CUF kutumia Helikopta (chopa) ktk kampeni Igunga

mzee wa mawe

Senior Member
Aug 2, 2011
151
15
CHAMA cha wanainchi (CUF), Kimesema wameenda Igunga kuchukua jimbo na kwamba wako tayari na wao kutumia Helkopta (chopa), kama vyama vingine vitafanya hivyo.

Kimesema kitatumia njia yoyote ile ili mradi hawavunji sheria za uchaguzi hadi wachukue jimbo hilo lililoachwa na aliyekuwa mbunge wake, Rostam Aziz wa CCM ambaye alijiuzulu.

Mratibu wa Uchaguzi jimbo la Igunga wa CUF, kirungi Ameir kirungi aliiambia Jambo Leo Dar es salaam jana kwa njia ya simu kuwa vyama vya ccm na chadema ni vilaini na havina ushawishi kwa wapiga kura wa jimbo hilo.

Kirungi alisema wagombea wa vyama vingine havina ushawishi kwa sababu wagombea wake si wakazi wa Igunga hivyo hatayajui matatizo ya jimbo hilo.
 
So what? Hata wakiamua kutumia ungo ushindi kwa CCM upo palepale.
 
CUF hawahitaji kuumiza vichwa vyao,wao watafanya kile wenzao wanachofanya.(copy and paste).
Hiyo ndio wanaiita "OPERESHENI LOLOTE NA LIWE".
 
Siasa za Kibongo bwana. Wakat ccm wametenga 800m cuf nao wanakuja na chopa. Mwananch wa Igunga anafaidka vip na haya?
 
cuf kweli mmeamua kama wakikimbia ardhini wakienda angani wafuateni huko huko angani mpaka kieleweke.
 
...

Kimesema kitatumia njia yoyote ile ili mradi hawavunji sheria za uchaguzi hadi wachukue jimbo hilo lililoachwa na aliyekuwa mbunge wake, Rostam Aziz wa CCM ambaye alijiuzulu.

....

kama hawajadhamiria kuvunja sheria za uchaguzi igunga, basi si washiriki wenye dhamira ya kuchukua jimbo. hakuna chama ambacho hakitavunja sheria Igunga.
 
Sipati picha. Siku CDM wakisema wanatumia Airbus kwenye kampeni kila chama kitatangaza kutumia Airbus. Akili za kudesa bana, taabu tu. Huumizi kichwa, halafu ukivuna mabua unalalamika.
 
Du!kaaz kwel kwel!
Ngoja tuone mtanange.kazi kwenu wanaigunga.nawashauri msidanganyike.mbwembwe za uchaguzi ndo zimetufikisha hapa tulipo.
 
Hapo cuf wanaiga tembo ,na watakuwa wamepewa chopa na ccm ili upinzani wagawane kura na ccm ishinde kiuraisi .Hawa cuf watatumika mpaka line?
 
Back
Top Bottom