Cuf ikishinda 2010, znz kuwa peponi tena!

Lampart

Senior Member
Sep 18, 2009
139
2
CUF IKISHINDA 2010, ZNZ KUWA PEPONI TENA!

  • ZNZ kurejea kuwa The Capital of East Africa
  • Union Bridge kuimarisha Muungano zaidi
Muandishi wa Wagagagigikoko aliefuatana na Jean Touchatte - yule diplomat kutoka Canada alieondoshwa Tanzania bila ya hata kupigwa kofi moja kwa kuwatemea mate na makohoo Watanzania pale Dar Es Salaam hivi majuzi na ambae alisema kuwa eti alifanya hivyo ili Watanzania waliolala fofofofo waamke katika nchi yao tajiri, ameondoka juzi Toronto (baada ya temperatures kushuka mpaka minus 40 degrees Centigrade) kurejea DSM kupitia Muscat, Oman, ili kuwajulia hali Watanzania wanaoishi katika nchi za Ghuba. Hii hapa chini ndio msg yake aliyoipeleka kwenye Central News Pool ya Wagagagigikoko mjini DSM, kwa njia ya email kama dakika 10 zilizopita:

From: <12345@wanene.com>
To: <ncp@wanene.com>
Sent: Tue, December 22, 2009 8:12:08 PM
Subject:
CUF IKISHINDA 2010, ZNZ KUWA PEPONI TENA!
Najua haiaminiki kwa wengi na kwa kila mtu katika ukumbi wenu wa JF, lakini nilijua kuwa nia hio ipo pale nilipomsikia Maalim Seif Sharrif amepatana na CCM ZNZ kwaajili ya maslahi ya Waznz. Kama haya yalikuwa hayaaminiki, basi niliyoyakuta hapa Muscat kwenye drawing boards hayatoaminika kabisa hapo ukumbini kwenu JF.
Kwa ufupi, Waznz wanaoishi nje wameamua kuifufua nchi yao ili irejee tena kuwa The Capital of East Africa and the Centre of Learning - kama ilivyokuwa hapo mwanzo, kwani kuna mipango kabambe ya kuanzisha projects chungumzima za kufufua uchumi wa ZNZ kama hali ya siasa ikiruhusu.
Project ya kwanza ni kuiunganisha ZNZ na Bara kwa bridge ambayo itakuwa inaurefu wa kama 30 km. Project inategemewa ku-cost kama USD 7.5 billion. Wasioijua historia ya ZNZ watasema kuwa hilo halitotokea na labda ZNZ iunganishwe na Oman na sio Bara. Hawa wamesahau kuwa kama sio Maalim Seif leo Muungano ungelikuwa haupo, kwani Aboud Jumbe alikuwa keshafika mbali na mipango yake ya kuuvunja Muungano baada ya kuona kuwa alipigwa ngwara na Nyerere pale alipokubali kuunganisha vyama. Seif ndie aliyetoa ripoti ya usaliti wa Jumbe kwa Nyerere na leo ni lazima tumshukuru Maalim wetu kwa kuwa bado Muungano upo. Kama sio Seif Sharrif basi leo Tanzania ingelikuwa ni nchi mbili kama zilivyokuwa kabla ya 1964. Kwahivyo, CUF inaposema kama inataka Muungano uendelee, basi hio sio kwasababu Bara tayari ishatekwa kiuchumi na wale wafanya biashara machachari wa kipemba waliozagaa kuanzia Ilala mpaka Kariakoo, bali ni kwasababu CUF ni Muungano na Muungano ni CUF.
Hii project ni feasible kabisa na wenye hela wanaishughulikia kisirisiri kwa manufaa ya Tanzania, na sote inabidi to keep our fingers crossed, because it will open up ZNZ to the 40 million brothers and sisters on the Mainland. Imagine 800,000 people to have an easy access to a market of 40 million people!!! Zanzibar will definitely benefit. Kama kweli hio consortium itazipata hizo hela za project au Waznz wa hapa Ghuba wameshiba kahawa na tende, au ndio wanangojea hayo mafuta &#8211; that remains to be seen, lakini kusikia idea kama hii ikizungumzwa peke yake inatia moyo sana. Kwa upande mwengine, habari ninazozipata hapa Muscat zinaelezea kuwa hii project itaendelea kubakia kwenye drawing boards kama ZNZ haitokuwa na serikali imara na ya mseto na kama Bara haitokuwa na Rais anaekubalika na wananchi wote. Kama JK ataendelea na ZNZ itaendelea kuwa chini ya CCM peke yake basi hii project itakuwa ni ndoto tu, kwani hakuna mwekezaji atakaekubali kutoa hata senti moja yake ikiwa hajui muelekeo wa nchi wa baadae utakuwaje.
 
...... kwa kuwatemea mate na makohoo Watanzania pale Dar Es Salaam hivi majuzi ..........

Wala sio uongo, kwani sote tunahisi kuwa Watanzania sote tumetemewa mate na hayo makohoo, na hasa ukisoma hizi habari za leo kuwa BoT wametumia billioni moja kuikarabati nyumba ya Gavana wakati watoto Mbagala wanasoma chini inazidisha uchungu.
Akitokea mtu mwengine akatutemea mate wala sitostaajabu, kwani tunastahiki kufanyiwa hivyo kwa kulala kwetu!!!
 
Kwa ufupi, Waznz wanaoishi nje wameamua kuifufua nchi yao ili irejee tena kuwa The Capital of East Africa and the Centre of Learning - kama ilivyokuwa hapo mwanzo, kwani kuna mipango kabambe ya kuanzisha projects chungumzima za kufufua uchumi wa ZNZ kama hali ya siasa ikiruhusu
Heee..!sikuijua hii...Ohh God, maisha ni kujifunza kumbe!
 
duhh kweli wa TZ tumekweisha na tunajiangamiza wenyewe na hatutofika kokote kule.
 
Hili suala la bridge hata mie niliwahi kuwa nalo kichwani kama ni ndoto, na si jambo ambalo haliwezekani kama pesa ipo.

Sisemi kama CUF wataleta bridge, lakini idea nzima ya bridge sio kama ni too fantasy.Inaweza kabisa kuwa designed na kuwa implimented, its a matter of cash!

Hata SMZ kama itakuwa na funds designers na engineers wanaweza kuitackle issue iyo na kuifanya reality!

Kama CUF wanataka kutetea muungano wa Tanzania, wazanzibari wengi watachomoa support yao kwenye chama hicho.Mimi sifati vyama, kwasababu sitaki muungano kabisa nataka shirikisho tuu la EA.Uhusiano wa Tanganyika na Zanzibar uwe kwa njia hii tuu ya EAC, not more!

Sasa kama CUF watakuja na sera za Nyerere za muungano udumishwe zaidi, naona kama Maalim yuko hatarini kuripuliwa bomu au kukatwa kichwa!
 
Hio consortium sio ya CUF wala CCM. Wanachotaka ni serikali zote 2 ziwe zinakubalika kwa watu!
Katika sisi Wabara, yoyote anaekataa Muungano basi huyo analo lake, kwani we have nothing to lose at all!!!
Hio bridge mimi personally ninaiunga mkono, lakini wazenj itabidi wawe makini zaidi, kwani tumeona hasara ya kuondoa p/port baina ya Bara na ZNZ - ujambazi wa silaha umeanza ZNZ kama inavyoripotiwa kila siku - jambo ambalo lilikuwa hakuna kabisa huko nyuma!
 
hapo ni mseto tu!

Wengi wanafurahia mseto, lakini mseto ni hatari kubwa kwetu Wabara, kwani tutakuwa hatujui nani anatuuma!
Bora kiwe chama kimoja, kwani tunaweza kukipa dawa, lakini vikiwa viwili pamoja kazi itakuwa ngumu sana kumjua nani ni adui yetu!
Kama wakiwa CCM peke yao na akina Yussuf Himid wanaleta taabu, basi tutawafanyia kama tulivyomfanyia Aboud Jumbe. Kama wakiwa CUF peke yao ni rahisi zaidi kwa Serikali ya Muungano kuwatimua under the pretext of endangering our national security na baadae tukaitisha uchaguzi mwengine. Lakini wakiwa pamoja tutamtimua nani? Au wote kwa pamoja?
 
Mawazo yako yanatisha sana! tena ni mabaya kabisa na ya kushangaza mno.
 
..huu Muungano hauko feasible.

..napendekeza uvunjwe na Zenj wawe majirani zetu Watanganyika kama zilivyo Kenya,Rwanda,Mozambique, etc.
 
..huu Muungano hauko feasible.

..napendekeza uvunjwe na Zenj wawe majirani zetu Watanganyika kama zilivyo Kenya,Rwanda,Mozambique, etc.

Muungano hauvunjiki kwa mapendekezo bana! kuwa serious

Tudumishe muungano, kuwepo na referendum aina ya muungano na mambo ya muungano yajadiliwe na yapigiwe kura iwe ni win-win situation
 
Muungano hauvunjiki kwa mapendekezo bana! kuwa serious

Tudumishe muungano, kuwepo na referendum aina ya muungano na mambo ya muungano yajadiliwe na yapigiwe kura iwe ni win-win situation

Tupe sababu 10 za kuutetea muungano huu wa shaghal baghala...
 
Tupe sababu 10 za kuutetea muungano huu wa shaghal baghala...
Muungano upo tayari wa kutoa sababu ni wale wanaotaka kuuvunja..mimi wala siumizi kichwa kutoa sababu ila niko tayari kujibu hoja zako "kwanini hutaki muungano"
 
Muungano upo tayari wa kutoa sababu ni wale wanaotaka kuuvunja..mimi wala siumizi kichwa kutoa sababu ila niko tayari kujibu hoja zako "kwanini hutaki muungano"
Sababu zangu binafsi za kutaka kuvunja muungano:

1.Sababu za kiuchumi na kimaendeleo, muungano unalenga kudumaza uchumi wa Zanzibar.
2.Sababu za kizalendo, Id feel better using Zanzibar Nationality rather than any other nationality.
3.Sababu za kiusalama, kuendeleza kufakamia miungano na kulazimishana mwishowe ni vurugu na umwagaji damu.

Naomba hoja za upande wa Tanganyika za kudumisha muungano kama zipo...

P:S
**Naamini Zanzibar na Tanganyika ni majirani, na wanaweza kuishi kwa ujirani mwema kwa kupitia shirikisho la EAC.Isifahamike kama sipendelei umoja, hii hoja ya umoja ni swafi kabisa lakini iwe na mslahi na sio babaisha ***** kama ilivyo muungano huu.
 
Ukianzisha chama na sera hizo nitakuwa Katibu wako!
 
Mzee ukiwa na maana kuwa na CCM nao waungojee au mtaendelea kuula wa peke yenu?
CCM ya sasa itaendelea kushinda katika majimbo ambayo imekuwa ikishinda, hali kadhalika CUF wataendelea kushinda katika ngome zao kubwa huko PBA na Mji Mkongwe.

Ili kuondoa misuguano iliyodumu kwa miaka kadhaa sasa, ushindi wa jumla utakuwa ni kuundwa kwa serikali ya mseto. Hili ndio lengo kuu!
 
Back
Top Bottom