili kunda kambi ya upinzani Bungeni mimi nadhani ni kinyume chake; CUF waombe kwanza talaka (na sio kutoa) - na bahati mbaya mwenye mke anaweza kuamua kutoitoa hiyo talaka - kazi ipo.

Sabodo unamjua wewe? anauza ile kitu mbaya..kabisa
 
Kama kuna kipindi Muhimu katika siasa za CHADEMA Basi ni hiki, Uamuzi wa CUF, NCCR,TLP,UMD wa Kumuandikia Baruwa Mhe Mbowe na Kumuomba awashirikishe katika Kambi ni Ujasiri na Ukomavu wa Kisiasa wa Vyama hivyo nasema Hongera hAMAD rASHID na Viongozi wa Kambi ndogo, Ushauri wangu kwa Mhe Mbowe kuwa jasiri yasahau ya Nyuma weka Maslahi ya Kambi Mbele ubinafsi utupe mbali, nyosha Mikono yako uwapokee wenzako kwania safi ufanmye nao kazi kwaaslahi ya Watanzania Wanyonge walio wengi waliokandamizwa na CCM, vyenginevyo ukiwapuuza na Kuwakatalia wenzako ukasahabikia Utengano na kusaikiliza Kiburi cha Wapambe wako basi majuto yatakuja baadae. nchi hii haiwezi kukombolewa na Chama Kimoja bali vyama vyote dhidi ya CCM.
Nakuomba tena Mwenyekiti Mbowe tujengee historia Mpya ya Upinzani ndani ya Mkutano Huu unaoanza sasa ndani ya Bunge. DAMU za Mashujaa waliodhulumiwa ARUSHA zinataka Kutetewa na zile zilizopotezwa kila palipo na wanamageuzi nazo zinataka Kuenziwa.
 
Wakaribishwe ila wapewe angalau vyeo vitatu,wakijikanyaga tu watimuliwe nadhani ita washisha zaidi wao na vyama vyao na kuonesha watanzania kwamba ni wasaliti My point ni kwamba: Huu ndo mda pekee wa kuonesha watanzania kwamba kuna chama kimoja tu cha upinzani,i wish ningekuwa mbowe au mbunge ndani ya chadema! Wakaribisheni,wakiharibu waharibieni vi-deadly
 
Hawa jamaa walishafunga ndoa na CCM, hapo hapo wanahitaji kujamiiana na CDM, je wana mapenzi kweli na CDM?
iNAWEZEKANA wakawa na nia ya ukombozi lakini approach yao haikuwa nzuri sana, kwani toka mwanzo wamekuwa wakiikandia CDM kama wao sio chama cha Upinzani.
Pili, kuwa kuwakubali kama wakiwa na nia nzuri will be a milestone idea kwa sababu kila hoja itakayoibuliwa bungeni wapinzani watakuwa na nguvu sana wala hawatayumbishwa...

Mkuu,
Hapo red
Ushabiki mwengine hauna maana.
Lugha hii haisaidii katika kuwaunganisha wananchi.
Hata kama wewe ni CHADEMA, huisaidii CHADEMA kwa matumizi ya lugha kama hii.
CDM wanahitaji kila nguvu itakayokuja upande wao.
Fikirieni kabla ya kuandika, kusema. Busara wana chadema.
 
1.Ibrahim lipumba UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
2.Juma Duni UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
3.Ismail Jussa UNIVERSITY OF HULL CITY. UK
4.Hamad Rashid UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
5.Julius Mtatiro UNIVERSITY OF DAR ES SALAA
6.Maalim seif UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
hiyo ndio safu ya viongozi wa CUF sasa sijui utasilimu dini kama ulivyosema..basi kama uwezi kusilimu nipe tig...unadhani watu wote wajinga kama wewe kwanza na wasiwasi na Elimu yako kama umesoma chuo basi chuo cha kata kama viongozi wako kina mbowe na wenzake..Viongozi wasomi Chadema ni wawili tu ZITTO na LISU..UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.
Hivi wewe una akili timamu kweli unafikiri kusoma UDSM ni usomi basi kuanzia leo niite msomi kwa vile nimesoma UDSM, sina haja ya kulumbana na wewe kwa sababu ndani ya uongozi wa CDM si kuwa kuna viongozi waliosoma pale tu kuna ma-lecturer bado wanafundisha pale leo.
 
Kama kuna kipindi Muhimu katika siasa za CHADEMA Basi ni hiki, Uamuzi wa CUF, NCCR,TLP,UMD wa Kumuandikia Baruwa Mhe Mbowe na Kumuomba awashirikishe katika Kambi ni Ujasiri na Ukomavu wa Kisiasa wa Vyama hivyo nasema Hongera hAMAD rASHID na Viongozi wa Kambi ndogo, Ushauri wangu kwa Mhe Mbowe kuwa jasiri yasahau ya Nyuma weka Maslahi ya Kambi Mbele ubinafsi utupe mbali, nyosha Mikono yako uwapokee wenzako kwania safi ufanmye nao kazi kwaaslahi ya Watanzania Wanyonge walio wengi waliokandamizwa na CCM, vyenginevyo ukiwapuuza na Kuwakatalia wenzako ukasahabikia Utengano na kusaikiliza Kiburi cha Wapambe wako basi majuto yatakuja baadae. nchi hii haiwezi kukombolewa na Chama Kimoja bali vyama vyote dhidi ya CCM.
Nakuomba tena Mwenyekiti Mbowe tujengee historia Mpya ya Upinzani ndani ya Mkutano Huu unaoanza sasa ndani ya Bunge. DAMU za Mashujaa waliodhulumiwa ARUSHA zinataka Kutetewa na zile zilizopotezwa kila palipo na wanamageuzi nazo zinataka Kuenziwa.
Mbowe alishaweka wazi kuwa CDM iko tayari kufanya kazi na chama makini but they are not bounded, kama CUF & co. wametubu na wamevunja kambi yao then they are welcome lakini wasije kwa nia ya kupata vyeo.
 
