CUF kimepoteza mvuto kwa Watanzania?

Pinokyo Jujuman

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
552
104
Prof.Ibrahim Lipumba amekanusha kauli hiyo leo asubuhi wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kirushwacho kila siku asubuhi kwenye Television ya Taifa; akijibu swali hilo Prof alisema kuwa CUF hakijapoteza mvuto kwa watanzania na kimsingi chama cha CUF ni chama kinachosimamia HAKI kwa watanzania na ni chama cha wanyonge hata Hayati Mwl Nyerere aliwahi kuweka bayana ya kuwa chama chenye upinzani wa kweli na chenye maslahi kwa Watanzania ni chama cha Wananchi CUF.
My take (........ )
 
prof.ibrahim lipumba amekanusha kauli hiyo leo asubuhi wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha jambo tanzania kirushwacho kila siku asubuhi kwenye television ya taifa; akijibu swali hilo prof alisema kuwa cuf hakijapoteza mvuto kwa watanzania na kimsingi chama cha cuf ni chama kinachosimamia haki kwa watanzania na ni chama cha wanyonge hata hayati mwl nyerere aliwahi kuweka bayana ya kuwa chama chenye upinzani wa kweli na chenye maslahi kwa watanzania ni chama cha wananchi cuf.
My take (........ )

rip cuf
 
Prof.Ibrahim Lipumba amekanusha kauli hiyo leo asubuhi wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kirushwacho kila siku asubuhi kwenye Television ya Taifa; akijibu swali hilo Prof alisema kuwa CUF hakijapoteza mvuto kwa watanzania na kimsingi chama cha CUF ni chama kinachosimamia HAKI kwa watanzania na ni chama cha wanyonge hata Hayati Mwl Nyerere aliwahi kuweka bayana ya kuwa chama chenye upinzani wa kweli na chenye maslahi kwa Watanzania ni chama cha Wananchi CUF.
My take (........ )

Hana washauri huyu Prof. Lipumba, inasikitisha kwa msomi mkubwa kama yeye anaburuzwa na kina Jusa, Kwa heshima yake binafsi nadhani angeachana tu na mambo ya siasa akajikita kwenye taaluma yake ya Uchumi. Heshima yake ingekuwa kubwa zaidi.
Chama kina kashfa ya Udini, Ubaguzi wa wazi kwa Wabara na Wazanzibar, Ana kipi cha kusema kuhusu Ubadhilifu wa fedha wa wazi uliotokea ndani ya CUF? Nasikia anamkataba wa miaka miwili huko US bora aende huko hiyo tar. 28/03/2012. Aibu
 
nilikuwa ctegemei professor akubali chama chake kama kimekufa, eti wanasema kimezidi kuimarika, kwa vp
 
wangetumia muda huu kufanya ziara mikoani hususan bara kukijenga chama,sasa wamemwachia jusa anaekuja na statement kwamba cuf imeshindwa uzini kwa sababu uzini wakazi wake wengi ni wabara
 
Kwahiyo hapa kama kweli Hayati Mwl JKN aliitoa kauli hiyo basi alikua na mtazamo butu au twaeza isema vipi hii?
 
Back
Top Bottom