CUF Kumjibu Kikwete Rasmi.-Upingwaji wa Hotuba ya Kikwete

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Habari zilizonifikia kutoka kwenye vyanzo vya habari zinasema Katibu Mkuu wa CUF MH.Seif Sharif Hamad anajiandaa kuwasilisha kwa wananchi majibu ya Mh.Kikwete kusema Zanzibar haitambuliki kimataifa kama Nchi.

Mbali ya hotuba yake kuanza kupata upinzani mkali ndani na nje ya Nchi ,hasa kuhusu suala la kuwashughulikia Mafisadi.CUF Zanzibar inasema inajipanga ili kumuelimisha Mkuu huyo kuwa mbali ya kusema Zanzibar si nchi nje ya Tanzania pia Mh.Kikwete atatakiwa airudishe Nchi nyengine iliyomo ndani ya Tanzania vinginevyo Zanzibar itaanza mkakati wa kujitafutia utambulisho mwengine nje ya Tanzania kwani mkakati huo upo na Zanzibar ni mwananchama katika umoja wa Mataifa kama Nchi zisizotambulika au zilizomezwa.
 
Am fed upa kwamba Zanzibar ni/si nchi?Whats the big deal anyways?kama wanataka kuwa nchi wapewe hiyo sovereignty and the so called Union Matters ziwe eradicated kila nchi ijitegemee!Kwa sababu hii issue ya Zanzibar being a country sasa inaanza ku bore sasa before JK hajatangaza vita na Zanzibar hao akina Shamhuna na wenzake nendeni huko Uarabuni maana ndio najua mnapopaita Kimataifa!
This is just pure gabble!
 
The Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar

--------------------------------------------------------------------------------
THE ARTICLES OF UNION

between

THE REPUBLIC OF TANGANYIKA AND THE PEOPLES' REPUBLIC OF ZANZIBAR

WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar being mindful of the long association of the peoples of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of furthering that associatio! n and strengthening of these ties and of furthering the unity of African peoples have met and considered the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples Republic of Zanzibar:

AND WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples'Republic of Zanzibar are desirous that the two Republics shall be united in one Sovereign Republic in accordance with the Articles hereinafter contained:-

It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.

(ii) During the period from the commencement of the union until the Constituent Assembly provided for in Article (vii) shall have met and adopted a Constitution for the united Republic (hereinafter referred to as the interim period) the united Republic

(i! ii) to (vi).

shall be governed in accordance with the provisions of Articles

(iii) During the interim period the Constitution of the united Republic shall be the Constitution of Tanganyika so modified as to provide for-

(a) a separate legislature and executive in and for Zanzibar from time to time constituted in accordance with the existing law of Zanzibar and having exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to the Parliament and Executive of the united Republic;

(b) the offices of two Vice-Presidents one of whom (being. a person normally resident in Zanzibar) shall be the head of the aforesaid executive in and for Zanzibar and shall be the principal assistant of the President of the United Republic in the discharge of his executive functions in relation to Zanzibar;

(c) the representation of Zanzibar in the Parliament of the United Republic;

(d) such other matters! as may be expedient or desirable to give effect to the united Republic and to these Articles.

(iv) There shall reserved to the Parliament and Executive of the united Republic the following matters-

(a) The Constitution and Government of the united Republic.

(b) External Affairs.

(c) Defence.

(d) Police.

(e) Emergency Powers.

(f) Citizenship.

(g) Immigration.

(h) External Trade and Borrowing.

(i) The Public Service of the united Republic.

(j) Income Tax, Corporation Tax, Customs and Excise.

(k) Harbours, Civil Aviation, Posts and Telegraphs.

And the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.

(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-

(a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

(b) to such provision as may be made by order of the President of the united Republic for the extension to Zanzibar of any law relating to any of the matters set out in Article (iv), and the revocation of any corresponding law of Zanzibar;

(c) to such amendments as may be expedient or desirable to give effect to the union and to these Articles.

