CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

Mtatiro nakufaham sana jinsi ulivyo strong tangu tulivyokuwa kwenye harakati chuo. Pole kwa matokeo ya Igunga, naamini ukitulia utaendelea kujifunza mengi kutokana na matokeo hayo!

Ushauri wangu mdogo kwako, Ikiwa kweli unadhamira ya kuijenga CUF, basi usijaribu kuibomoa kwa kuiponda CDM! Tumia nguvu zako nyingi kupambana na wadhalimu CCM na utashinda. Kuiponda CDM ni kujijengea chuki mbele ya wananchi wengi ambao kwa sasa wanaiona kuwa ni mkombozi wao! Kwa hiyo kupambana na CDM kutapelekea kuiua CUF...
hapo kwenye red sasa!! watawezaje kupambana na mtu waliefunga nae ndoa?
 
Kila mtu alijua mtashindwa vibaya. Wakati kampeni zimepamba moto Igunga mwenyekiti wenu alijitokeza kwenye tvs akiwa tayari mkononi ana tiketi ya kwenda USA! Sasa ulitegemea mfanye kipi cha ajabu? Siasa za CUF zimejikita Pemba na sio huku kwa Watanganyika!
 
Umesema huwezi hamia kwenye chama chenye nguvu kama CHADEMA, hongera kwanza kwa kukiri kuwa CHADEMA wana nguvu, sasa nyie CUF hamna nguvu mnafanya nini sasa, maana ni sawa unaenda kupigana huku ukisema hauna nguvu, mimi binafsi nakuona wewe ni mpambanaji, tatizo ni chama chako, ushauri wangu kwako, HAMIA CHADEMA, 2015 nenda kachukue jimbo la RORYA, maana TARIME, yupo Rais wako WAITARA.
 
actually CUF co tu mmefanya vibaya, zaidi mmetia AIBU! yaani almost kila kituo mmepata SINGLE DIGIT! that the price ya USALITI wengine wanasema....

Kaka Mtatiro kaeni chini mtafakari wapi mmeshindwa! na jitahidini kutafuta na ushauri kwa wataalamu wa siasa na masuala ya uchumi na kijamii.
 
Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi.

Hivi nifasheni ya siasa za CUF na CCM sikuhizi kwamba ni lazima uitaje CHADEMA ndiyo hoja yako ikamilike?
 
hivi na nyie mlikuwepo,,,, si mlitumwa kupunguza kura chadema..
 
Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.
Msisitizo kwenye RED inaonekana hujiamini..Unasema umeshindwa ina maana una matokeo husika...Sasa tuambie nani kashinda Uchaguzi wa Igunga usikae kimya ina maana kila kitu unakijua kwa umesha prove failure.....Tupe mshindi.
 
Mkuu Mtatiro huo ndiyo ukomavu kuna msemo kuwa 'If you walk like a duck and quack like a duck, you are probably a duck'. CUF kilikuwa ni chama kilicholeta matumaini ya kuondokana na CCM katika chaguzi za 1995, 2000 and Yes a bit in 2005. Ninajua kuwa CCM ili-invest resources nyingi za Taifa kubadili image ya CUF kwa kuwa-print kama chama cha kiislam, magaidi etc. Strategy nyingine ilikuwa kuhakikisha uchaguzi wa 2005 hawawatangazi washindi wa ubunge hata kiti kimoja Bara japo mgombea wenu wa urais alipata kribia 10% ya kura za bara. Kwa kuwadhoofisha ninyi wakajikuta kuwa kiu ya watanzania ya mabadiliko inazidi kuwa imara zaidi na hivyo watanzania kuona kuwa CHADEMA kinaziba ombwe hilo.

Ninyi CUF baada ya kuingia mkataba wa kutawala na CCM kule visiwani mkajisahau na kufuta nafasi yenu kama wapinzani. Mkawaona CDM kuwa wamechukua nafasi yenu bara hivyo kuanzisha vita ya wazi na matumaini ya mabadiliko ya watanzania kwa kuwatumia wabunge wenu wanaotoka visiwani waliochaguliwa kwa kura 1,500 ili kuidhibiti CDM bungeni kupitia kama HAMAD RASHID na kulazimisha kubadili kanuni bungeni. Hilo lilikuwa kosa kubwa la kwanza kisiasa kwa CUF.

Kama haitoshi mkaendelea kuungana na CCM katika kila move ya kupinga harakati za CDM, wananchi wanaona, wananchi wanaufahamu na kwa hivyo basi msemo wa hapo juu kwenye bold bwana Mtatiro una maana sana kuwa huenda ninyi ni 'CCM B' Japo inawezekana kuwa mnafanya siasa za kuisaidia CCM bila kujijua.

Kitu mlichotakiwa kufanya ni kufocus na 'MONSTER WA WATANZANIA-CCM' ambao ndoto yao ni KUMUANGAMIZA na kuachana nae kabisa baada ya miaka 50 ya uhuru. Mshindi mkuu katika uchaguzi wa IGUNGA ni CDM regardless kama atatangazwa mshindi wa Ubunge ama LA! and Biggest loser ni CUF ikifuatiwa na CCM ambayo inatumia msuli mkubwa kupita kiasi ili kulitetea jimbo ililoshinda miezi 11 iliyopita.

Kushindwa vibaya kwa CUF si propaganda maana propaganda ni huwa ni mambo ya uwongouwongo kama vile CCM inavyojaribu ku-paint CDM kuwa chama cha vurugu wakati wame-demonstrate otherwise katika kampeni za Igunda, au kama walivyo waki-paint kuwa ninyi ni chama cha kiislam huko nyuma. Suala la ninyi kuwa CCM-B ni suala lililo practical zaidi kuliko propaganda. Tulitarajia CCM pekee iwashambulie CDM na ninyi CUF muishambulie CCM kama CDM wanavyofanya kwa kuwa ndiyo chama kilichoshika dola. Sasa kama chama kilichopo madarakani kinakishambulia chama ambacho kinatishia uwepo wake madarakani na ninyi mnaungana na chama kilichopo madarakani kukishambulia chama kinachotishia madaraka ya CCM ni dhahiri kuwa ninyi ni counterparty wa CCM mkiwa na lengo lilelile la kuizuia CDM kuwa popular enough ili kisishinde uchaguzi.

CUF mlitakiwa kila wakati ku-side na CDM strategically, no mater what kwani CDM inabeba imani ya wananchi wengi kuwa chama tawala mbadala kwa sasa, kwa kufanya hivyo nanyi mngeweza kupata imani hiyo ya wananchi wenye uchu wa mabadiliko.

Wabunge wa visiwani na CUF visiwani adui mkuu no 1 wa CUF bara, mkilijua hilo mkalirekebisha tunatarajia kuwa uchaguzi ujao CUF itaambulia chochote kitu
 
Mura poti hawa warisya ni wanafiki sana,mnachoongea barazani wakiingia misikitini wanakubaliana kingine nawe hupo.Cuf hawana interest na muungano na nina hakika hilo unalijuwa,mura wanataka kukutumia tu km kondom na bdae wakudump.MURA ebu fikiria kwanini watu wote humu wanakubaliana kuwa ww ni mpiganaji wa kweli wa haki za wanyonge wa nchi hii ,tatizo ni hao ulio nao ni wanafiki sana mnachoongea huwa hakitoki moyoni.MURA NKHOGHOSASAMANDE TAYA CHADEMA NKYO KYA BHAMURA TATIGHA ABHARISYA BHAYO ABHAIKARA AMANCHE KEBHONO TEBHANTOHE MURAAAA!!!!!!!.
 
MTATIRO a.k.a MWANAMPOTEVU hebu rudi kundini, Nenda kaunganishe nguvu na CHADEMA, Achana na Hao wazushi!
 
wewe jamaa una akili sana ..naamini ccm hakuna watu kama wewe ..hawa watu kama nyie mpo wachache na mpo kwenye vyama vya upinzani..ombi langu ni kuombeni msiwe na siasa za udini ..najua hata nyinyi mnasimama katika hili kupinga udini ...
 
Chama kimekufa rasmi Tanzania bara kwa ile sera ya CCM-B.

Utajikuta unabaki alone na mabendera ya chama utayafanya mapazia pale kwako. Kama kwenye kituo mnapata kura 0 inamaana hata wakala wenu anawachinja. Kafanyeni biashara nyingine, hasa wewe mkuu kwa usafi wa kinywa chako unapendezea ukiwa msimamizi wa choo cha stand somewhere.
 
Tatizo lenu CUF mlidhani kuwa Watanzania ni wapumbavu na hivyo mkategemea kupata kura nyingi sana katika uchaguzi mdogo Igunga. Watanzania wameshakishtukia chama chenu kama ni kitengo kingine cha CCM tangu pale mlipoamua kuingia katika muafaka na CCM na hivyo kuunda Serikali ya mseto Zenj.

Pia kuwa kwenu mstari wa mbele katika kuipinga na kuifanyia vurugu CHADEMA badala ya CCM kumewafunua macho Watanzania kwamba nia yenu kubwa kama chama si kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania bali kulinda maslahi ya mamluki wachache ndani ya CUF na pia kuilinda Serikali ya kifisadi ya CCM ambayo ipo madarakani hivi sasa.

Inabidi mbadili mwelekeo wenu ili Watanzania tukione chama chenu kama kweli kinatetea maslahi ya Watanzania vinginevyo chama chenu kipo hatarini kufutika katika anga za siasa ndani ya Tanzania.
 
wewe jamaa una akili sana ..naamini ccm hakuna watu kama wewe ..hawa watu kama nyie mpo wachache na mpo kwenye vyama vya upinzani..ombi langu ni kuombeni msiwe na siasa za udini ..najua hata nyinyi mnasimama katika hili kupinga udini ...
Usizunguke sana, mwambie asiwe na siasa na maji ya chooni kama alizokua anazitumia kwenye kampeni hizi.
 
Tatizo lenu CUF mlidhani kuwa Watanzania ni wapumbavu na hivyo mkategemea kupata kura nyingi sana katika uchaguzi mdogo Igunga. Watanzania wameshakishtukia chama chenu kama ni kitengo kingine cha CCM tangu pale mlipoamua kuingia katika muafaka na CCM na hivyo kuunda Serikali ya mseto Zenj. Pia kuwa kwenu mstari wa mbele katika kuipinga na kuifanyia vurugu CHADEMA badala ya CCM kumewafunua macho Watanzania kwamba nia yenu kubwa kama chama si kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania bali kulinda maslahi ya mamluki wachache ndani ya CUF na pia kuilinda Serikali ya kifisadi ya CCM ambayo ipo madarakani hivi sasa.

Inabidi mbadili mwelekeo wenu ili Watanzania tukione chama chenu kama kweli kinatetea maslahi ya Watanzania vinginevyo chama chenu kipo hatarini kufutika katika anga za siasa ndani ya Tanzania.
Yani walifikia hatua na wao wakajiona eti ni chama, Alafu mie navyojua msindani huwa ni mmoja tu ila nashangaa Mtatiro anavusema eti washindani wakubwa wa CUF ni CDM na CCM anajilinganisha na nani wakati chama chake kina kosa hata kura moja kwenye kituo kana kwamba hata wakala wao hawapi kura.
 
Yani walifikia hatua na wao wakajiona eti ni chama, Alafu mie navyojua msindani huwa ni mmoja tu ila nashangaa Mtatiro anavusema eti washindani wakubwa wa CUF ni CDM na CCM anajilinganisha na nani wakati chama chake kina kosa hata kura moja kwenye kituo kana kwamba hata wakala wao hawapi kura.

Muache huyu aendelee kudhania kwamba CUF wana ubavu wa kushindana na CDM. Magamba yenyewe inabidi ichakachue kura kupitia kitengo kingine cha CCM kinachoitwa Tume ya uchaguzi ya CCM ili wahakikishe wanaibuka kidedea vinginevyo hawana ubavu wa kupambana na CHADEMA katika majimbo mengi ya uchaguzi nchini.
 
I'm sure CCJ ndio right choice kwako kwa muda huu cz ur a dead walkn body just like it
 
Kwanza karibu kwenye jukwaa letu la JF...maaana ndo kwaaanza nimekuona...
Pili enzi za ujinga wa CCM zimeisha na wananchi wanajua wanachokifacha....
Matokeo haya yawe onyo kali na mjue 2015 hata Zanzibar mwaweza msipate kiti....kama huamini ngoja uchaguzi mwingine uje...
Msalimie NAPE na Makamu wa Rais Zanzibar
 
Huko uliko unapoteza muda mkuu,hama huko ww wamejaa wadini huko ndugu Mtatiro,nenda Rorya wadau wameshakushauri ndugu,pole yako
 
Back
Top Bottom