Elections 2010 CUF kuweka mambo hadharani leo

Ilulu

Senior Member
Mar 22, 2008
161
31
CUF kuweka mambo hadharani leo Friday, 17 December 2010 09:19 Na Waandishi Wetu, jijini

CHAMA Cha Wananchi (CUF) leo kinatarajia kuweka mambo hadharani katika viwanja vya Temeke mwisho ambapo pia Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalism Seif Sharif Hamad, anatarajiwa kuhudhuria.Akizungumza na gazeti hili leo asubuhi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, amesema mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

“Lengo la mkutano ni kumpongeza Maalim Seif kwa kuteuliwa kwake na pia tutazungumzia maana ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hivyo tunawaomba wananchi na wanachama kufika kwa wingi katika viwanja hivyo,” amesema

Pia amesema katika mkutano huo watazungumzia suala la umuhimu wa kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano na kutoridhishwa na usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Hatukuridhishwa na tume hiyo kwenye uchaguzi, kwa hiyo hilo ni kati miongoni mwa mambo tunayotarajia kuyazungumza kwenye mkutano huo. Tunataka tume huru isiyopendelea upande wowote,” amesema mwenyekiti huyo.

Pia amesema Maalim Seif atazungumzia changamoto mbalimbali zilizojitokeza Zanzibar katika kipindi cha uchaguzi.

Ameelezea kuwa Maalim Seif ataelezea kwa kina juu ya uchaguzi mkuu uliopita na tathimini ya kina kwa kujiimarisha zaidi ili kukabaliana na siasa za wakati uliopo na matokeo ya undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo ili kufahamu masuala mbalimbali na mikakati iliyowekwa na chama hicho kuhakikisha kuwa kunakuwa na mabadiliko.

Source: CUF kuweka mambo hadharani leo
 
You can never have your cake and eat it. So CUF should not confuse us, they have decided deliberatly to walk in CCM shadow. In Zanzibar they have abandoned their own election manifesto and instead they have teamed up with CCM to assist in the implementation of its manifesto. Given that situation whatwill CUF tell the electrate come 2015
 
Maalim is in Zanzibar and in political marriage with the corrupt party ,then how dare can he put mambo hadharani? Lipumba went to congraduate Kikwete for becoming a legimate president in his words,then today how? We are not sobber! Mh.go with other business,in that you lost a trademark.
 
Maalim is in Zanzibar and in political marriage with the corrupt party ,then how dare can he put mambo hadharani? Lipumba went to congraduate Kikwete for becoming a legimate president in his words,then today how? We are not sobber! Mh.go with other business,in that you lost a trademark.

Wakuu,

Ukiwa tayari umejiamulia msimamo basi inakuwa unapata tabu ku-digest ujumbe wowote utakaousikia.
Waacheni jamaa waanike, waweke hadharani whatever they want to say. Halafu tuchambue.

Tusiwe watu wa misimamo mikali.
 
Wanataka kurudisha imani kwa watu wa bara maana wanajua kuwa wameshapoteza muelekeo na watu hawana imani nao tena! Nahisi wanaona itawasaidia kuwaeleza wanachi juu ya wao kushiriki kutekeleza ILANI ya CCM!

kazi wanayo........
 
Kutokana na mwenendo wake siku za karibuni dhidi ya vyama vya upinzani kama CHADEMA ambacho kinaungwa mkono na watanzania wengi wa bara siyo kwa ushabiki bali kwa hoja, CUF itakuwa na kibarua kigumu sana kurudisha imani yake kwa wabara walio wengi. Nadhani jambo la kwanza ambalo CUF watatakiwa kufanya ni kuwadhihirishia watanzania kuwa uwepo wao siyo kwa manufaa ya CCM, siyo kwaajili ya kufifisha jitihada za CHADEMA kuleta mabadiliko, na wala wao siyo vibaraka wa CCM. Maana kauli na mienendo ya CUF kwa siku za karibuni imekuwa ya kutatanisha mno na imegeuka kuwa mpinzani wa vyama vya upinzani.
 
CUF ni chama kinachoongozwa na watu wasomo na waliokomaa kisiasa, wanjua wanachikifanya ngoja nikawasikilize
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom