Ndivyo Ilivyo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 243
- 4
Ah Ndugu yangu Bwana. Mkataba gani uliokubaliwa. Kamati ya Muafaka ni kama Kamati ya Wataalmu iliyofanya "spade work" kutayarisha hayo mambo. Wewe unayaita Mkataba , umekubaliwa wapi, umetiwa saini wapi. CUF wamepeleka kikao cha juu -kimekubali, sawa. Huo ni upande wake. CCM nao wamepelka kikao cha juu (Halmshauri), haikukataa, lakini imeona kuna mapendekezo (ya kuboreshwa) inafaa yafanywe. Kosa liko wapi? Kuwa mtulivu, na pitia vizuri hayo mambo uyafahamu, kuliko kuweka mbele kulaumu tu.Kuhusu maoni ya Muungano ni jambojengine hilo subject to discussion wakati unapowadia.naona unajichanganya hapa...
Kuna sehemu unasema kuwa pande zote mbili zimekubaliana na kuna sehemu pia unasema kuwa ccm wamebadilika na kuamua mambo yaende kwa wananchi. Katika hili aliyekataa makubaliano ni ccm. Sheria za mikataba zinasema kuwa upande mmoja ukibadili vipengele vya mkataba basi hiyo ni sawa na kukataa mkataba.
Kuhusu hii ya kusikiliza wananchi, je ccm iko tayari kuwaruhusu wananchi wa zanzibar watoe maoni yao kuhusu muungano?