devide and rule.......GET DIVIDED SO YOU CAN BE RULED EASILY.......! tehe tehe tehe upinzani bwana
 
Mbowe alishaweka wazi kuwa CDM iko tayari kufanya kazi na chama makini but they are not bounded, kama CUF & co. wametubu na wamevunja kambi yao then they are welcome lakini wasije kwa nia ya kupata vyeo.

Give and take rule, hivi mnawataka bila kuwapa chochote..

Wakikubali watakuwa maf..ala
 
Nafasi ya Waziri Kivuli ina maslahi gani? Ni ni nini mchango wao? Ni vyema tukajadili nafasi ya waziri kivuli bungeni ili tuweze kufika mahali tujue ni nini hasa CDM wanaweza kufanya wakati Baraza hilo linaundwa. Hili linatokana na concept ya ....cheo/vyeo....ambayo imejitokeza.
 
Ushirikiano wa upinzani ni kitu kizuri na tunapaswa kuwashajihisha CHADEMA kulifikiria jambo hili kwa upana wake.
Kwa bahati mbaya , mleta mada amekuja na "CUF sasa wawapigia magoti chadema". Amefanikiwa kuwapandisha mashabiki wa CHADEMA mzuka, lugha iliyotumika katika michango inaonesha hivyo.
Hivi kweli watanzania hatutaki ushirikiano wa vyama vya upinzani?
Hivi tunafikiri CHADEMA na wabunge wake 45 ina sauti ya kutosha bungeni?
Ushabiki mwengine ni utoto!
Katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.
 
Hivi wewe una akili timamu kweli unafikiri kusoma UDSM ni usomi basi kuanzia leo niite msomi kwa vile nimesoma UDSM, sina haja ya kulumbana na wewe kwa sababu ndani ya uongozi wa CDM si kuwa kuna viongozi waliosoma pale tu kuna ma-lecturer bado wanafundisha pale leo.

Wewe Chadema ni nani mpaka mimi nikuite msomi wala mimi siitaji kujua umesoma wapi. mimi sijakujibu wewe nashangaa unafata post yangu mimi kama sina akili timamu sawa nadhani wewe ndani ya Chadema ni loose ball Meretricis..unataka kufokea watu utadhani JF ya baba ako.
 
1.Ibrahim lipumba UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
2.Juma Duni UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
3.Ismail Jussa UNIVERSITY OF HULL CITY. UK
4.Hamad Rashid UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
5.Julius Mtatiro UNIVERSITY OF DAR ES SALAA
6.Maalim seif UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
hiyo ndio safu ya viongozi wa CUF sasa sijui utasilimu dini kama ulivyosema..basi kama uwezi kusilimu nipe tig...unadhani watu wote wajinga kama wewe kwanza na wasiwasi na Elimu yako kama umesoma chuo basi chuo cha kata kama viongozi wako kina mbowe na wenzake..Viongozi wasomi Chadema ni wawili tu ZITTO na LISU..UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.

Ahsante sana kwa taarifa yako ya elimu. Imetusaidia pia kupata taarifa nyingine muhimu;

Uongozi wa juu wa CUF.... 5:1 yaani Waislamu 5 Mkristo Mmoja.

Uongozi wa CDM .....1:1 yaa Muislamu 1 Mkristo 1

Hoja ya udini mara nyingi ni hisia. Hisia hutokana na vitendo au maneno yanayotrigger hisia!! Najiuliza, ndio maana Prof Safari kajitoa? Ndio maana hakushinda uenyekiti?

Umeamsha hisia za 'huenda uislamu' upo CUF. Ni jukumu lako kuthibitisha vinginevyo. Kuthibitisha huko kusiwe 'CDM kuna ukabila au CDM kuna udini pia'....

Ni hisia!
 
Kwani CUF ni chama cha upinzani tena? CUF wanasaidiana na CCM kuunda serikali kule Zanzibar, na CUF haina viongozi wa juu tofauti ( meaning viongozi wa juu wa CUF Zanzibar ndo hao hao upande wa bara). Sasa iweje CUF ijiite chama cha upinzani?

CHADEMA, msije mkaingia mkenge hapa, mmeona kwenye chaguzi za jiji na halmashauri jinsi hao jamaa walivyopiga kura zao. Walisimama na wakahesabika. This is not a time for playing GAMES.
 
CUF ni chama tofauti na CCM na CHADEMA.. CUF kimekaa kitaifa zaidi kina wabunge sehemu zote za Tanzania. Bara kina viti vya ubunge. Pemba kina viti vya ubunge, Unguja kina vitu vya ubunge. nadhani umeona tofauti ya CUF na vyama vingine

Hivi kumbe bado Zanzibar kuna upinzani??
 
Back
Top Bottom