CUF na Chadema waungana kuipinga bajeti

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,507
Bajeti imepita na wabunge 81 wameipinga dhidi ya 234 kwa hesabu ya harakaharaka wabunge karibu wote wa upinzani wameungana kuipinga, hongera wabunge wetu naona huo ni mwanzo wa ushirikiano kwa makubwa yajayo.
 
Sasa hivi CUF, TLP, NCCR Mageuzi hawana jeuri maana chadema wamewekeza kwa wananchi - nguvu ya umma. Nadhani hii inaweza kuwa tiba ya u-mamluki maana wanasiasa walizi kuwa vigeugeu. Unashindwa kujuwa wanasimamia nini maana leo yuko huku kesho kule ili mradi posho inaingia. Sasa wananchi tunatakiwa kuwa wakali, hatutaki ulaghai.
 
Nilishtuka kuona msafara wa mheshimiwa fulani ulivyo na msululu mrefu wa magari mpaka nikachoka kuyahesabu, ilikuwa ni siku moja tu nimeingia nchini toka nchi moja ya ughaibuni. Nilichoshangaa nchi ya ughaibuni msafara wa rais haukuzidi magari 12, na hakuna ufungaji wa barabara kama bongo. Tutafika wapi na mwendo huu?
 
Nataka niseme kitu kimoja kwa watanzania wenzangu kuwa
kweli wamepinga tena kwa hoja za msingi na manufaa ya watanzania.
Lakini it was a bad strategy kutafuta uhalali wa bajeti hiyo kwakuipigia kura wakati mnaelewa Demokrasia tanzania ni kimvuli tu!.

Bajeti hii ilipaswa kupitishwa/kukataliwa kwakuzingatia hoja za msingi zilizofanyiwa utafiti na sio vinginevyo.


Demokrasia gani hii? Loo!
Watu wanavote kwa ushabiki wa vyama vyao badala yakutazama hatima ya kizazi cha mtanzania ili kesho serikali iwe na uwezo wakuongeza bajeti na kuimarisha maendeleo na pato la taifa.

Kweli mbuzi anaakili fupi kama mkia wake.
WAR FRONT CHADEMA LETS GO!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom