CUF Ina mgogoro na Vyombo vya Habari?

CUF haihitaji waandishi wa habari ,wala hawana haja nao ,chama imara hakitegemei neema ya waandishi ,na haswa siku hizi za utandawazi,Gadafi ,Mubarak na wengine wameondolewa na wananchi walioamua kwa kupitia mtandaoni na sio magazetini.

CUF imeiteka Pemba imeiteka Unguja ,kumbuka huko walikuwa hawapati aina yeyote ya chombo ambacho kilikuwa kinawatangaza ,sasa akili kichwani mwako ,inajulikana wazi hata watoto wadogo wanaijua CUF kuliko CCM au mashoga zake.
 
nyie cuf! hata wabunge wenu wengi sana watapungua bungeni!2015! maana mambo yenu mengi yamekaa ki uamsho zaidi!
 
nyie cuf! hata wabunge wenu wengi sana watapungua bungeni!2015! maana mambo yenu mengi yamekaa ki uamsho zaidi!

Usije ukawacha domo wazi ukisikia CDM wamepata mbunge mmoja ,andika pahali haya maneno ili uweke kumbukumbuka !
 
Sheikh ponda, mtutano wa juzi walihamasisha waislamu kujiunga na CUF eti kwa sababu watu wanasema hivyo.

Soma thread ya uhusiano wa CUF na Wandishi wa habari ya leo asubuhi

Sheikh Ponda ana wadhifa gani ndani ya CUF mpaka kauli yake iwe ndio msimamo au mtazamo wa chama? Unaweza kutuwekea speech nzima ya Ponda tujiridhishe na maelezo yako!
 
Kwa nini mnasahau mwaka 2005 wafuasi wa CUF waliwapiga waandishi wa ITV pale mako makuu ya chama hicho Buguruni?
 
juzi chama cha cuf kilifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya jangwani.

Nilikuwepo binafsi nikichukua picha na kusikiliza hotuba mbalimbali. Pamoja na mambo mengine, cuf inaonekana kutokuwasema vizuri wana habari na nilisikia mwenyewe kutoka hotuba za viongozi, isipokuwa lipumba pekee mashambulizi, ama vijembe kwa wanahabari.

Viongozi wa cuf wanaamini vyombo vya habari havipendi, ama vinapotosha, ama vinabeza habari kuhusu chama chao, na nilisikia watu wa kawaida wakiazimia kupiga waandishi watakaohudhuria mkutano wao baadaye ikiwa ule wa jangwani hautaonekana kupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari,hususani magazeti.

Na kweli nimefuatilia magazeti ya jana, mengi hayakutoa uzito wowote kwa habari ya cuf. Mtanzania waliweka picha ya umati,lakini habari yao kuu ilihusu taarifa ya awali ya mkutano wa kamati kuu ya chadema, vivyo hivyo magazeti mengine.


sasa ni kweli upo mgogoro kati ya waandishi na cuf? Kama ndiyo, umesababishwa na nini, na kama hakuna ugomvi, nini kinapelekea habari za cuf kutopata uzito unaostahili kwenye vyombo vya habari? Je, yawezekana ni mikakati ya washindani wao kisiasa yaani ccm na chadema kwamba cuf wasipewe uzito? Ama ni udhaifu wa idara ya habari ya chama cha cuf yenyewe kutotenda kazi ipasavyo?

Maana nikiri pia kuwa japo mimi ni mwanahabari sikumjua afisa habari wa cuf hadi juzi alipotambulishwa mkutanoni. Na katika mengi ama yawezekana hii ni kutokana na cuf kushuka umaarufu kisiasa kiasi kwamba habari zake hazivuti wasomaji?

Naomba mitazamo yenu

chanzo: Mjengwablog

mgogoro hkuna ila ni mfumo kristo ndio unafanya kazi..so long uongozi wa juu wa cuf ni waislam basi wandishi na vyombo vya habar kwa jumla huwa hawatoi ama wanapotosha..

Hili ni tatizo moja kwa mfumo huu hatari
 
Hivi majuzi Chama Cha wananchi CUF Kilifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, CUF walionekana kutokua na imani na wana habari wa Tanzania. Viongozi karibu wote, isipokuwa Lipumba(ambae alifunika kwa kuongea vizuri) hawakuficha hisia zao na kuonyesha kubaguliwa kwa chama chao na wana habari wa Tanzania,na walipeleka mashambulizi,ama vijembe kwa wanahabari wa bongo wote.Viongozi wa CUF wanaamini vyombo vya habari havipendi,ama vinapotosha,ama vinabeza habari kuhusu chama chao, na kuna wanachama wa kawaida walisikika wakiazimia kupiga waandishi watakaohudhuria mkutano wao baadaye ikiwa ule wa jangwani hautaonekana kupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari, hususani magazeti.

Nikajitolea kufanya ka research kasiko rasmi kuchunguza madai,shutuma na tuhuma hizo nzito za wana CUF dhidi ya wana habari wetu na magazeti yao,research yangu imekamilika na nimeifunga rasmi leo. Nilichokigundua kutokana na ka research kangu ako madai ya CUF yanaonekana kuwa na msingi, Nimejiridhisha kwamba ni kweli siku iliyofuata baada ya CUF kutoa madai yao na mpaka leo nimefuatilia magazeti karibu yote, mengi hayakutoa uzito wowote kwa habari ya CUF. Mengine yalijitahidi japo inaonekana kwa shingo upande ku cover story ya mkutano huo wa cuf jangwani, Mtanzania kwa mfano ambalo ni gazeti linalomilikiwa na kada wa CCM huku mtendaji wake mkuu pia akiwa ni kada matata wa ccm waliweka picha ya umati,lakini habari yao kuu ilihusu taarifa ya awali ya mkutano wa kamati kuu ya CHADEMA,hivyo hivyo magazeti mengine.

Sasa ni kweli upo mgogoro kati ya waandishi na CUF? kama ndiyo,umesababishwa na nini,na kama hakuna ugomvi,nini kinapelekea habari za CUF kutopata uzito unaostahili kwenye vyombo vya habari? je yawezekana ni mikakati ya washindani wao kisiasa yaani CCM na CHADEMA kwamba CUF wasipewe uzito?

Naomba tuwe huru kwenye kutoa maoni kwenye hili lengo likiwa ni ustawishaji wa demokrasia na maendeleo ya kweli hapa nchini,jazba na unazi wa vyama tuviweke pembeni kwa muda ili tuweze kuwa huru kutoa maoni yetu.

Nawasilisha.
 
Si kweli, mimi nijuavyo hapa waandishi wa habari huandika habari ambazo wananchi watahitaji kuzisoma, hivi katika hali ya kawaida kuna mtu yeyote anategemea kusikia jipya ndani ya CUF, mimi kama mwandishi wa habari ni andike habari za CUF ili Gazeti lisinunuliwe? haiwezekani.
 
Magazeti ni biashara, wao wanaangalia kichwa ambacho kitauza sana.

Unaweza kukuta Simba imeshinda jana lakini leo magazti yana habari kuu za Yanga kuidhinishiwa rasmi Mbuyu Twite na Yondani.
 
SAM_5157.JPG


SAM_5162.JPG


SAM_5163.JPG

baadhi ya magazeti siku moja baada ya mkutano wa CUF
 
CUF ilijiua yenyewe ilipokubali ndoa na CCM ambayo wananchi tayari kwa hisia zao wanaona haina jipya, kwa mantiki hiyo CUF kuwa mshiriki wa serikali isiyo na jipya na iliyoshindwa kutoa majibu ya shida zao indrirect nayo inadharaulika.

CDM wao wanoanyesha nia ya dhati hata kama ni ya kinafiki lakini bado unafiki wao haujagundulika. CUF wamelala sana, hawana mapya.
 
CUF ilijiua yenyewe ilipokubali ndoa na CCM ambayo wananchi tayari kwa hisia zao wanaona haina jipya, kwa mantiki hiyo CUF kuwa mshiriki wa serikali isiyo na jipya na iliyoshindwa kutoa majibu ya shida zao indrirect nayo inadharaulika.

CDM wao wanoanyesha nia ya dhati hata kama ni ya kinafiki lakini bado unafiki wao haujagundulika. CUF wamelala sana, hawana mapya.

kama ni hivyo mbona habari za ccm na chadema zinaandikwa vizuri tu,kwanini ccm iliyojiunga na cuf iendelee kuwa maarufu huku cuf ndio ionekane imepoteza umaarufu kisa madai kwamba imeungana na ccm ilhali haijaungana na ccm
 
kama ni hivyo mbona habari za ccm na chadema zinaandikwa vizuri tu,kwanini ccm iliyojiunga na cuf iendelee kuwa maarufu huku cuf ndio ionekane imepoteza umaarufu kisa madai kwamba imeungana na ccm ilhali haijaungana na ccm

mbona unajikanganya ... CUF na CCM wameungana ili kuunda ya umoja wa kitaifa ... au ni uongo?
 
Ulimsikia Makamu Mwenyekiti, CUF Taifa juzi pale Jangwani na wito wake kwa waislamu? Aliongea as if yuko kwenye Islamic Republic.

Hiyo ni true hata mi nakubaliana nawe tena walisema 'waislam njooni mjiunge na cuf ccm na cdm haviwataki ' .
 
Back
Top Bottom