CUF na Usiri??

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,154
70
Na Salim Said


CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimesema mazungumzo yake na serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni siri inayopaswa kuwekwa wazi kwa makubaliano maalumu.

Juzi Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alikutana na rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika Ikulu iliyoko mjini Unguja.

Mkutano ambao unatarajiwa kufanyika leo mjini Unguja utahudhuriwa pia na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye aliwasili Zanzibar tangu jana jioni.

Kumekuwa na maswali mengi baina ya wananchi na wadau wengine wa masuala ya kisiasa, kuhusu nini kilichowakutanisha rais Karume na Hamad Ikulu mjini humo.

Awali Mwananchi ilifanya juhudi ya kumpata Katibu Mkuu huyo wa CUF kuzungumzia mazungumzo hayo, lakini hazikufanikiwa na hivyo kufanikiwa kumpata Mkurugenzi wa Mambo ya Nje Jussa Ismail Jussa, ambaye pia alikataa kuzungumzia kikao hicho.

“Si siri nzito ila kwa sababu mazungumzo yamehusisha pande mbili, utaratibu hauruhusu upande mmoja kuzunguza yaliyozungumzwa katika kikao, ni utaratibu tu.

“Lakini kesho (leo), tuna mkutano wa hadhara mjini hapa ambapo baadhi ya mambo hayo, yatazungumzwa katika mkutano huo na viongozi wa kitaifa wa CUF,” alisema Jussa.

Hata hivyo, Mwananchi haikuishia hapo kwani ilimtafuta Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alithibitisha kuwa na taarifa ya kikao hicho na kwamba ni kimepangwa kwa muda mrefu sasa.

“Yaa nina taarifa juu ya kikao hicho, lakini kimepangwa kwa muda mrefu kuzungumzia mambo mbalimbali yanayowahusu watu wa Zanzibar.

“Lakini kesho (leo), tutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao utafanyika Zanzibar na mimi ndio nitakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo,” Profesa Lipumba.
Alisema baadhi ya madhumuni ya kikao hicho, yatazungumzwa kwa kina katika mkutano huo na kuondosha kiu ya Wazanzibar, wanaotaka kuelewa kilichozungumzwa baina ya maalim Seif na rais Amani.
 
My take: it does not work always on their favour???
 
My Take: ...Patience pays..!Let the time talk, kuweni na subira, yote yatakuwa hadharani in no time!
 
Back
Top Bottom