(v) (a) The first President of the united Republic shall be Mwalimu Julius K. Nyerere and he shall carry on the Government of the united Republic in accordance with the provisions of these Articles and with the assistance of the Vice-Presidents aforesaid and of such other ministers and officers as he may appoint from Tanganyika and Zanzibar and their respective public services.

(b) The first Vice-President from Zanzibar to be appointed in accordance with the modifications provid! ed for in Article (iii) shall be Sheikh Abeid Karume.

(vii) The President of the united Republic: in agreement with the Vice-President who is head of the Executive in Zanzibar shall-

(a) Appoint a Commission to make proposals for a Constitution for the united Republic.

(b) Summon a Constituent Assembly composed of Representatives from Tanganyika and from Zanzibar in such numbers as they may determine to meet within one year of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the united Republic.

(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

IN WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.

Passed in the National Assembly on the twenty-fifth day of April, 1964.
 
Hapo naona kihindi hindi tu, wapeni hao wazenji ka nchi kao mbona hata wake tunaoana kuzaa nao watoto na tunapeana talaka??? Hebu tuwapeni talaka yao period!

Ila usanii wa Muungwana wa kutaka kuridhisha na kuwa mwema all the time matokeo yake ndo haya, hakukuwa na haja ya kusema ni nchi ndani ya nchi lakini nje ya nchi si nchi! huu ni usanii ulio tukuka!
 
Wanachanganya btween territory na sovereignity . Zanzibar ni territory wala sio Sovereign state. Wakitaka kudai sovereignity wajue ni UHAINI ebo?

''Kuungana ni hiari ,kuvunja muungano ni JINAI '' Thanks Pro.f Shayo
 
Hivi mbona naona kama watanganyika viongozi ndo kama wanang'ang'ania sana huu Muungano? Kama wazenj hawataki si muwape nchi yao jamani? Mbona hata ndoa zinavunjika? Wapeni zenj yao halafu na Pemba nao wajitenge ndo watakumbuka umuhimu wa Union waliokuwa wanaikashifu na kuibeza.
 
It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.
 
i like the statement "kuungana hiari, kuvunja muungano uhaini"!!! unajua adhabu ya kupatikana na hatia katika kosa la uhaini? KIFO therefore muungano ni kifo kwa sasa
 
It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.


See, I did told you, kwamba Maalim Seif Hamad, ni tatizo... tusubiri.
 
It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.

HILO NDIO JIBU, FULL STOP. Kwa yeyote anayedai Zaa-nzi-bar ni nch mpe hiyo quote. Mi binafsi nina wazo kuna uwezekano wa kutafsiri hiyo so called 'CONTRACT' NA KUITOA LIVE KWA WATU WOTE?
 
It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.

Everthing is possible under the sun!If they wanna be sovereign let it be na huo Muungano uvunjwe maana sasa imekuwa kama vile Tanzania Bara ndio imekuwa wanang'ang'ania huo Muungano na kama ni usalama wetu tunaweza kuugarantee wenyewe!
 
Muungwana anajua lakini anataka kujifanya hajui. Amesema kuwa kina watu wanadai zaidi ya hiki wanachokisema, yeye nina hakika anakijua wanachokidai, lakini katuvuga katika hotuba yake kana kwamba hajui, sasa moto utamwakia
 
Swala la Muungano ni la kikatiba. As long as Katiba ya sasa ni active, yeyote anyepinga Muungano anavunja sheria na anastahili kuchukuliwa hatua za kisheria hadi pale katiba iliyopo itakapositishwa.
 
Hao Viongozi wanaopiga kelele Zanzibar ooh Zanzibar eeeh wakistaafu wananunua viwanja bara wanajificha hawataki ata kurudi Zanzibar...Wanafiki wakubwa hao hao ndio wameongoza kwa kupeleka wake, watoto na ndugu zao na kujilipua nchi nyingine wanakuja na kelele za kudai nchi yao ebo!! wapeni Zanzibar yao tubaki na Tanganyika yetu.
 
Mbali ya hotuba yake kuanza kupata upinzani mkali ndani na nje ya Nchi ,hasa kuhusu suala la kuwashughulikia Mafisadi.CUF Zanzibar inasema inajipanga ili kumuelimisha Mkuu huyo kuwa mbali ya kusema Zanzibar si nchi nje ya Tanzania pia Mh.Kikwete atatakiwa airudishe Nchi nyengine iliyomo ndani ya Tanzania vinginevyo Zanzibar itaanza mkakati wa kujitafutia utambulisho mwengine nje ya Tanzania kwani mkakati huo upo na Zanzibar ni mwananchama katika umoja wa Mataifa kama Nchi zisizotambulika au zilizomezwa

Wakuu naomba kupewa somo ktk maneno haya ya Seif Sharrif Hamad..
Ikiwa anachukua kujiunga kwa Zanzibar mwaka 1963 ndio sababu ya wao kuwa wanachama inakuwaje huyo huyo Seif anakubali kuwa Tanganyika sio nchi wakati nayo ilijiunga UN mwaka 1961?..Bila shaka wanatumia Articles of Union kuikana bara (Tanganyika) kama nchi lakini inapofikia swala la Zanzibar wanatazama nje ya Articles....jamani hata Chungwa huitwa chungwa pamoja na kwamba ndani yake lina chanya tofauti hivyo nje linaonekana ni kitu kimoja lakini ndani lina hizo tabaka...
Kisha sidhani kama kuna utaratibu UN wa kuandikisha uanachama nchi ambazo hazitambuliki au zimemezwa!..hiyo ni historia mabyo inaweza kuzirudisha ama kuziondoa nchi nyingi sana zisizokuwa na idadi, hata sijui alikuwa akizungumzia kitu gani kwa sababu nimetazama hata list ya wanachama wa UN nimekuta haya kuhusiana na Tanzania:-

Tanganyika was a Member of the United Nations from 14 December 1961 and Zanzibar was a Member from 16 December 1963.
Following the ratification on 26 April 1964 of Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964...
Kwa hiyo hata UN wana mwanachama mmoja tu!

Wakuu, tatizo kubwa limeanzia pale tulipoondoa vice President wawili toka bara na visiwani kulingana na makubaliano ya awali, kiasi kwamba Zanzibar leo wanajikuta hawana sauti ndani ya uchaguzi wa kiongozi wa juu ndani ya serikali ya Muungano kama zamani.
Huyo Shein sio chaguo la Wa Zanzibar ila Karume na huyo Karume hana madaraka kama ilivyotakiwa na Articles wala na sio second in command kama yalivyokuwa makubaliano..UHESHIMIWA..

Halafu jambo jingine ambalo nimelikuta ktk Article na linaweza kuleta kesi nzuri kwao ni kile kifungu cha (H) kinachohusiana na Trade na Borrowing!.... Hapa kusema kweli mikopo mingi inakwenda bara na kuinufaisha bara zaidi ya Zanzibar... Itakuwa vizuri kama serikali yetu inaweza kuorodhesha matumizi ya mikopo hii ktk maendeleo ya serikali ya Muungano kwa sababu inakuwa vigumu sana kwa Mzanzibar kufahamu kuwa Kikwete anpokwenda marekani na kuomba mkopo hua anaomba kwa niaba ya nani?... Mathlan fedha za Bush zime/zitawasaidia nini Zanzibar!..
 
Nimetazama hata list ya wanachama wa UN nimekuta haya kuhusiana na Tanzania:-

Tanganyika was a Member of the United Nations from 14 December 1961 and Zanzibar was a Member from 16 December 1963.
Following the ratification on 26 April 1964 of Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964...
Kwa hiyo hata UN wana mwanachama mmoja tu! .

Hapo ulipopigia mstari ndipo kinaonekana kipo kizuizi fulani ...zimeendelea kama ni single member kwa mtazamo huo unaweza kusema nchi moja tu kati ya hizo ikipeleka maombi kuwa sasa basi kila mmoja kivyake vyake tumechoshwa na matatizo yanayotokana na kuendelea kama nchi moja,wandugu hakuhitaji kura ya maoni wala maono hapo, ni kazi ya UN kutengua au kutegua mstari tu pamoja na kutangazia katika Baraza la UN kuwa kumewakilishwa hoja hii na upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,yeyote mwenye pingamizi alete mbele hoja yake .
Tatizo nchi iliyopo na inayojulikana ndani ya Tanzania ni Zanzibar ,Tanganyika haipo ,hivyo kama Zanzibar wakiamua kupeleka ombi hilo mbele basi hakutakuwa na msemaji wa Tanganyika ambae ataweza kuisemea au kuitetea ,ndio ikasemwa machogo wameshikwa pabaya ,ndio mkasikia Muungwana akisema itumike busara ,anajua fika kuwa suala hili likifika UN halitachukua hata wiki ,ndio itakuwa mwisho wa Muungano na Tanganyika itabidi waanze kulana nyama kila mmoja anataka kuwa Raisi mpya wa Tanganyika na waziri mpya waTanganyika.

Hili ni jambo la kuvutia sana ,WaZanzibari wanaonekana kuishika amani ya Tanganyika mikononi mwao japo hilo watanganyika vichwa mchungu hawalioni mbali na usomi wao, hatari iliyopo sio kwa WaZanzibari ambao akili zao zimeshaona mengi tofauti na WaTanganyika ambao bado damu za kikabila zinachemka ,mapigano mangapi yamezuka ndani ya Tanzania ,ardhi na mifugo ,madini na kadhalika ,hilo WaTanganyika wanalifumbia macho lakini ukichunguza ni kiini cha mapambano ya ndani ya nchi katika nchi nyengine ,ukiweka mbali mambo ya siasa na uchu wa madaraka ,kama wengi wa MaCCM wanavyoitupia Zanzibar suala hilo.

Leo hii Zanzibar ikiamua kwenda huko UN ,basi Tanganyika itakuwa kwenye matatizo makubwa na si kama mnavyofikiria,hilo napenda mlifahamu na pia mlitafakari kwa akili yenye kuona mbali ikichanganya na matokeo.

Wazanzibari wanasema mambo na kero za Muungano ambazo si kuwa hazipo zipo na zinajulikana na walio wengi , madai ya WaZanzibari na serikali zao zinazopita kila siku yanajulikana na viongozi na maraisi wote walioshika wadhifa wa kuingoza Jamhuri hii ya Muungano wa Tanzania ,wanasema yashughulikiwe yatatuliwe ,uwepo uwiano wa nchi mbili zilizoungana ,iwepo heshima kwa Raisi wa Zanzibar (siwezi kusema na waTanganyika kwa sababu wanazozijua wao hawataki iwepo Tanganyika ,japo kuna ushahidi wa huyu Kikwete kudai kuwepo kwa Tanganyika)

Haiwezekani awepo Raisi wa Nchi iliyokuwemo ndani ya Muungano halafu mumfanye kama mwandishi wa habari ,hii itasomeka kama dharau kwa WaZaznibari na kwa hali ilipofikia sasa hivi huwezi tena kuiondoa Zanzibar kwani hali ya hewa hairuhusu kufanya jambo hilo kwa njia za amani ni too late kinachowezekana ambayo naona ni busara aliyosema Muheshimiwa Kikwete ni kuivuta na kuiamsha serikali ya Tanganyika na kuendelea kwa msemo uleule uliotumika UN kuwa :-

United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964...

Lakini kusema watu wagawane mbao nakuhakikishieni WaTanganyika mtauwana na kugawana mapande mapande na msitarajie kama mtakuwa wamoja kuigandamiza Zanzibar kama mnavyofanya sasa ,hio ni ndoto mbaya sana kwenue asiefahamu historia za mapambano ,hivi kunakoonekana kujikaza kwa baadhi yetu ,kuwa tuwaachie Zanzibar yao na tuchukue Tanganyika yetu ,basi hayo sio maneno ya kuitakia mema Tanganyika mtauwana kama ngedere ila kama mnataka hivyo basi kwanza ni kuirudisha Tanganyika wakati Tanzania ipo as a transit ,natumai nimefahamika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom